Alhamisi, 25 Mei 2017

SENTENSI ZA KISWAHILI

SENTENSI ZA KISWAHILI
Sentensi ni ulio kamili kisarufi ambao unajitegemea kimaana.
Kila sentensi lazima kijitegemee kimaana na kisarufi.
Haya ni ya lazima;
  1. Neno/fungu la maneno
  2. Maana kamilifu
  3. Mpangilio wa kisarufi unaokubalika
Mifano.
Alimchezea .
Baba ameondoka kwenda dukani.
Mtoto analala.
Tungo hizi zinaleta ujumbe kamili na hazihitaji maneno zaidi ili kujikamilisha.
Tazama mifano ifuatayo;
i.mtoto
ii. anayekuja
iii.kiroboto mkubwa
iv.ameondoka dukani kwenda baba.
Mifano hii ina dosari kuwa katika (i) na (iii) haileti ujumbe kamili.nao mfano wa (iv) haina mpangilio mzuri wa kisarufi.
Sentensi huweza kutokea kama;
  1. Taarifa
     i.kisu cha mama kimepotea.
     ii.saa hii imeharibika kabisa.
  1. Swali
i.Nani amemwona mwanangu?
ii.Umeleta pesa ngapi?
  1. Amri
i.fungua mlango mara moja!
ii. Toka hapa haraka!
  1. Ombi
i.Niongezee tafadhali.
ii. Mama nisamehe.
  1. Mshangao
i.Lo! Wezi walituvamia jana usiku.
ii.Mmmh! Kwani umeleta chakula kingi namna gani!
                   Kirai
Ni neno au fungu la maneno linalodokeza maana.halina kitenzi.
Mifano ya virai
Hapa na pale                punda mzee              msichana mrefu           Lo! Babu Yule.
Kirai ni sehemu ya sentensi , na ili kuunda sentensi ni sharti kiongezwe maneno mengine yakiwamo vitenzi.mifano;
Hapa na pale panavuja.
Aina za sentensi
  1. Sentensi sahili-ni sentensi yenye kitenzi kimoja.Yaweza kuwa ya neno moja tu. Mifano
i.Ameondoka
ii.Baba na mama wanapendana.
iii. Punda mzee amekufa.
     
  1. Sentensi ambatano-ni sentensi zinazoundwa kutokana na sentensi sahili mbili au zaidi. Hizi sentensi mbili huwekwa pamoja kwa kutumia kiunganishi.
Mifano

Mtoto analia.                Sentensi sahili mbili
Mama anacheka.           

Mtoto analia ilhali mama anacheka.{ambatano}
  1. Sentensi changamano-ni sentensi ya vitenzi viwili au zaidi ambapo kimoja hujitosheleza na kingine hakijitoshelezi kimaana.
Sentensi hii ina vishazi viwili;
  i.kishazi huru
  ii.kishazi tegemezi
mifano
              Mtoto ameenda kulala.
           Kishazi huru               kishazi tegemezi
             Mtoto anakula tunda lilioza.
                   Kishazi huru          kishazi tegemezi
Tanbihi sentensi sahili= kishazi huru
Sentensi ambatano =kishazi huru(kiunganishi) kishazi tegemezi
Sentensi changamano=kishazi huru+kishazi tegemezi
Uchanganuzi wa sentensi
Ni mwainisho wa viambajengo / vipashio vilivyotumika katika kuunda sentensi.
Kwa kuzingatia vishazi na virai.
Amempiga.{kishazi}


Mwanafunzi anasoma.
Kirai              kishazi
Mama na baba wanacheka.
Kirai                   kishazi
Mwanafunzi Yule mtiifu anasoma kitabu kipya kabisa.
Kirai                                                             kishazi
Susa na Sota wanalima ilhali Mwelusi na Andua wanacheza.
Huu ni mfano wa sentensi ambatano , imeundwa kwa sentensi mbili;
i.Susa na Sota wanalima.
ii.Mwelusi na Andua wanacheza.
Aidha ina kiunganishi kinachoziunga hizi sentensi mbili chenyewe ni ‘ilhali’
Kwa mujibu wa vishazi na virai ,

                 Muundo
Sentensi huwa na kirai na kishazi, aidha sentensii huundwa kwa kundi nomino na kundi tenzi.
Kundi nomino ni sehemu yenye nomino au kiwakilishi chenye (kiima) pamoja na maneno mengine isipokuwa kitenzi.
Kundi tenzi huarifu kuhusu kundi nomino na kutambuliwa kwa kuwapa vitenzi pamoja na maneno mengineyo pia huitwa kiarifa.

KN=N/+W                            KT= T+/E +U+…..-N/W
Mifano
Susa na Sota wanalima.
Kirai                   kishazi
Kundi nomino      kundi tenzi
Sakafu ile inateleza sana.
Kirai                   kishazi
Kundi nomino     kundi tenzi
Pana mtindo wa kuchanganua kama vile kutumia vistari/vishale
Kutumia mchoro wa matawi
Kutumia jedwali{visanduku}

Maoni 9 :