Alhamisi, 25 Mei 2017

KIGOGO


                                                ONYESHO LA KWANZA.

                                                   TENDO LA KWANZA.
Ni katika karakana ya soko la Chapakazi,Sudi, Boza na Kombe wanafanya kazi ya uchongaji.Sudi amefungulia radio huku wakiendelea na kazi yao.Ashua anawaletea chai ya mkandaa na mahamri na kuondoka.
Habari inatolewa kwa wananchi wa Sagamoyo kuwa wana kipindi cha mwezi mzima kusheherekea uhuru wao, wawaku buke majagina wao waliopigania uhuru na kuwanasua kutoka utumwani, wimbo wa kizalendo unachezwa mara kwa mara.
Sudi anatofautiana na mpango wa kusheherekea uhuru kwa mwezi mzima; kwake majagina wanaosheherekewa hawakufanya lolote katika historia ya Sagamoyo.
Kuna uchafuzi wa mazingira, viongozi hawajawajibika kusafisha soko wanadai kodi na kitu juu pia vitisho kwa wanasagamoyo.

WAZO KUU.
Kuna wale ambao wanaunga viongozi mkono kwa sababu wanafumbwa kwa mambo yasiyo ya kimsingi.Aidha kuna wale ambao wamezinduka na kuhisi kuwa viongozi hawajawajibika. Sudi haoni umuhimu wa  sherehe za uhuru kupewa maandalizi ya kifahali na kipindi cha mwezi mzima.

TENDO LA PILI.
Katika karakana sokoni,Kenga anawatembelea Sudi, Boza na Kombe.Ametumwa na Majoka kuchukua vinyago vya mashujaa.Ni msimu wa mashujaa Sagamoyo, Sudi anachonga kinyago cha shujaa wa kike ambaye kwake ni kiongozi halisi wa Sagamoyo.Shujaa huyo hakufanya lolote, bali analifanyak sasa katika jimbo la Sagamoyo.
Miradhi ya kuchonga vinyago inafadhiliwa kutoka nje na wananchi wanatakiwa kulipa baada ya mwaka mmoja.
Sudi anashawishiwa kuchonga kinyago cha Ngao ili maisha yake yabadilike na jina lake kushamiri; aidha apewe likizo ya mwezi mmoja ughaibuni.Sudi anakataa kuchonga kinyago, Kenga anawapa keki lakini Sudi hali kwa kuwa ni makombo.Kombe anazinduka kutokana na kauli hii, anamuunga mkono Sudi.Kenga anaondoka kisha Tunu anawasili huku akihema na kusema kuwa mzee Kenga anapanga njama ya kuhutubia wahuni.Wote wanaondoka.


WAZO KUU.
Maskini wanatumikizwa, wanadhalalishwa, kuletewa makombo na kukumbukwa katika kipindi fulani tu ili kufaidi viongozi wao.
Miradi isiyo muhimu inafadhiliwa na wananchi kupakia na jukumu la kulipa ufadhili huo kupitia kodi.Viongozi hushawishi wanyonge ili kuwatumikia.

TENDO LA TATU
Ni katika nyumba ya Sudi barazani baada ya soko kufungwa.Tunu na Sudi wanafika kiwandani anapofanya kazi Siti, wafanyakazi wanagoma na vijana watano kuuliwa na wafanyakazi kuumia.
Kiini cha maandamano ni bei ya chakula Kupandishwa soko linapofungwa.
Sudi na Tunu wamejitolea kutetea haki na uhuru wa wanasagamoyo hata kama ni kwa pumzi zao za mwisho baada ya kufaulu.

WAZO KUU.
Kuna maandamano na migomo,walimu na wauguzi wanagoma.Migomo hiyo inatokana na kutowajibika kwa viongozi ambao wana nia ya kujifaidi.

                             ONYESHO LA PILI

TENDO LA KWANZA.
Ni ofisini mwa Mzee Majoka, anaongea kwa simu Chopi anapoingia.Ashua anafika kumwona Majoka,anataka kumkumbatia lakini Ashua anakataa.Majoka anakasirika Ashua anapomwita mzee na kufurahi anapomwita Ngao, jina lake la ujana.

Ashua amefika kuomba msaada lakini Majoka anamtaka kimapenzi.Anajaribu kumbusu  lakini Ashua anakwepa.Majoka anamshawishi, anajisifu na kujilinganisha na Lyonga wa uswahilini na Samsoni Myaudi.
Majoka anasema kuwa soko limefungwa kwa sababu ya uchafu, anatenga eneo hilo ili kujenga hoteli ya kifahari.Wanasagamoyo wanalitegemea soko hilo kula, kuvaa na kuendesha maisha yao.
Ashua anakataa kazi ya ualimu anayopewa Majoka and Mahoka academy, angekuwa mwalimu mkuu katika shule mojawapo ya kifahari.

WAZO KUU.
Viongozi hunyanyasa wachochole ili kujifaidi, Majoka anafunga soko na kunyakua eneo hilo kujijengea hoteli ya kifahari.Anataka kutumia mali na mamlaka yake kumteka Ashua kimapenzi.




TENDO LA PILI.
Husda anamkabili Ashua kwa hasira, anamtusi kuwa kidudumtu, shetani wa udaku na mwenye kuwinda wanaume wa watu.Wanaangushana na Ashua kuzabwa makofi.
Sauti ya kenga inamjia Majoka akilini kuwa soko lifungwe ili kulipiza kisasi kwa Sudi na Ashua, kisha Ashua aitwe ofisini na Husda wakabiliane.
Mwango na Chopi wanawachukua Ashua na Husda ndani, agizo linatolewa Husda atolewe ndani baada ya nusu saa.

WAZO KUU.
Wanyonge hutafutwa kwa lolote lile na kunyanyaswa.Viongozi hutumia mamlaka yao hata kupanga njama kuwateka wanyonge,Ashua kutiwa ndani ni njama iliyopangwa.

                                   ONYESHO LA TATU

TENDO LA KWANZA.
Ni ofisini mwa mzee Majoka, wana mazungumzo ya faragha na mshauri wake Kenga.
Njama yao ya kumtia Ashua ndani inatimia kisha wanamtarajia Sudi, achonge kinyago cha shujaa ndiposa Ashua aachiliwe.
Kenga anamwonyesha Majoka picha za waandamanaji gazetini.Kuna habari kuwa Tunu aliongoza maandamano kisha kuwahutubia wanahabari kuwa:
  • pesa za kusafisha soko zimefujwa,
  • soko lilifungwa badala ya kusafishwa,
  • haki za wauzaji zimekiukwa,   
  • hawatalegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.

Majoka anapanga kumwadhibu Tunu.
Maoni ya wengi gazetini ni kuwa,Tunu apigigwe kura za kuongoza Sagamoyo.Kenga anamshauri Majoka kutangaza kuwa maandamano hayo ni haramu kisha Polisi watumie nguvu, Majoka anapinga wazo hilo kwa kuwa;

      maandamano yatatia doa sherehe za uhuru,
      Tunu atazidi kupata umaarufu.

Tunu ana mpango wa kuleta wachunguzi kutoka nje kuangalia ajali ya Jabali.Majoka anasema wazuie uchunguzi huo naye Kenga anakiri kuwa itawagharimu kwa kuwa watatumia mbinu tofauti.
Majoka anaamua kuwashughulikia Tunu na Sudi.
Kuhusu mishahara ya wauguzi na waalimu, wanaafikiana waongezwe kwa asilimia kodogo kisha kodi ipandishwe.


WAZO KUU.
Viongozi wanatumia mbinu tofauti kutawala;

  • kupanga njama,
  • kuadhibu waandamanaji,
  • kutojali maslahi ya wanyonge.

Hata hivyo, wananchi wamezinduka na nia yao ni kubadili uongozi usiofaa.

TENDO LA PILI.
Majoka akiendelea kusoma gazeti,Kenga anarejea kwa vishindo kuwa kuna habari zinazoenea katika mitandao ya kijamii na kupeperushwa katika runinga ya mzalendo.
Kenga anashauri kuwa, runinga ya mzalendo ichukuliwe hatua, maandamano yanaonekana kuharibu sherehe za uhuru.Majoka anamlaumu Chopi kwa polisi kutowatawanya waandamanaji.
Tunu na Sudi wanafika, wanaagizwa kuingia na Majoka anatoa bastola, na kuwaambia Kenga wamzuie na askari.

WAZO KUU.
Habari za maandamano zinazidi kuenea na Majoka ana wasiwasi kutimuliwa mamlakani kwa kuwa Tunu anazidi kupata imaarufu.
Viongozi hutumia vyombo vya dora visivyo, Majoka anapanga vituo vya habari vifungwe na kibakie kituo kimoja tu Sagamoyo.

TENDO LA TATU.
Ni ofisini mwa mzee Majoka,Tunu na Sudi wanaingia.Majoka anataka kusema na kila mmoja lakini wanakataa kwa kuwa na nia moja.
Sudi anaarifiwa kuwa Ashua mkewe yuko ndani kwa kuleta fujo katika ofisi ya kiserikali.
Majoma anamshawishi Tunu kuwa amampangia jambo la kifahari, kumwoza Ngao Junior atakaporejea kutoka ng`ambo.
Tunu hakubaliani ma kauli hii, anamkabili Majoka na kumwambia ukweli kuwa wao ni wahuni na wauaji.Tunu anatishiwa kutiwa ndani.Tunu anafichua ukweli, Majoka walipie kila tone la damu  waliyomwaga Sagamoyo
Majoka anagharamia masomo ya Tunu hadi ng`ambo; ni haki yake kuwa babake alifia Majoka company

WAZO KUU.
Viongozi hushawishi wapinzani kwa ahadi ili wawaunge mkono, hata hivyo wanamapinduzi wanashikilia msimamo wao.




TENDO LA NNE.
Ni katika chumba cha wafungwa.Sudi amefika kumwona Ashua ambaye anadai kuwa ni kosa lake Sudi kutiwa ndani.Ashua anaomba talaka.
Ashua hataki tena mapenzi ya kimaskini, amechoka na kuchukua mkondo tofauti.Kwake anahisi kuna kitu baina ya Tunu na Sudi.

WAZO KUU.
Asasi ya ndoa inaonekana kuwa na changamoto.Kuna kutoaminiana katika ndoa,Ashua anashuku uhusiano baina ya Tunu na Sudi.

                   ONYESHO LA NNE.

TENDO LA KWANZA.
Ni nyumbani kwa kina Tunu, Bi.Hashima anapepeta mchele huku akiimba.Siti anafika na habari kuwa wahame Sagamoyo sio kwao.
Hali Sagamoyo inaonekana kubadilika  ardhi inateketea na mito na maziwa yanakauka. Kigogo amefungulia  biashara ya ukataji miti.

Tunu anafika akihema baada ya kuota kuwa Mzee Marara anamfukuza akitaka mkufu wake wa dhahabu.
Tunu amaumizwa mfupa wa muundi,uvumi unaenea kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.
Tunu anataka kukutana na Majoka na watu wake.Hashima anaona hatari Tunu akienda kukutana nao.

WAZO KUU.
Hali Sagamoyo inazidi kubadilika, kiangazi kimesababishwa na kigogo kufungulia ukataji miti, viongozi hawajali maslahi ya wananchi.
Viongozi hueneza uvumi ili kutawanya wananchi, hata hivyo; vijana wamejitolea kujenga jamii mpya licha ya vikwazo vinavyowakumba.

TENDO LA PILI.
Tunu na Sudi wanafika Mangweni ambapo shughuli za ulevi zimeshika kani, wanaletewa  kileo lakini wanakataa.
Ngurumo anaonekana kusheherekea uhuru, kwa mujibu wa Sudi,mashujaa Sagamoyo ni waliouliwa msituni wakipigana, waliohangaisha wakoloni na kuwatimua.
Tunu amefika Mangweni kuwaalika katika mkutano mkubwa utakaofanyika katika soko la Chapakazi siku ya maadhimisho ya uhuru.
Kulingana na Ngurumo, mkutano huo si muhimu, cha muhimu kwake ni kuendelea kulewa kwa mamapima
Mtu mmoja anagaragara kwa sababu yu hoi, wengine walizikwa kwa sababu ya pombe na wengine kuwa vipofu.Mtu huyo anamshawishi Tunu asipoteze bahati yake ya kuolewa na Ngao Junior.

WAZO KUU.
Watu wanapumbazwa hasa walevi kwa pombe na kuendelea kutetea viongozi wasiofaa.
Tunu na Sudi wamejitolea kutetea wanyonge Sagamoyo, wameandaa mkutano kuzindua umma.

                     ONYESHO LA TANO.

TENDO LA KWANZA.
Ni katika hoteli ya Majoka and Majoka modern resort, Husda anafika kutoka kuogelea.Kenga naye anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga,Tunu hakuvunjwa mguu.Chopi anapangiwa kwenda safari kwa kutotekeleza njama hiyo.
Sokoni, taka zote zimeondolewa, vibanda vimeng`olewa, vifaa vya ujenzi vimewasili kutoka bandarini na kuna ulinzi mkali.
 Chopi anafika na habari mbaya kuwa Ngurumo amenyongwa na chatu akitoka Mangweni.Majoka anaagiza Ngurumo azikwe kabla ya jua kutua.
Ushauri wa Majoka ni kuwa chatu mmoja atolewe kafara, na baada ya watu kuandanana waachwe katika hali ya taharuki.
Chopi tena anarejea na habari kuwa Ngao Junior kapatikana katika uwanja wa ndege akiwa na sumu ya nyoka, Majoka anazirai.

WAZO KUU.
Viongozi hupanga njama za kuwaangamiza wapinzani wao.
Viongozi wanaishi maisha ya kifahari huku maskini wakihangaika.
Viongozi hawajali hata vifo  vya wananchi vikitokea.

TENDO LA PILI.
Ni ndani ya ambulensi, Majoka hataki kufungua macho kuliona ziwa la damu.Majoka anasema yuaelekea jongomeo, kuwa amefungwa minyororo.Anataka safari isitishwe kwa kuwa haina stara.
Majoka anamfananisha Husda kama mke anayeishi ndani ya ngozi ya kondoo (kuwa Husda ni mnafiki). Husda anapenda mali ya Majoka na alilazimishwa kumwoa lakini moyo wake unampenda Ashua.
Daktari anamjuza Husda kuhusu kifo cha Ngao Junior,anazirai.




WAZO KUU.
Asasi ya ndoa imesawiriwa kuwa na changamoto; Husda hakumpenda Majoka ila aliolewa naye kwa sababu ya pesa.
Ili kuokoa asasi ya ndoa, wanaume wanapaswa kujidadisi, wawe na heshima na waseme na wake zao.Wake nao wajirudi ili ndoa zidumu.

                         ONYESHO LA SITA.

TENDO LA KWANZA.
Ni katika chumba cha wagonjwa, hali ya Majoka inaonekana kurejea.Anahukumiwa kuwa msaliti kwa wanasagamoyo na mashtaka mengine mengi.
Mayowe yanasikika na Majoka anadai kuwa hivyo ni vilio, wanalilia damu yake kisha Majoka anazungumza na babu ndotoni.
Majoka anawachukia marubani kwa kuwa waongo ilihali yeye pia ni rubani(kiongozi), hang`amui mambo kwa vile hajapambua ngozi yame ya zamani.Safari haijaanza au pengine chombo kinaenda kinyume badala ya mbele.
Safari ya babu na Majoka inatofautiana, Majoka anashauriwa asalimu amri, achague sauti ya moyo na babu yake.
Babu anamshauri Majoka  afungue masikio, macho na moyo wake kwa kuwa maisha yana ncha mbili.
Kulingana na babu, kuna misimu ya fanaka na ya kiangazi, kadhia na kuishi kwa kutojali ni muhali. Mkwea ngazi huteremka hivyo mtu achague kutenda mema, kwa maana wema hauozi. Mtu akiishi kwa wema, atajiandikia tarijama njema huku ahera.

WAZO KUU.
Maovu yana mwisho na kila aliye juu hatakaa juu milele.Wema ni muhimu katika maisha ya binadamu.

                            ONYESHO LA SABA.

TENDO LA KWANZA.
Ni katima uwanja wa ikulu ya Majoka palipoandaliwa sherehe.Ni saa nne na watu kumi tu ndio wamefika, wengine wako sokoni.
Sauti inasikika kwa mbali watu wakimsifu Tunu.Majoka anaelekea ilipo sauti, Kenga na umati wanawafuata.

WAZO KUU.
Wananchi wana nguvu zaidi kuliko viongozi .Wananchi wana mchango mkubwa kujikomboa kutokana na shida wanazozipitia zinazoletwa na uongozi mbaya.
Ili kujenga jamii mpya, wanachi hawana budi kuzinduka na kuleta mapinduzi.

TENDO LA PILI.
Ni katika lango la soko la Chapakazi, Majoka anawahutubia watu na kuwaita wajinga.Kenga anamnyanganya kinazasauti.
Tunu anabebwa juu juu na watu, anawahutubia huku wakimpigia makofi.Amejitolea kutetea haki za wanasagamoyo ili;

  • wapate maana halisi ya uhuru,
  • watendewe haki,
  • soko lifunguliwe na kujengwa upya,
  • huduma muhimu ziletwe karibu kama vile; hospitali, barabara, maji, vyoo, nguvu za umeme, elimu, ajira kwa vijana na kadhalika.

Tunu anahimiza wanasagamoyo wachague viongozi wanaolinda haki za wanyonge na kuwajibika.
Majoka kwa hasira anaamuru watu wapigwe risasi, Kingi anapokataa kwa kuwa ni kinyume cha katiba kufyatua risasi anafutwa. Kenga anasalimu amri, anajiunga na umati.
Kingi na Kenga wanajiunga na umati, wanashangiliwa, walinzi nao wanajiuzuru.Majoka kwa hasira anadai kuwa hata asipopigigwa hata kura moja atashinda.
Tunu anasindikizwa jukwaani, mamapima anafika kuomba msamaha.Anajuta sana kwa kuwalaghai walevi na kukiri kuwa aliwapunja kwa kuongozwa na tamaa ya pesa, sasa wamemgeuka.
Sudi anafika na kinyago, anasema kuhusu maana ya uhuru: shujaa ni mmoja tu Sagamoyo, ambaye ni Tunu.

WAZO KUU.
Kila kilicho na mwanzo kina mwisho, uongozi wa Majoka unafikia nwisho.Juhudi za wanamapinduzi zimezaa matunda.Maana ya uhuru sasa imepatikana na wananchi wanatarajia mengi mema.

                  JALADA LA TAMTHILIA.
Kuna sura ya mwanamme ambaye ameketi akiwa na rungu mkononi.Huyu ni Majoka ambaye ni kiongozi Sagamoyo na rungu mkononi mwake inaashiria uongozi.

Mwanamme huyo anatazama jabali lenye rangi nyeusi ambalo si laini. Jabali ni Sagamoyo na kutokuwa laini ni ishara kuwa Sagamoyo kuna shida,wanasagamoyo wana matakwa mengi. Weusi wa jabali ni uongozi mbaya unaoendelezwa Sagamoyo na viongozi.

Juu ya jabali hilo kuna mwanga, ishara kuwa kuma matunaini ambayo yanatarajiwa Sagamoyo, wanamapinduzi wanapigania haki ili kujenga jamii mpya.

                                        ANWANI YA TAMTHILIA.
Kigogo ni mtu mwenye madaraka makubwa kiutawala.

Majoka anatumia madaraka yake kulaghai wananchi, anachukua vilivyo vyao.

Anatangaza kipindi cha mwezi mzima cha kusheherekea uhuru kutumia madaraka aliyonayo.

Majoka anafunga soko la Chapakazi ili sehemu hiyo ajenge hoteli ya kifahari kwa kutumia madaraka aliyonayo.

Anapandisha bei ya chakula katika kioski kwa vile ana madaraka.

Majoka anatumia mamlaka yake kumteka na kumtia ndani Ashua.Anamtendea ukatili, Ashua ana majeraha kutokana na kichapo.

Majoka anapanga kifo cha Jabali, mpinzani wake. Anampangia ajali na kuangamiza wapinzani wake pamoja na chama chake kwa kutumia mamlaka yake..

Majoka anapanga kutumia mamlaka yake kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu kifo cha Jabali.

Majoka anafuja pesa za kusafisha soko huku akijua hakuna wa kumhukumu kwa kuwa ndiye kiongozi.

Majoka anatumia mamlaka yake kudhibiti vyombo vya habari Sagamoyo, anasema sagamoyo kitabakia kituo kimoja tu cha habari; sauti ya mashujaa, vingine havina uhai.

Majoka kwa mamlaka yake anaamuru polisi kutawanya waandamanaji.

Majoka anafungulia biashara ya ukataji miti Sagamoyo kwa kutumia mamlaka yake bila kujali athari zake kwa wananchi.

Majoka anampa mamapima kibali cha kuuza pombe haramu kwa kutumia mamlaka yake.

Kwa mamlaka yake, Majoka anafadhili miradi isiyo muhimu, anafadhili mradi wa kuchonga vinyago kutoka nje.

Majoka anaamuru wafadhili wa wapinzani kuvunja kambi zao Sagamoyo. Anamfuta Kingi kazi kwa kutomtii apige watu risasi.

                            DHAMIRA YA MWANDISHI.
Mwandishi anadhamiria kuonyesha uongozi mbaya na athari zake hasa katika mataifa yanayoendea.Viongozi hutumia mbinu mbalimbali kuongoza zinazowanyanyasa wananchi huku wakijinufaisha wenyewe bila kujali.

Kuonyesha kuwa ili kijenga jamii mpya, mapinduzi ni muhimu na ni sharti wananchi wajitolee kwa uzalendo ili kupigania haki zao na usawa na kupinga viongozi wasiofaa.

Mwandishi anaonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mwanamke katika jamii, mwanamke ana nafasi muhimu katika uongozi na kuleta maendeleo katika jamii.

                                       MAUDHUI.

1) UONGOZI MBAYA.

Viongozi huangaisha wanyonge, Ashua anasema,
          "...na kuhangaishwa na wenye nguvu ndio
           hewa tunayopumua huko." (uk 2)

Wachochole hutumikizwa na viongozi, Kombe, Boza na Sudi wanafanya kazi ya kuchonga vinyago vya mashujaa kwa ajili ya sherehe za uhuru.

Viongozi hawajawajibika, kazi yao ni kukusanya tu kodi.Ni jukumu la viongozi kuhakikisha kuwa soko ni safi lakini hawajawajibika kulisafisha. Licha ya wananchi kutoa kodi,soko ni chafu.(uk 2)

Viongozi kutangaza kipindi kirefu cha kusheherekea  uhuru ni ishara ya uongozi mbaya. Mashujaa wanaenziwa kwa kipindi kirefu ilhali mambo ya kimsingi hayajazingatiwa.Wanasagamoyo wana matakwa mengi kuliko kipindi kirefu cha kusherehekea uhuru.

Majoka anafadhili mradi usio na msingi wa kuchonga vinyago huku watu wakiwa na njaa na wao ndio watalipia mradi huo.

Viongozi hushawishi wananchi kwa ahadi ili wawaunge mkono. Sudi anashawishiwa na Kenga kuchonga kinyago ili apate malipo mazuri; kuwa mradi huo utabadilisha maisha yake na jina lake lishamiri. Pia atapata tuzo nyingi na likizo ya mwezi mzima ughaibuni na familia yake (uk 11)

Aidha viongozi hutumia zawadi kufumba wananchi kuwa wanawajali na kujali hali zao.Kenga anawaletea Sudi, Boza na kombe keki ya uhuru.
Kulingana na Sudi, hayo ni makombo na keki kubwa imeliwa kwingineko.

Viongozi hawalindi usalama wa wananchi, wananchi wanaishi kwa hofu. Ashua anahofia usalama wao kuwa huenda wakashambuliwa.(uk 15)

Migomo inayotokea Sagamoyo na maandamani ni kwa sababu ya uongozi mbaya.Wauguzi wanagoma na pia walimu wakidai haki zao. Wafanyakazi wananyanyaswa.

Majoka hajali maslahi ya wanasagamoyo. Anafunga soko ambalo wananchi wanategemea na kupandisha bei ya chakula. Uchumi Sagamoyo unasorota kutokana na soko kufungwa, watu hawana mahali pa kuuzia bidhaa zao.

Majoka anafungulia biashara ya ukataji miti bila kujali hali ya anga Sagamoyo, hasara ni kwa maskinii, viongozi wamejichimbia visima. Mito na maziwa yanakauka na mvua isiponyesha, hata maji ya kunywa yatatoka ng`ambo.

Majoka hajali kuhusu kifo cha Ngurumo licha ya kuwa mfuasi wake. Anaagiza Ngurumo azikwe kabla ya jua kutua (uk 69)

Viongozi hupanga njama ili kuangamiza wapinzani wao;

a) Majoka na Kenga wanapanga njama ya kumtia Ashua ndani.Wanapanga aitwe ofisini mwa Majoka kisha Husda aitwe ili wafumaniane. Ashua anazingiziwa kuzua sogo katika ofisi ya serikali na kutiwa ndani. Husda anafunguliwa baada ya nusu saa.

b) Kifo cha Jabali kilipangwa. Jabali alikuwa mpinzani wa Majoka mwenye wafuasi wengi. Akapangiwa ajali barabarani  kisha wafuasi wake wakazimwa na kumfuata jongomeo, chama chake cha mwenge kilimfuata ahera.

c) Tunu anapanga kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali ya Jabali. Majoka anapopata habari hizi, anapanga kuzima uchunguzi huo.

d) Kenga na Majoka wanapanga kuondoa chatu mmoja. Chatu hapa wanarejelea Sudi au Tunu kwa kuwa ndio wanaoongoza mapinduzi. Wanahofia kutolewa uongozini na ili kuzuia hali hii, wanapanga kumwondoa mmoja wao.
        "...chatu mmoja atolewe kafara ili watu wajue usalama upo, wakereketwa waachwe katika hali ya taharuki"

e) Majoka anapanga njama Tunu auliwe, anaumizwa mfupa wa muundi nia yake ikiwa ni kumkomesha asimpinge. Majoka anatumia polisi wake kutekeleza ukatili huo.

Katika hotuba ya Tunu anayowahutubia waandamanaji, Sagamoyo kuna uongozi mbaya.Anasema kuwa;

  • pesa za kusafisha soko zimefujwa,
  • soko linafungwa badala ya kusafishwa,
  • haki za wauzaji zimekiukwa.

Viongozi hawasikilizi matakwa ya wananchi. Majoka hana wakati wa kuwasikiliza waandamanaji. Hataki kujua chanzo cha maandamano wala suluhu lake.

Majoka anadhibiti vyombo vya habari Sagamoyo, habari zinazopeperushwa katika  runinga ya Mzalendo na picha za watu wengi sokoni wakiongozwa na Tunu zinamfanya Majoka kufunga runinga hiyo ya mzalendo.

Viongozi hutumia vitisho. Majoka anatishia Chopi kumwaga unga wake kwa vile polisi hawakuwatawanya waandamanaji, wanasagamoyo wanatishiwa kuhama Sagamoyo kwa juwa sio kwao, wanarushiwa vijikaratasi. (uk 52)

Majoka anatumia askari kutawanya raia badala ya kulinda uhuru wao.

Viongozi ni waongo. Majoka anatumia uongo ili kumteka Tunu. Anamhaidi jambo la kifahari, kumwoza Ngao Junior akirudi kutoka ng`ambo.

viongozi hutendea wananchi ukatili, watu wanaotiwa jela huchapwa na haki zao hukiukwa. Ashua ana majeraha kutokana na kichapo.

Viongozi hupanga uvamizi, Sudi anavamiwa (uk 54)

Viongozi wamekiuka sheria. Mamapima anadai kuwa anauza pombe haramu kwa kibali kutoka serikali ya Majoka. Ni hatia kuuza pombe haramu lakini viongozi huvunja sheria na kuwapa wauzaji kibali. (uk 61)

Sagamoyo hata viongozi hawafuati katiba.
         "...huku ni Sagamoyo, serikali na katiba ni mambo mawili tofauti." (uk 61)

Uongozi wa Majoka una ubaguzi, unafaudi wachache tu, wanaomuunga mkono. Asiya bibiye Boza anapata mradi wa kuoka keki mwa vile anauunga uongozi wa Majoka Mkono.

Viongozi hujulimbikizia mali. Kuna hoteli ya kifahari Sagamoyo, Majoka and Majoka modern resort.
Viongozi ni wanafiki. Majoka amepanga kuficha maovu yake mbele ya wageni. Ukumbi unapambwa na kurembeshwa huku kukiwa na maovu mengi Sagamoyo. Kuna mauaji, unyakuzi, njaa,maziara yamejaa Sagamoyo.

2) UZALENDO.
Wananchi wa Sagamoyo ni wazalendo, wanalipa kodi ili kuleta maendeleo licha ya kulaghaiwa.

Katika enzi za ukoloni, mashujaa walijitolea mhanga wakahatarisha maisha yao na hata kufa ili wavune matunda baada ya uhuru. (uk 4)

Wimbo unaoimbwa katika rununu ni wa kizalendo kuonyesha kuwa wanasagamoyo wanalipenda jimbo lao, sagamoyo.(uk 5)

Sudi anaelewa kuwa uongozi wa Majoka haufai. Anawaeleza Boza na Kombe umuhimu wa kuandika historia ya Sagamoyo upya. Kinyago anachokichonga Sudi ni cha shujaa halisi wa Sagamoyo, anaelewa kuwa Tunu ndiye anapaswa kuwa kiongozi halisi.

Tuni ni mzalendo katika taifa lake. Anasema kuwa jukumu lake ni kulinda uhai, haki na uhuru. Amajitolea kwa vyovyote  vile kutetea haki Sagamoyo .Wamekula kiapo kutetea haki Sagamoyo hata kama ni kwa pumzi zao za mwisho baada ya mafanikio. (iuk18). Akiwa mwanafunzi katika chuo kikuu walipambana kama viongozi wa chama cha wanafunzi chuoni hadi kuleta mafanikio.

Tunu ni mzalendo Sagamoyo, anawahutubiawananchi na kuwaarifu hali ilivyo Sagamoyo.Pesa za kusafisha soko zimefujwa,soko limefungwa badala ya kusafishwa na haki za wauzaji kukiukwa. Wamejitolea kutolegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.

Tunu anamkabili Majoka kwa uovu wake. Anamwambia wazi kuwa atalipa kila tone la damu alilomwaga Sagamoyo, yeye na watu wake. (uk 43)

Tunu anatetea maslahi ya wanyonge, anamwambia Majoka kuwa Wanasagamoyo wana haki ya kuishi, anamwambia ugatuzi si unyakuzi na kumkashifu kwa kubomoa vioski katika soko la Chapakazi.(uk 45)

Tunu anamkashifu mamapima kwa kuuza pombe haramu kwa vile ni kinyume cha sheria. Anatetea katiba ya nchi  inayofafanua sheria zinazohusiana na uuzaji na unywaji wa pombe.

Tunu anajitolea kuwatumikia wanasagamoyo. Yeye ni mtu wa vitendo na wala si vishindo. Anaita mkutano ili soko lifunguliwe na kuapa kutoondoka hadi soko litakapofunguliwa. Tunu amejitolea kuikomboa Sagamoyo ili kuleta mabadiliko, anakiri kuwa mambo hayatapoa, kumewaka moto na kutateketea.(uk 55)



3) NAFASI YA MWANAMKE.
Sudi anapochonga kinyago cha shujaa mwanamke, Kenga anamwambia Sagamoyo haijawahi kuwa na shujaa mwanamke. Katika historia ya Sagamoyo wanawake wametengwa katika uongozi.(uk 10).
Kenga anasema kinyago hicho hakitanunuliwa na afadhali achonge kinyago cha Ngao.

Wanawake wamesawiriwa kuwa hawara, Sudi anapokataa kuchonga jinyago, Kenga anamwambia kuwa amelishwa kiapo na hawara wake.(uk12)

Wanawake hutumiwa kama pambo katika jamii ya Sagamoyo. Majoka anamwambia Ashua kuwa, urembo wake hauna mfanowe.

        "...nikufanishe na nini? urembo wako hauna mfanowe Ashua" (uk 20)

Majoka anamshauri Ashua atumie urembo wake kwa kuwa ni wa muda.(uk 25)

Husda anakiri kuwa mwanamke ni pambo mbele ya mwanamme.(uk67)

Wanawame wamesawiriwa kuwa wenye maringo. Majoka anadai kuwa Ashua alikataa kazi ya ualimu kwa sababu ya maringo. (uk25)

Wanawake wamadharauliwa. Majoka anawadharau Ashua na Husda kwa kusema wanawake ni wanawake tu, si kitu mbele yake. (uk 26)

Adui wa mwanamke ni mwanamke. Husda anamwita Ashua mdaku, kimada wa kuwinda wanaume wa watu. Hali halisi ni kuwa, Ashua hana nia hii.

Majoka anamweleza Sudi kuwa mkewe Ashua hajui maana ya ndoa. Anasema kazi yake ni kuzururasurura .wanawake hulaumiwa.

Mwanamke amedharauliwa, mvamizi anamkanya Tunu aache kunyemelea wanaume wa watu.

Ngurumo anamdharau Tunu kwa kuwa mwanamke. Anaposema soko lifunguliwe, Ngurumo anamdharau na kumuuliza yeye ni nani Sagamoyo, wanawake hawatambuliwi.

Mwanamke katika jamii ya Sagamoyo ni kuolewa na kumtumikia mwanamme. Wimbo wa Ngurumo kwa Tunu unamshauri aolewe, kwa kuwa ana elimu asije akazeekea nyumbani kwao.

Wanawake wamechukuliwa kuwa dhaifu kwamba hawawezi kuongoza. Majoka anasema hawezi kuaibishwa na mwanamke.(uk 90)

Hata hivyo, wanawake ni wasomi,Ashua ana shahada ya ualimu.

Wanawake wamajipigania kujikomboa. Tunu anakataa kuozwa kwa Ngao Junior na kujitetea kuwa anaweza kusubiri aolewe na mume ampendaye.(uk42)

Mamake Tunu anajifunga kibwebwe baada ya kifo cha babake ili Majoka agharamie masomo ya Tunu.

Wanawake ni wanamapinduzi na viongozi bora.Tunu anaongoza mapinduzi ili kuleta haki Sagamoyo.

4) MIGOMO/MAANDAMANO.
Wauguzi Sagamoyo wanaandamana.

Walimu Sagamoyo wanagoma wakiwa likizoni.

Kiwandani Majoka and Majoka company anapofanya kazi siti, watu wanagoma. Vijana watano wanauliwa..

Wachuuzi sokoni wanaandamana, wengine wanaumizwa. Wanaandamana kwa sababu ya soko kufungwa. Wanaume Sagamoyo ni kukimbizana na waandamanaji.

Waandamanaji huandamana kila siku, kuna picha za waandamanaji gazetini kila siku.

Habari gazetini zinaonyesha kuwa Tunu ameongoza maandamano na anaandamana na wanaojiita wanaharakati. (uk 32)

Tunu anawahutubia wanahabari na kusema kuwa pesa za kusafisha soko zimefujwa, soko kufungwa badala ya kusafishwa. (uk 33)

Kenga anamshauri Majoka ayapuuze maandamabo yanayoendelea. (uk 34)

Kuna habari kwenye mtandao wa mijamii kuhusu maandamano. Watu wengi wanaandamana sokoni wakiongozwa na Sudi. Maandamano yanazidi kuharibia sherehe ya uhuru.







5) MATUMIZI MABAYA YA VYOMBO VYA DORA.

Majoka anatunia polisi kuwatawanya waandamanaji na kuwaumiza wapinzani wake, Tunu anaumizwa mguu.

Runinga ya mzalendo haina maisha Sagamoyo kwa sababu ya kupeperusha habari za maandamano. Majoka anaamua kufunga vituo vya habari na kibakie tu kituo kimoja.

Kenga anamshauri Majoka waichukulie hatua runinga ya mzalendo kwa kuwa haipendi yeye.

Majoka anatumia vyombo vya habari kuimba nyimbo za kizalendo ili kumsifu yeye.

Vyombo vya habari hueneza propaganda, kuna habari katika vyombo vya habari kuwa Tunu hawezi kupigania haki za Wanasagamoyo kwa kuwa amelemazwa mguu.

6)ASASI YA NDOA

a)NDOA KATI NYA ASHUA NA SUDI.

Ni ndoa yenye mapenzi yanayoegemea upande mmoja. Sudi anampenda Ashua kwa dhati, anajitahidi kwa udi na uvumba ili kumkidhi Ashua. Kila kitu anachokipata humletea.

Sudi ni mwaminifu katika ndoa yake, hajamwenda Ashua kinyume hata Ashua anapotiwa ndani na Majoka.

Aidha, ndoa hii imejengwa katika misingi ya kutoaminiana. Ashua anamshuku mumewe kuwa ana mipango ya kimapenzi na Tunu.

Ashua amechoshwa na Sudi na anaswema kuwa ni afadhali alipo jelani. Anadai kuwa, mawazo ya Sudi,hisia zake, nafsi yake ma kila kitu chake kimesombwa na Tunu.

Ashua ametawalwa na tamaa ya mali na kumwambia Sudi kuwa amechoka kupendwa kimaskini, anabadilika akiwa ndani kwa Majoka, awali alimpenda mumewe kwa dhati lakini baadaye anaomba talaka. Anafurikwa na tamaa na ubinafsi.




b) NDOA KATI YA MAJOKA NA HUSDA.

Ni ndoa ambayo imejaa lawama, Majoka anamlaumu Husda kuwa hampendi bali aliolewa na mali yake.( uk 75)

Hakuna mapenzi ya dhati katika ndoa hii. Majoka hampendi Husda. Alimoa ili kutimiza wajibu wake katika jamii na kama kiongozi, alipaswa kuoa. Alilia usiku huo baada ya kumwoa Husda lakini moyo na nafsi yake viko kwa Ashua. (uk75)

Majoka anampenda Ashua zaidi ya kumpenda hata anaweza kumfia. Anapanga njama ili kumpata. Majoka anakiri kuwa Ashua anamuua moyoni kwa penzi. Anamkondesha na kumkosesha raha kwa kumkataa. Ashua kumkimbia Majoka alimwachia Majoka  aibu na penzi lake kwa Ashua linamsongoa. (uk 76).

Asasi ya ndoa imo hatarini kwa kutawaliwa ma tamaa ya mali. Baadhi ya wanaume huoa ili kutimiza matakwa yao na wanawake huolewa kwa sababu ya tamaa ya mali na ubinafsi.

Wanaume wanapaswa kujidadisi na wakae na wake zao kwa heshima. Wanawake nao wanapaswa kujirudi vinginevyo asasi ya ndoa imo hatarini. (uk 77)
Uaminifu na mapenzi ya kweli ni kigezo muhimu ili ndoa idumu.

7) ULEVI NA ATHARI ZAKE.

Mangweni kwa mamapima shughuli za ulevi zimeshika kani.

Ngurumo ni mlevi kupindukia, anajulikana Sagamoyo kwa uraibu wake wa vileo. Anajunywa pombe zaidi ili kusherehekea sherehe za uhuru.

Vijana ni walevi kwa mamapima hadi wanasimama kwa taabu.

Ulevi umepotosha baadhi ya vijana, Ngurumo alisoma darasa moja na Tunu lakini ni mlevi kupindukia, hajitambui.

Kwa mamapima kila mtu hupewa vileo kwa raha zake.

Ulevi umemfumba Ngurumo hadi haoni athari za soko kufungwa, yeye anadai kuwa yuko sawa na hataki soko lifunguliwe. (uk60)

Mamapima hatambui hatari za ulevi, anaona kulewa ni raha, anawaambia Tunu na Sudi wajipe raha kwa kulewa.

Mtu mmoja ni hoi kutokana na ulevi, anaanguka chini na kuanza kugaragara.

Tunu anasema kuwa juzi waliwazika watu kutokana na pombe na wengine kugeuka vipofu kwa sababu ya pombe.

8) VIFO/MAUAJI.

Vijana watano wanauliwa watu wanapoandamana katika kampuni ya Majoka.

Watu huuliwa Sagamoyo.

     "Natumai hakuna aliyeuliwa, sitaki kujipaka matope tena" (uk 31)

Kifo cha Jabali kilipangwa katika ajali kwa kuwa mpinzani wa majoka hata chama chake cha Mwenge kikamfuata ahera.

Tunu anamwambia Majoka kuwa yeye na wenzake ni wauaji. (uk43)

Viongozi humwaga damu Sagamoyo. Tunu anamwambia Majoka kuwa atalipa kila tone la damu lililomwagwa Sagamoyo.

Babake Tinu anakufa katika Majoka and Majoka company. Marara na watu wake walimtemdea ukatili.

Hashima anasema damu nyingi imemwagika Sagamoyo hadi ardhi imeingia najisi.

Mashujaa wengine walienda jongomeo kwa kuleta uhuru Sagamoyo.

Ngurumo ananyongwa na chatu akitoka Mangweni.

Majoka anapanga kutekeleza mauaji kwa kumwondoa chatu mmoja ili pawe na usalama Sagamoyo. Kuomdoa chatu ni kuua Sudi au Tunu.

Kifo cha Ngao junior kinatokea, anapatikana katika uwanja wa ndege akiwa na sumu ya nyoka.

Majoka anasema kuwa ziwa kubwa limefurika damu furifuri kumaanisha vifo vya watu wengi vimetokea Sagamoyo. Watu wanalilia damu ya Majoka, wanataka kumuua.(uk 79)



9) UFISADI.

Serikali ya Majoka ina ufisadi, inampa mamapima kibali cha kuuza pombe haramu.

Mamapima ni fisadi, anawapunja walevi.

Majoka anatumia pesa za umma visivyo kugharamia njama ili kuzima uchunguzi wa Tunu kuhusu ajali ya Jabali.

Viongozi Sagamoyo ni fisadi, wanaitisha kitu kidogo kutoka kwa wananchi. Wakati mwingine viongozi hudai kitu kikubwa au kitu chote. (uk 3)

Viongozi hutumia mali ya umma visivyo kufadhili miradi isiyo muhimu, kufadhili mradi wa muchonga vinyago ni kufisidi wananchi maana watalipia mradi huo.

Majoka anafisidi wananchi kwa kufunga soko ili ajenge hoteli ya kifahari. Soko ni chafu ilihali wananchi wanalipa kodi ya kusafisha soko. Majoka anadai kuwa ana mradi muhimu wa mushughulikia kuliko kusafisha soko.

Majoka ni fisadi, alikuwa na mpango wa kumpa Ashua kazi ya ualimu katika Majoka and Majoka academy kwa njia isiyo halali.

10) USALITI.
Majoka anawasaliti wanasagamoyo, watu wote wanamhukumu kwa kuwasaliti.

Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo badala ya kulinda usalama wao akiwa kiongozi wao.

Kingi anamsaliti Majoka wakati wa mwisho, anampinga amri yake kuwapiga watu risasi, siku zote alimtii Majoka.

Majoka anawasaliti wanasagamoyo kwa kuwafungia soko, anapaswa kulisafisha badala ya kulifunga.

Majoka anawasaliti wanasagamoyo kwa kupanga mauaji badala ya kulinda na kutetea haki zao.

Ashua anamsaliti Sudi kwa kuomba talaka licha ya kuwa sudi anampenda kwa dhati.

Boza na Kombe wanawasaliti wanamapinduzoi kwa kuunga mkono uongozi mbaya wa Majoka.

Majoka anamsaliti Husda kwa kukiri kuwa hampendi licha ya kuwa mkewe.

11) UTABAKA.

Jamii ya Sagamoyo imegawika katika matabaka mawili ;tabaka la watawala na tabaka la watawalwa. Watawala wanaishi maisha ya kifahari huku watawalwa wanaishi maisha ya uchochole.

a.   watawala/walalahai.

Viongozi wana madaktari wao wa kuwahudumia, Majoka anapozirai, daktari wake anaitwa.

Watawala wana shule za kifahari, Majoka and Majoka academy ni shule ya kifahari.

Watoto wa viongozi huishi ng`ambo palipo na maisha bora. Ngao Junior yuko ng`ambo.

Watawala wanaishi maisha ya starehe,
           Mzee Kenga ana gari la kifahari na walinzi,
           Majoka anasema apikiwe kuku kwa chapati
           Majoka ana hoteli la kifahari

Watawala wamejichimbia visima, Majoka anafungulia biashara ya ukataji miti huku wanasagamoyo wakiteseka kwa kiangazi.

Ofisini mwa Majoka anakalia kiti cha kifahari, kando yake kumepangwa medhali kadhaa, anaishi maisha ya kifahari.

               b)Watawalwa/wachochole.

Soko la Chapakazi ni la wachochole.

Wachochole wana njaa, watoto wa Sudi wanalia njaa, Sudi anakula embe bovu.

Maskini wanateseka, mvua isiponyesha hata maji ya kunywa wayatoa ng`ambo.

Wauguzi wanagoma kwa sababu ya mishahara duni huku viongozi wakiwa na madaktari wa kuwahudumia.



12) UNYANYASAJI

Wanasagamoyo wananyanyaswa. Kilicho chao kinachukuliwa na wanatishwa.

Wananchi wanatumikizwa, Sudi wanaambiwa wachonge vinyago ili kufaidi viongozi.

Wanasagamoyo wananyanyaswa, keki ya uhuru inaliwa kwingineko na wanaletewa makombo.

Wananchi wanafungiwa soko ambalo ni tegemeo lao. Hawana mahali pengine pa kuuzia bidhaa zao.

Sagamoyo watu wananyanyaswa kwa kulazimishwa kulipa kitu kidogo wakati mwingine kitu kikubwa au kitu chote.

Ashua ananyanyaswa kwa kutiwa ndani bila kosa.

13) TAMAA.

Majoka ana tamaa ya uongozi, hataki kuondoka mamlakani. Anafanya kila awezalo kuondoa wapinzani wake.

Anataka kumtambulisha Ngao Junior rasmi kuwa mrithi wake kwenye siasa.
Majoka anadai kuwa hata asipopigigwa kuta moja atashinda. Ana tamaa ya uongozi.

Majoka ana tamaa ya mali, ananyakua uwanja wa soko ili kujenga hoteli ya kifahari.

Majoka anawafisidi wananchi ili kujilimbikizia mali kwa sababu nya tamaa

Mamapima ana tamaa ya mali, anawapunja walevi.

Husda ana tamaa ya mali, anaolewa na Majoka kwa sababu ya mali yake.

Tamaa inamtawala Ashua hadi anaomba talaka. Anadai amachoka kupendwa kimaskini kwa kuongozwa na tamaa ya mali.





14) UCHAFUZI WA MAZINGIRA.

Kuna maji chafu ambayo yametabakaa mitaroni Sagamoyo. Povu jeupe limechacha

Soko la Sagamoyo limegeuka uwanja wa kumwaga jemikali na taka.

Uchafuzi wa mazingira unaatharisha maisha ya wanasagamoyo. Sudi anakiri kuwa nusra wafe kwa sababu ya mazingira chafu.

           "...Mungu anatupenda, vinginevyo tusingekuwa hai."

Sagamoyo hakukaliki kwa sababu ya uvundo kila mahali.

      MBINU ANAZOTUMIA MAJOKA KUONGOZA SAGAMOYO

Uvumi. Watu wa Majoka wanaeneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.

Ahadi za uongo. Madai ya Majoka kuwa atatoa chakula kwa wasiojiweza si ya kweli.
Kenga mshauri wa Majoka anawashawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao ili apate malipo mazuri na maisha yake kubadilika. Kuwa jina lake litashamiri na apate tuzo nyingi zaidi ya hayo apate likizo ya mwezi mzima ughaibuni. Ahadi hizi zote ni za uongo.

Zawadi. Kenga anawaletea Sudi, Boza na Kombe zawadi ya keki kuwafumba ili wamuunge mkono Majoka.

Vitisho. Wanasagamoyo wanatishwa kwa kurushiwawa vijikaratasi wahame.
Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo. Matokeo yake ni watu kuhofia usalama wao.
Majoka anamtishia Chopi kuwa aramwaga unga wake kwa kutomamrisha polisi kutawanya waandamanaji.

Mapendeleo. Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika Majoka and Majoka academy akakataa, sasa angekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule za kifahari, viongozi hupendelea wengine kutumia njia sisizo halali.
Majoka alimpa Tunu kazi kiwandani akakataa.

Jela. Viongozi hufungia wanaowapinga jela. Ashua anatiwa ndani, kuna washukiwa wengi ndani.

Polisi. Majoka anatumia polisi kutawanya waandamanahi wanaodai haki zao.
Viongozi hutumia nguvu. Majoka anadai wafadhili wa wapinzani lazima wavunje kambi zao Sagamoyo, kuwa Sagamoyo yajiweza.
Anapanga kumkomesha Tunu dhidi ya kuongoza maandamano kutumia nguvu zake kiutawala.
Kenga anamshauri Majoka atangaze maandamano ni haramu kwa mutumia nguvu kisha maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.

Ulaghai. Majoka anapanga kuongoza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi.

Kudhibiti vyombo vya dora. Majoka anapanga kufunga vituo vya runinga sagamoyo ili abakie na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.

Wavamizi. Majoka anatumia wavamizi, Tunu anaumizwa mfupa wa muundi, Siti ana majeraha kutokana na uvamizi.

Ulinzi mkali. Majoka na watu wake wana ulinzi mkali. Kenga ana walinzi, Majoka analindwa na maafisa wa polisi.
Tunu na watu wake nanafurushwa wanapojaribu kukaribia soko la Chapakazi.

Kufuta kazi wasiomuunga. Majoka anamfuta kazi kingi kwa kutomtii kupiga watu risasi sokoni Chapakazi.

                                  MATAKWA  YA WANASAGAMOYO.
  • Soko ambalo ni tegemeo lao linafungwa. Waataka soko lao lifunguliwe na kujengwa upya pia lisafishwe.

  • Hawana usalama, askari wanatumiwa kuwatawanya na kuwatishia. Wanaishi kwa hofu.

  • Hawana uhuru wa kutangamano kwani viongozi wao wahahofia maanamano.

  • Haki zao zimekiukwa. Mauaji yanapangwa kwa njama za kuwaangamiza.

  • Wanataka kujengewa hospitali, barabara na vyoo.Waletewe nguvu za umeme.

  • Wanataka wapate elimu Sagamoyo na ajira kwa vijana.

  • Wanasagamoyo wana njaa

  • Walimu na wauguzi Sagamoyo wana mishahara duni.

  • Kuna vilio Sagamoyo, mauaji yanapangwa. Wanasagamoyo wanataka mauaji haya yakome na haki kutendwa.

  • Wanasagamoyo wananyanyaswa na viongozi, bei ya chakula inapandishwa ilihali wengi wa wananchi ni maskini.

  • Mazingira Sagamoyo ni chafu hadi kuhatarisha maisha yao. Wanataka soko kusafishwa.


                                           WAHUSIKA
MAJOKA.
Ni kiongozi wa jimbo la Sagamoyo.

Ni katili.
Anaamuru Tunu auliwe, anavunjwa mfupa wa muundi.
Anamwambia kingi awapige watu risasi katika soko la Chapakazi.

Ni mkware.
Anapanga njama ya kumpata Ashua, anamtaka kimapenzi licha ya kuwa na mke na mtoto.
Ashua anapofika ofisini mwake, anataka kumkumbatia na kumbusu.

Mwenye hasira.
Anakasirika Ashua anapokataa asimkumbatie na kusema kuwa hasira yake imeanza kufunganya virago. (uk 20)

Mwenye majisifu.
Majoka anataka sifa, anauirahi sana Ashua anapomwita Ngao jina lake la ujana.
Anajisifu kuwa yeye pia anajua kuzaa na wala si kuzaa tu bali kuzaa na kulea. (uk22)

Mwenye dharau.
Anawadharau watoto wa Ashua  kwa kuwaita vichekechea. (uk22)
Anamdharau Sudi mumewe Ashua kwa kumwita zebe.
Anamdharau Tunu kuwa  ni daktari na hana kazi ya maana.
Tunu anapokataa poza ya Ngao Junior anamdharau kuwa msichana mdogo hata ubwabwa wa shingo haujamtoka.

Mpenda anasa.
Majoka anamwambia Ashua asilie bali aseme na ampendaye, astarehe kwenye kifua cha shujaa wake.(uk22)
Anataka kumpa Ashua huba ,anamwita muhibu wake.(uk21)

Mnafiki.
Anamwambia Ashua kuwa,

    "...haja zako ni haja zangu, shida zako ni shida zangu na kiu yako ni kiu yangu."

 Nia yake ni kumteka Ashua kimapenzi, hana moyo wa kujali.

Anadai kuwa hapendi rafu Ashua wanapopigana na Husda ofisini huku ni yeye huzua rafu Sagamoyo kwa kupanga mauaji hadi watu kuandamana.

Mpyoro.
Anawatusi wanasagamoyo kuwa wajinga katika soko la Chapakazi.
Anamwita Sudi mumewe Ashua Zebe.
    "...uliona nini kwa huyo zebe wako."  (uk24)

Mwenye kiburi.
Anajiita mwana wa shujaa kwamba ana akili ndipo kuwa mwana wa shujaa. Anasema kuwa aliitwa Ngao kwa kuwa na sifa.

Anajifananisha ma Samsoni Myaudi na shujaa Lyona wa Waswahili.
Anadai kuwa Ashua amembandika jina la kumkwaza kwa kumwita mzee.

Ni katili.
Anamfungia  Ashua licha ya kumwomba msamaha kuwa ananyonyesha.
Anapanga njama za mauaji bila kujali haki za raia.
Anawafungia wanasagamoyo soko ambalo ni tegemeo lao biala kujali.

Ni dikteta.
Majoka hutoa amri, polisi watawanye waandamanaji.
Kenga anasubiri amri ya Majoka ili amkomeshe Tunu kufanya uchunguzi kuhusu kifo cha Jabali.

         UMUHIMU WA MAJOKA.
Ametumika kuonyesha jinsi ambavyo viongozi hutumia mamlaka yao vibaya kunyakua ardhi ya umma, kuvunja sheria za katiba, kudhibithi vyombo vya dora, kupanga njama za mauaji, kunyanyasa maskini na kudhulumu wnawake kimapenzi.

Ni kielelezo cha viongozi katika mataifa yanayoendelea na shida zinazoyakumba kutokana na uongozi mbaya.


                                                             TUNU.
Ni mwanamke Sagamoyo ambaye anapinga maovu ya Majoka, rafikiye Sudi na mtoto wa Hashima.

Ni mwanamapinduzi.
Anaongoza maandamano Sagamoyo.
Anahutubia wanahabari kuhusu hali halisi Sagamoyo.
Anakiri kutolegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe.

Ni msomi.
Ana shahada ya sheria kutoka chuo kikuu.

Ni mtetezi wa haki .
Anapanga kuleta wachunguzi kutoka nje ili kuchunguza kuhusu kifo cha Jabali .
Anamwambia Majoka wazi kuwa kila mtu Sagamoyo ana haki nya kuishi.

Mwenye msimamo dhabiti.
Anakataa wazo la Majoka kumwoza kwa Ngao Junior.
Licha ya kuumizwa mguu, halegezi kamba kuwapigania wanasagamoyo.

Ni jasiri.
Haogopi yeyote, anataka kukutana na viongozi katili ili awakashifu.
Anamwambia Majoka wazi kuwa hawezi kuolewa na mhuni, kwanba wanakula watu kwa jina la ugatuzi. (uk42)

Ni mzalendo.
Tunu anapigania haki za Wanasagamoyo, anamwambia Majoka kuwa wanasagamoyo wana haki ya kuishi na kuwa ugatuzi si unyakuzi.

Mdadisi.
Anamdadisi mamake ili ajue maana ya ndoto ya Mzee Marara kumfukuza ili amnyanganye mkufu wake wa dhahabu.
Anapanga kuchunguza ajali iliyosababisha kifo cha Tunu.

Mwajibikaji.
Tunu amawajibika, anaelewa athari ya pombe, na kukataa pombe anayopewa kwa mamapima.

Mwenye usawa
Anapigania usalama wa kila mtu Sagamoyo, habagui yeyote. Hambagui mamapima anapomwomba msamaha.

                                           UMUHIMU WAKE.

Tunu ametumika kuonyesha kuwa kuna wazalendo katika jamii ambao wamejitolea kupinga uongozi mbaya ili kuleta haki na usawa katika jamii.

Mwandishi amemtumia mhusika Tunu kuonyesha kuwa licha ya changamoto zinazomkumba mtoto wa kike, bado ana nafasi muhimu katika ujenzi wa jamii mpya, wanawake ni muhimu katika uongozi ili kuleta maendeleo.

                                                 ASHUA
Ni mkewe Sudi, mamake Pendo na Pili

Ni mwenye msimamo thabiti.
Licha ya kushawishiwa kimapenzi na Majoka, hakubaliani na kauli  yake. Anashikilia msimamo wake kuwa ana mume na hataki kuvunja ndoa yake, anakataa huba kutoka kwa Majoka.

Ni jasiri.
Anamkabili Majoka kwa kupasa sauti ofisini mwake, haogopi. Anamwambia kwa ujasiri kuwa anefika kwake kuomba msaada.

Ni mnyenyekevu.
Ananyenyekea mbele ya Majoka ofisini mwake na kumwomba msamaha, anamwomba Majoka amkanye Husda asimtusi.

Ni mwenye heshima.
Anakiri kuwa anamheshimu Majoka.

Ni mwaminifu.
Ashua ni mwaminifu katika ndoa yake. Anakataa kufanya mapenzi na Majoka kwa kuhofia talaka yake.
Anathamini ndoia yake, anakataa pendekezo la Majoka kwa madai kuwa yeye ni mke wa mtu.

Ni msomi.
Ashua amesoma na ana shahada ya ualimu.

Amezinduka.
Anadai kuwa kampuni ya Majoka ni ya wahuni. Anaelewa kuwa wanasagamoyo wamenyanyaswa hivyo kujiunga na wanamapinduzi kupigania haki.

Ni mkali.
Ashua anamkabili Husda kwa ukali ofisini mwa Majoka.

Ni mwenye tamaa.
Ashua baada ya kutiwa ndani kwa Majoka, tamaa inamjaa. Anamwambia Sudi kuwa amechoka kupendwa kimaskini, tamaa ya mali inamtawala.

Asiye na subira.
Subira inamhama Ashua. Hawezi kusubiri hadi Sudi awe na uwezo wa kumtunza.


                                  UMUHIMU WAKE.

Ametumika kuwakilisha wanawake ambao wanathamini na kuzienzi ndoa zao, wanawake waaminifu lakini kwa sabavu ya kutawaliwa na tamaa ya mali na ubinafsi, huaribu ndoa zao.

                                       SUDI.

Ni mumewe Ashua, fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo ambaye anashirikiana na Tunu kupinga maovu ya Majoka.

Ni mzalendo.
Kwake taarifa za Majoka hazimfai, za kutangaza mashujaa waliopigania uhuru Sagamoyo.
Haoni maana ya uhuru huo hivyo kutomuunga mkono.
Ana jukumu la kulinda uhai, kulinda haki na kulinda uhuru.
Wanaitaji kuandika historia ya Sagamoyo upya.

Ni mwenye bidii.
Anafanya kazi ya kuchonga vinyago kwa bidii.

Ni mwenye msimamo thabiti.
Licha ya kushawishiwa na kuhaidiwa mengi na Kenga ili achonge kinyago cha Ngao, anakataa na kushikilia msimamo wake.

Ni jasiri.
Anamwambia Kenga kwa ujasiri wamemulikwa mbali. (uk12).
Haogopi kuchonga kinyago cha mwanamke.

Amezinduka.
Hali keki ya uhuru wanayoletewa na Kenga kwa madai kuwa ni makombo. Anaelewa kuwa viongozi wanawanyanyasa.

Ni mwajibikaji.
Sudi amewajibika, anajitahidi kwa udi na uvumba ili kumkidhi Ashua. Kila kitu anachokipata humletea Ashua.

Ni mwenye mapenzi ya dhati .
Sudi anampenda mkewe kwa dhati. Hufanya kila kitu ili kumkidhi.

Ni mwaminifu.
Sudi ni mwaminifu katika ndoa yake. Anampenda Ashua na anajelea kumpa talaka Ashua anapoiomba.

Ni msomi.
Sudi ana shahada, walisoma shule moja na Tunu.

                    UMUHIMU WAKE.

Mwandishi amemtumia mhusika Sudi kuonyesha kuwa kuna, wazalendo katika jamii ambao wamejitolea kuoigania haki ili kujenga janii mpya, watu ambao wamejitolea kupinga uongozi mbaya.

                                           KENGA.

Ni mshauri mkuu wa Majoka.

Ni mshauri mbaya.
Anamshauri Majoka visivyo. Anamwambia atangaze kuwa maandamano ni haramu kisha aamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.

Ni kikaragosi.
Anamuunga Majoka mkono hata kwa mambo yasiyofaa nia yake ikiwa ni kujinufaisha kutokana na uongozi wake.

Ni fisadi.
Yeye na  Majoka wanadai kitu kidogo kutoka kwa wanasagamoyo.
Baada ya soko kufungwa, Majoka anamwambia kuwa kipande chake cha ardhi kipo. Anakipata kwa njia isiyo halali.

Ni mwoga.
Kenga abahofia maandamano yanayoendelea na kumshauri Majoka asiyapuuze

Ni mwenye matumaini.
Hafi moyo, anasema atarudi tena na tena ili kusema na Sudi ili achonge kinyago.

                                  UMUHIMU WAKE.
Kenga anawakilisha washauri wabaya wa viongozi katika jamii, watu ambao nia yao ni kujinufaisha wenyewe bila kujali maslahi ya wanyonge.
Washauri ambao ni katili na hata hupanga njama za mauaji ili kuendelea jufaidi kutoka kwa viongozi.

                                                NGURUMO.

Ni kijana mpenda anasa, mfuasi wa Majoka.

Ni mlevi.
Ngurumo ni mlevi kupindukia,anajulikana Sagamoyo kutokana na ulevi wake.

Ni msaliti.
Anasaliti wanamapinduzi kwa madai kuwa Sagamoyo ni pazuri tangu soko kufungwa.
Anasaliti katiba ya nchi yake kwa kunywa pombe haramu, kinyume na sheria.

Ni mpenda anasa.
Ngurumo anapenda anasa, kwake kulewa ni starehe.

Mwenye taasubi ya kiume.
Anamdharau Tunu kwa kuwa mwanamke, anadai kuwa yeye si kitu Sagamoyo.
Anamwimbia wimbo wenye ujumbe kuwa aolewe ili asije akazeekea kwao

Ni kikaragosi.
Yeye ni  mfuasi wa Majoka, anaunga uongozi wake mkono licha ya kuwa haufai.

                              UMUHIMI WAKE.
Mwandishi amemtumia Ngurumo kuonyesha kuwa kuna vijana ambao wamepotoshwa na anasa katika jamii na kukosa mwelekeo. Ngurumo ni kijana lakini mlevi kupindukia.

                                             BOZA

Ni fundi wa kuchonga vinyago Sagamoyo, mumewe Asiya (mamapima)

Ni mwenye hasira.
Anamwambia Sudi kwa hasira kuwa embe lake linanuka fee. (uk1)

Ni kikaragosi.
Anatetea viongozi kuwa ni jukumu lao kusanya kodi, kuwa huku ndilo kujenga nchi na kujitegemea. (uk3)

Anafurahia wimbo wa uzalendo unaosifia uongozi wa Majoka ilhali hali ni tofauti  Sagamoyo kulingana na maudhui katika wimbo huo.
Anamuunga Majoka mkono ili afaidi.

Mwenye majisifu.
Anajisifu kuwa keki ya uhuru imeokwa na mke wake mwenyewe.

Ni msaliti.
Anawasaliti wanamapinduzi kwa kuunga mkono uongozi Mbaya wa Majoka mkono.

                                    UMUHIMU WAKE.
Boza ametumika kuonyesha watu ambao hawajazinduka katika jamii, wanaotumikizwa na viongozi na kufumbwa kwa mambo madogomadogo ili waendelee kuunga uongozi mbaya mkono.

                                                 HUSDA
Ni mkewe Majoka.

Ni mwenye tamaa ya mali.
Anaolewa na Majoka kwa sababu ya pesa na wala si mapenzi halisi

Ni mkali.
Anasema atamuua  mtu anapompata Ashua na Majoka.

Mpyoro.
Anamtusi Ashua na kumwita kidudumtu na mdaku.

Mbinafsi.
Husda ana ubinafsi, anaolewa sababu ya mali ili kujinufaisha.

                                            UMUHIMU WAKE.

Husda ni kielelezo cha wanawake wanaoongozwa na tamaa ya mali hata hata katika ndoa, wanawake wanaoolewa kwa sababu ya mali na wala si mapenzi ya kweli.


                                          MAMAPIMA
Huyu ni Asiya mkewe poza anayeuza pombe Sagamoyo.

Ni laghai.
Anawapunja walevi.

Ni mwenye tamaa ya pesa.
Anawapunja walevi kwa sababu ya tamaa ya pesa.

Amekiuka sheria.
Anauza pombe haramu kinyume cha sheria.

                                         UMUHIMU WAKE.
Mamapima ametumika kuonyesha watu ambao  huongozwa na tamaa hadi kiwango cha kukiuka sheria.

                                          BABU.

Ni babuye Majoka ambaye ametokea ndotoni.

Ni mshauri mwema.
Anamshauri Majoka abadili mienendo yake na asikie vilio vya wanasagamoyo na aone maovu aliyoyatenda. (uk 83)

Ni mwenye hekima.
Anathibitisha kauli kuwa maisha ni mabadiliko na maovu yana mwisho.
Anamwonya Majoka dhidi ya kuishi kwa kutojali, kuwa hasara itamwandama akataliwe na watu asiwe mtu tena.

Anampa Majoka wosia kuwa binadami ni mavumbi na atarejea mavumbini kwa hivyo asihishi kwa kuwanyanyasa wengine wala asiongozwe na tamaa maishani.
Anamshauri kuwa mkwea ngazi huteremka. (uk84).
 Anamwambia Majoka atende wema daima na ataishi maisha mema iwapo atakufa, atajiandikia tarijama njema huko ahera.

                            UMUHIMU WA BABU.

Mwandishi amemtumia kuonya umma kuwa si vyema kutendea wengine mabaya, maana maovu yana mwisho. Wanadamu wasiishi kwa kuwanyanyasa wengine wala kuongozwa na tamaa bali watende mema daima.

                                  MBINU ZA UANDISHI.

         KINAYA.

Habari zinazotolewa na mjumbe katika rununu ni za kinaya, kuwa wanasagamoyo wasirudishe maendeleo nyuma bali wafurahie ufanisi ambao umepatikana katika kipindi cha miaka tisini baada ya uhuru.
Ujumbe huu ni kinaya kwa vile Sagamoyo hakuna maendeleo wala ufanisi. Watu wana njaa na wanakosa mambo ya kimsingi kama vile maji, elimu na matakwa mengine mengi.

Boza anadai kuwa kulipa kodi ni kujenga nchi na kujitegemea. Kauli hii ni kinaya kwa vile kodi wanayolipa wanasagamoyo haitumiki kujenga nchi kwa vyovyote vile.

Sudi anasema kuwa katika kipindi cha mwezi mzima wa uhuru wale mali walizochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa kuwa hakuna walichovuna, viongozi hujilimbikizia mali.

Boza anamwambia Sudi kuwa wanatia doa kwa kila jambo nzuri. Ni kinaya kwa vile hakuna mambo mazuri ambayo Majoka amefanya Sagamoyo. (uk5)

Wanasagamoyo kusheherekea miaka sitini ya uhuru ni kinaya kwani hakuna cha muhimu kusheherekewa, hakuna maendeleo Sagamoyo.

Boza anadai kuwa kinyago chake chapendeza na kufanana na shujaa Marara Bin Ngao, ni kinaya kwani kinyago hicho hakifanani na shujaa huyo.

Mzee Majoka kudai kuwa anamheshimu sudi ni kinaya. Majoka hana heshima kwa raia wake, nia yake ni kutaka Sudi amchongee kinyago. (uk13)

Kenga kumwambia Sudi kuwa ipo siku atamtafuta mzee Majoka ni kinaya kwani Sudi hana haja naye.

Majoka kudai kuwa takataka za soko zitaaribu sifa nzuri za jimbo la Sagamoyo ni kinaya kwa vile hakuna sifa nzuri Sagamoyo. Viongozi wanaendeleza maovu na hata kupanga mauaji.

Kauli ya Husda kuwa Ashua ni kimada wa Majoka ni kinaya kwa vile Ashua hana nia yoyote na Majoka. Amefika kwake kuomba msaada.

Ni kinaya kwa polisi Sagamoyo kutawanya waandamanaji. Polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi.

Majoka kusema kuwa Sagamoyo wanajiweza  ni kinaya. Watu wana matakwa mengi, ni maskini, wana njaa na hata kupata ufadhili kitoka nje kwa miradi isiyo muhimu.

Ni kinaya Kenga anapomwambia Majoka aache moyo wa huruma, kwa sababu Majoka hana hata chembe cha huruma. Anapanga mauaji na kunyanyasa raia.

Majoka anaposema kuwa juhudi za Tunu kuandaa migomo hazitamfikisha mahali ni kinaya kwa vile Tunu wanafanikiwa katika maandamano yao na hata kuungwa mkono na wengi.

Ni kinaya kwa Ashua kumwambia Sudi kuwa ni kosa lake kutiwa ndani. Kosa ni la Majoka na njama yake ya kutaka kuchongewa kinyago.

Ashua anasema kuwa katika jela kuna amani na amechoshwa na Sudi. Ni kinaya kwani Ashua anapata maumivu akiwa jelani.

Uvumi unaoenea kuwa Sudi na Ashua ndio wanaowinda roho ya Tunu ni kinaya kwani wote hawa ni wanamapinduzi wanaopigania haki Sagamoyo.

Madai ya Ngurumo ni kinaya kuwa tangu soko kufungwa Sagamoyo ni pazuri mno. Eti mauzo ni maradufu ilihali watu hawana mahali pa kuuzia bidhaa zao, kifungwa kwa soko kunawaangaisha raia hata zaidi.

Ngurumo kusema kuwa pombe ni starehe ni kinaya kwani watu wanaangamia kutokana na pombe, wengine kuwa vipofu.

Watu wengi wanatarajiwa kufika katika uwanja wa ikulu ya Majoka kusherehekea uhuru siku ya sherehe lakini ni kinaya kwa kuwa ni watu kumi tu ambao wanafika.




                                    JAZANDA.

Kinyago cha shujaa anachochonga Sudi kwamba shujaa huyo ni mkubwa kuliko jina lake na urembo wa shujaa huyo ni bora zaidi. Shujaa anayerejelewa hapa ni Tunu, yale ambayo anatendea Sagamoyo ni makuu kuliko jina lake, kutetea haki za wanyonge. (uk10)

Husda anamwambia Ashua kuwa hawezi kumtoa bonge kinywani hivi hivi. Bonge ni Majoka bwanake Husda kuwa Ashua hawezi kumnyanganya bwana.

Husda kumwita Majoka pwagu, pwagu ni mwizi na Majoka amewaibia wanasagamoyo; ananyakua ardhi, anaiba kodi na kuwalaghai wanasagamoyo. (uk27)

Husda anamwambia Ashua kuwa ameshindwa kufuga kuku na kanga hatamweza. Kuku ni mumewe Sudi, na Kanga ni Majoka, kwamba Ashua ameshindwa kumtunza Sudi na Majoka hampati. (uk28)

Tunu kuwekewa vidhibitimwendo ni kukomeshwa au kuwekewa vikwazo ili afe moyo kutetea haki za wanasagamoyo.

Majoka anasema kuwa hatatumia bomu kuulia mbu. Anamrejelea Tunu kuwa mbu kunaanisha hatatumia nguvu nyingi kumwangamiza. (uk35)

Majoka anasema ili kuongoza Sagamoyo ni lazima uwe na ngozi ngumu, kumaanisha ni lazima uwe mkali na mwenye nguvu.

Jukwaa kupakwa rangi kwa ajili ya sherehe ya uhuru ni kufunika uozo ulio Sagamoyo.

Majoka anaposema salamu zinamgoja Sudi kwake, salamu ni Ashua mkewe aliye ndani ya jela.

Majoka anamshauri Sudi anawe mikono iwapo anataka kula na watu wazima. Kunawa mikono ni kukubali kuchonga kinyago ndiposa Ashua mkewe aachiliwe.

Chopi anamwambia Sudi iwapo shamba limemshinda kulima aseme. Shamba anarejelea Ashua kuwa iwapo Ashua amemshinda kutunza, aseme atunziwe na Majoka.

Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza. Siafu ni wanasagamoyo ambao ni wengi kuliko Majoka na si rahisi kuwashnda. Hatimaye raia wanamshinda Majoka. (uk52)

Tunu anasema kuwa moto umewaka na utateketea wasipouzima. Moto ni harakati za mapinduzi Sagamoyo .Kuteketea nice kumng`oa Majoka mamlakani.

Hashima anamwonya Tunu asijipeleke kwenye pango la joka.Pango la joka anarejelea majoka na watu wake ambao ni kati na wauaji.

Majoka anadai lazima mtu mmoja atolewe kafara ili watu wajue kuwa kuna usalama Sagamoyo. Chatu anamrejelea Sudi au Tunu ambao ni tishio kwa uongozi wake na kuwatoa kafara ni kuua mmoja wao ili kukomesha maandamano.

Majoka anaposema yupo kwenye chombo cha safari ya jongomeo anamaanisha kuwa mwisho wake uko karibu kuondolewa mamlakani.

Kinyago cha mke mrembo shujaa anachochonga Sudi kinaashiria Tunu ambaye ni shujaa wa kweli Sagamoyo

Husda anafananishwa na chui anayeishi ndani ya ngozi ya kondoo kuashiria kuwa yeye ni mnafiki. Hana mapenzi ya kweli kwa Majoka ila aliolewa naye kwa sababu ya mali.

Jazanda ya marubani ambao hawaendesha vyombo vyao vizuri ni viongozi ambao hawaingozi kwa haki. wamejawa na ulaghai na tamaa. (uk80)

Babu anamwambia Majoka kuwa hawezi kuelewa mambo kwa vile hajapambua ngozi yake ya zamani. Majoka anapaswa kubadili mienendo yake mbaya.

Chombo anachopanda Majoka kinaenda kinyume badala ya kwenda mbele, Majoka hajafanya maendeleo Sagamoyo kwa sababu ya ufisadi na tamaa. (uk81)

Kisima kuingiwa na paka maji hayanyweki tena. Sagamoyo ni dhiki tele, hakukaliki kwa kuwa na shida nyingi; soko kufungwa, mauaji kutekelezwa na unyakuzi.

                                    SADFA.

Majoka akiwa ofisini mwake, Ashua anaingia bila kutarajiwa.

Ashua akiwa na Majoka ofisini, Husda anaingia bila kutarajiwa, Ashua anamaka na kubakia kinywa wazi.

Majoka anaposoma gazeti anaona maoni kuwa Tunu awanie uongozi Sagamoyo, hakutarajia kuyaona maoni hayo gazetini.

Chopi wanapozungumza na Majoka Mwango anafika na habari kuwa Majoka ana wageni, Tunu na Sudi ambao hakutarajia.

Majoka anapongojea Husda katika hoteli ya kifahari Sagamoyo, Kenga anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga, kuwa Tunu bado yupo, hakuvunjwa miguu, Majoka hatarajii Tunu kuwa mzima.

Ni sadfa kwa kifo cha Ngao Junior kutokea sawia na kifo cha Ngurumo.

Majoka anazirai siku kabla ya sherehe ya uhuru, anapopata habari kuhusu kifo cha Ngao Junior.

Inasadafu kuwa siku ya sherehe ndio waandamanaji wanakuwa na mkutano katika soko la chapajazi wakati ambapo wanatarajiwa juhudhuria sherehe.

                                               WIMBO.

WIMBO WA UZALENDO.
Wimbo huu unaimbwa katika kituo cha habari cha wazalendo, ni wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake kuwa;

Sagamoyo ni jimbo tukufu, wanamtukuza Ngao kuwa kiongozi shupavu.
Maudhui katika wimbo huu ni kinaya kwa vile Majoka sio kiongozi shupavu, uongozi wake una dosari. (uk5)

WIMBO WA HASHIMA.
Anaimba wimbo huu akiwa nyumbani kwake. Wimbo huu unaashiria kuwa mambo hubadilika, kila siku wasema heri yalipita jana. (uk51)

WIMBO WA MAMAPIMA.
Ni wimbo wa kishairi unaorejela Sudi na Tunu. Mamapima anawashauri wajipe raha kwa kujiunga nao katika ulevi. (uk60)

WIMBO WA NGURUMO.
Ngurumo anaimba wimbo kwa mamapima akimrejelea Tunu. Ni wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwanamke anapaswa kuolewa.

WIMBO WA UMATI.
Umati unaimba wimbo katika lango la soko la chapakazi. Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka. Wimbo huu unasifia juhudi za Tunu kuikomboa Sagamoyo na kuleta uhuru halisi.


WIMBO WA ASHUA.
Ashua anaimba kuwa soko lafunguliwa bila chopi kumaanishwa vikaragosi hawana nguvu dhidhi ya wanamapinduzi. (uk92)

                         USHAIRI.

Majoka anatunia ushairi kupitisha ujumbe wake kuwa Ashua anamuumiza Majoka moyoni kimapenzi. Kuwa anamkondesha na kumkosesha raha kwa kumkataa. Ashua kumkimbia alimwachia aibu Majoka na penzi lake kwa Ashua linamsongoa. (uk76)

Ushairi wa babu, anamshauri Majoka abadili mienendo yake, asikie vilio vya wanasagamoyo ,aone maovu  anayoyatenda, ahisi dhiki zinazowakumba wanasagamoyo.
Anamshauri kuwa maisha ni njia mbili: mema na maovu na kuwa maovu yana mwisho.

                                             NDOTO.

Tunu anaota ndoto kuwa anafukuzwa na mzee Marara akitaka mkufu wake wa dhababu.
Mzee marara kumfukuza Tunu ni ishara kumkomesha asiwe kiongozi Sagamoyo (kumnyanganya mkufu), mkufu wa dhahabu ni ishara ya uongozi. (uk53)

Majoka anasema na babu katika  ndoto. Babu anamshauri Majoka abadili mienendo yake na asikie vilio vya wanasagamoyo.
Babu anamwonya Majoka dhidi ya kuishi kwa kutojali na kumwambia Majoka atende mema.

                                  TAHARUKI.

Kombe na Boza wanaagizwa wachonge vinyago, je wanavichonga?

Majoka anampenda sana Ashua, anampata? kama hakumpata, alifanya nini?

Ashua anaomba talaka yake akiwa jela, je anapewa?

Kuna wafungwa ambao wamefungiwa, walifanya kisa gani?  je wanaachiliwa? iwapo hawakuachiliwa, hatima yao ilikuwa ipi?

Wageni wanatarajiwa Sagamoyo siku ya uhuru. Je wanafika?

Mpango wa Majoka kumsafirisha Chopi kwa kushindwa kumvunja Tunu mguu, je anasafirishwa? iwapo anasafirishwa, anachukuliwa wapi na kufanyiwa nini?

Anwani ya tamthilia, kigogo ni nani? anafanya nini na wapi?

Kuna taharuki kuhusu kifo cha Ngao Junior. Ni kipi kinasababisha kifo chake? Majoka na Husda wanafanya nini? ni nani atakuwa mrithi wa Majojka katika siasa?

Hoteli la kifahari Majoka analotaka kulijenga baada ya kufunga soko, je anafaulu kulijenga?

Majoka anaagiza Ngurumo azikwe kabla ya jua kutua, je anazikwa? watu wanasema nini kuhusu kifo chake.

                           MBINU REJESHI/KISENGERE NYUMA.

Majoka anakumbuka hadithi kuwa binadamu siku zote humwauni kuku na kumhini kunguru. (uk22)

Majoka anarejelea siku Ashua alipokataa pete yake ya uchumba kuwa hiyo ndiyo siku aliyojikosea heshima na sasa hangekuwa ombaomba.

Majoka anarejelea kisa cha kifo cha Jabali na wafuasi wake, jinsi walivyopanga njama na kumwangamiza.

Ashua anakumbuka mengi Sudi aliyomwahidi siku zao za kwanza za mapenzi.

Tukio la Mzee Marara kumfukuza Tunu ndotoni ni la zamani, la utotoni.

Hashima anakumbuka jinsi alivyoathirika na marehemu mume wake, Marara na watu wake waliwatendea ukatili.

Sudi akiwa kwa mamapima anakumbuka mashujaa waliofungwa wakati wa ukoloni. Mashujaa hao waliangaisha wakoloni na hata wengine wakaenda jongomeo. (uk59).

                             KIANGAZAMBELE.
Maoni gazetini kuwa Tunu awanie uongozi Sagamoyo, baadaye Tunu anakuwa kiongozi baada ya kumpindua Majoka.

Majoka anahofia kuwa maandamano yatatia doa sherehe za uhuru, siku ya sherehe, watu hawahudhurii.

Majoka anahofia kuwa waandamanaji watafika ofisini wammalize. Mwishowe wanammaliza wanapomtoa mamlakani.

                            TAMATHALI ZA USEMI.

METHALI.

Fuata nyuki ule asali (ukitaka kula asali kaa na nyuki) (uk7).
Methali hii imetumika kuonyesha kuwa ukitaka kupata kitu, kaa na walionacho.
Asiya na Ngurumo walimwandama Bi. Husda hadi wakapata kandarasi ya kuoka keki.

Chelewa chelewa utapata mwana si wako.
Boza, Kombe na, Sudi wasichelewe kuchonga vinyago ili wafaidi, na majina yao yajulikane nje.(uk9)

Mbio za sakafuni, huishia ukingoni.
Kenga anatumia methali hii kurejelea kuwa harakati za Tunu kuleta mabadiliko Sagamoyo hayatafanikiwa. Kauli hii ni kinaya, (uk12).

Udongo haubishani na mfinyanzi.
Wenye nguvu hawabishani na wanyonge. Boza anatumua methali hii kumwonya Sudi asibishane na Majoka anapodai kuwa keki wanayoletewa ni makombo. (uk13)

Aketiye na cha upele, haishi kujikuna.
Sudi anatumia methali hii kurejelea Kombe anapomuunga mkono na kusema mambo yamekwenda kombo Sagamoyo. (uk15)

Simba hageuki paka kwa kukatwa makucha.
Kuwa Majoka alikosa fursa ya kumwoa Ashua haimanishi hana uwezo wa kumfanyia lolote. (uk21)

Kuvuja kwa pakacha ni nafuu kwa mchukuzi.
Kuvunjika kwa ndoa ya Ashua au Ashua kutalikiwa itakuwa heri kwa Majoka ili ampate Ashua

Heri kufuga mbuzi, binadamu wana maudhi.
 Majoka anatumia methali hii Ashua anapokataa ombi lake. (uk26)

Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake.
Kenga anarejelea wafadhili wa gazeti kuwa walimtetea Tunu na habari kumhusu zimetiwa chuvi. Waandishi wa gazeti ni wafadhili wa Tunu. (uk33)

Dalili ya mvua ni mawingu.
Tunu huenda akaongoza Sagamoyo.(uk34)

Ukitaka kuwafurusha ndege, kata mti.
Kenga anamrejelea Jabali, kuwa ukitaka kuwaangamiza maadui ua kiongozi wao. Jabali alikufa na wafuasi wake kumfuata ahera. (uk35)

Udongo uwahi ungali mbichi.
Wangemkomesha Tunu kabla ya kupata umaarufu.

Asante ya punda ni mateke.
Majoka anamrejelea Tunu kwa kumpinga baada ya kugharamia masomo yake baada ya kifo cha babake.

Maji ukiyavulia nguo yakoge.
Majoka amekubali kuhukumiwa na kujibu mashtaka  kwa kutowajibika kwake na kusaliti nchi yake. (uk79)

                                  MASWALI BALAGHA.

Hiyo rununu hitulii mfukoni, yakuuma? (uk1)

Kwani umeota pua ya pili?  (uk1)

Kwani u mjamzito? (uk1)

Kwa nini washerehekee mwezi mzima? (uk5)

Eeh! viini ni nini? (uk16)

Hujayaacha hayo?

Siwezi nini? (uk21)

umenizidi kwa nini?
*mwanafunzi atoe mifano zaidi.

                                 KUCHANGANYA NDIMI.
look at the bigger future man (uk18)

Its for our good

what? (uk35)

But one stone is enough (uk36)

Live coverage. (uk38)

Over my dead body (uk45)

Ni afadjali iwe one touch (uk68)

Chopi, time is money. Humjui Asiya (uk71)
*mifano zaidi.

                                  NIDAA.

Linanuka fee! (uk1)

Enhe! (uk19)

Kisa na maana ni wewe! (uk26)

Chunga ulimi wako! (uk27)

 Na wewe! (uk27)

                                       TAKIRIRI.

Siwezi suwezi, mimi siwezi.
Kila kitu ni Tunu,Tunu,Tunu,Tunu (uk48)

                      TASHBIHI.
Ashua angeishi kama malkia.

Husda hataki jua lifanye  ngozi yake ngumu kama ya mamba  (uk67)

Pengime Tunu atambae kama nyoka. (uk69)

Siku hizi wake hawashikiki, ni kama masikio ya syngura. (uk76)

Kuishi kulivyo ni kama mshumaa. (uk80)

                           MASWALI.

           A) Maswali ya insha.

1) Jadili jinsi maudhui ya uzalendo yamejitokeza katika tamthilia ya Kigogo. (al 20)

2) "Mwandishi wa tamthilia ya kigogo anadhamiria kujenga jamii mpya"  Thibitisha ukweli wa kauli hii. (al 20).

3) "Maandamano na migomo ni tatizo sugu katika mataifa yanayoendeleaa." Kwa kurejelea tamthilia ya kigogo, eleza chanzo na athari za maandamano na migomo. (al20)

4 )Jadili ufaafu wa anwani "kigogo" katika tamthilia ya kigogo. (al 20)

5) "Mataifa mengi ya Afrika yamekumbwa na tatizo la uongozi mbaya."  Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)

6) "Katika jamii ya kisasa, asasi ya ndoa imo atharini."  Kwa kutoa mifano katika tamthilia ya kigogo, tetea ukweli wa kauli hii. (al 20)

7) Jadili jinsi mwandishi wa tamthilia ya kigogo alivyofaulu kutumia mbinu ya kinaya katika kazi yake. (al 20)

8)  "Majoka ni mfano halisi wa viongozi katika mataifa mengi ya Afrika." Thibitisha kauli hii. (al20)

9) Eleza umuhimu wa mhusika Tunu katika tamthilia ya Kigogo. (al 20)

10) Fafanua mbinu anazotumia Majoka kuongoza Sagamoyo. (al 20)

11) "Wananchi katika mataifa ya Afrika hukumbwa na matatizo si haba." Thibitisha kauli hii kwa kutolea mifano kutoka tamthilia ya kigogo. (al 20)

12) Jadili nafasi ya mwanamke katika jamii kwa kurejelea tamthilia ya kigogo. (al 20)

13) Vifo/mauaji ni suala ambalo mwandishi wa tamthilia ya kigoo ameangazia. Eleza chanzo cha vifo/mauaji haya. (al 14)

b) eleza umuhimu wa mhusika babu katika tamthilia ya kigogo. (al 6)



        B) Maswali ya dondoo.

14) "...mmemulikwa mbali."

a) eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)

b)Taja na ueleze sifa mbili za msemaji wa maneno haya. (al 4)

c) kulingana na dindoo hili, ni nani na nani wamemulikwa? (al 2)

d)Fafanua mambo ambayo warejelewa waliyafanya ambayo yamemlikwa Sagamoyo.
(al 10)

15)  "...kulinda uhai, kulinda haki, kulinda uhuru..."

a)Weka dondoo hili katika muktadha,wake. (al 4)

b)Taja na ufafanue maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo hili. (al 4)

c)Msemaji wa maneno haya alifanikiwa kulinda uhai, kulinda haki, kulinda uhuru. Thibitisha kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 12)

16) " Sitaki kazi ya uchafu hapa Sagamoyo."

a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (al 4)

b) Taja na ueleze maudhui mawili yanayojitokeza katika dobdoo hili. (al 4)

c)Sagamoyo kuna uchafu.Thibitisha kwa kurejekea tamthilia nzima. (al 12)

17) "...wa kujichunga ni wewe pwaguzi."

a) Eleza muktadha wa dondoo hili.(al 4)

b)Eleza sifa ya msemewa kutokana na dondoo hili (al 2)

c)Taja tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili. (al 2)

d) Kwa kurejelea tamthilia nzima, thibitisha kuwa msemewa wa maneno haya alikuwa pwagu Sagamoyo. (al 12)



18)  "Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza."

a)Eleza muktadha wa dondoo hili.(al 4)

b)Eleza mbinu ya uandishi iliyotumika katika dondoo hili.(al 2)

c) Ni maudhui yepi yanayojitokeza katika dondoo hili? (al 2)

d) Thibitisha ukweli wa kauli kuwa siafu ni wengi, na si rahisi kuwamaliza kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 12)

19) "Kimba ni kimba tu."

a)weka dondoo hili katika muktadha wake. (al 4)

b)Taja sifa  mbili za msemaji kulingana na dondoo hili.(al2)

c) Kwa kutolea mifamo mwafaka, fafanua mambo yaliyosababisha kuwepo kimba Sagamoyo. ((al 14)

20)  "Kuishi kwa kutojali ni muhali."

a)Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4)

b)Fafanua sifa mbili za msemaji wa maneno haya. (al2)

c) Msemewa wa maneno haya aliishi kwa mutojali. Thibithisha kwa kurejelea tamthilia nzima. (al 8)

d )Ni vipi kutojali kwa msemewa hapo juu kulikuwa muhali Sagamoyo? (ak 6)



                                               Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni