Alhamisi, 25 Mei 2017

KIIMBO

KIIMBO
Namna ya kupaza na kushusha mawimbi ya sauti pale mtu anapotamka maneno.
Baadhi ya maneno hufanana kiimbo lakini kwa jinsi mawimbi ya sauti yanavyopanda na kushuka yakawa yana maana tofauti.
Mifano
Bara’bara-njia kuu
Ba’rabara-sawasawa
Wa’lakini-dosari
Wal’akini-ingawaje
Kata’kata-kukataa
Ka’takata-kugawa vipande
Kiimbo hutusaidia kubainisha lengo la msemaji wa lugha inayohusika, hivyo tunaweza  kutambua kama mzungumzaji anatoa maelezo ,anauliza swali,anaamuru ama anarai.
Aina za viimbo
Katika kusikiliza mazungumzo ya watu mbalimbali tunaweza kutambua kama mzungumzaji anatoa maelezo ,anauliza swali,anaamuru au anarai . tunatambua hivyo kutokana na namna kiimbo kinavyobadilika.
Vipo kama ifuatayo;
Kiimbo cha maelezo/taarifa
Kiimbo cha maulizo
Kiimbo cha mshangao
Kiimbo cha amri
Kiimbo cha rai
Sentensi za taarifa
Saparata anaandika barua.
Mama Resi anakoroga uji.
Sentensi za maswali
Dinda anaandika nini?
Mama Resi anakoroga nini?
Sentensi za rai/sentensi za maombi
Tafadhali nikorogee uji.
Niongezee tafadhali.
Sentensi za amri
Tembea haraka!
Funga mlango!
Kwenda kabisa!
Sentensi za mshangao

Muone Yule mrembo!

Maoni 2 :

  1. Asante sana kwa kutusaidia katika kipindi hiki

    JibuFuta
  2. Na ukiambiwa ueke kiimbo katika neno amri

    JibuFuta