Wednesday, 24 May 2017

KAMUSI

                 Kamusi
Kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno yaliyopangwa kwa kufuata utaratibu wa alfabeti/abjadi pamoja na maana zake.
Kamusi ni kitabu cha marejeleo .(cha kuangalia mara kwa mara) ambacho hukusanya msamiati au maneno yanayopatikana katika lugha inayozungumzwa na jamii Fulani.
Kamusi ni chombo muhimu na cha kimsingi kwa yeyote anayejifundisha lugha Fulani.
         Umuhimu wa kamusi

Husaidia jinsi ya kuliendeleza neno Fulani kwa njia ifaayo-yaani kwa njia sahihiza maneno mbalimbali
Huonyesha maana/fasili mbalimbali ili kumsaidia mtumiaji kupanua ujuzi wake wa lugha hiyo.
Huonyesha misemo ,nahau na methali mbalimbali –kwa neno Fulani latokana na lugha Fulani .hata hivyo si kamusi zote zenye taarifa hizi.
Huonyesha jinsi mbalimbali za kunyambua vtenzi ikizingatiwa kuwa si vitenzi vyote vinavyonyambuliwa katika hali zote.
Kamusi hubainisha ngeli  za nomino  na hivyo kutuelekeza katika upatanishi mzuri wa sarufi.
Huonyesha miktadha mbalimbali ya matumizi ya maneno, Miktadha hii ni kama vile ya dini, ushairi,ubaharia.
Huonyesha vifupisho mbalimbali vinavyotumiwa katika lugha inayohusika kwa mfano;
Mifano agh-aghalabu             nm-nomino             kl-kielezi                 kv-kivumishi
            ms-msemo                mf-mfano                my-maana yake       mt-methali
            kt-kitenzi
aina za kamusi
aina za kamusi hutegemea ;
  1. Idadi ya lugha ambazo zimetumiwa katika kamusi moja.
  2. Walengwa wa kamusi
  3. Mambo yanayoshughulikiwa katika kamusi.

  1. Kwa kutegemea idadi ya lugha

  1. Kamusi wahidiya- kamusi yenye lugha moja.
Maneno yake (vitomeo/vidahizo) . Huwa ya lugha ile ile inayotumiwa kuyaelezea. Ikiwa lugha ni Kiswahili basi itakuwa ni hiyo hiyo katika kamusi nzima.
Kamusi ya aina hii humsaidia mtumiaji kuukuza katika lugha Fulani moja.
Mifano
Kamusi ya Kiswahili sanifu (TUKI)
Kamusi kamili ya Kiswahili sanifu{longhorn}
Kamusi ya Kiswahili {F.Johnson}      
Kamusi ya shule za msingi {oxford}
            (b) kamusi thaniya
Ni kama inayotumia lugha mbili . hivi vidaa hinaweza kuwa vya Kiswahili halafu vikaelezwa kwa kiingereza au kupewa visawe vyake vya kingereza.kamusi hii humsaidia mtumiaji kujua maneno katika lugha mbili tofauti.
Kwa mfano;
Kamusi ya Kiswahili-kingereza  {TUKI}
Aconsise English-swahili dictionary{R.aisnoxall na .mshinde}      
Kamusi thulathia .
Ni kamusi inayohusisha lugha tatu. Vidaizo vyake hupewa visawe katika lugha nyingine mbili.
  1. Kwa kutegemea uwanja

  1. Kamusi ya visawe /thesauri

Huwa na maneno pamoja na maneno yenye maana sawa na hayo.
Kamusi hizi ni nzuri katika  kuupanua msamiati wa mtumiaji mfano;
Kamusi ya visawe(S.A Mohamed na M.Mohamed)
           Mifano ya maneno ni kama;
Maharagwe-mandondo
Insani-mahuluki/insi/mlimwengu/mwanadamu
Mstari(n) mi –foleni/mlolongo/msururu/mkururo/moza/safu
  1. Kamusi ya istiahi
Ni kamusi ambazo zinahusu uwanja fulani maalum, kwa  mfano somo Fulani.kamusi hii humsaidia mtumiaji kuongeza msamiati wake au kujua maneno maalum ya uwanja huu. Mifano za kamusi hizi ni;
Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha(TUKI)
Kamusi Sanifu ya BIologia,fizikia na kemia(TUKI)
Kamusi ya fasihi /Istilahi na nadharia.(KW Wamitilia)

Ensaiklopidia
Ni kamusi maalum kuhusu uwanja Fulani maalum.kamusi hizi huwa na taarifa nyingi sana kuhusu uwanja huo.zipo za sayansi ,za lugha za fasihi,za uchumi n.k.kwa kawaida kamusi hizi huwa na taarifa nyingi ambazo hazipatikani katika kamusi za kawaida za lugha.
3.kutegemea walengwa
      a) kamusi za wanafunzi
hulenga wanafunzi wa shule za msingi au wa upili, kamusi hizi huwa na idadi ndogo ya maneno zikilinganishwa na kamusi za kawaida ambazo hulenga watumiaji wa kawaida wa lugha.
     b)kamusi za kawaida-huwalenga watumiaji wa kawaida :wanafunzi,wataalamu na    wasiokuwa wataalamu .kamusi ya Kiswahili sanifu ni mfano wa kamusi ya kawaida ya lugha .

No comments:

Post a Comment