NGELI
Ngeli ni mkusanyiko wa majina ya Kiswahili yaliyo na sifa sawa kisarufi.
.majina katika ngeli moja hutumika kwa kuzingatia kawaida sawa.
Hivyo ni makosa kuchanganya sheria za ngeli tofauti ndiposa ni muhimu kuhusisha kila nomino na ngeli yake.
Ngeli za Kiswahili.
A-Wa I-Zi U-Zi
U-I Ya Ku
Ki-Vi I U
Li-Ya U-Ya pa-ku-mu
Ngeli ya A-WA
Ina majina ya viumbe wenye uhai yakiwa katika hali wastani.
Hujumuisha ;
1.Majina ya wanyama
Ngamia pundamilia paka fisi kondoo
Nyani ndovu simba farasi swara
2.Majina ya ndege
Mbuni heroe jiwa kasuku kunguru
Tai batamzinga tausi chiriku kasuku
Kifaranga
3.majina ya samaki na viumbe wa baharini
Dagaa mkizi mamba chewa papa
Mkunga kaa pweza kiboko kambare
Nyangumi
4.majina ya binadamu
Mtu mwalimu mkunga mpishi kipofu
Mtoto daktari dereva kiziwi mjomba
Mwanafunzi mkulima seremala kiwete
5.majina ya wadudu
Kupe kunguni chawa siafu panzi
Nzi mende kimatu jongoo nzige
Kipepeo nyuki mchwa
6.viumbe wasioonekana
Mungu malaika shetani
Upatanishi kisarufi
1.viambishi ngeli
Nomino hizi huambiswa A –kwenye vitenzi katika umoja na Wa-katika wingi.
Mifano
Umoja wingi
Nzi ametua kwenye kidonda . Nzi wametua kwenye kidonda.
Mjomba amefikishwa kortini. Wajomba wamefikiswa kortini.
2.vimilikishi
Kumiliki ina maana ya kuwa na.
Vimilikishi hubadilika kutegemea nafsi sawa na hali yaumoja ama wingi.
Sentensi
Mjomba wangu ameniletea zawadi. Wajomba wetu wametuletea zawadi.
Farasi Yule ni wake mwanafunzi. Farasi wale ni wao wanafunzi.
3.a-unganifu
Huonyesha uhusiano wa kumiliki.huwakilishwa na Wa katika umoja na wingi.
Mifano
Malaika wa Mungu alifikisha ujumbe Malaika wa Mungu walifikisha ujumbe.
Mdudu wa shambani amekufa. Wadudu wa shambani wamekufa.
4.viashiria
Kuashiria ni kuonyesha umbali wa kitu.
Mfano
Umoja wingi
Karibu huyu hawa
Mbali kiasi huyo hao
Mbali sana Yule wale
5.virejeshi
Ni maneno/ viambishi vinavyomrejesha msomaji katika nomino .ni ya aina mbili;
- Amba rejeshi
- –o-rejeshi
o-rejeshi mifano
kitabu kilichopotea kimepatikana. Vitabu vilivyopotea vimepatikana.
Katika ngeli ya A-WA –ye- hutumika katika umoja na –o- katika wingi.
‘ambaye’ hutumika katika umoja na ‘ambao’ kwenye wingi.
Matumizi
Aliyetoka hapa ni mtu huyu. Waliotoka hapa ni watu hawa.
Mnyama ambaye ni mkubwa zaidi ni nyangumi wanyama ambao ni wakubwa zaidi ni nyangumi.
Hali ya mazoea
-o-rejeshi inaweza kutumiwa kuonyesha mazoea . huja mwishoni mwa kitenzi na katika hali hii kiambishi cha wakati lazima kipotee.-o-rejeshi ya tamati haitumiki pamoja na kiambishi ‘hu’ cha mazoea.
Mifano
-o-ya kati -o-tamati {ya mazoea}
Waliotembea watembeao
Aliyefaulu afauluye
Aliyenifaa anifaaye
Watakaoruka warukao
Atakayefika afikaye
mifano katika sentensi
hali ya wastani
mtoto anayetii ndiye anayefaulu. watoto wanaotii ndio wanaofaulu.
Hali ya mazoea
Mtoto atiiye ndiye afauluye . watoto watiio ndio wafauluo.
Wastani mazoea
Mtoto aliyeumia ni huyu. Mtoto aumiaye huwa huyu.
Mwanafunzi aliyepita ametuzwa. Mwanafunzi apitaye hutuzwa.
Amba-rejeshi ya mazoea
Wastani mazoea
Fisi ambaye alikula mzoga amenaswa. Fisi ambaye hula mzoga hunaswa.
6.vivumishi vya pekee
Kivumishi cha pekee
|
umoja
|
wingi
|
-enye
|
mwenye
|
wenye
|
-enyewe
|
mwenyewe
|
wenyewe
|
-ingine
|
mwingine
|
wengine
|
-ingine-o
|
mwingineo
|
wengineo
|
-ote
|
©
|
wote
|
-o-o-te
|
yeyote
|
wowote
|
-ingi
|
©
|
wengi
|
NGELI YA U-I
Ina majina ya miti na mimea.
Mifano
Mchungwa mparachichi mpera mgomba mnazi
Mzabibu mpunga mpapai mlimau muhogo
Mbuni mbuyu mchenza mkwaju mzambarau
Mtomoko mnanasi mfenesi mhindi mharagwe
Mwarubaini mbibo mkalatusi mkuyu mtini
Majina ya baadhi ya sehemu za mwili
Mkono jino mfupa moyo mdomo
Munda mgongo msuli mshipa mundi
Mkundu mtulinda mguu
Majina ya vitu/maumbile
Mlima mto msitu mwamba mwezi
Mwaka msimu muhula mkeka mkoba
Mlango mkebe mwamba muhula mchi
Mkate mshale mpira mtego
Viambishi majina katika ngeli ya U-I
- m-mi mifano
mti-miti
- mu-mi muhula-mihula
muwa-miwa
- mw-mi mwamba -miamba
NGELI YA KI-VI
Ngeli hii inahusisha baadhi ya sehemu za mwili ;
Kichwa kisogo kisigino kiganja kiuno
Kiwiliwili kifua kibofu kinywa kiwiko
Kidole kipaji.
Majina ya vyomba/vifaa
Kikombe kisu kinu kifaru kiboko
Kioo kiberiti kiberenge kitabu kichana
Chandarua choo chakula kinanda kitanda
Kiti kijiko kikapu
Majina yote ya Kiswahili katika hali ya udogo
Wastani udogo wastani udogo
Nazi kijinazi kidole kijidole
Kikombe kijikombe gari kijigari
Mtoto kijitoto mpira kijipira
Mti kijiti mbwa kijibwa
Shati kijishati sindano kijisindano
NGELI YA LI-YA
Husheheni majina ya mazao ya mimea.
Mifano
Hindi haragwe chungwa tini
Buyu pera nanasi kanju
Tango peasi dafu parachichi
Ua bibo tomoko embe
Fenesi boribo limau chenza
Tongonya izu tikiti bungu
Baadhi ya viungo vya mwili
Jino bega jicho pafu
Sikio figo kalio goti
Kwapa tumbo ini paja
Titi kende tombo
Majina ya Kiswahili katika ukubwa.
Wastani umoja wingi
Mtu jitu majitu
Mbwa jibwa majibwa
Jicho jijicho majijicho
Redio jiredio majiredio
Unyasi jinyasi majinyasi
Nomino za dhahania
Wazo swali neno
Shauri pigo tangazo
Jambo jibu jambo
Jibu jina jinni
Zimwi tokeo pengo
Ombi penzi
Vitu
Tawi duka jamvi
Shamba jiko yai
Jiwe figa jifya
Daraja darasa jipu
Gunia jumba boma
Ngeli ya I-ZI
Majina ya ngeli hii huwa hayabadiliki katika umoja na wingi
Baadhi ya nomino ya ngeli hii ni zile zilizokopwa kutoka lugha zingine.
Mifano;
Shati soksi lori basi
Klabu komputa televisheni redio
Kalenda penseli shule eropleni
Shilingi skuli tai baiskeli
Kamera geti senti wiki
Kioski
Majina mengineyo
Sabuni nyumba ndizi karata
Ngoma ngazi nguo ndoo
Kalamu kengele nundu shida
Taa chupa rununu runinga
Kufuli saa nazi chaki
Habari pikipiki sahani nyama
Karatasi samani pua dawa
Upatanishi wa kisarufi
Viambishi ngeli
Umoja ‘I’
Wingi ‘Zi’
Mifano
Kalamu yangu imepotea . kalamu zetu zimepotea.
-a unganifu
Umoja ‘ya ‘
Wingi ‘za’
Sabuni ya mama imeanguka,
Sabuni za kina mama zimeanguka
Virejeshi
Umoja ‘yo’
Wingi ‘zo’
Vimilikishi
Nafsi umoja wingi
1 yangu zetu
2 yako zenu
3 yake zao
Matumizi
Tai hii ni yangu. Tai hizi ni zetu.
Redio tangu imeharibika redio zetu zimeharibika
Ngeli ya U –ZI
Viambishi majina
u-nd u-ny u-nj
u-mb w-ny
u-©
u-nd
ulimi ndimi uele- ndwele udevu –ndevu
udifu -ndifu
u- ©
ukuta-kuta ukucha-kucha ukebe-kebe uteo-teo
ufagio-fagio ufunguo-funguo ufalme-falme utambi-tambi
unyasi-nyasi ukurasa-kurasa ubeti-beti unywele-nywele
ukumbi-kumbi
u-ny
uzi-nyuzi ua-nyua ufa-nyufa uwanja-nyanja
ungo-nyungo uwaya-nyaya uta-nyuta uso-nyuso
undu-nyundu uti-nyuti
u-mb
ubinda-mbinda ubavu-mbavu
ubati-mbati ubawa-mbawa
w-ny
wembe-nyembe wimbo-nyimbo waraka-nyaraka
waya-nyaya wanja-nyanja wayo-nyayo
wadhifa-nyadhifa wanda-nyanda
Upatanishi Kisarufi
Viambishi ngeli
Umoja ‘U’ wingi ‘zi’
-a unganifu
Umoja ‘wa’ wingi ‘za’
Vimilikishi
Nafsi Umoja wingi
1 wangu zetu
2 wako zetu
3 wake zao
Viashiria
Karibu mbali kiasi mbali
Umoja huu huo ule
Wingi hizi hizo zile
Mifano
Waya wa umeme umekatika.
Nyaya za umeme zimekatika.
Viambishi ngeli.
Matumizi
Uzi umekatika.
Nyuzi zimekatika.
a-unganifu
waya wa umeme umekatka. Nyaya za umeme zimekatika.
Uso wa dada umerebeshwa . Nyuso za kina dada zimerembeshwa.
Viashiria
Wembe huu umekatika. Nyembe hizi zimekatika.
Virejeshi
‘o’-rejeshi
Umoja ‘o’ Wingi ‘zo’
Amba rejeshi
Umoja ambao wingi ambazo
Uzi ambao ulikatika ni huu. Nyuzi ambazo zilikatika ni hizi.
Ulimi ambao uliuma umepona. Ndimi ambazo ziliuma zimepona.
Mazoea/desturi
Uzi ambao hukatika huwa huu.
Nyuzi ambazo hukatika huwa hizi.
Ulimi uumiao hupona – Ndimi ziumazo hupona.
Uzi ukatikao huwa huu. Nyuzi zikatikazo huwa hizi.
Vivumishi vya pekee
-enye
|
wenye
|
zenye
|
-enyewe
|
wenyewe
|
zenyewe
|
-ingine
|
mwingine
|
zingine
|
-ingine-o
|
mwingineo
|
zinginezo
|
-ote
|
wote
|
zote
|
o-o-te
|
wowote
|
zozote
|
Matumizi
Ukuta mwingine umeanguka. Waya wote umekatika.
Kuta zingine zimeanguka. Nyaya zote zimekatika.
Ubawa wenyewe umeumia. Nipe uzi wowote.
Mbawa zenyewe zimeumia. Tupe nyuzi zozote.
Ngeli ya U-YA
Nomino za ngeli hii huchukua viambishi awali ‘u’ na ‘ya’ katika upatanisho wake wa kisarufi. Kiambishi cha umoja ni u- na cha wingi ni ma- (viambishi majina)
Ulezi-malezi uzuri –mazuri upana-mapana ukubwa -makubwa
Upendo -mapendo uzinduzi-mazinduzi ubongo-mabongo uovu-maovu
Ubawa-mabawa uvutaji-mavutaji uwele-mawele uboga-maboga
Upatanishi kisarufi
Ulezi huu utamfaa mtoto –malezi haya yatawafaa watoto.
Uzuri wa mkakasi ndani yake kipande cha mti. –mazuri ya mikakasi ndani yao vipande vya miti .
Ubele ule unavutia .-mabele yale yanavutia.
Virejeshi
Ukubwa uliozidi una hatari – makubwa yaliyozidi yana hatari .
Ukubwa ambao umezidi una hatari. Makubwa ambayo yamezidi yana hatari.
Ukubwa uzidio huwa hatari.- makubwa yazidiyo yana hatari.
Vivumishi vya pekee.
Umoja wingi
-enyewe wenyewe yenyewe
-enye wenye yenye
-ote wote yote
-ingineo mwingineo mengineyo
-o-o-te wowote yoyote
-ingine mwingine mengine
Ngeli ya I
Ina majina ya nchi .
Mifano
Kenya Tanzania Uhabeshi Unguja
Misri Bukini Uswizi Marekani
Visiwa vya ngazija Uganda Bukini Ushelisheli
Majina ya miji
Nairobi kampala Dar –es-salaam Kisumu Mombasa
Majina ya masoko /vijiji
peponi Katito kahawa Butangi
Mabara Butangi
Afrika uropa Asia Amerika Kaskazini Amerika kusini
Australia
Majina ya madini
Dhahabu Almasi Shaba Fedha kiberiti vito lulu
Risasi chuma yakuti
Majina mengine
Chumvi sukari chai kahawa ngano petrol damu pizeli baridi afyuni poda kaaba sufu sarufi Adhuhuri
Sufi ni kitu kama pamba kinachotokana na tunda la msufi kinachoweza kutiwa kwenye magodoro .
Sufu –manyoya hasa ya kondoo yanayotengenezwa nyuzi ambazo hutumiwa kutengenezea nguozinazoleta joto mwilini.
Samli –ni mafuta yanayotokana na maziwa ya wanyama kama vile ng’ombe , ngamia au mbuzi yanayotumiwa kupika.
Shahamu- mafuta ya mnyama au samakiambayo aghalabu hutengenezwa sifa ya kupaka katika chombo cha baharini au kwenye mbao ili kuziimarisha na kuzura kuliwa na wadudu.
-mafuta yanayopatikana kwa mnyama aliyenona.
Kaaba-jumba takatifu lililoko Maka ambalo waislamu hulielelea wanaposwali na hulizunguka wakati wa kufnya ibada mojawapo ya Hija.
Afyuni –kileo aghalabu kidongo kinachotengenezwa kwa utomvu wa mmes Fulani,kasumba ,majuni.
Kiambishi ngeli ni ‘I’
Mifano
Damu ilimchirizika alipokatwa.
Sukari imemwagika barabarani.
Mji wa Nairobi i Kenya.
-a unganifu huwakilishwa na ‘ya’
/i/+/a/=ya
Asali ya nyuki huwa tamu sana.
Kahawa ya mfanyabiashara Yule imetoweka.
Vimilikishi
Petrol yangu imetoweka. Safu yake ataijaza mtoni.
Siigawi samli yangu.
Virejeshi
Kenya ni nchi ambayo inapendeza.
Petroli iliyomwagika ni ya gari.
Ngeli ya u
Nyingi za nomino hizi ni zile zisizoweza kuhesabika kwa mfano;
Ugali udongo wali wino umande uji
Nyingine za dhahania (zinazorejelea hali tunayohisia kuwapo ingawa hazishikiki)
Umaskini utoto ujinga wepesi umeme uchawi
Wema ulaghai uhodari ushindi utajiri uchoyo utoto
Werevu uwezo uchache umoja uganga wokovu uume
Ujana ukarimu uzito usingizi wingi ushirikina wivu ulafi uke
Upatanishi kisarufi
Viambishi ngeli ni ‘u’
Ugali ule ni mtamu.
Vimilikishi
Utajiri wetu umetufaa. Wema wangu umeniponya.
-a unganifu (u+a=wa) ni wa
Ugonjwa wa ukimwi ni hatari sana.
Virejeshi
Udongo unaofaa ni huu. Uji ambao umemwagika ni wangu.
Uchawi aushirikio hautusaidii.
Vivumishi vya pekee
Uji wenyewe umemwagika. Nipe wino wowote usingizi wote umeisha.
Werevu mwingine hausaidii. Nipe ugali mwingineo.
mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm
JibuFutanini?
FutaMungu uko katika ngeli gani?
JibuFutajiongeze
FutaA - Was
FutaA - wa
FutaNomino mungu hupatikana katika ngeli ya a-wa
FutaMungu iko katika ngeli ya a-wa
Futawoooooooioooow😁😁😘😘😍😍
JibuFutaVyema
Futanice and lovely notes,thank
JibuFutaNimejifunza mengi kupitia hii. Ahasante Sana kwa kunielimisha ngeli.
JibuFuta,am crying
JibuFutaThen keep up the good work
Futa👍
Futa👍
FutaTafadhali nitumie majina ya nomino zilizo katika ngeli ya li-li
JibuFutaKWA nini hamzungumzii ngeli inayohusisha nebo vita?
JibuFutaWoowowowowowoowwowo
JibuFutaHaujaonyesha jua iko katika ngeli gani??????
JibuFutaJua liko katika ngeli ya li
FutaAsanteni sana
JibuFutaHii mtandao wenu umenisaidia👍👍👌👌👏👏
Karibu tena
FutaKitanda iko ngeli gani 😢
FutaNgeli ya mw mi majina
JibuFutaPa Ku mu tafathali
JibuFutaPamba iko katika ngeli gani
JibuFutaBora zaidi
JibuFutaNgeli ya uzuri ni
JibuFutaSimu iko katika ngeli gani?
JibuFutaI-zi
FutaNitumie nomino katika ngeli ya Li Li
JibuFutaNeno kiswahili liko katika ngeli gani
JibuFutaNeno maji ipo katika ngeli ya?
JibuFutaYA-YA
FutaHi in boo
JibuFutaMalaika iko kwa ngeli gani
JibuFutaneno jifya liko ngeli gani
JibuFutaHmjk
JibuFutaMifano ya kauli ya kutendesheana
JibuFutaPigo liko katika ngeli ya
JibuFutaMama
FutaNambari iko katika ngeli ya????????????
JibuFutaLi-ya
JibuFutaN
JibuFutaNinindio ngeli ya kiziwi
JibuFutaNinindio ngeli ya kiziwa
JibuFutaNilikuwaa na swali, Je? Kuna ufanano na utoauti kati ngeli za kiswahili na lugha za asili au kibant
JibuFutaWema Iko katika ngeli Gabi?
JibuFuta