Alhamisi, 25 Mei 2017

USEMI HALISI NA USEMI TAARIFA

USEMI HALISI NA USEMI WA TAARIFA
kauli zipo za aina mbili;
  1. kauli ya moja kwa moja kutoka kwa mnenaji hadi kwa msikilizaji jinsi ilivyo bila ya kufanyiwa mageuzi yoyote, kauli hii huitwa usemi halisi.
  2. Kauli inayopokewa kama maelezo ya yaliyosemwa pale awali na ambayo hufanyiwa mabadiliko fulani fulani ya hapa na pale, kauli hii huitwa usemi wa taarifa.
  1. Usemi halisi
Katika usemi huu yafuatayo huzingatiwa;
  • Alama za mtajo hutumiwa mwanzo na mwisho wa maneno yaliyosemwa.{“  “}
  • Kila baada ya kufungua ,sentensi huanza kwa herufi kubwa m.f
     “Hamjambo?”
“Shuhuda, tafadhali njoo tukatembee.”
  • Alama ya hisi,kiulizo,koma,nukta za dukuduku na kituo kikuu pia hutumiwa pamoja na alama za mtajo.Lazima zije kabla ya alama za kufunga. m.f
“Hunipendi?”
  • Msemaji mpya anapoanza kusema tunaanza aya  mpya maneno ya wazungumzaji wawili tofauti yasiwekwe katika aya moja.
Mwalimu akamhoji, “vipi?”

Mwanafunzi alijibu, “salama”
  • Kauli moja ikivunjwa katika vitengo, kitengo cha pili hata baada ya kuwekewa alama za kufungua ,neno lake la kwanza litaanza kwa herufi ndogo isipokuwa neno lilo likiwa nomino maalum.
  • Iwapo sentensi mpya inaanza baada ya msemaji kutajwa, herufi kubwa hutumika mwanzoni mwa hiyo sentensi mpya.
“Tukifika mjini Voi ,tutapumzika kwa muda wa saa moja.” Kiongozi wetu alisema. ”Baadaye tutaondoka na kwenda moja kwa moja hadi kisiwani Mombasa.”
“Haya! Habari ndiyo hiyo,” mwalimu alisema.
“Haya ,habari ndiyo hiyo.” Mwalimu alisema.
“Wiki ijayo tutakwenda kujionea mechi kati ya Harambee stars na Uganda Craines.” Rafiki yangu aliniambia.
“Mara nyingi binadamu uhitaji kutumia 'common sense.’ ”
  1. usemi wa taarifa
Hii ni ripoti kuhusu yaliyosemwa hapo awali. Yafuatayo huzingatiwa;
  • Alama za mtajo haziwekwi
  • Baadhi ya maneno yanaweza kubadilika lakini ujumbe uwe ni ule ule.
  • Alama za hisi na kiulizi hazitumiwi.
  • Aghalabu wakati uliopita ndo hutumika

                                              Mabadiliko



Usemi halisi
Usemi wa taarifa
                                                         viulizi
-ngapi?
Idadi
-ipi
Sifa/o-rejeshi/amba-rejeshi
-gani
o-rejeshi/amba-rejeshi/sifa
Je ,…?
Iwapo/ikiwa
…..je?
Jinsi/namna
Lini?
Wakati
Mbona?
sababu
Kwa nini?
Sababu
Vipi?
Jinsi/namna
                                                    Wakati/hali
-me-
-li-
-ta-
-nge-
Mwaka ujao
mwakani
sasa
Wakati huo
kesho
Siku iliyofuata
Jana
Siku iliyotangulia
                                            Nafsi
-ni-
-a-
-ku-
-ni-/m-

       
   
                                                                   viashiria
Hapa
Pale/hapo/alipokuwa
huku
Kule/huko/alikokuwa
huyu
Yule/huyo
                                                                      vihisishi
Tafadhali
alisihi
Salaala!
alishangaa
Nkt!
alifyonza
Uuuuwi!
Piga mayowe/npiga usiyahi
alhamdullilahi
alishukuru
Mungu wangu eeeh
aliomba
Arusi tunayo
shangilia
kwenda
Laani/puuza
Katika usemi wa taarifa matumizi ya maneno ‘kuwa’ na kwamba huruhusiwa  kwa mfano ;
“Mtoto ni mtoto, awe wa kiume au wa kike,” akasema mjomba,
Mjomba alisema kuwa…
Mjomba alisema ya kwamba mtoto ni mtoto awe wa kiume au wa kike.
“Mabasi hayapiti hapa siku hizi, kwa nini?” Neshboch aliuliza.
Neshboch alihoji/aliuliza/alitaka kujua sababu ya mabasi kutopita hapo katika siku hizo.
Madereva wakasema ,”Tutatii sheria za barabarani.”
Madereva walisema kuwa wangetii sheria za barabarani
“Leo nitakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya,” Seki akamwambia Katango.
Seki alimwambia Katango  kwamba angemwonyesha kilichomtoa kanga manyoya siku hiyo.
“Afida , kwa nini  leo umechelewa darasani?” Kiranja akauliza.
Kiranja alitaka kujua sababu ya Afida kuchelewa darasani siku hiyo.
“Serikali ina mkono mrefu, hata ukijificha wapi utapatikana. ” Akakumbusha Chausiku .
Chausiku alikumbusha kwamba serikali ilikuwa na mkono mrefu na hata mtu angejificha popote angepatikana.
Mwanafunzi alisema kuwa angepita katika somo la Kiswahili.
“Nitafaulu katika somo la Kiswahili,”akasema mwanafunzi.
Mwanafunzi akasema,”Nitafaulu katika somo la Kiswahili.
Chifu aliwakumbusha kuwa ukimwi ulikuwa  ulikuwa ugonjwa hatari sana.
“Ukimwi ni ugonjwa hatari sana,”  chifu akawakumbusha.
Chifu akawakumbusha, “Ukimwi ni ugonjwa hatari sana.”
“Nawakumbusha kuwa ukimwi ni ugonjwa hatari sana.” Chifu akasema.
Kazimoto alishauriwa na kasisi kuwa  aache tabia za ulevi.
“Acha tabia ya ulevi,”kasisi akamshauri Kazimoto.
“Kazimoto  acha tabia ya ulevi,” kasisi akamshauri.
“Alimaliza fyu!”
Akamaliza yote
“Van persie , Van persie, goool!”
Alishangilia vanpersie alipofunga bao.
“Ni siku arubaini pekee ambazo zimebaki kabla ya Nineve kuangawizwa ikiwa hamtatubu dhambi zenu.” Jona akawatadharisha.
Jona aliwatadharisha watu kuwa siku arubaini pekee ndizo zilizobaki kabala ya Nineve kuangamizwa ikiwa awangetubu dhambi zao.
“wanipendeani mrembo?”
Alimuliza mrembo alikuwa anampendea nini.
"Anayenitesa si  adui yangu bali ni rafiki yangu tuliyojuana zamani,"Dzombo akasema.
Dzombo alisema kuwa aliyekuwa akimtesa hakuwa adui yake bali alikuwa rafiki yake waliojuana siku zilizopita.

Maoni 48 :

  1. Je ni sawa kusema
    "Naam," akasema,"nitakusaidia."
    "Naam," akasema, "Nitakusaidia."
    Ni ipi sawa?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Sentensi ya Pili ni sahihi.

      Futa
    2. Sentensi ya Pili ni sahihi.

      Futa
    3. Alinibali ili anisaidie

      Futa
    4. Ya kwanza kwa sababu ya koma

      Futa
    5. Kanuni huwa rahisi hapa: Iwapo kauli ya kwanza imekamilika na hivyo inajisimamia, ile ya pili itaanza kwa herufi kubwa. Iwapo kauli ya kwanza haijakamilika na hivyo ni sehemu ya ile ya pili, basi ile ya pili itaanza kwa herufi ndogo. Kazi kwako.

      Futa
    6. sentensi ya pili ndio sahihi

      Futa
  2. Sentensi ya Pili iko sahihi.
    Katika usemi halisi herufi ya kwanza huandikwa kwa herufi kubwa

    JibuFuta
  3. Ninataka kula chakula.!je sentensi hii ipo katika usemi gani

    JibuFuta
  4. Kwann katika kauli taarifa inatumika Ange..

    Mf "Nitafua Nguo"

    Inabadilika kuwa angefua nguo

    JibuFuta
    Majibu
    1. Usemi taarifa hali ya mazoea

      Futa
    2. Kwa sababu kitu kingefanyika

      Futa
    3. Wazazi wanawahimiza watoto wao kusoma kwa bidii. Hii sentesi ipo katika kauli gani?

      Futa
  5. Hali ya mazoea hu hubadilishwa vipi in

    JibuFuta
  6. Usemi wa halisi na taarifa waweza kukosea nini

    JibuFuta
  7. Hakimu alimtaka "umepatikana na hatia ya uwizi utafungwa jela miezi minane" unisaidie kuandika kwa usemi taarifa

    JibuFuta
  8. "fanya hivi futa ubao leo"mwalimu animwambia

    JibuFuta
  9. enu katika semi taarifa

    JibuFuta
  10. Kiswahili sanifu.. Tuko kusanifisha lugha tukufu

    JibuFuta
  11. Mwalimu alishangaa kuniona pale.

    JibuFuta
  12. Hongeraaa kwa kuthubutu...

    JibuFuta
  13. Ku ni kiambishi cha nafsi? Ni vipi -ku-itabadilika kuwa ni au a ? Nielezee tafadhali

    JibuFuta
  14. asanteni kwa kuandaa somo hili

    JibuFuta
  15. Mwalimu alisema adurusukazi yake Siku hiyo badilisha

    JibuFuta
  16. Naomba sentensi hii it we usemi was taarifa ,,"sitathubutu kumpa pesa zangu."maluti Alisema

    JibuFuta
  17. Eleza maana ya usemi Halisi.

    JibuFuta
  18. Haya ni maneno ya moja kwa moja yanayonenwa na msemaji

    JibuFuta
  19. Je ukitaka kuandika sentensi hili Kwa usemi halisi utaandikaje?; Jirani alitaka kujua iwapo tutakwend au la

    JibuFuta
  20. Asante sana. Nimeshaa elewa utofauti kati ya Semi halisi na semi taarifa

    JibuFuta
  21. Mwalimu kwa hasira aliwaamuru wanafunzi wote wapige magoti na kumaliza kazi yao ya ziada. Je ? Sentensi hii itakuwa vipi katika usemi halisi ?

    JibuFuta
  22. Kazii safi BW.Edwin kwa kutupa fursa ya kujifunzaa lugha nantharii

    JibuFuta
  23. keshokutwa katika usemi wa taarifa ni?

    JibuFuta
  24. "Mtoto wako amefika,"_katika usemi taarifa

    JibuFuta
  25. Ningelipenda kujua, neno juzi itabadilika na kuwa nini katika taarifa

    JibuFuta