Jumatano, 24 Mei 2017

AINA ZA MANENO

AINA ZA MANENO
Lugha ya Kiswahili ina aina nane kuu za maneno;
Nomino{N}
Vitenzi{T}
Viwakilishi {W}
Vivumishi{V}
Vielezi{E}
Vihisishi{I}
Vihusishi{H}
Viunganishi{U}
1.nomino /Jina{N}
Ni neno linalotaja mtu ,kitu, mahali, mnyama au hali
Mifano
Njaa-hali               wema-hali          ukorofi –hali           Nahomi-mtu           Nyabondo-mahali      kalamu-kitu
Tai-mnyama         gari-kitu             marekani-mahali     mkulima-mtu    uzembe-hali                  Bramwel-mtu  
2.vivumishi{V}
Ni maneno yanayoharifu kuhusu nomino au kiwakilishi.
Mifano
Wanafunzi wa Kenyatta ni wangwana.
       N          V        N         T       V          
Msichana Yule mrembo ana miguu mizuri.  
    N            V          V           T     N           V      
3.vitenzi {T}
Kitenzi ni neno linaloonyesha jambo linalotendwa,lililotendwa na litakalotendwa.
Kitabu changu kimeteketea     
   N           v               T         
4.Vielezi{E}
Ni maneno yanayoharifu kuhusu vitenzi. Hueleza jambo limefanywa lini wapi ,vipi na kwa kiasi gani.
Kwa mfano
Alikimbia .
Vipi? Haraka/kasi
Wapi?uwanjani/barabarani?
Lini?juzi/leo
Kiasi gani? Mara saba /mara nyingi
Alitembea polepole akielekea shuleni.
T                      E               T               E
Alimnyemelea kipaka akamwangusha  pa!
 T                         E         T                        E
5. Viwakilishi
Ni maneno yanayotumiwa kama kibadala cha nomino.
Mifano
          A                                            B
    Seth ni mrefu,                      yeye ni mrefu./Yule ni mrefu/mimi ni mrefu..
    Kitabu kimepotea                hicho kimepotea./kimepotea.  
   Nairobi inapendeza             inapendeza./pale panapendeza/kule kunapendeza.
Tanbihi- maneno yaliyopigwa mstari upande wa B ndiyo viwakilishi.

6.Vihisishi{I}
Maneno yanoonyesha hisia.kwa mfano hisia za
Mshangao,furaha mshtuko ama za  amri
Hoyee! Tumeshinda!(furaha}
I
Lo! Kumbe alikuwa mwizi!{mshtuko}
I
7.Vihusishi{H}
Ni maneno yanayoonyesha uhusiano kati ya maneno.
Uhusiano huu unaweza kuwa wa mahali, wakati,kiwango au hali
Mifano
Maria ametembea
Mifano
Maria ametembea  hadi shuleni.
Gari limekwama  kando ya barabara,
Kuna mechi kati ya ManU na Arsenal.
Mifano ya vihusishi
Nje ya           karibu na           juu ya            ubavuni mwa         mvunguni mwa      chini ya         kati ya
Kutoka           mbele ya   usoni mwa        katika

8. Viunganishi{U}
Ni maneno yanayounga maneno,vifungu vya maneno, au sentensi.
Mifano
                           
kaka              kaka au dada
Dada            kaka ama dada
                    Kaka na  dada
                                        Baba anacheka  ilhali mama anaimba.
Baba anacheka.            Baba anacheka  naye mama anaimba.
Mama anaimba.           Baba anacheka huku mama anaimba.

Hukunpa chai               hukunipa chai wala maziwa
Hukunipa maziwa    


 Vivumishi
Ni maneno yanayoharifu kuhusu nomino au kiwakilishi
Aina za vivumishi
v.sifa             v.idadi             v.vimilikishi               v.vionyeshi/viashiria   v.majina
v. vya pekee        v.a-unganifu          v.virejeshi               v.viashiria vya kusisitiza       vi.viulizi
vivumishi vya idadi
hutaja idadi ya nomino husika . vipo vya aina mbili kuu;
vivumishi vya idadi maalum
vivumishi vya idadi jumla
mifano   mili,nane,saba,tisa                                                          wachache,wengi
                        nne, tano         idadi maalum                                baadhi                      idadi jumla
katika kuhesabu idadi 1,2,3,4,5 na 8 huambishwa lakini 6,7,9 na 10 haziambishwi.
Mifano katika matumizi
Ng’ombe mmoja amechinjwa.                      Madaftari matatu yameletwa.
Vitabu tisa vimepotea.                                  Ng’ombe saba wamenunuliwa.
Ni wagonjwa wachache waliotibiwa.           Magari mengi hayafai.
b)vivumishi viulizi
i.-pi?
hutumika katika umoja na wingi. Huambishwa viambishi ngeli.huhitaji kutambuliwa nomino kwa sifa zake.
NGELI
UMOJA
WINGI
A-WA
Yupi?
Wapi/wepi
KI-VI
Kipi?
Vipi?
I-ZI
Ipi?
Zipi?
Pa
                                  Papi?
Ku
                                  Kupi?
Mu
                                  Mupi?
ya
Yapi?
Yapi?
U-ZI
Upi?
Zipi?
LI-YA
Lipi?
Yapi?

Tanbihi: lazima itumiwe na alama za kulizia.
matumizi
Kiti kipi? Kimevunjika?
Gari lipi? Limebingirika?
Maji yapi? Yamemwagika?
ii.ngapi
hutumiwa katika wingi pekee, huambishwa,huhitaji idadi.
Matumizi
Watu wangapi wamefika?               Magari mangapi yameharibika?          
Vitabu vingapi vimepotea?           Migomba mingapi imeanguka?
iii.gani
hakiambishwi!
Hutumika katika umoja na wingi
Nyumba gani imeteketea?-  Nyumba gani zimeteketea?
Gari gani limeharibika?    - magari gani yameharibika?
Maji gani yamemwagika?-  Maji gani yamemwagika?
c).vivumishi majina/nomino
ni majina ambayo hutumiwa kuvumisha majina.
Mifano
Batamzinga amechinjwa.                 Askarikanzu walimnasa.      Mama mzee ana mkongojo.
Watoto maskini wamelipiwa karo.     Mwanamke mlevi haheshimiwi.  
Mama mzazi alinitembelea shuleni.
d).vivumishi viashiria /vionyeshi
hujitokeza katika sura tatu; karibu,mbali kiasi, mbali
                        matumizi
Mtoto huyu analia.          Kisu hiki ni butu.           Ukuta ule unajengwa.    Jiko lile ni la nani?
Kusema huko ni kuzuri.  Mahali hapa ni pangu.

  1. Vivumishi viashiria vya kusisitiza/kuthibitisha
Hutumiwa kutilia mkazo /kusisitiza juu ya nomino iliyotajwa.
Vya karibu
A-wa        yuyu huyu                PO      papa hapa           I-ZI       ii hii
                          Wawa hawa                                                                   zizi hizi
Vya mbali kiasi
Muundo wake huwa ni kiambishi ngeli na kirejeshi
LI-YA   li+lo=lilo       (hilo /hayo)          U-ZI          u+o=uo          (huo/hizo)    U-I  u+o=uo
             Ya+yo=yayo                                                 zi+zo+zizo                                i+yo=iyo
Vya mbali
Viashiria vya mbali huradidiwa
KI-VI                    kile   kile                     I   ile       ile           YA    yale yale       MU mle mle
                             Vile   vile
Matumizi
Gari lili hili ndilo liliibwa.                  Magari yaya haya ndiyo yaliibwa.
Amependezwa na weupe uu huu.        Wamependezwa na nyeupe zizi hizi.
Kitambaa kile kile ndicho kilipotea.     Vitambaa vile vile ndivyo vilipotea.
Mtoto atayanywa maziwa yayo hayo.   Watoto watayanywa maziwa yayo hayo
  1. Vivumishi vimilikishi
Ni vivumishi vinavyoleta dhana ya kuwa na .Hubadilika kutegemea nafasi na hali ya umoja /wingi
Nafsi                   umoja           wingi
1                          -angu           -etu
2                          -ako            -enu
3                           -ake            -ao
                Sentensi
Mtoto wangu amepita mtihani.           Watoto wetu wamepita mitihani.

  1. Vivumishi vya sifa
Ni maneno yanayoeleza tabia au jinsi nomino ilivyo auinavyoonekana. Huweza kuonyesha pia umbo la nomino au hali ya nomino.
Mifano;
Mzigo niliobeba ni mzito.     Mwanamke mnene amepita.
 Umeshindwakutatua jambo rahisi hilo.
Pana vivumishi vya sifa ambavyo huongezewa viambishi tofauti tofauti kutegemea ngeli inayohusika.mifano;
-embamba             -refu              -fupi             -zuri      -baya              -eusi           -ekundu
-eupe                      -nene             -bovu           -kali       -kubwa           -zito
Aidha pana vivumishi vya sifa ambavyo haviongezwi viambishi ngeli katika ngeli zote;
             Safi                          hodari          ghali            stadi       nadhifu             dhaifu
              Duni                        jasiri            rahisi
  1. Vivumishi vya a-unganifu
Huonyesha hali ya umilikaji ,yaani kuna uhusiano wa nomino moja nay a pili.
Mfano;  mtoto wa mama.
Hapa pana uhusiano baina ya mama na mtoto ,yaani mama anammiliki mtoto.
Jino la pembe si jino.      Meno ya pembe si meno.
Njia ya mkato haifai.       Njia za mkato hazifai.
Mahali pa Juma ni hapa.
Mwahali mwa Juma nihumu.
Kwahali kwa Juma ni huku.
  1. Vivumishi vya pekee
Huitwa vivumishi vya pekee kwa sababu ;
  1. Kila kimoja huwa na matumizi mengine ya pekee zaidi ya kuwa vivumishi ya nomino.huleta maana ya kipekee
  2. Kila moja kina sheria za pekee katika upatanisho wa kisarufi. Vivumishi vya pekee ni hivi; -enye,-enyewe, -ote,-o-ote,-ingine na –ingineo

  1. –enye     huonyesha dhana ya umiliki wa mali,tabia,sifa,hali au cheo.
              Huambishwa ,matumizi
           Mwanafunzi mwenye ukoma ameanguka.{hali}
            Nyumba yenye kuteketea ni yetu.{sifa}
               Meneja mwenyekiti amewasili. {cheo}
              Tajiri mwenye shamba ameondoka.{umiliki}
              Askari mwenye ukora amepatikana.{tabia}
Tanbihi :  -ennye ikifuatiwa na kitenzi ,sharti hicho kitenzi kiambishwe ‘ku’
Mfano  mtoto mwenye kucheza ameondoka.          Nyumba yenye kuteketea ni yetu.

  1. –enyewe  
Hutumiwa kusisitiza/kutilia mkazo
Huambishwa
Mfanyikazi mwenyewe alikuwa mvivu.            Sikio lenyewe lilikuwa linauma.
  1. –ote
Huleta maana ya ujumla yaani kuhusika kwa jambo au kitu kikamilifu.
Mifano
Mti wote umekatwa.          Kuchora kwote kulikuwa bure.
Shambani mote mlijaa.
  1. –o-ote
Huonyesha kutochagua au kutobagua.
Huambishwa.
Chakula chochote kitanifaa ila sumu.
Ukuta wowote wenye ufa utabomoka.
  1. –ingine
Huambiswa
Huleta maana ya ,sehemu ya,baadhi ya{ziada} au tofauti na.mifano
i.uteo mwingine unahitajika.{ziada}
ii.sikihitaji kitabu hiki nipe kingine.{tofauti na }
iii. wanafunzi wengine hawajawasili.{baadhi ya}
iv. pahali pengine pameharibika.{sehemu ya}
  1. –ingineo
Huleta maana ya ziada
Mna ufa humu na mwingineo umo ukutani.{ziada}
Alipata ndimi za ng’ombe katika duka hili na zinginezo akapata kwenye duka lingine.
  1. Vivumishi virejeshi
Ni viwili;
-o-rejeshi     na amba- rejeshi
Vivumishi hivi hutumiwa kurejelea nomino iliyotajwa katika hali ya umoja na wingi.
Amba-rejeshi huambishwa viambishi tamati pekee.
‘o’-rejeshi hutumika kama kiambishi awali hali kadhalika kama kiambishi tamati.Ikitumika kama kiambishi tamati huleta maana ya desturi/mazoea.
Mifano ya matumizi

Mtu ambaye anasifika ni huyu.             Watu ambao wanasifika ni hawa.
Kalamu iliyonunuliwa imepotea.           Kalamu zilizonunuliwa zimepotea.
Kalamu inunuliwayo hupotea.               Kalamu zinunuliwazo hupotea.



Vitenzi(T)
Kitenzi ni nenolinalodhihirisha jambo linalotendwa au kutendewa nomino.
Aina za vitenzi;
T.halisi       T.vikuu         T.visaidizi        T.vishirikishi      T.sambamba

  1. Vitenzi halisi
Kitenzi halisi hudhihirisha kitendo mahususi katika sentensi. Aghalabu vitenzi halisi huchukua viambishi awali na viambishi tamati.
Mifano katika sentensi;
       Mimi ninalima shamba langu.       Sisi tunalima shamba letu.           
       Kikulacho ki nguoni mwako .       vimlavyo vi nguoni mwenu.
       Fumbo mfumbie mjinga.               Nimenunua samaki sokoni.
  1. Vitenzi vikuu
Kitenzi kikuu ni kiarifu kinachobeba maana kuu ya sentensi . Huwezakujitokeza ikiwa sentensi ina vitenzi vingine.Aidha kitenzi kikuu huweza kutambulishwa kwa kiambishi awali ku-  mifano;
Anapenda kusoma.                           Babake atampeleka kusajiliwa shuleni.
                 T.kikuu                                          T.halisi         T.kikuu
Babake atampeleka shuleni.      Nilijaribu kumhimiza asome kwa bidii.
           T.halisi/kuu                        T.halisi     T.kikuu
Walijaribu kufanya kazi hiyo kwa bidii kubwa.
    T.halisi      T’kikuu
     c.     vitenzi visaidizi
kitenzi kisaidizi    ni kitenzi ambacho huandamana na kitenzi kikuu katika sentensi. Kawaida hutangulia kitenzi kikuu .Huchukua viambishi awali vya nafsi,wakati,virejeshi na vinginevyo,lakini havichukui viambishi tamati.
mifano
viambishi
T.kisaidizi
T.kikuu
Kitenzi halisi
A-li-
weza
kusoma
alipoamka
Tu-me-
kwisha
wasili

A-me-
kuja
kutuzuru
tunapoishi
I-li-
bidi
tusome

Wa-li-
kwenda
kutembea
tulipofika
Tu-na-
enda
kucheza

Ni-li
wahi
kufika
ankokutaja
Ku-
ngali
kunanyesha

Ya-
pasa
tufike

Tu-li-
pata
kufika
alikotuelekeza
Ali-
taka
kutongoza
akakataa

Vitenzi hivi hudhihirisha sifa au hali inayorejelewa katika sentensi. Vitenzi visaidizi aghalabu huunda vitenzi vishirikishi.
  1. Vitenzi vishirikishi
Ni ya aina mbili:
  1.  Vitenzi vishirikishi vipungufu
  2. Vitenzi vishirikishi vikamilifu
      Vitenzi vishirikishi vikamilifu huchukua viambishi vya nafsi na viwakilishi vya wakati. Ni          
        sawa na vitenzi visaidizi..
     Vitenzi vishirikishi vipungufu huwa havina viambishi vya wakati .vinachukua viwakilishi   
       Vya nafsi ama viambishi ngeli.
       Mifano :
  1. ndi
Ndi+yeye=ndiye                  ndi+wao=ndio           ndi+sisi=ndisi        ndi+wewe=ndiwe
Ndi+nyinyi=ndinyi               ndi+mimi=ndimi
Sentensi
Wewe ndiwe msemaji wetu.        Sisi ndisi tuliyempiga yeye.        Sisi ndisi tuliompiga ninyi.    
  1. Ni/si
Wewe ni msemaji wetu           Maria ambaye ni msichana mrefu amenichekesha.
  1. Viambishi ngeli
Vitabu vi juu ya meza.      Soksi zi sandukuni mwangu.           Mwalimu yu darasani.
  1. Vitenzi sambamba
Matumizi ya vitenzi viwili huwa pamoja ili kutoa maana moja kamili ya kutupatia muundo wa vitenzi sambamba.Muundo unaweza kuwa vitenzi visaidizi na vitenzi halisi au vikuu, mifano.
Amekuwa akiimba.           Sijaenda kumtembealea tangu atoke marekani.
Tumeweza kuona picha ya rais wetu.
Amekwisha kusoma  kitabu hicho mara tatu.

VIWAKILISHI
Ni neno linalotumiwa kama kibadala cha nomino katika sentensi.
Aina za viwakilishi;
  1. Viwakilishi vya nafsi
Ni vya aina mbili;
  1. Viwakilishi nafsi huru
Nafsi
                umoja
                wingi

huru
tegemezi
huru
tegemezi
1
mimi
Ni-
sisi
Tu-
2
wewe
u-
ninyi
m-
3
yeye
a-
wao
Wa-
  1. Viwakilishi nafsi tegemezi/ ambata


Sentensi
Anacheza uwanjani.             Wanafinyanga viungo.       Sisi tunasoma.
  1. Viwakilishi vya ngeli
Hurejelea ngeli katika tungo.(sentensi)
ngeli
viwakilishi
matumizi
KI
Ki
Chake kimepotea.
VI
Vi
Vyao vimepotea.
U
U
Wake umepotea
ZI
Zi
Zao zimepotea.
LI
Li
Limeharibika
YA
ya
yameharibika
  1. Viwakilishi vya pekee
Ni sita;
-enye         -enyewe         -ingine       -ingineo        -ote      -o-ote
(i)  –enye
Huonyesha sifa .
Huonyesha umiliki
Huonyesha cheo/hali
Mifano
Mwenye macho haambiwi tazama.
Mwenye nguvu mpishe.
Penye nia pana njia.
Penye budi hubidi.
Mwenye pupa hadiriki kula tamu.
(ii)  -enyewe
Hutmiwa kusisitiza.           
Chenyewe kimepotea.           Yenyewe yamemwagika
Mwenyewe anakula.              Penyewe pametoboka.
(iii)  -ote
Huonyesha ujumla(ujumla wa kitu)
Mifano
Wote wamekaribia.          Yote yamemwagika.       Sote tumefika .
Nyote mmekaribishwa.





Matumizi ya ‘po’
  1. Huonyesha mahali maalum/ pahali panapodhihirika.
Matumizi
Anapoenda hapafai.             Alipo si pake.
  1. Huonyesha wakati
  1. Wakati hasa /hususan/maalum
Anapolia nahuzunika.               Walipoondoka tulifurahi.
Tulipofika hatukuwapata.
  1. Mazoea/desturi
Waondokapo sisi hufurahi.         Tufikapo huwa hatuwapati.
Aliapo    huhuzunika.
  1. ‘po’ ya o-rejeshi
Lazima ihusishwe na ngeli ya pahali {maalum}
Mfano
Panapopendeza ni pale.      Paliponivutia ni Ushelisheli.
Palipolimwa hapafai.
NOMINO(N) JINA
Ni neno linalotaja mtu,kitu,jambo Fulani,mahali,mnyama n.k
       AINA ZA NOMINO
  1. Nomino maalum/pekee
  2. Nomino za kawaida
  3. Nomino za jamii
  4. Nomino za wingi
  5. Nomino za dhahania
  6. Vitenzi nomino/vitenzi jina
  1. Nomino za pekee/maalum
Ni nomino za vitu watu walio na maumbile tafauti, yaani majina husika yana upekee yake.
Hutaja kitu kwa kutambulisha waziwazi kwa jina au majina yake kamili.
    Aina za nomino za pekee
  1. Majina ya watu; Ethel,Amoth,Embo,Shadi,Seth,Joy
  2. Majina ya miezi : Oktoba, Februari ,Septemba
  3. Majina ya siku; Jumapili, Alhamisi, Ijumaa
  4. Majina ya mahali: Nairobi,kisumu, Narok
  5. Majina ya masomo;Kiswahili,Sayansi,Fizikia,Kifaransa
  6. Majina ya milima: Mlima Kenya ,Mlima Elgon,Mlima Longonot,Kilimanjaro
  7. Majina ya mito na maziwa;      
Mito;nzoia ,nile.tana,Zambezi,
Ziwa ;Victoria,Magadi,Nakuru
  1. Nomino za vitabu,magazeti,majalada na machapisho k.m Kiswahili Kitukuzwe,Chemchemi za Kiswahili,Bibilia Takatifu,Kamusi ya Kiswahili sanifu,Taifa leo.
  1. Nomino za kawaida/nomino  jumla
Hutaja kitu bila kutambulisha katika jina halisi.
Aghalabu hupatikana katika umoja na wingi k.m ;baiskeli,kalamu,kiti,dawati,sabuni ,mti,chupi,soksi,nguo,karatasi,darasa,mlango,tai,suruali,kiatu,sweta,sakafu,dirisha,chaki,ukuta,paa n.k
  1. Nomino za dhahania.
ni nomino zinazotaja hali,sifa ama matendo ya watu .Ni nomino za kufikirika tu,ni vitu/hali visivyoonekani wala kushikika. Mifano-uhai, utu,ujinga,werevu,hekima,ugonjwa,sauti,uchoyo,wema,wovu,uhodari,njaa,shibe,utamu,upole,ukali,usanii,ufisadi,upendo,uzee,ujana,utoto,ulemavu,uzima,uzembe,majaliwa,
harufu,hewa n.k
  1. Nomino za jamii/makundi
Hutaja vikundi kadha vya viumbe ama vitu .Nomino moja huwa hutaja jumuiya ya vitu vyenye sifa moja.Nomino hizi hazirejelei kitu kimoja bali hurejelea kundi la watu au vitu.
Mifano
Darasa la wanafunzi           bunge la wanasiasa            kicha cha funguo    bunda la noti
Mlolongo wa magari          msafara wa ngamia            thurea ya nyota       tita la kuni
Kikosi cha wanajeshi         kikikosi cha askari              bunda la ngozi/karatasi/magazeti Safu ya mlima                    baraza la wazee                   robota la pamba
Mkunga wa ndizi                shungi la nywele                 jozi  la viatu/soksi/karata/glavu
Kilinge cha wachawi         kilinge cha waganga            umati wa watu
  1. Nomino za wingi
Nomino hizi haziwezi kuhesabika wala kugawika katka umoja ama wingi. Hatuwezi kizitenga katika vitengo vya hesabu bali hubaki katika hali moja tu.
Mifano
Maji             machozi           maziwa         mate            sharubati        sukari        mchanga
Uji                chai                  chumvi         wino            damu             soda           moshi  
Mafuta         marashi             unga              manukato  
  1. Vitenzi nomino/majina
Ni nomino ziundwazo kutokana na vitenzi. Huwa na umbo la kitenzi lakini hutumika kama nomino.
Kuimba kwa Juliani kulituvutia.
Kulala kwa mtoto kumenitia wasiwasi.
Kustaafu mapema kunatatiza.



                                         VIELEZI
Vielezi ni maneno yanayoharifu kuhusu kitenzi,kivumishi ama kielezi kingine. Mifano,
Anatembea polepole.
Maria ni mrembo sana.
Alilima vizuri sana
Aina za vielezi
  1. Vielezi vya namna/jinsi.
Ni vya aina sita hivi:
 Vielezi namna viigizi      vielezi namna ala/vitumizi      vielezi namna vikariri
 Vielezi namna mfanano  vielezi namna hali                   vielezi namna halisi
  • Vielezi vya namna ala/kitumizi
Huonyesha kifaa au ala iliyotumika kufanikisha kitendo ,aidha hutambulishwa kwa mtumizi ya ‘kwa’ namna kwa ala ama kitumizi kutajwa.
                          Mifano
              Amekata nyama kwa msumeno.
              Zamani watu walienda Ulaya kwa meli.
              Majambazi waliotuvami kwa bunduki wametiwa mbaroni.
  • Vielezi vya namna viigizi
Hivi hutoka kwenye tanakali za sauti. Hufuatiliza sauti za vitendo vinavyotendeka. Mifano;
Mawe yalibingiria bingiri bingiri toka mlimani.
Amemaliza chakula chote fyu!
Alianguka tifu! Mchangani.
Alilia kwi kwi kwi baada ya kupata viboko vitatu.
  • Vielezi namna vikariri
Hutokana na kielezi kimoja kurudiwa kwenye sentensi.
Mifano
Ametembea harakaharaka.
Njoo taratibu taratibu.
Aliondoka upesi upesi.
  • Vielezi vya namna mfanano
Hutumiwa kulinganisha /kufananisha aghalabu uhusisha nomino za kawaida.Mizizi ya nomino husika huambishwa ‘ki’ mwanzoni.
Mifano;
Ki                    mzizi
Ki         +         paka  -  kipaka
Ki          +       sungurakisungura
Ki        +         tausi   -    kitausi
Ki         +         levi    -    kilevi
Matumizi ;
Amina ameondoka kinjiwa.           *   Amina ana miondoko ya kinjiwa.{v.sifa}
Simpendi kwa kula kifisi.                   Alimnyemelea panya kipaka kwa kigongo.
                             E.mfanano                                                E.mfanano    E.ala
  • Vielezi vya namna hali
Huonyesha kitendo kilitendeka katika hali Fulani.
Mifano katika sentensi.
Alitoka mbio .                          waliimba vizuri.                   Alitembea taratibu.
Alimkaribisha kiungwana.        Ameyasema kinaganaga.
  • Vielezi vya namna halisi.
Ni maneno ambayo awali ya yote hujitokeza kama vielezi.m.f
Asali ni tamu mno.                     Barabara imenyooka bar’abara.    
Awi  anampenda Risper sana.    Anapenda kutembea ovyo.
  • Vielezi vya wakati
Huarifu wakati wa kutukia kwa jambo.Huweza kujitokeza katika sura mbalimbali kama vile;
  1. Majina katika siku ;asubuhi ,alfajiri,jogoo la pili na jogoo la kwanza,macheo/matlai/mashariki,mafungulia ng’ombe,adhuhuri,alasiri,jioni,machweo,mchana,isha,usiku mkuu,usiku wa manane
  2. Majira katika juma; jumatatu [jana], Jumanne[leo], Jumatano[kesho],alhamisi[kesho kutwa] Ijumaa[mtondo],Jumamosi[mtondogoo] Jumapili[juzi/kitojo]
  3. Majira katika mwaka;
Masika – majira ya mvua nyingi za mfululizo katika ukanda karibu na ukweta.
Kupupwe-majira ya baridi yanayotokea katika miezi ya Juni,Julai na Agosti katika Afrika ya mashariki.
Vuli-majira ya mvua ngogondogo ambazo huja wakati pepo za kaskazini zianzapo kuvuma.
Kiangazi-majira ya mwaka wakati jua jua linapokuwa kali baina ya vuli na masika.
Mapukutiko-msimu baada ya majira ya kiangazi ambapo majani hunyauka na kuanguka na matunda yakawa .
Machipukpo-msimu baada ya kipupwe ambapo miti huotesha upya na majani na maua yakaanza kuchipuka.
Kusi-wakati katika mwaka ambao katika Afrika ya mashariki upepo huvuma  kutokea kusini aghalabu kati ya Aprili.
Mchoo-majira ya mvua ndogondogo kati ya Julai na Oktoba katika Afrika ya mashariki.
Kaskazi-msimu wa upepo unaovuma kutoka kaskazini kuelekea kusini na wenye joto hasa katika uwanda wa pwani.
  1. Majira katika miaka.
Mwaka wa 2010
Mwaka wa 1994
Mifano katika sentensi
Tutaondoka kesho kutwa na tutarejea mwakani.
Nilizawa mwaka wa 1900
Paka alikunywa maziwa yetu jana.
Waliofika leo ni wanafunzi.
  • Vielezi kiasi{idadi}
Hutuarifu kuhusu viwango vya utukiaji wa jambo. Jamno laweza tukia mara moja au mara kadha.
Vielezi kiasi ni vya aina mbili;
-Vielezi kiasi maalum
-Vielezi kiasi jumla
Mifano katika sentensi.
Aliimba mara tatu jana asubuhi.
Amenitembelea tena.
Nyumba hii imekarabatiwa upya.
Sanasana anachoweza ni kuua mende.
  • Vielezi vya mahali
Hutuharifu kuhusu mahali kitendo hutukia.Huweza kujitokeza kama viambishi ama maneno kamili. M.f
Alienda huko jana.                      Nitarudi sokoni.                  Alimo mnapendeza.
Alijitosa katika mto yala jana.     Ametoka kwa Embo.

                                

Maoni 40 :

  1. Seriously, I want it to be like this;
    Synonymous of words in kiswahili. Main thing to be kiswahili

    JibuFuta
    Majibu
    1. Tumefurahishwa na maoni yako japo hujaeleweka vizuri.

      Futa
    2. Chaganua haya,mtoto huyu mzuri ameandika kwa hati safi

      Futa
  2. Asante kwa kazi nzuri, tafadhari jitahidi kuweka marejeleo.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Shukrani sana kwa wazo hili nzuri, marejeleo ya kazi hii tayari inachapishwa.

      Futa
  3. NIMEIPENDA KAZI.
    LAKINI VIPI KWA SHULE ZA MSINGI WANAKOJIFUNZA AINA SABA ZA MANENO BADALA YA NANE?

    JibuFuta
  4. Kiswahili kitukuzwe kabisa

    JibuFuta
  5. Asante Sana kazi nzuri hiii

    JibuFuta
  6. Siku njema😘😘💜👄💜

    JibuFuta
  7. asante kwa kazi nzuri imenisaidia

    JibuFuta
  8. Asante kiswahili kitafika pazuri

    JibuFuta
  9. Asante kwa maelekezo mazur ya aina za maneno ila vipi kuhusu solo
    la njeo?

    JibuFuta
  10. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  11. Kazi safi naipenda bali umelisahai marejeleo

    JibuFuta
  12. okiutred vuiredsw piysaun redswaw buytirew viizwi mookewsa

    JibuFuta
  13. Kazi nzuri hongereni sana

    JibuFuta
  14. Jibya no Aina gani za maneno mwalimu?

    JibuFuta
  15. Kazi nzuri nimeipenda nimejifunza zaidi

    JibuFuta
  16. Hongereni ninyi mliokusanya mafunzo haya

    JibuFuta
  17. Nivizuli na inafundisha thanks to you 😘😘😘😘😘

    JibuFuta
  18. Yule anaitwa mwajuma Paulo Marko .neno Marko ni aina gani ya neno

    JibuFuta
  19. Asante sana kazi nzuri hii

    JibuFuta
  20. Sasa mnaweza kunipa mambo ya kuthibitisha sentensi

    JibuFuta
  21. Kiswahili ni lugha yetu sote watanzania,💓💚💚💚💯

    JibuFuta
  22. Bainisha Sina za maneno katika mvu inanyesha Sana leo

    JibuFuta
  23. Kiswahili kitukuzwe aina za nomino

    JibuFuta
  24. Kazi kuntu kabisa

    JibuFuta
  25. Hongera kwq.kazi nzuri lakin pia umebainisha aina nane za maneno Kwa KIGEZO.cha kisintaksia changamoto.yake.ni.kwqmba kuna.baadhi.ya maneno yanai gia kwenye kategoria mbili hivyo ni vyema kubainisha aina.za maneno Kwa kuzingatia vigezo viwili pamoja yaani kigeO.cha kimofosintaksia
    Ambapo tunapata aina 9 kwqsababu kivumishi kina sifa Moja tu.ya kutoa sifa ya nomino au kiwakiliahi.hivyo kategoria.ya kibainishi I aingia hapo
    Kibainishi huonesha ukomo wa nomino.

    JibuFuta
  26. ASANTENI WAKWASI WA LUGHA HII

    JibuFuta
  27. Asante saana Kwa kazi nzuri watafiti

    JibuFuta