Jumatano, 24 Mei 2017

MUKHUTASARI

KUANDIKA MUKHTASARI
Mukhtasari hutoa maelezo makuu kwa ufupi huku ukidumisha kiini cha habari au taarifa.
Ni njia ya kuwasilisha hoja kuu na muhimu katika taarifa.
Umuhimu wa mukhtasari
Humsaidia mtu kusema  mambo  mengi kwa wakati mfupi bila kupoteza maana yake kuu.
Husaidia kujua jinsi ya kuandika kumbukumbu, matangazo mbalimbali kama vile ya kifo,biashara,ripoti, barua n.k
Husaidia kupunguza muda ambao mtu anautumia katika kusema vifungu au habari Fulani.
Hukuza stadi za kuweza kuelewa na kueleza taarifa ulioisoma kwa njia rahisi na fupi.
hatua za usomaji na uandishi wa mukhtasari
  • soma kifungu ulichopewa na kwa makini na uangalifu .
  • ipitie tena ukiyadondoa mawazo makuu.
  • Andika nakala ya kwanza au nakala chafu ukitaja mawazo makuu kwa vidokezo.viunganishi vya aina mbalimbali kama vile; yaani,na,ili,kwa vile na alama za kuakifisha hutumika ili kuunganisha mawazo makuu.
  • Usitumie mfano ,tamathali za usemi au maelezo ya kujaliza na kuyafafanua.
  • Linganisha hoja zako na swali uliloulizwa.
  • Hakikisha ya kwamba hakuna hoja muhimu zilizoachwa.
  • Usitumie maelezo mengi pale ambapo neno moja lingefaa kwa mfano;
Badala ya kusema ‘ Yule mtoto aliugua ule ugonjwa wa watoto unaofanana na kifafa’  unaweza kusema  ‘aliugua degedege’
  • Chunguza ikiwa maneno yamezidi ama yamepunguka kulingana na maaizo uliyopewa, ikiwa yamezidi ,tafuta njia ya kuondoa maneno au hoja zisizo na uzito ama umuhimu.
  • Hakikisha kwamba kila kitu kiko sawa kisha andika nakala safi.
  • Hakikisha kuwa maneno yameendelezwa vizuri kwa mtiririko mzuri, hakuna  makosa ya sarufi au ya kuakifisha.
  • Jumla ya maneno katika ufupisho hayapaswi kuzidi au kupungua maneno matano.
  • Andika jumla ya maneno uliyoyatumia katika ufupisho.

Maoni 1 :