UUNDAJI WA MANENO
Maneno ya Kiswahili huweza kuundwa katika njia mbalimbali, kwa mfano; nomino inaweza kuundwa kutoka kwa nomino nyingine au hata kivumishi, aidha tunaweza kuunda nomino kutokana na vitenzi.
- Uundaji wa nomino kutokana na vitenzi.
Katika kuunda nomino kutokana na vitenzi, viambishi mbalimbali hutumika.Viambishi hivi hutokea mwanzoni au mwishoni wa mzizi wa kitenzi kwa vyovyote vile mzizi lazima idumishwe.
Mifano ;
Vitenzi
|
nomino
|
l.a
|
Mlo,chakula,mlaji,mlafi,ulaji,ulafi
|
f.a
|
Mfu,kifo,ufu,maafa,ufuo
|
p.a
|
Mpaji,kipaji,kipawa
|
Pw.a
|
Pwani
|
Ny.a
|
Kinyesi,manyunyu
|
Nyw.a
|
Kinywaji,kinywa,mnywaji,unywaji
|
Ch.a
|
Uchao,macheo,mchana
|
Chw.a
|
Machweo
|
Kimbi.a
|
Mbio ,mkimbizi,mkimbiaji,ukimbizi,ukimbiaji
|
Hukum.u
|
Mhukumiwa,mahakama,hekima,hukumu,hakimu
|
Tembe.a
|
Mtembezi,matembezi,utembezi/utembeaji
|
Lip.a
|
Malipo,ulipaji
|
Lind.a
|
Mlinzi,ulindaji,ulinzi
|
Hukum.u
|
Hadimu,mhudumu,uhadimu,huduma
|
Andik.a
|
Maandishi,maandiko,mwandindishi,uandishi
|
Chor.a
|
Mchoraji,mchoro,uchoraji
|
Ogop.a
|
Mwoga ,woga
|
Oko.a
|
Mwokozi,wokovu,mwokovu,mkoaji
|
Takat.a
|
Mtakatifu ,utakatifu,mtakaso
|
Sem.a
|
Msemaji,usemaji,usemi
|
Simam.a
|
Usimamo,msimamizi,usimamizi
|
Lim.a
|
Mkulima,ukulima,kilimo
|
Chek.a
|
Mcheshi,ucheshi,kicheko
|
li.a
|
Mlio,kilio,mluzi,mlizi
|
Chez.a
|
Mchezo,mchezaji,uchezaji
|
Imb.a
|
Wimbo,mwimbaji,uimbaji
|
Matumizi
Tulicheza vizuri sana ndipo timu yetu ikashinda.
T T
Ushindi wa timu yetu ilitokana na uchezaji mzuri.
N N
Jaji amemhukumu miaka minne gerezani.
Jaji ametoa hukumu ya kifungo cha miaka minne.wazazi hupata furaha kutokana na na utiifu mtoto.
Mtoto mwenye utiifu huwapa wazazi furaha.
Farasi aliyenona hawezi kukimbia.
Farasi mwenye unono hawezi mbio.
Mbio humshinda farasi mwenye unono.
Unono wa farasi humzuia kukimbia mbio.
- Uundaji nomino kutokana na nomino
nomino
|
nomino
|
mtu
|
Utu
|
Rafiki
|
Urafiki
|
Riziki
|
Ruzuku
|
Tabibu
|
Utabibu,tiba,matibabu/utibabu
|
Utungo
|
Mtunzi,utunzi
|
Mpenzi
|
Mapenzi,upendo,pendo
|
shujaa
|
Ushujaa
|
Elimu
|
Mwalimu,ualimu,alimu
|
kilimo
|
Mkulima ,ukulima
|
Mhadhiri
|
Uhadhiri,mhadhara,hadhira
|
siasa
|
mwanasiasa
|
salama
|
usalama
|
jengo
|
Mjenzi, ujenzi
|
- Kuunganisha nomino na nomino nyingine kuunda nomino ambatano
Nomino+nomino=nomino
Mja+mzito=mjamzito
Mwana+siasa=mwanasiasa
Mwana+hewa=mwanahewa
Mcha+Mungu=mchaMungu
Mwana+nchi=mwananchi
Miti+shamba=mitishamba
- Kuunganisha mikato ya nomino
Upungufu wa kinga mwilini-ukimwi
Chakula cha jiooni – chajio
Teknolojia ya habari na mawasiliano –teknohama
- Kuunganisha kitenzi na nomino
Vunja +jungu=vunjajungu pima+maji=pimamaji
Pima+joto=pimajoto pima+mvua=pimamvua
- nomino kutokana na kivumishi
kivumishi
|
nomino
|
kitenzi
|
-refu
|
urefu
|
Refusha/refuka
|
-fupi
|
Ufupi
|
Fupisha/fupika
|
-eusi
|
weusi
|
©
|
-ekundu
|
wekundu
|
©
|
-erevu
|
werevu
|
erevusha
|
Matmizi
Werevu wake ulimsaidia. Ufupi wa Zakayo haukumfaa.
Hadhira ya watu imewasili. Mhadhiri wetu amesafiri.
Fupisha kamba hiyo ili ikufae. Ufupi wa kamba hiyo itakufaa.
ni nzuri
JibuFutaKongele,,,,, vyema sana
JibuFutaPerfect
JibuFutaukweli
Futahili kipindi ni kizuri
Futahili kipindi ni kizuri
FutaSanaa katika kitenzi ni
JibuFutaSanaa
FutaSifa kutokana na neno sali ni
JibuFutaAdimika kitenzi yake ni gani
JibuFutaKitenzi kutokana na kivumishi karimu ni?
JibuFutaKarimu kitenzi ni
FutaFitina
FutaUnda vitenzi kutokana na nomino zifuatazo;
JibuFutaa) Hakimu
b) Fitina
c) Funza
d) Ulezi
Kindly assist
Hukumu fitna funza lea
FutaUnda kielezi kutokana na: 'enda'..tafadhali mbiombio🙏🙏
JibuFutaChapisho hili limeondolewa na msimamizi wa blogu.
JibuFutakivumishi cha ule zi
JibuFutaKivumishi kutokana na kitenzi
JibuFutaUjuzi
JibuFutaKitenzi Cha mlinzi
JibuFuta