Dhana ya lugha
Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na ambazo zimekubaliwa na jamii ya
watu Fulani zitumike katika mawasiliano.
Sauti huunda silabi ,silabi huunda maneno ambazo huunda sentensi.hata hivyo maneno mengi
katika lugha ya Kiswahili huwa ya kinasibu tu na hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya
kiashiria na kiashiriwa. Kwa mfano hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kifaa kalamu na
neno kalamu.
Fikra huathiri lugha lakini lugha haiji kabla ya fikra.
DHIMA YA LUGHA
Dhima kuu ya lugha ni kuwasiliana na kupasha habari. Mawasiliano yote si lugha.lugha ni
sehemu ya utamaduni wa watu ambao huweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Ni chombo cha kuelimisha na kutoa elimu kwa mtoto anapozaliwa.anaweza kufundishwa
maadili ya kijamii kupitia kwa lugha.
Lugha hutumiwa kutatua migogoro na vita za kijamii .
Ni chombo cha kuendeleza taaluma aina nyingi kama vile: elimu, sheria
ukulima,teknolojia,utawala,siasa,sayansi nk
Lugha huleta maendeleo duniani kupitia mawasiliano ambayo huwapa watu uwezo wa
kubadilishana mawazo .hivyo watu huanzisha miradi aina aina na kuinua uchumi wao binafsi,wa
jamii na hata nchi zao kwa jumla.
UMUHIMU WA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA MAWASILIANO
Imekubaliwa kuwa lugha ya taifa ya Kenya. Takriban wakenya wote hujitambulisha kwa njia
moja au nyingine kwa lugha ya Kiswahili.
Hukuza uzalendo kwa wakenya.
Ni kielelezo cha utamaduni ya wakenya.
Husaidia katika kuwashirikisha wananchi katika shughuli za kijamii,kisiasa na maendeleo.
Huwezeha wakenya kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya taifa na jamii.
SAUTI ZA KISWAHILI
Ni za aina mbili;
1. Vokali/irabu
2. konsonanti
Vokali/irabu
Ni tano nazo ni /a/ ,/e/ ,/i/, /o/ , /u/
Vigezo vya kuanisha irabu
Tunatumia vigezo vitatu vifuatavyo:
sehemu ya ulimi
Hurejelea sehemu ya ulimi inayotumika katika utamkaji wa irabu itatumia. Hutumia
sehemu ya mbele, kati , na nyuma
hali ya mwinuko
hali ya mwinuko wa ulimi
Ikiwa sehemu ya ulimi inayohusika inainuliwa juu , irabu inayotolewa huitwa irabu ya juu .ikiwa sehemu husika I chini itaitwa irabu ya chini.
*hali ya midomo
Hurejelea hali ya midomo kwa mfano /o/ na /u/ zinapotamkwa mdomo huwa imefutuka na yenye msimamo wa mviringo ambapo /e/ na /i/ zinapotamkwa midomo huwa ni tandazi.
Sifa bainifu za irabu
/a/ +irabu
+ulimi chini
+ulimi kati
+midomo tandazi
/u/ +irabu
+ulimi nyuma
+mdomo mviringo
/e/ + irabu
+mdomo tandazi
+ulimi kati
+ulimi mbele
konsonanti za Kiswahili ni;
/k/, /ch/, /d/, /dh/,/f/, /g/, /gh/,/h/,kh/,/j/, /b/, /l/, /m/, /n/,/ny/, /ng/,/nj/ ./nd/ ,/mb/ ,/p/, /r/, /s/, /sh/, /t/,/th/, /v/,/w/, /y/ na /z/
VIGEZO VYA KUAINISHA KONSONANTI
Tutazingatia:
*Namna ya utamkaji
*mahali pa kutamkia
*mghuno/msepetuko
1. Namna ya utamkaji
kwa kutumia kigezo hiki konsonanti huainishwa hivi
a)vipasuo/vikatizwaji
b)vikwamizo/viendelezwaji
c)kitambaza/likuidi
d)kimadende
e)nazali/ving’ong;o
f)viyeyuso/nusu irabu
vipasuo/vikatizwaji
Ni sauti zinazotoka wakati hewa inapozuiliwa kabisa ambapo ala husika hubanana au kufunga kabisa ule mpenyo wa hewa kisha kufunguliwa na kuachilia hewa kwa ghafla.
Huo ukatizwaji wa hewa huwa ni wa kwa muda mfupi tu.sauti hizi ni ;
/b/,/d/, /g/ (ghuna)
/p/,/t/ ,/k/, /ch/(hafifu}
Vikwamizo/viendelezwaji
Wakati wa kutamka konsonanti hizi ala sogezi n a ala pahala huwa zimekaribiana(kukwaruzana) na kufanya mpenyo finyu hivyo hewa huachiliwa kwa utaratibu Fulani. Mifano ni
/s/,/f/,/th/ na /h/ (hafifu)
/z/,/v/, /dh/./gh/,/j/ (ghuna)
Kitambaza/likwidi
Hutamkwa wakati ncha ya ulimi imetambaa juu ya ufizi . mzungumzaji anaweza kuitamka kwakuilaza ncha ya ulimi ufizini lakini awe hajaifunga hewa yote na baadhi ya hewa iwe imeachiliwa itoke kwenye pande za ulimi .mfano ni /l/
Kimadende
Konsonanti hii inapotamkwa ncha ya ulimi hugota ufizi. Sauti hii ni /r/
*konsonanti /r/ na /l/ pia huitwa vilainisho
Nazali/ving’ong’o
Ni sauti ambazo wakati wa kutamkwa baadhi ya hewa hupitia kwenye pua.mifano ni /ng/, /ng’/,/n/,/ny/ ,/nd/,/nj/,/mb/
Viyeyuso/nusu irabu
Ni konsonanti ambazo hutamkaji wake hukaribia ule wa vokali za juu pamoja na za chini.
Irabu za juu ni /i/ na /u/
Irabu za chini ni /a/ hivyo basi
/i/+/a/= /y/
/u/+/a/=/w/
Viyeyuso ni konsonanti /w/ na /y/
Tanbihi konsonanti /ch/ pia huitwa kizuio -kwamizo.hii ni kutokana na kuwa na sifa za vipasuo na vikwamizo kwa wakati moja.pia huitwa kipasuo kwamizo.
2.Mahali pa kutamkia
a) vimdomo chini –meno juu
hutamkwa kutokana na msogeano kati ya mdomo ya chini na meno ya juu. Mifano /f/ na /v/
b)vimdomo
hutamkwa kutokana na mbanano kati yam domo wa chini na ule wa juu mifano ni /p/,/b/,/m/,/mb/
c)viulimi ncha- kati meno
hutamkwa kutokana na mbananao ama msogeano kati ya ncha ya ulimi na meno ya juu na chini mifano/th/ na /dh/
d)viulimi ncha-ufizi juu
hutamkwa kutokana na mbanano au msogeano kati ya ncha ya ulimi na ufizi wa meno ya juu
mifano /t/,/n/,/s/ ,/nd/,/d/,/l/,/z/,/d/na/r/
e) viulimikati burutio gumu
hutamkwa kutokana na mbanano au msogeano kati ya ulimi na burutio gumu.
Konsonanti hizi ni;/k/, /ch/, /nj/ /j/ /y/
f)viulimi nyuma burutio laini
hutamkwa kutokana na mbanano au msogeano kati ya sehemu ya nyuma ya ulimi na burutio laini. Mifanoni /g/,/gh/,/ng/,/ng’/
g) kiglota
hutamkwa kwenye koromeo . mfano ni /h/
3.mghuno/ msepetuko
Ni mrindimo (mtetemeko) wa nyuzi za sauti pale zinapokumbana na mkondohewa.
Konsonsnti ghuna ni zile ambazo zinapotamkwa ,hewa ina.
Konsonsnti ghuna ni zile ambazo zinapotamkwa ,hewa inaotoka mapafuni huzitetemesha nyuzi za sauti na kuzua mrindimo wa kuhisiwa.
Konsonanti ghuna ni kama /b/, /d/, /g/, /j/, /v/ ,/dh/ ,/mb/ ,/nd/, /j/, /ng,/, /m,/ /n/, /ny/, /v/, /z/ na /sh/
Konsonanti hafifu/sighuna ni kama /p/, /t/ /k/, /ch/, /f/,/th/ na / s/
marejeleo
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Sauti /j/ na /CH/ ni vizuio-kwamizo
JibuFuta/J/ na /CH/ ni vizuio-kwamizo kwakuwa zinapotamkwa ala husika hugusana kisha hewa huzuiliwa kwa muda mfupi na kuachiliwa polepole
FutaAsante nime jifunza mengi
JibuFutaasante nimejifunza mengi
FutaIrabu ilitoka katika nchi gani.
JibuFutaHivi ukitaka kutoa tofauti kati ya konsonanti na irabu unaelezea kwa kuanza upande mmoja tu na umalizie na mwingne au unabainisha kwa kutoa paoint koja moja
JibuFutaYaa
Futa