Jumatano, 24 Mei 2017

ISIMU JAMII

                ISIMU JAMII

Isimu jamii ni taaluma inayochunguza matumizi ya lugha katika mazingira/mikatadha mbalimbali.
Katika jumuiya ya watu /jamii, matumizi ya lugha hutofautiana kutegemea mahali inamotumiwa. Mfano mazungumzo sokani ni tofauti nay a darasa au shuleni.
Matangazo ya mpira nayo hutofautiana na mahubiri kanisani. Haya mazingira tofauti pia huitwa miktadha/muktadha. {sajili au rejesta}

  1. Sajili ya hotelini ama mkahawani
Hoteli ni jengo mnamouzwa vyakula na vinywaji.
   Sifa  
-Wahusika wakuu huwa wawili: hadimu na mteja
-hadimu{mtumishi} aghalabu atatumia lugha yenye upole ,adabu na   unyenyekevu ili kumrai mteja apate huduma ndipo atoe pesa zake.
-wakati Fulani, wateja wateja huonyesha ujeuri katika mazungumzo yao.
-msamiati wa hotelini hutaja vyakula, vinywaji pamoja na bei yao.
-kuna kauli ya kuulizana maswali na hata kujibizana
-sentensi huwa fupifupi,kwani hakuna maelezo marefu yanayohitajika.
Kuna matumizi ya viziada lugha katika mawasiliano.

  1. Mazungumzo dukani
-Hutumia lugha ya kibiashara.
 Pana matumizi ya msamiati na istilahi maalum kama vile:
  mteja/mnunuzi.mwuzaji, mwenye duka,bidhaa,pesa.
-matumizi ya sentensi fupifupi ili mteja na mwuzaji wasichoshane kwa
  Maelezo marefu.pia pana wateja wengine na pana haja ya kuwapisha.sarufi
  Huenda isizingatiwe sana bora mawasiliano.  Mfano;
    Nataka sabuni, hii miti, majan majan.
-majibizano/mvutano huzuka ili kupana bei au ubora wa bidhaa. Mvutano
  Huu unaweza kuhusisha lugha ya kushawishi.
 -Matumizi ya mafumbo yanayoeleweka tu na mteja na muuzaji ili pawepo
     Siri ujumbe usifahamike na wateja wengine.
-matumizi ya methali, misemo na misimu inayohusiana na biashara na ya
Kuzoa mvuto ama ukaribu kati ya muuzaji na mteja.mfano;
Bei kupanda ,bei kushuka,kuteremka kwa bei,biashara haikomi.
-kuchanganya ndimi ili kuwanasa wateja wote na kuwaonyesha ukaribu ili
 Waweze kununua kwa muuzaji .
-inaweza kuhusisha matangazo kwa sauti au maandishi ya kubandikwa
 Ukutani au katika mabango.
Aidha matangazo haya huweza kuchukuana na muziki.
                        Mfano wa tathmini
Mtu I : umetumana?
Mtu II: ndiyo.
Sauti :nani ng’ombe
Mtu I:huyu hapa choma bwana.
Sauti :(kwa mtu II) wewe mbuzi au ng’ombe?
Mtu II:mimi ng’ombe
Mtu III:mbuzi mimi
Maswali
Hii ni sajili gani (alama1)
Toa ushaidi wa jibu lako(alama 1)
Toa sifa zote tano zinazohusishwa na sajili hii (alama 5)
Toa viziada lugha ambayo hutumika katika uwanja huu wa mazungumzo.(alama 3)
Ni sajili ya hoteli.pana matumizi ya misamiati wa vyakula kama vile ng’ombe(nyama ya ng’ombe),wahusika wanaojibizana ni hadimu na mteja
  1. Sajili ya maabadini
  • Maabadi ni mahali ambapo wahumini hukusanya kwa shughuli za kumwabudu Mungu .Kanisani ,Msikitini,Hekaluni au mahali maalum. Palipotengwa kwa mfano uwanjani chini ya miti n.k
Hupatikana katika vitabu vya dini {misahafu} kama vile Bibilia. Kurani, vitabu vya mafunzo na masimumizi ya kidini, ibada ,mahubiri na mijadala ya kidini.
Msamiati wa kawaida huwakilisha maana za kidini zinazofasili uhusiano bora wa watu na Mungu au miungu kwa upande mmoja na uhusiano adilifu wa waumini wenyewe.
Baadhi ya maana na sifa ambazo zinatumika sana ni ;
  • Mungu – ni muumba wa dunia na mbingu
  • Wokovu-ni usalama utakaodumu milele
  • Mbinguni-ni kule kwema ahera
  • Dhambi-ni kosa la kirohoPana matumizi mengi ya maneno ya kikale yaani msamiati uliopokezwa kutoka kizazi hadi kingine kwa sababu ya kuhifadhi ujumbe kama ulivyotolewa katika maandishi au mawasiliano ya asili, aidha waumini uhisi kuwa mabadiliko ya lugha utabadilika ujumbe ulivyotolewa katika maandishi ya asili.
‘Ibrahimu akamjua Sara wakapata mwana.’
  • Pana  msamiati maalum kutegemea dini . msamiati mgumu hautumiwi kwa sababu utazua ufahamu kwa mfano ;
Mwanakondoo shetani ashindwe, bwana asifiwe,jehanamu/ahera,ibilisi/shetani , allahu akbar!,wokovu.
Tanbihi : dini mbalimbali hutumia misamiati yao ya kipekee .huwezi kuchanganya msamiati wa uislamu na ukristo kwa mfano .
  • Kudondoa/ kunukuu kutoka katika misahafu; mhubiri atafanya hivi ili kusisitiza au kuthibitisha mambo anayoyasoma.huku  ni kuonyesha kuwa anayoyasema si yake bali ni ya watu wengine wenye ataha zaidi.Aidha, maandishi huonyesha kauli kama zilivyosemwa na Mungu, Mitume,Malaika na hata shetani.
  • Aghalabu huwa ni lugha ya msisimko hasa kasisi anapowahubiria wahumini{jazba /jadhba}
  • Pana matumizi ya sentensi ndefu katika mahubiri.
  • Pana uradidi/takriri-maneno aghalabu hurudiwa ili kuonyesha utukufu,wema na uwezo wa Mungu na ukarimu wake kwa waja.
  • Matumizi ya miondoko,ishara  pamoja na kusimama, kupiga magoti, kuruka ruka, kusifu n.k
  • Maelezo katika sajili huwa na wingi wa masimulizi yenye mafumbo na vielelezo.Dhamira zake kubwa ni tatu; kuelimisha, kushawishi na kuwagiza.
  • Ni lugha yenye heshima na upole, upendo na undugu.
  • Ina mvuto na mshawishi kwa wapokezi.
  • Ina maneno yenye asili ya kigeni ambayo hujitokeza kama majina ya wahusika, macheo au matukio ya zamani.
  1. Lugha ya majambazi/sajili ya wizi
  • Ni lugha ya vitisho kwa wahasiriwa .
  • Hutumia sentensi fupifupi kwa sababu ya uhaba wa wakati wa kutoa maelezo zaidi.
  • Haina heshima ila matusi na utovu wa adabu
  • Huchanganya ndimi na aghalabu haina usanifu wa lugha.
  1. Lugha ya magazeti
Magazeti ni machapisho yanayotoa habari na makala mengine kila siku, juma au kila mwezi.
Yapo magazeti ya kitaifa, kimkoa, kidini, ya shule , ya mashirika ya kitaifa n.k.
                              Sifa
  • Hugawanywa katika kurasa na safu kutegemea mambo Fulani k.v habari motomoto za mikoani, za uliumwengu, za kisiasa n.k. Kurasa hizi huwa kwenye karatasi zinazogawanywa kurasa mbili kila upande , hivyo karatasi moja huwa na kurasa nne.idadi ya kurasa hutegemea aina ya gazeti.Kurasa huwa na safu kwanzia tatu hadi tano au zaidi.kila safu hutengewa makala maalum.
  • Hujumuisha tahariri, barua kwa mhariri, matangazo ,makala maalum,michezo , burudani n.k
          Vitengo kwenye magazeti
  1. Habari za kitaifa
Msomaji huweza kujihusisha na matukio yenyewe kwa sababu mazingira yanayozungumziwa yanaeleweka .Aidha mambo mengi yaliyomo si mageni sana.
Vianzo vya habari za kitaifa ni matukio.navyo habari hizi aghalabu huwa zina ukweli.Lugha inayotumiwa huwa rasmi ama lugha ya taifa.Majina ya waandishi wa taarifa hizi hutajwa.
  1. Habari za kimataifa .
Habari hizi zinahusu matukio nje ya nchi(barani au kwingineko)
Mazingira ya habari hizi huenda yakawa ni mageni sana kwa kuwa huenda hatuna mwao nazo.
Vianzo vya habari za kimataifa vinaweza kuwa vya mashirika mbalimbali kama vile reuters na associated press {AP}
Aghalabu huwa si rahisi kwa msomaji kujihusisha na matukio yaliyomo.
Taarifa ama habari hizi huwa na usahihi.
  1. Ripoti za michezo
Ripoti hizi hutumia msamiati maalum unaohusishwa na uwanja wa michezo, vichwa vya habari hizi huwa na mnato mkubwa sana.
Lugha huwa imejaa matumizi ya chuku.
Vichwa vya habari ama ripoti huwa na mnato mkubwa.
Huweza kuwa na maelezo yaliyochanganywa na lugha nyingine.
  1. Matangazo ya tanzia
  2. Taariri
  3. Barua kwa mhariri
  4. Matangazo yz nafasi za kazi
  5. Burudani {mafumbo}
   Vichwa kwenye habari
Vichwa vya habari huwa vifupi vifupi ,wazi na vya kuvutia. Wakati mwingine huwa ni vichwa vya kushtusha .Aidha huweza kuwa na utata kwa mfano”mjukuu aoa nyanya”
Vichwa huandikwa hivi ili kuteka na kushikilia shauku ya msomaji, makala yakiwa marefu hugawanywa katika mafungu madogomadogo yanayopewa vichwa kwa nia hiyo hiyo.
  1. Mazungumzo hospitalini
Hospitali ni pahali pa kupata tiba kwa maradhi mbalimbali na ikibidi mgonjwa hulazwa.
Zahanati ni kituo kidogo cha afya cha kuwashughulikia wagonjwa na aghalabu wagonjwa hutibiwa na kurejea nyumbani.
Mara nyingi mazungumzo huwa ni kwa lugha ya taifa au lugha rasmi. Ikibidi , lugha hutegemea itakachotumiwa na pakiwa na lazima pakaletwa mkalimani.
Ni lugha yenye matumaini kwa mgonjwa ,jamaa na hata marafiki.
Ni lugha ya upendo , upole,heshima na maliwazo nz hisio na utani.


Maoni 13 :