Jumatano, 24 Mei 2017

UAKIFISHI


      UAKIFISHI
Lengo kuu la lugha ni kuwasiliana ,mawasiliano haya  yanapaswa kueleweka moja kwa moja bila kuzua utatanishi wowote.
Mawasiliano yanaweza kutokea kwa njia mbili; kwa mazungumzo au kwenye maandishi.Njia hizi mbili hutumia mbinu tofauti kwa mfano katika maongezi tuna uhuru mwingi wa kujieleza ,maneno kutoka kwa mfululizo kana kwamba yameshikana. Tunatua mara chache ,Aidha tunaweza kuteremsha ama kupandisha sauti ,kuchezesha miguu,macho,vidole, kutembea tembea nakadhalika.haya hufanyika kwa urahisi bila kutajika kwa juhudi zozote kutoka kwa wazungumzaji.
Kwa upande mwingine lugha ya maandishi haina uhuru kama huo.ili kufanya maandishi yaeleweke inatubidi kutumia mbinu tofauti .kwanza inatubidi kuacha nafasi iliyo wazi kutenganisha neno moja na nyingine kwa kufanya hivi maandishi husomeka kwa urahisi.
Pili inatubidi kutumia alama za kuakifisha . hii ni kwa sababu tunadhamiria maandishi yetu yawafikie wasomaji yakiwa na maana ile ile tuliyokusuhusia.
Ili kupata ustadi wa kuandika , ni muhimu kufahamu jinsi kutumia alama za kuakifisha.kuna alama mbalimbali za kuakifisha;
            Herufi  kubwa[ H]
hutumiwa mwanzoni mwa sentensi.
      Mifano
Kuku huyu ni wangu.
Mwanzoni wa mshororo wa ubeti wa shairi
Mfano
Vazi jema kivaliwa,huongeza heshima,
Staha mtu akapewa,pote endapo daima,
Mavazi duni si sawa, kina dada ninasema,
Mavazi rekebisheni,usherati umezidi,
Hutumika mwanzoni mwa nomino za pekee;
Kahawa ,Kifaransa ,Jumatatu,Krismasi ,septemba,
Nomino za vitabu
Magazeti   majarida               
Hekaya Za Abnuasi
Nomino za dini.
Ukristo            Uislamu           
Nomino za filamu
The Ten Commandments.
The Ten Plagues
Majina ya mito ,milima,maziwa,mabonde; Everest,Nile,Bonde la ufa.

             Nukta/kitone/kikomo/kituo kikuu (.)
Hutumika mwishoni mwa mwa sentensi .mifano
Jana nilienda msikitini.
Tutaondoka asubuhi.
Hutumika kuandika maneno kwa kifupi.kwa mfano
S.L.P (sanduku la posta)
Hutumika kutenga fedha  shilingi na senti
5.40(shilingi tano na senti arubaini)
10.50(shilingi kumi na senti hamsini)
Hutumika katika herufi ndogo(i) na (j)
                  mabano/parandesi/vifungo  (  )
Huonyesha maneno yasiyo ya lazima katikausemi. Mfano
Akija (ingawa sina matumaini) mwonyeshe kwangu.
Baba yangu mdogo(ni mtu mkaidi kweli ) alifika kutoka Nairobi.
Huonyesha nambari au herufi .mifano (i),(c),(2)
Huonyesha mambo ya ziada mifano
Vyombo vya kupikia (sufuria,visu na vijiko) vitahitajika kesho.
Hutumika sana katika mawasiliano ya kitamthilia kutoa maelezo kwa waigizaji.
      Mfano
Mama:(anaita)  Shadi! Shadi
Shadi  : yes memsahib.(anakuja mbio.
Mama: tazama ile cabbage kama inawika.
Shadi: yes Memsahib.(anaondoka)
Mama: na …….
(Ebrahim Hussein 1971 mashetani)

          Ritifaa/ Kibainisho (‘)
Hutumika kutofautisha sauti /ng’/ na /ng/
   Ngoma ile inang’ang’aniwa.
  Ng’ombe wote wanang’ang’aniwa.
Kuandika maneno kwa kifupi kwa mfano;
S’endi (sauti /i/ imetolewa)
‘shasema
Huonyesha iliyoachwa
Kwa mfano
Alifanya kazi kutoka 1968-199’.

          Mstari mshazari(/)
Hutmika kuonyesha kuwa maneno Fulani yana maana sawa
k.m ritifaa/kibainishi
    mwanadamu/nsi/mja
huonyesha ‘au’
km    wazee/vijana watahudhuria mkutano.
       Wawe wanawake/wanaume wana jukumu sawa.
Kuonyesha tarehe ama kumbukumbu
Tarehe 4/7/2017
Kumb.Na,Ab/11/C


           Kistari kifupi(-)
Kutenganisha silabi ili kuonyesha kuwa neno linaendelea  katika mstari wa pili, kwa mfano
Mama ana-                                 mama a-
Pika                                                  napika
Huonyesha silabi za neno .mifano
Ba-ba
Ku-ran
Kudokeza jambo kuhusu neno kama vile mzizi
Michezo
Uchezaji                    -chez-
mchezaji
kutenganisha maneno katika maneno ambatano.
Isimu-jamii
Elimu-viumbe
Kipima-joto
Nusu-kaputi
Kudumisha sauti.
Niliteleza mara moja chwa-a-a-a
    Sa-la-la-la
Hutumika katika tarakimu kuonyesha  mwanzo hadi mwisho wa habari.
Mwaka 1902-1997
Ukurasa 11-17
Nairobi –Thika

           Nukta za dukuduku (….)
Hutumika kuonyesha kuwa maelezo yanaendelea  kwa mfano.
Leo ni siku ya furaha kwa kuwa…
Kuonyesha maelezo yanatanguliwa na mengineambayo hayajaandikwa.
Mfano
…ingawa wote walijua wazi kuwa asiyekubali kushindwa si mshindani.
Huonyeshwa kukatizwa kwa usemi mfano
Mtoto: mama siendi…
Mama: nisikilize kwanza.
Mtoto:nimechoka nataka kupumzika …
Wakati wa kunukuu  dondoo , iwapo kuna maneno ambayo yameachwa , alama hizi hutumika kuonyesha hali hiyo.
Mwalimu alisimama akasema” mimi kama mwalimu mkuu wa shule hii …kwa hivyo ninawaonya mkome kutoka leo.”
                 Kupigia mstari   
Kutilia mkazo neno au fungu la maneno
Wazee walifika  saa moja  asubuhi.
Nilimwelekeza upande wa kushoto.
Hutumiwa kuonyesha anwani ya vitabu na majina ya machapisho mengine kama magazeti , majarida n.k
Kitabu kiitwacho  Kiswahili kitukuzwe kimenifunza mengi.
Magazeti ya Daily Nation Taifa Leo, East African Standard na majarida ya  Weekly Review  na Finance huchapishwa nchini Kenya .
Tanbihi;haifahi kupigia mstari maneno mengi zaidi kwani kufanya hivyo kutafanya maandishi yapoteze uzito uliokusudiwa.
                Nukta mbili{:}
Huweza kuandikwa kwa nukta mbili pekee au kama nukta mbili na kistari.{:-}
Matumizi
Kutenganisha saa na dakika.
saa        1:40 asubuhi.
Kuandika tarakimu maalum kama vile madondoo ya maandiko matakatifu , kutenganisha milango na mistari kwa mfano
Mwanzo 7:10-13
Mathayo 6:9-11
Hutumika katika maandishi ya kitamthilia.
Juma : habari yako rafiki?
Awi  : njema u hali gani?
Juma : njema rafiki.
Awi   : tukutane shuleni rafiki.
              Alama za mtajo/usemi {“  “}
Hutumika kudondoa maneno halisi yalivyosemwa au kuandikwa bila kugeuza chochote , mfano
Rais alisema,”mimi nitalinda katiba ya nchi yetu bila woga.”
Kuonyesha lugha ngeni
Tulipofika kisumu tulikaribishwa kwa chakula kiitwacho ”nyoyo.”
Mara nyingi binadamu anahitajika kutumia “common sense.”

Kuonyesha majina ya vitu kama vile filamu na makala.
Watoto walitoroka shuleni ili kujionea filamu ya “sixth day.”
Itokapo kuwa dondoo dogo linatokea ndani ya dondoo kuu, dondo lililo dogo hunukuliwa kwa alama moja moja(‘    ‘) na lile kuu  lile kuu huwa alama mbili mbili (“    “)
Mifano
“Mbona hukusema ‘jambo’ tulipokutana?” Martha aliniuliza.
                  Alama ya hisi {!}
Hutumiwa kuonyesha hisia za moyoni kama vile mshangao,furaha,huzuni, n.k
Mfano
Toka hapa mara moja!
Kumbe! Wewe ulikuwa kachero!
Alama hii isitumike pamoja na kikomo au koma.Hutumika pamoja na alama za mtajo na pia mabano.
                   Kiulizo {?}
Una pesa ngapi?
Si ninaona wewe ni mtu mzima?
Alama ikitumika pamoja na alama za mtajo ama mabano , ni sharti iandikwe ndani ya alama hizo .
Mfano
Nitampa pesa kidogo tu( si hata yeye anajua kuwa sina pesa?)
“Ilikuwaje mkafika kuchelewa ?” Nyanya alitufoka.
              Nukta na mkato /semi koloni(;}
Kutenganisha sehemu kuu ya sentensi .
Tulipofika nyumbani ; tulimkuta mama amelala kitini lazima alikuwa mgonjwa.,
Nitakwenda mapema sana; sitaki kuchelewa kama jana.
Alama hii haitumiki pamoja na  nukta ; nukta mbili, alama ya kulizia au ya hisi. Lakini huweza kutumika kwa mfuatano na alama za mtajo,mabano,au nukta za dukuduku.
                      Kinyota (*)
Huonyesha kuwa neno Fulani limeendelezwa vibaya.
*guludumu –gurudumu
*wanafunsi-wanafunzi
Aidha huonyesha kuwa sentensi Fulani ina makosa ya kisarufi au kitahajia
*nani amechukua viatu zangu,-nani amechukua viatu vyangu.
Huficha maneno yanayoelekea kukera ama kuudhi katika maandishi.
m.f          m***a wewe!
              M**i wewe!
Hutumika vitabuni na katika na katika magazeti ili kutoa maelezo zaidi kuhusu maandishi Fulani. Maelezo hayo hutolewa pembeni upande wa chini wa karatasi mfano
*Kaloo na *Denno kwa miaka mitatu sasa.wameishi Motoni kwa miaka kumi sasa.
                   Herufi nzito (H)
hutumika kusisitza ama kutilia mkazo maandishi ya aina mbalimbali mifano
baba na mama wameondoka.{mkazo kwenye nomino}
msichana mrembo  amevaa nguo maridadi {msisitizo katika vivumishi}

      Alama za mlazo  (MN)
hutumika kutilia mkazo maandishi mbalimbali
kwa mfano
kuku na bata  ni ndege wa kufugwa{msisitizo kwenye nomino}

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni