Alhamisi, 25 Mei 2017

MNYAMBULIKO WA VITENZI

MNYAMBULIKO WA VITENZI
Kunyambua ni kurefusha
Kunyambua kitenzi ni kukirefusha kwa kuvipa /kuviongeza viambishi katikati ya mzizi na viishio. Minyambuliko yote huanzia kwa vitenzi kuwa katika hali ya kawaida /hali ya kutenda /hali ya kufanya.
Mifano
Mzizi                 kiishio
Pig-                 a
Chez -              a
Lim-                 a
Kimbi-             a
Jinsi ya kunyambua vitenzi

Vitenzi hunyambuliwa katika jinsi mbalimbali ;
Kauli ya kutendea               kauli ya kutendatenda
Kauli ya kutendewa            kauli ya kutendama
Kauli ya kutendeka             kauli ya kutendata
Kauli ya kutendesha           kauli ya kutendua
Kauli ya kutendeshea         kauli ya kutenduka
Kauli ya kutendeshwa        kauli ya kutendana

Tanbihi ;si vitenzi vyote ambavyo hunyambuliwa katika hali zote.
Kawaida                  kutendea                       kutendesha
Pig.a                        pigia                              pigisha
Chez.a                     chezea                            chezesha
l.a                            lia                                   lisha
f.a                           fia                                   fisha
to.a                        tolea                                 toza
imb.a                    imbia                                imbisha
tembe.a                    tembelea                         tembeza
li.a                        lilia                                      liza
1.kauli ya kutenda/kufanya/kawaida
hivi ni vitenzi ambavyo havijaongezewa viambishi vyovyote vya tamati isipokuwa kiishio  -a.
kiishio –a si sehemu ya mzizi wa kitenzi kwa vile ni kawaida kwa vitenzi vya Kiswahili vyenye asili ya kibantu kuishia kwa herufi –a katika hali yakinishi.
Vitenzi hivi ndivyo msingi wa kunyambua vitenzi vyote.
Mifano
Tembe.a                 kop.a
Simam.a                 end.a
Chom.a                  twa.a
Shik.a                    kos.a
Ingi.a                     chap.a
2.kauli yakutendea/kufanyiwa
Kauli hii huwakilishwa kwa viambishi hivi;
-e-        -li-
-i-        -le-
Mifano
Kawaida                             kutendea
li.a                                        lilia
tembe.a                                tembelea
kos.a                                     koselea
end.a                                    endea
choma                                 chomea
chap.a                                  chapia
lal.a                                       lalia
l.a                                        lia
o.a                                       olea
kasirik.a                               kasirikia
to.a                                      tolea
sentensi
mtoto alimlilia mama.
Abdala amemlia mtoto chakula.
Amenipigia mpira.
Nalia mikono.
Babu anatembelea mkongojo.
Maelezo
Mtoto alilia kwa sababu pengine mama alimwacha, hakumnyonyesha, alitaka abebwe n.k
Msemaji ala kwa kutumia mikono.kauli hii hivyo basi hutumiwa kuonyesha jinsi au kifaa kinachotumiwa kutendea jambo.
Abdala amekula chakula badala ya mtoto kukila hicho chakula.
Amenipiga kwa kutumia mpira. {ala/kitumizi}
Amenipiga kwa sababu pengine nimeupoteza mpira wake,nimeutoboa n.k
Ameupiga mpira unielekee .{kunitolea pasi}
Ameupiga kwa niaba yangu vile pengine nina jeraha.
Mkongojo ni kifaa kinachomsaidia babu kutembea.
Aidha kauli hii huweza kuonyesha kuwa kitendo kilitendewa mahali Fulani. Mifano
Askari alimshikia uwanjani
Nilivalia nguo chumbani mwangu.
Serikali iliwazuilia mateka wapi?
3 kauli ya kutendwa na kutendewa
Kauli hizi huwakilishwa na viambishi hivi;
-ew-                    -lew-                -liw-
-w-

                     Mifano ya vitenzi

vitenzi
kutendwa
kutendewa
Chez.a
chezwa
Chezewa
Imb.a
imbwa
Imbiwa
Lim.a
limwa
Limiwa
f.a
©
Fiwa
l.a
©
Liwa
Ch.a
©
Chiwa/chewa
j.a
©
Jiwa
Chw.a
©
Chwewa
Chor.a
chorwa
Chorewa
Tobo.a
©
Tobolewa
Chom.a
chomwa
Chomewa
Kat.a
katwa
Katiwa
Le.a
©
Lelewa
Bomo.a
©
Bomolewa
Pak.a
pakwa
Pakiwa
Anguk.a
©
Angukiwa

Kauli hizi huonyesha;
Kwamba kitu Fulani kimetendewa kitendo na kimeathirika moja kwa moja.
Watoto waliimbiwa wimbo mzuri na mwalimu wao.-wimbo mzuri uliimbwa na mwalimu kwa watoto.
Ukuta unapakwa rangi ya kijani kibichi.
3.Kauli ya kutendesha/ kufanyisha.
Huonyesha kuwa kitendo kimesababishwa na mtu au kitu Fulani.
Ina viambishi mbalimbali;
-esh-          -ish-              -lesh-                 -lish-                       -sh-           -ez-          -iz-
-lez-           -liz-              -fy-                    -vy-                          -s-               -z-      


Mifano
Cheza  -    chezesha            ruka     -       rusha                         ig.a     -   igiza
Lima    -     limisha              takat.a    -    takas.a                       tok.a  -      tokeza
Pon.a   -        ponya               ogop.a   -    ogofya                      lew.a       -levya
Shuk.a     - shusha                 tikita       -tikisa                            toroka     -torosha
Kos.a       -kosesha                shuka   -    shusha                        chemk.a  -     chemsha
Va.a     -visha                       wez.a         -wezesha
Sentensi
Dereva aliwashusha abiria kituoni.
Simba huwaogofya watu wengi.
Dawa za kulevya zimewaathiri vijana.
Nguo zimefuliwa na sasa zinatakasa.
4.kauli ya kutendeka /kufanyika
Huonyesha; a) kuwa kitendo kimetendeka na kimetimilika bila kuonyesha mtendi wake au kilichohusika .
Mfano    kikombe kimevunjika.
Haijulikani mtu aliyekivunja wala kitu kilichokivunja kikombe.
b)uwezekano wa mtu/ kitu Fulani kupatwa na tukio fulani katika hali ya uyakinisho.
Mfano,  machungwa haya yanalika.
Maana ni kuwa kuna uwezekano wa kuyala machungwa hayo.
Viambishi vya kauli hii ni;
-ik-                 -lek-            -lik-              -ikan-


vitenzi
Kauli ya kutendeka
twaa
twalika
kaa
kalika
chukua
chukulika
vunja
vunjika
noa
noleka
pata
Patika/patikana
taka
Takika/takikana
kopa
Kopeka
tega
Tegeka
samehe
Sameheka
osha
Osheka
vaa
Valika
vua
Vulika

vitenzi
Kauli ya kutendeka
Funga
fungika
Fungua
funguka
Imba
imbika
Pita
pitika
Cheza
Chezeka
Lima
Limika
Pasua
Pasuka
Rarua
Raruka
Toa
Toka/toleka
Nyoa
Nyoleka
Ng’oa
Ng’oleka
Soma
someka
Nena
neneka
Tia
tilika





MATUMIZI
Nimemaliza kuutega mtego. (kawaida)
Mtego umetegeka.
Niliuosha mkoba wangu.{kawaida}
Mkoba uliosheka./mkoba wangu uliosheka.
Baba alivaa shati lake.{kawaida}
Shati lilivalika.
Mtoto  anataka maziwa.{maziwa yanatakikana}



5. kauli ya kutendana
Huleta maana kuwa mtu mmoja ametenda jambo kwa mwingine na huyo mwingine akatenda jambo hilo kwa aliyemtendea.
Kitenzi katika kauli hii lazima kihusishe mashiriki zaidi ya mmoja.huwakilishwa na –an-
Kitenzi
Kauli ya kutendana
Pig.a
pigana
Suk.a
sukana
Kut.a
kutana
On.a
onana
Vut.a
vutana
Teg.a
tegana

Sentensi
Simba na chui wanaogopana.
Mbabekazi na Kikubi wamezoea kubishana.
Sote tulielezana mikasa iliyotusibu.
Mnyamuliko wa vitenzi vyenye silabi moja
kitenzi
kutendea
kutendeka
kutendesha
kutendana
kutendewa
Ch.a
chea
©
©
©
chewa
Ch.a
chia
chika
chisha
chana
chiwa
f.a
fia
©
fisha
fana
fiwa
j.a
Ji.a
jika
©
©
jiwa
l.a
lia
lika
lisha
lana
liwa
p.a
pea
peka
pesha
pana
pewa
Ny.a
Nyia/nyea
©
nyesha
©
Nyiwa/nyewa
Nyw.a
nywea
nyweka
nywesha
©
nyewa
Pw.a
©
©
©
©
©
Pa.a
palia
palika
paza
©
paza
Pa.a
palia
palika
©
©
paza
Lal.a
lalia
lalika
laza
©
laliwa
w.a
wia
wika
wisha
©


Ch.a      chomoza kwa jua.
            Kuwa na woga.
Ny.a      enda haja kubwa
            Toa kitu cha majimaji ama nyauka .
w.a       tokea/tendeka/fanyika
pw.a     toka kwa maji ufuoni na kwenda mpaka sehenu ya mbali ya bahari.
f.a        tokwa na uhai /kata roho
           ishiwa na nguvu
          kupenda kupita kiasi
          kuwa katika hali ya kutoendelea
          kufikia mwisho
pa.a     ondoa mamba ya samaki
           enda juu
           chukua makaa kutoka kwenye jiko
                             Matumizi
mama ameyanywa maziwa ya mtoto.{kutenda}
maziwa ya mtoto yamenywewa na mama.{kutendewa}
mtoto amenywewa maziwa na mama.
Asifuye mvua imemnyea.
Mvua humnyea asifuye.
Mvua imekunya.
Huku kumenyeshewa sana.  
Mvua imenyesha sana.

Maoni 47 :

  1. Thanks so much for that

    JibuFuta
  2. na je ...hali ya kutendeshana

    JibuFuta
  3. asante kwa data lakini mbona kauli ya kutendwa na kutendewa umezichanganya fulan kwenye upande wa viambishi

    JibuFuta
  4. kuna kauli ya tendata? oshwa itakua nini tafadhali. Asante

    JibuFuta
    Majibu
    1. Hakuna kitu Kama hiyo

      Futa
  5. fya ni tu moja siwezani lakini asante

    JibuFuta
  6. nauliza kuwa hakuna kauli ya kufanyiza?

    JibuFuta
  7. otherwise it was really helpful

    JibuFuta
  8. Neno nawa katika kauli ya kutendesha

    JibuFuta
  9. Kauli ya kutendua naomb unitumie za neno Lia,suka,songa,pika,soma,Lima,imba,omba na cheza

    JibuFuta
  10. Na je,neno tia kauli ya kutendesha

    JibuFuta
  11. Nyambua tembea kwa Hali zote

    JibuFuta
  12. Sandakta kabisa! Kazi shwari.

    JibuFuta
  13. Merkur 23C Futur Double Edge Safety Razor - deccasino
    This Merkur 23C Futur Double Edge Safety Razor is an elegant, stylish 메리트카지노 and stylish razor 1xbet korean with an elegant looking handle. The finished product of this  Rating: 4.3 rb88 · ‎19 reviews · ‎€69.50 · ‎In stock

    JibuFuta
  14. Nawa kwa tendwa

    JibuFuta
  15. Nahitaji kauli ya kutendata

    JibuFuta
  16. It was helpful thanks

    JibuFuta
  17. Very good work

    JibuFuta
  18. na hitaji kauli ya kutendeana

    JibuFuta
  19. Kazi nzuri,,,,,Tumia kitenzi wa kutunga sentensi katika kauli ya kutendeana

    JibuFuta
  20. Nimefaidika mno

    JibuFuta
  21. Toa kwa kauli ya kutendwa

    JibuFuta
  22. nyambua maneno haya katika kauli ya kutendeka la,lea na oa

    JibuFuta
  23. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

    JibuFuta
  24. this is very helpful it has helped me a lot

    JibuFuta
  25. Dadisi katika kauli ya kutendesha

    JibuFuta
  26. shukrani sana mdao uliongozwa na nadharia gani?

    JibuFuta