Jumatano, 24 Mei 2017

BAHARI YA MASHAIRI

BAHARI ZA MASHAIRI
  1. Utenzi  Utendi
Ndiyo mashairi marefu katika shairi, huwa na kina aghalabu huzungumzia maswala ya kihistoria , mashujaa ,mapenzi na mengineyo. Huwa na kipande kimoja tu. Idadi ya mizani katika kila mshororo huwa kati ya mizani nne na kumi na mbili .kina cha mshororo wa mwisho aghalabu huwa kilele katika beti zote nacho huitwa  kina bahari
       Mfano
Nakuita hima janabi,
Njoo katika ukumbi,
Unipeyo rambi rambi,
Ya hiki changu kilio,

Kilio changu muhubiri,
Nataka kukukatibu,
Kiwe katika vitabu,
Pamo na msaadao,
Mifano ya utenzi
Utenzi wa fumo liyongo         
 utenzi wa uhuru wa Kenya 
  1. Msuko
Ni shairi lenye kibwagizo kifupi.
Mfano  i

Mwajiona asumini, nanyi mmebahatika,
Na waridi vitaruni,mwahisi hamna shaka,
Pia viluwanmitini, nanyi mmeburudika,
Mtahizika!

Mfano  ii
Naomba kazi ni kazi,vyovyote vile iwavyo,
Madamu si ubazazi, kwa mwanadamu ndivyo,
Kushona na upagazi, piavile vyenginevyo,
Kazi ni kitu azizi,wala vyenginevyo sivyo,
Mtu hachagui kazi,

  1. Kikai
  • Ni shairi ambalo lina mizani michache katika kipande kimoja cha mshororo kuliko kingine,
  • Ni shairi ambalo asili yake ni mizani 12 katika vipande viwili, aidha huweza kuchukua mizani 10 hadi14. Mizani hii huweza kugawiwa katika mikondo mbalimbali   kama vile .
           Nne kwa tano           tatu kwa sita       tano kwa saba    n.k
Mfano

Moja kwa watatu, hugawika aje?
Mpe kila mtu , sawa wampaje?
Kigawanye kitu , wakigawanyaje?
Kisha twailaje?

  1. Msuko-kikai
Huwa na sifa za kikai lakini kibbwagizo kikawa kifupi{msuko}
      Mifano

Viwanda vile  vya nani, nitauliza,
Vitamba saini, kujipumbaza,
Maelezo si vitu,


Shule ajili ya nani, nitauliza,
Na ubingwa wa kichwani , unolemeza,
Kama wengi mwawahuni, nitatangaza,
Maendeleo si vitu,

8:5
8:5            kikai
8:5
8              msuko            

  1. Kikwamba
Ni shairi ambalo kwalo neno Fulani huradidiwa katika mazingira yaleyale.
Mfano

Pasha ni kuwa julisha, yaani pasha khabari,
Pasha ni kuwa kopesha mwenziyo ukikhiyori,
Pasha piya ni kanzisha,kitu kwa juwa na nari,
Pasha yane ni tahubiri,yaani pasha tohara,

Mfano 2
Wananambia, naharibu utu wangu,
Wananambia ,nalizika jina langu,
Wananambia, nakutaja siri zangu,
Bali wanashindwa , kuchungua kisa changu.
  1. Ngonjera
Ni shairi ambalo kwalo wahusika wawili au zaidi hujibizana ama kusemezana.
   Mfano
Mwanafunzi : mwalimu ni lako jina
                       la heshima na maana.
                       Shikamoo bwana,
                        Mwalimu nakuamkia.
                     Mwalimu : marahaba  mwema mwana,
               Uliyefunzwa kijana,
                   Uliomzuri kunena,
                   Kwa heshima na tabia.
  1. Malumbano
Ni mashairi yanayotungwa kwa minajili ya kujibizana au kusemezana kuhusu swala Fulani.kulumbana huku huwa ni katika mashairi mawili au zaidi tofati.
  1. Ukawafi
Ni shairi lenye vipande vitatu katika kila ubeti ; ukwapi, utao na mwandamizi.
Mfano

Umeanguka,inuka,simama kama mnazi ,
Umechunika, inuka,tia dawa kuwa ujuzi,
Sasa inuka, inuka, kijana,kijana ianze kazi,
Sikate tamaa,

Usife tama ,nyanyuka, ni mwenza wa kutenda,
Kuna hadaa, nyanyuka,anza tena kujipinda,
Dunia baa, nyanyuka, ama tena kujiunda,
Sikate tama,

Umbo
Shairi hili lina beti mbili,kila ubeti una mishororo minne. Mishororo mitatu ya awali  ina vipande vitatu vyenye mizani kumi na sita , kila mshororo umegawanywa katika mkondo wa tano kwa tatu kwa nane na hivyo kulifanya shairi la ukawafi.
Hata hivyo kibwagizo ni kifupi kwa kuwa na mizani sita hivyo kulifanya shairi  kuwa la msuko.
Katika ubeti wa kwanza ,utao unaradidiwa katika mishororo mitatu kwa neno ‘inuka’ na katika ubeti wa pili kwa neno nyanyuka.Hili likalifanya shairi liwe la kikwamba.
  1. Tumbuizo
Ni aina ya ukawafi kwa sababu ina vipande vitatu katika kila ubeti, hata hivyo , tumbuizoina upekee wake; huwa na mizani ishirini na nne katika kila mshororo uliogawanywa sawa katika mkondo wa nane kwa nane kwa nane

                   
Mfano


Binadamu hatosheki , ni kiumbe chenye zani,kweli mja hapendeki,
Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani ,la wazi ni unafiki,
Ukwelikweli haafiki ,njama zake  zi moyoni, usimwone ni rafiki,
Mtu akiwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka,

Wengine watakuua, wakiona una pesa, hata zikiwa kidogo,
Hizo kwao ni maua, hupupiwa zikatesa, wakizifuata nyago,
Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa,wala kukupa kisogo,
Mtu kumia na tama,akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
  1. Sakarani
Ni shairi lenye zaidi ya aina moja za mashairi au bahari za shairi.ni shairi linalofululiza mchanganyiko wa bahari kadha katika shairi moja.



  1. Ushairi wa abjadi
Ni shairi ambapo herufi ya kwanza ya kila mshororo  hufuata mpangilio wa kialfabeti. Penginepo fatahi ya kila ubeti hufuata utaratibu wa abjadi.
Mfano
Afadhali  kuyasema moyoni yalonijaa,
Pengine huisha salama,ikaepuka balaa
Mapenzi yana zahama, na nyinyi mna nazaa,

Bahari kuu jamani, ni bahari ya mahaba,
Upendapo kwa yakini, huyakosa matilaba,
Huna unacho tamani, kwa mambo yalokukaba,

Chungu pendo lilo kweli, hulali usiku kucha,
Hutamani wala huli, daima wauma kucha,
Kumbe huna akili,mahaba yanapochacha,

Dhiki yote waelewa,basi fanya jitihadi,
Hakika unapokawa, maradhi yatakuzidi,
Pendo ni sumu lalia, dhiki kwa yako fuadi,
  1. Pindu /unyoka/mkufu
Pia huitwa mkufu  .katika shairi hiki, vipande,mishororo au beti zake huanza kwa neno au maneno yaliyo mwishoni mwa utao wa mshororo unaotangulia.
              Mfano
Kulla aliyemwelewa,agahalabu hupongezwa,
Hupongezwa na kupawa, tunu bora ya kutuzwa,
Kutuzwa na kuambiwa , wana si wanapendezwa,
Mcheza kwao hutuzwa , au la kushangiliwa.
  1. Zivindo
Ni shairi ambalo kimpangilio huchukua sura sawa na kikwamba hata hivyo neno linalorudiwa rudiwa huwasilisha maana mbalimbali.
Mfano;
Mbuzi ni kifaa cha, kukunia  nazi
   

Mbuzi  ni mnyama,
   
  1. Mavue
Ni shairi lenye vipande vinne katika kila mshororo
Ukwapi                          utao                     mwandamizi                ukingo

               15 .  Taabili

    Ni shairi la kutilia mkazo kifo cha mtu Fulani.
    1. Msemele
    Ni shairi ambalo linawasilisha ujumbe kwa kutumia methali na mafumbo.
    1. Shairi guni  
    Ni shairi ambalo mtunzi amenuia kizingatia kanuni za ushairi lakini kikatokea upungufu au kasoro Fulani ambayo inawweza kubainika kupitia kwa vina,mizani,mishororo n,k
    1. Mandhuma
    Ni shairi ambalo kipande kimoja hutoa hoja,wazo ama swali huku kipande cha pili kikitoa jibu au suluhisho.
        Hoja/swali ____________________             
          jibu


    1. Sabilia
    Ni shairi lisilokuwa na kibwagizo{shairi ambalo mshororo wa mwisho haurudiwirudiwi.
    Istilahi za ushairi
    Ukwapi –kipande cha kwanza cha mshororo.
    Utao – kipande cha pili  cha mshororo
    Mwandamizi-kipande cha tatu cha mishororo
    Ukingo-kipande cha nne cha mshororo.
    Mshtata- ni mshororo usiokamilika
    Ubeti-ni kifungu cha mishororo kadha katika ushairi
    Mizani – ni siabi au vitamkwa katika kila mshororo wa shairi.
    Kifu- mshororo uliokamilika
    Utoshelezi-kila ubeti unahitajika kuwa na maana kamili inayojitsheleza au inayojisimamia bila kutegemea maana ya ubeti unaotangulia au unaofuata.ubeti uwe na mtiririko mzuri wa habari zinazoeleweka.
    Muwala-ni mtiririko wa mawazo na fani ulio na mantiki katika ushairi.
    Mawazo katika  kila ubeti yanapaswa kufuatana kwa ufasaha kutoka mwanzo{fatahi,molto, mleo hadi kituo ili kuyajenga mawazo kikamilifu
      Mtindo wa lugha-tashbihi,tashihisi,methali,misemo,istiara,idaa,mafumbo  ,chuku n.k
    Maudhui –ni jumla ya ujumbe na mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika shairi.
    Dhamira-ni lengo , madhumuni au nia aliyo nayo mshairi katika kuutungashairi lake.
    Nafsineni –ni msemaji katika shairi{sauti ya msemaji}
    Toni –ni hisia za nafsi  neni zinazoibuka kutokana na uteuzi wake wa maneno kwa mfano hisia za furaha,bezo/dharau,mapenzi,masikitiko huruma n.k
    MUUNDO/UMBO WA MASHAIRI
    Hurejelea muundo wan je wa mashairi
    Vipengele vifuatavyo huzingatiwa katika kueleza umbo ama muundo wa mashairi;
    • Beti-beti ngapi{idadi}
    • Idadi ya mishororo katika kila ubeti
    • Idadi ya vipande katika kila mishororo
    • Kituo{kimalizio ama kibwagizo}
    • Vina –zingati vina vya kati na vya mwisho
    • Idadi ya mizani
    Izingatiwe kwamba hivi vipengee sita ndivyo msingi wa arudhi.
                LUGHA YA NATHARI/TUTUMBI
    Pia huitwa lugha ya kawaida/mjazo/mfululizo
    Huku ni kuufasiri ubeti na kueleza kwa kutumia maneno ya kawaida. Yafuatayo huzingatiwa.
    • Mishororo hugeuka kuwa sentensi.
    • Ubeti huwa aya,
    • Mizani na vina huangaziwa.
    • Misamiati migumu huangaziwa
    • Vipande hutoweka
    • Lazima ujumbe udumishwe.
    • Hisia za mtunzi  zizingatiwe
    Kwa mfano  
    Mshairi/ mtunzi
    Anaonya …
    Anapongeza…
    Anasifu…
    Anakashifu …
    Anatoa tahadhari…
    Anakumbusha…
    Anashangazwa na…

    Maoni 50 :

    1. Asante sana kwa ujumbe huu

      JibuFuta
    2. Nauliza ikiwa Kituo sio kisawe change kimalizio?
      He nini maana ya Kinying'inya katika ushairi.

      JibuFuta
      Majibu
      1. Kimalizio ni mshororo wa mwisho kwa shairi;waweza ukawa kibwagizo aunkituo
        Kituo ni mshororo wa mwisho usiorudiwarudiwa...

        Futa
    3. nawahongera kwa kazi njema mnayotekeleza kwani mchezo mwema si kazu mbi.Heko !

      JibuFuta
    4. Asante sana nimejifunza mengi kweli

      JibuFuta
    5. Nini maana ya kituo bahari katika ushairi?

      JibuFuta
    6. Asante sana kwa matini haya yamenifaa .

      JibuFuta
    7. naomba jinsi ya kuhakiki vitabu vya mashairi kidato cha nne

      JibuFuta
    8. gwiji bora

      JibuFuta
    9. Shukran Hecko! kwa funzo lako..

      JibuFuta
    10. asante kwa funzo twashukuru

      JibuFuta
    11. Nisaidieni kujua umuhimu wa kubainisha bahari za ushairi

      JibuFuta
    12. Bahari ni nini?

      JibuFuta
    13. Ningependa kupata shairi lenye "mwalimu ni lako jina la hesjima na maana

      JibuFuta
    14. Ningependa kupata ushairi "mwalimu ni lako jina. La heshima na maana

      JibuFuta
    15. Nimependa kazi hii.Kongole☆☆☆☆☆

      JibuFuta
    16. Maoni haya yameondolewa na mwandishi.

      JibuFuta
      Majibu
      1. who told you peteere mmmn

        Futa
    17. Nimefurahi kwa ujezi wa taifa la kiswahili

      JibuFuta
    18. Nimeipenda kazi hii.
      Shukran.

      JibuFuta
    19. Kazi nzuri nimefurahi sana

      JibuFuta
    20. Shairi lenye beti Tano huitwaje?

      JibuFuta
    21. Twashukuru

      JibuFuta
    22. Asante sana nimesaidika sana

      JibuFuta
    23. Kazi safi bwanaaaa

      JibuFuta
    24. asante sana

      JibuFuta
    25. Heko.kazi nzuri

      JibuFuta
    26. Asante sana

      JibuFuta
    27. Asanteni kwa kazi yenu nzuri

      JibuFuta
    28. Asante Sana mwalimu

      JibuFuta
    29. Ninakipenda kiswahili mno asanti kwa kazi hii hongera

      JibuFuta
    30. Nice ss siema

      JibuFuta
    31. Nini maana ya ngoi

      JibuFuta
    32. kazi nzuri heko

      JibuFuta