FASIHI

                       FASIHI
Fasihi ni sanaa ambayo hutumia lugha kama chombo chake cha kupitisha ujumbe kwa binadamu.fasihi imegawanywa katika vifungu viwili vikubwa;
     i}  fasihi simulizi
      ii}fasihi andishi
fasihi simulizi ni sanaa ya fasihi ambayo hupokezwa/hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya masimulizi.
Watoto walirithi tungo za fasihi simulizi kutoka kwa mababu au nyanya zao..tungo hizi zilisimuliwa kwa njia tofauti kama vile; hadithi/ngano, mafumbo, methali, misemo, miiko,  maigizo,vitendawili,nyimbo nk.
Fasihi simulizi ina matawi haya;
Hadithi              semi                maigizo                     ushairi simulizi          
Ngomezi        mazungumzo
Fasihi andishi ina tanzu zifuatazo;
Riwaya    tamthilia           ushairi            hadithi fupi
     USHAIRI
Huu ni utanzu wa fasihi unaotumia mpangilio wa lugha ya mkato ,ya picha(taswira)  na yenye mapigo mahususi katika kuainisha maudhui yake
    Umbo la shairi
Mashairi ya fasihi andishi ni ya aina mbili;
Mashairi ya arudhi /jadi/kimapokeo
Mashairi  huru.
Arudhi ni sheria zinazoongoza utunzi wa mashairi ya jadi.
Vigezo vyake ni hivi;
Beti(ubeti) jumla ya mishororo inayowekwa pamoja.
Mshororo   - mstari katika ubeti
Mizani –silabi zinazounda mshororo.
Vipande-  mgao katika ubeti yaani ukwapi, utao na mwanandamizi

Vina /kina – silabi zenye sauti za namna moja zinazotokea katika sehemu ya katikati au mwishoni mwa kila mstari wa ubeti
Mishororo ya mwisho unaporudiwa katika kila beti huitwa kibwagizo/mkara/kiitikio/kipokeo
Vinginevyo huitwa kimalizio.
Mshororo wa kwanza huitwa futahi/mwanzo/kifunguo.
Mshororo wa pili huitwa molto,
Mshororo wa tatu huitwa mleo.

AINA ZA MASHAIRI YA ARUDHI
a).kigezo cha mishororo

1. Tathmina/umoja  –shairi lenye mshororo katika kila ubeti,
2.  Tathnia /uwili-shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti ,
3. tathlitha/utatu/wimbo-shairi lenye mishororo mitatu
4. tarbia /unne- shairi la mishororo minne katika kila ubeti.
5.takhmisa/utano-shairi lenye mishororo mitano  katika kila ubeti.
6.tasdisa/sitaia/usita- shairi la mishororo sita katika kila ubeti.
7.tasbia/sabaia-shairi lenye mishororo sba katika kila ubeti
8.thamina-shairi lenye mishororo tisa katika kila ubeti
9.ukumi-shairi lenye mishororo kumi  katika kila ubeti
b) kigezo cha vipande
1.utenzi/tenzi –ni shairi lenye kipande pekeekatika kila ubeti
2.mathnawi/manthawi-shairi lenye vipande viwili yaani ukwapi na utao katika kila ubeti.
3.ukawafi-shairi lenye vipande vitatu katika kila beti zake.
c) kigezo cha vina
1. mtiririko shairi lenye vina vya kati hulingana katika beti zote ambapo vina vya mwisho pia hufanana katika shairi zote.
8Ka,                                     8  li,
8Ka,                                     8  li,
8Ka,                                     8  li,
8Ka ,                                    8  li,

2.ukara
Shairi ambalo vina vya mwisho hulingana katika shairi lote lakini vina vya kati hubadilika kutoka ubeti hadi mwingine.

3.ukaraguni –shairi ambalo vina vya  kati hubadilika katika ubeti hadi mwingine na vina vya mwisho pia hubadilika  kutoka ubeti hadi mwingine.
Ka,                8  li,
Ka ,               8  li,
Ka,                8  li,
Ka,                8  li,

8Sa                  8 ri        
8Sa                 8 ri
8Sa                 8 ri
8Sa                 8 ri
4.masivina
Mashairi yasiyo na vina.
Wa,                   li,
La,                    pi,
Ka,                    wi,
Ta,                    mi,

Sifa za fasihi simulizi
Huwasilishwa kwa masimulizi yam domo kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.
Ni mali ya jamii na hakuna anayeweza kudai kuwa ni mali yake binafsi.
Fasihi simulizi ni ya tangu jadi .
Masimulizi yanaweza kubadilishwa papo hapo wakati  masimulizi anapowasilisha.
Hadhira huweza kuchangia na hivyo kuathiri masimulizi .
Hutumia ishara na sauti
Hufaidi wote waliojua kusoma na wasiojua kusoma.
Maundo ya fasihi simulizi ni rahisi na hivyo hufuatika kwa urahisi.
Sifa za fasihi andishi
Huwasilishwa kwa maandishi hasa vitabuni.
Ni mali ya mwandishi.
Imezuka baada ya binadamu kufumbua kuandika
Maandishi hayabadiliki isipokuwa mwandishi anapoyaandika upya.
Hadhira haina mchango wa moja kwa moja katika fasihi andishi.
Hutumia mbinu mbalimbali za kimaandishi kuwasilisha ujumbe.
Hufaidi wanaojua kusoma na kuandika pekee.

Majukumu ya fasihi./dhima ya fasihi
Hueleza umuhimu wa fasihi
a} huelimisha
hadithi,misemo,vitendawili na mengineyo yana  mafunzo mengi kuhusu tabia nzuri ,mienendo ifaayo nk. Mafunzo kutokana na fasihi huitwa maadili.
b}huburudisa
baadhi ya visa katika hadithi huchekesha na kuchangamsha . nyimbopia huburudisha.
c}hufikirisha
fasihi hukuza uwezo wetu wa kufikiri .si mambo yote yanayokuwa wazi katika fasihi kwa hivyo hulazimu kuwazwa ili kupata suluhu.
d} huendeleza utamaduni
fasihi hueleza na kuwapokeza watu mambo yanayothaminiwa na jamii ili wayaendeleze na kuyahifadhi . uzingatiaji wa mambo kama vile mila hudumisha jamii.
e} hushauri
methali ,vitendawili , nyimbo,misemo na zinginezo huonya na kushauri.visa katika hadithi hutumiwa kuwashauri na kuwaonya binadamu.
f}hukuza usanii
fasihi huwapatia binadamu uwezo wa kujifunza njia na mitindo mbalimbali ya kutumia lugha na kujieleza.
g} huajiri
waandishi wa vitabu , waigizaji, waimbaji, na wengine hupata ajira kutokana na kazi hizi.

HADITHI
Utambaji wa hadithi
Utambaji wa ngano katika jamii za waafrika ilifanywa wakati wa magharibi, ama juani au katika chumba kuzunguka moto. Mara nyingi watambaji walikuwa wazee au watu wazima.
Mtambaji alihitajika kuwa na vipawa hivi;
Ubunifu ili kutunga hadithi upya.
Kufahamu hadhira ili kuweza kutimiza matarajio yao.
Ufahamu wa lugha na utamaduni wa jamii ili kuwasilisha hadithi yake kwa ufasaha,heshima na hekima.
Uwezo wa kunasa makini ya hadhira yake.
Uwezo wa ufaraguzi katika mbinu za sanaa ya maonyeshokwa mfano ishara,mabadiliko ya sauti nk
Awe mcheshi ili kusisimua hadhira .
Hadithi zilitanguliwa na methali au vitendawiliili kuteka nathari ya hadhira na kwa sababu  za kuwatayarisha.
Aidha hadithi nyingi zilikuwa na fomula/utangulizi.
Mifano
               A
Mtambaji:    paukwa!
Hadhira  :    pakawa
Mtambaji: hapo zamani za kale…….
                B
Mtambaji: paukwa!
Hadhira:pakawa
Mtambaji:sahani
Hadhira:ya mchele
Mtambaji:giza
Hadhira:la mwizi
Mtambaji:na baiskeli je?
Hadhira:  ya bodaboda
Mtambaji:hapo zamani za kale…..
   C
Mtambaji: kaondoka chanjagaa kajenga nyumba kaka mwanangu mwana siti vijino kamachikichi,nitamjengea nyumba na vilango vya kupitia. Hapo zamani za kale….
                  AINA ZA HADITHI
Mighani/mughani/visakale
Ni hadithi zinazosimuliwa kuhusu mashujaa walioishi au wanaoaminiwa kuwahi  kuishi miongoni mwa jamii mbalimbali . mifano ni kama Luanda magere wa luo na fumo liyongo.
Visasili
Ni hadithi zinazohusishwa na mizungu na imani ya watu kuhusu mambo mbalimbali kwa mfano
Asili ya kifo.

Khurafa/hurafa
Hurafa ni hadithi ambazo wahusika wake huwa wanyama mbalimbali ambao huwakilisha binadamu wenye sifa tofautitofauti.
Hekaya /ngano za ayari
Ni hadithi zinazohusu binadamu au wanyama ambapo kinachotawala ni ujanja.
Ngano za mtanziko
Ni hadithi ambazo mhusika mkuu hujipata katika njia panda.hukabiliwa na hali mbili au zaidi ambapo zote huvutia lakini atalazimika kufanya uamuzi wa kuchagua njia moja tu.
Ngano za usuli
Ni hadithi ambazo hueleza chanzo cha tabia au sifa Fulani kama vile; kwa nini sungura ana masikio marefu,ama kwa nini nyoka hana miguu.
Ngano za mazimui


Mazimui ni viumbe vya hadithi vyenye maumbile yasiyo ya kawaida .kwa mfano kuwa na jicho moja kubwa.viumbe hivi husemwa kuwa vilafi sana na vyenye ujinga wa aina yake.

Maoni 5 :

  1. well presented and easy for learners to understand but shallow in content

    JibuFuta
  2. It's was so much good

    JibuFuta
  3. It was great 👍

    JibuFuta