MISINGI YA MANENO
- Mofimu
Mofimu ni dhana ambayo ni maana ambayo/zo huwakilishwa au kusetiriwa katika neno(mofu) ambalo tunaweza kulisikia linapotamkwa au kuliona linapoandikwa.
Dhana hii huweza kujitokeza kwenye mzizi au kiambishi
Mifano mofimu
Maria +msichana
+mmoja
+mtu/binadamu
Kuku +ndege
+mmoja/wengi
+anayefugwa
+ mayai
Ndege +kiumbe +chombo
+anayepaa +kupaa
+mmoja/wengi +moja/nyingi
Nitacheza
Ni +umoja
+mtenda
+nafsi ya kwanza
Ta +wakati ujao
Chez +mzizi
-a +kiishio
Aina za mofimu
- Mofimu huru/mofimu za kimsamiati
Ni mofimu zenye maana kamili hata bila kuambatanishwa na mofimu zingine.
Mofimu hizi hupatikana katika nomino,viwakilishi na hata vivumishi.mifano ya mofimu huru
- Katika nomino
Kuku dawati samaki mama baba
Shangazi kabati Kenya Chaki karatasi
- Katika viwakilishi
Mimi sisi wewe nyinyi yeye
Wao
- Mofimu katika vivumishi
Robo bora nadhifu hodari jasiri
Mofimu huru pia huitwa mofimu za kimsamiati.
- Mofimu tegemezi/ambata/funge
Ni mofimu ambazo haziwezi kujisimamia ,ni sharti zihusishwe na mofimu zinginezo.
Mifano;
Kiti -ki+ti mtume mjamzito walimoingia mtu madarasa
Changamoto matunda kipofu gugumaji amenionea.
Uhainisho wa mofimu
- Mtoto
M +umoja
toto +mzizi
- Auma
A + ngeli
+ mtenda
+ nafsi ya tatu
+ umoja
Um + mzizi
a + kauli ya kutenda
- Hakukukumbuka.
Ha +ukanusho
+nafsi ya tatu
+mtenda
Ku +ukanusho
+wakati uliopita
Ku +nafsi ya pili
+mtendwa
kumbuk +mzizi
a +kauli ya kutenda
bainisha mofimu katika sentensi hizi na utaje kama ni huru ama tegemezi.
Amekimbia sana. Kiti hiki ni kizito.
Tegemezi huru tege tege huru tege
fukia viazi hivyo endesha gari
huru huru tegemezi tegemezi huru
kaa chini. Amejipamba
huru huru tegemezi
- Viambishi
kiambishi ni kipashio cha kisarufi kinachoambatishwa au kinachofungamanishwa au kinachopachikwa katika mzizi wa neno ili kulipa neno maana mbalimbali.
Kiambishi ni mofu
Aina za viambishi
- Viambishi awali-hupachikwa kabla ya mzizi wa neno.
- Viambishi tamati –hujitokeza /huja baada ya mzizi wa neno.
Mifano
Viambishi awali
|
mzizi
|
Viambishi tamati
|
maneno
|
m
|
geni
|
©
|
mgeni
|
Ki
|
geni
|
©
|
kigeni
|
U
|
geni
|
©
|
ugeni
|
U
|
geni
|
ni
|
ugenini
|
Ku
|
l
|
a
|
Kula
|
M
|
l
|
o
|
mlo
|
A
|
l
|
a
|
ala
|
Wa-me-ku
|
l
|
a
|
wamekula
|
©
|
li
|
a
|
lia
|
Hu
|
li
|
Liw-a
|
huliwa
|
M
|
li
|
o
|
mlio
|
Ki
|
li
|
o
|
kilio
|
li-li-li
|
li
|
li-a
|
lilililia
|
a-li-m
|
li
|
li-a
|
alimlilia
|
Matumizi ya viambishi vya masharti
- –nge
- Huweza kutumiwa maradufu katika sentensi. Katika hali hiyo huonyesha kuwa vitendo vyote viwili havikutukia. Hata hivyo bado pana uwezekano wavyo kutukia. Kwa mfano;
Ningemwona ningemwambia. Katika mfano huu msemaji hakumwona anayerejelewa kwa hivyo hakumharifu alilopasa. Hata hivyo huenda akamwona baadaye na kisha kumwambia.
- Katika hali kanushi, ni sharti vitenzi vyote vinavyosheheni –nge lazima vikanushwe .hukanushwa kwa njia mbili;
- Kwanza kutumia ‘si’ baada ya kiambishi nafsi lakini kabla ya -nge mfano
Nisingemwona nisingemwambia. Katika hali kanushi maana hubadilika na kuonyesha kuwa vitendo vyote vilitukia.
- Aidha tunaweza kuzingatia nafsi husika pekee.
Singemwona singemwambia.
Ungeniharifu mapema ningekuletea.
Usingeniharifu mapema nisingekuletea.
Hungeniharifu mapema singekuletea.
- Ngali
Ikijitokeza maradufu kwenye sentensi, huonyesha vitendo vyote viwili havikutukia na hamna uwezekano wavyo kutukia kwa vyovyote vile.
m.f
Ningalimwona ningalimwambia .
Ukanushaji
Nisingalimwona nisingalimwambia.
Singalimwona singalimwambia.
Ikitumika mara moja kwenye sentensi huonyesha kuwa kitendo kiko katika hali ya kuendelea,m.f
Angali anacheza. Mama angali anapika. mtoto angali analia.
Kukanusha
Hachezi mama hapiki. Mtoto halii.
Tanbihi : ‘nge’ na ‘ngali’ havitumiwi katika sentensi moja
*ningemwona ningalimwambia.
Marejeleo
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Marejeleo
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni