USEMI HALISI NA USEMI WA TAARIFA
kauli zipo za aina mbili;
kauli ya moja kwa moja kutoka kwa mnenaji hadi kwa msikilizaji jinsi ilivyo bila ya kufanyiwa mageuzi yoyote, kauli hii huitwa usemi halisi.
Kauli inayopokewa kama maelezo ya yaliyosemwa pale awali na ambayo hufanyiwa mabadiliko fulani fulani ya hapa na pale, kauli hii huitwa usemi wa taarifa.
Usemi halisi
Katika usemi huu yafuatayo huzingatiwa;
Alama za mtajo hutumiwa mwanzo na mwisho wa maneno yaliyosemwa.{“ “}
Kila baada ya kufungua ,sentensi huanza kwa herufi kubwa m.f
“Hamjambo?”
“Shuhuda, tafadhali njoo tukatembee.”
Alama ya hisi,kiulizo,koma,nukta za dukuduku na kituo kikuu pia hutumiwa pamoja na alama za mtajo.Lazima zije kabla ya alama za kufunga. m.f
“Hunipendi?”
Mwalimu akamhoji, “vipi?”
Mwanafunzi alijibu, “salama”
Kauli moja ikivunjwa katika vitengo, kitengo cha pili hata baada ya kuwekewa alama za kufungua ,neno lake la kwanza litaanza kwa herufi ndogo isipokuwa neno lilo likiwa nomino maalum.
Iwapo sentensi mpya inaanza baada ya msemaji kutajwa, herufi kubwa hutumika mwanzoni mwa hiyo sentensi mpya.
“Tukifika mjini Voi ,tutapumzika kwa muda wa saa moja.” Kiongozi wetu alisema. ”Baadaye tutaondoka na kwenda moja kwa moja hadi kisiwani Mombasa.”
“Haya! Habari ndiyo hiyo,” mwalimu alisema.
“Haya ,habari ndiyo hiyo.” Mwalimu alisema.
“Wiki ijayo tutakwenda kujionea mechi kati ya Harambee stars na Uganda Craines.” Rafiki yangu aliniambia.
“Mara nyingi binadamu uhitaji kutumia 'common sense.’ ”
usemi wa taarifa
Hii ni ripoti kuhusu yaliyosemwa hapo awali. Yafuatayo huzingatiwa;
Alama za mtajo haziwekwi
Baadhi ya maneno yanaweza kubadilika lakini ujumbe uwe ni ule ule.
Alama za hisi na kiulizi hazitumiwi.
Aghalabu wakati uliopita ndo hutumika
Mabadiliko
Usemi halisi
|
Usemi wa taarifa
|
viulizi
|
-ngapi?
|
Idadi
|
-ipi
|
Sifa/o-rejeshi/amba-rejeshi
|
-gani
|
o-rejeshi/amba-rejeshi/sifa
|
Je ,…?
|
Iwapo/ikiwa
|
…..je?
|
Jinsi/namna
|
Lini?
|
Wakati
|
Mbona?
|
sababu
|
Kwa nini?
|
Sababu
|
Vipi?
|
Jinsi/namna
|
Wakati/hali
|
-me-
|
-li-
|
-ta-
|
-nge-
|
Mwaka ujao
|
mwakani
|
sasa
|
Wakati huo
|
kesho
|
Siku iliyofuata
|
Jana
|
Siku iliyotangulia
|
Nafsi
|
-ni-
|
-a-
|
-ku-
|
-ni-/m-
|
viashiria
|
Hapa
|
Pale/hapo/alipokuwa
|
huku
|
Kule/huko/alikokuwa
|
huyu
|
Yule/huyo
|
vihisishi
|
Tafadhali
|
alisihi
|
Salaala!
|
alishangaa
|
Nkt!
|
alifyonza
|
Uuuuwi!
|
Piga mayowe/npiga usiyahi
|
alhamdullilahi
|
alishukuru
|
Mungu wangu eeeh
|
aliomba
|
Arusi tunayo
|
shangilia
|
kwenda
|
Laani/puuza
|
Katika usemi wa taarifa matumizi ya maneno ‘kuwa’ na kwamba huruhusiwa kwa mfano ;
“Mtoto ni mtoto, awe wa kiume au wa kike,” akasema mjomba,
Mjomba alisema kuwa…
Mjomba alisema ya kwamba mtoto ni mtoto awe wa kiume au wa kike.
“Mabasi hayapiti hapa siku hizi, kwa nini?” Neshboch aliuliza.
Neshboch alihoji/aliuliza/alitaka kujua sababu ya mabasi kutopita hapo katika siku hizo.
Madereva wakasema ,”Tutatii sheria za barabarani.”
Madereva walisema kuwa wangetii sheria za barabarani
“Leo nitakuonyesha kilichomtoa kanga manyoya,” Seki akamwambia Katango.
Seki alimwambia Katango kwamba angemwonyesha kilichomtoa kanga manyoya siku hiyo.
“Afida , kwa nini leo umechelewa darasani?” Kiranja akauliza.
Kiranja alitaka kujua sababu ya Afida kuchelewa darasani siku hiyo.
“Serikali ina mkono mrefu, hata ukijificha wapi utapatikana. ” Akakumbusha Chausiku .
Chausiku alikumbusha kwamba serikali ilikuwa na mkono mrefu na hata mtu angejificha popote angepatikana.
Mwanafunzi alisema kuwa angepita katika somo la Kiswahili.
“Nitafaulu katika somo la Kiswahili,”akasema mwanafunzi.
Mwanafunzi akasema,”Nitafaulu katika somo la Kiswahili.
Chifu aliwakumbusha kuwa ukimwi ulikuwa ulikuwa ugonjwa hatari sana.
“Ukimwi ni ugonjwa hatari sana,” chifu akawakumbusha.
Chifu akawakumbusha, “Ukimwi ni ugonjwa hatari sana.”
“Nawakumbusha kuwa ukimwi ni ugonjwa hatari sana.” Chifu akasema.
Kazimoto alishauriwa na kasisi kuwa aache tabia za ulevi.
“Acha tabia ya ulevi,”kasisi akamshauri Kazimoto.
“Kazimoto acha tabia ya ulevi,” kasisi akamshauri.
“Alimaliza fyu!”
Akamaliza yote
“Van persie , Van persie, goool!”
Alishangilia vanpersie alipofunga bao.
“Ni siku arubaini pekee ambazo zimebaki kabla ya Nineve kuangawizwa ikiwa hamtatubu dhambi zenu.” Jona akawatadharisha.
Jona aliwatadharisha watu kuwa siku arubaini pekee ndizo zilizobaki kabala ya Nineve kuangamizwa ikiwa awangetubu dhambi zao.
“wanipendeani mrembo?”
Alimuliza mrembo alikuwa anampendea nini.
"Anayenitesa si adui yangu bali ni rafiki yangu tuliyojuana zamani,"Dzombo akasema.
Dzombo alisema kuwa aliyekuwa akimtesa hakuwa adui yake bali alikuwa rafiki yake waliojuana siku zilizopita.