MHANGA NAFSI
YANGU
Mhanga nafsi yangu ni riwaya iliyoandikwa na
Ammed Said Mohamed katika mwaka wa 2012, kimechapishwa na Longhorn
publishers. Inazunguka katika maisha ya Mhusika wake mkuu ambaye ni Afida
MAHUDHUI
Usaliti
Usaliti unajitokeza kwenye wahusika wengi
wakiwemo Afida anayesaliti ukoo wake na kukata minyororo yao huku akilalamika
kurudishwa nyuma na utegemezi wa motoni.Afida pia anamsaliti mpenziwe Shabaan
aliyemwandikia barua kila wakati tangu alipoenda peponi, Afida anakataa kujibu
hizo barua, anadai kwamba mapenzi yake kwa Shabaan yaliisha. Usaliti huu
unampelekea Shabaan kuugua ugonjwa wa moyo na hatimaye Shabaan anafariki. Vile
vile Afida anawasaliti wazazi na walezi wake huku akisingizia kuwa alishafika
alikotaka, Afida na Shuhudia wanaisaliti dini yao,kulingana na dini yao hakufaa
kuingilia ulevi ambayo ni uasi wa kidini. Neshbosh bwanake Afida vile vile
anasaliti ndoa yao na hatimaye kumfukuza Afida nyumbani pake. Majirani wake
Afida wanamsaliti kwa kumsingizi Afida kwamba alikuwa akimlelea mtoto akiwa
mlevi na kumdhalilisha, jambo hili linampelekea korti kutoa uamuzi wa
kunyang’anyanywa mtoto wake Dinda.
Umaskini
Mataifa haya ya peponi wameyadhibiti masoko ya
Motoni ambapo tunawaona wageni hawa wakija Motoni na kununua matunda kwa bei ya
chini. Hii inasababisha umasikini kwa Wamotoni kwani hawafaidiki katika juhudi
zao za kuzalisha mali.Kuhamia kwa Afida Peponi kulikuwa na msukumo wa kuasi
ulitima na kusaka mali Peponi.Tunaelezwa kuwa Motoni kulikumbwa na umasikini
kiasi kwamba hakuna jambo njema lolote lililoweza kumea, kuwa au kukua katika
nchi hii . Afida alilalamika Jinsi kule kutegemeana kwa ukoo wa motoni
kunavyozidisha umasikini hivi kwamba, mtu akionekana kufaulu, lazima ukoo
ugawane mafanikio yenyewe hata kabla hayajazalisha. Eti mtu akifanikiwa kidogo,
anakuwa mateka wa ukoo unaomnyofoa nyama harakaharaka na kumegwa kila upande
hadi mtu huyo abaki mifupa mitupu. Hii ni ishara tosha kuwa Afida ametoka
katika jamii iliyokumbwa na umasikini. Pia Katika maelezo ya Bi Sinangoa,
tuanona kuwa Afida alilelewa kwa ukata kwani mara nyingi akienda kwa bibi huyu
(Sinangoa) kupata angalau chakula. Wakati mwingine Afida akipata kwa Singangoa
hakukuwa na chakula, bibi huyu alikuwa akimtafutia angalau visenti vidogo
ilikununua chakula duni huko vijijini.Kazi aliyoifanya Bi. Mwamda baada ya kifo
cha mumewe ni ishara tosha ya umasikini.
Ndoa
Kunazuka ndoa kati ya bwana Bawa na bibiye
Marneti ambaye ni mmotoni, ndoa hii inadumu ila inasongwa na tatizo la kutopata
mtoto, jambo hili linawapelekea wapange njama ya kumsawishi Afida kuwapa mtoto
wake Dinda. Afida anakataa jambo hili na kupelekea uhusiano wake na shangaziye
Murneti kusambaratika.
Pia kunazuka ndoa kati ya Afida na Neshboch,
ndoa hii imejawa na matatizo ya kila aina.Afida anadhalilishwa na kuulizwa
maswali ya kumdhalilisha na dadake Neshboch kwa jina la Sheshaiza, anamwuliza
siku ya harusi kama huko kwao Motoni amewahi kula vyakula vitamu kama vilivyo
huko peponi, hatimaye ndoa hii inavunjika Neshboch anapomfukuza bibiye, Afida
anajipata katika ndoa ya pili kwa lengo la kupata mtoto baada ya kunyanganywa pinda
mtoto wake, anakuwa katika ndoa na saparata na wanapata mtoto kwa jina
mkombozi.
Tamaa
Wamotoni wengi wana tamaa ya kwenda peponi,
wengine wameishi kufa kwa tamaa hii. Mwandishi anasema kuwa kuna wengine
waliojaribu kukata jangwa la Sahara na kuishiwa kukumbwa na joto, kiu na
kitaushi cha maji mwilini na ambacho mara humpoteza mtu uhai wake, jambo
hili linawapelekea wamotoni kuhamia Peponi wanakobaguliwa na kudhalilishwa,
Afida pia anahamia peponi kwa tamaa ya kujiboresha kimaisha na kuiacha umaskini
uliomkumba.Tamaa ya utashi unampelekea Afida kuolewa na mzee Neshbosh
aliyemzidi umri.
Ulevi
Ulevi inajitokeza kupitia kwa wahusika kama
Afida, Neshboch, saparata na shuhuda, Afida na saparata wanaathiriwa zaidi na
ulevi. Punde tu Neshboch anapomfunza ulevi, ndoa yao inaingia msukomsuko. Baada
ya Afida kutalakiana na mumewa Neshboch anasingiziwa ulevi na majirani wake na
hatimaye kunyang’anywa mtoto wake Dinda, hapo ndipo Afida anajipagaza hilo jina
na hatimaye kuwa mlevi wa kupindukia. Ulevi huu unampelekea Afida
kuishiwa na pesa kwani baada ya talaka hakupata pesa tena kutoka kwa Neshboch.
Hatimaye mtoto wake Mkombozi anapata katika harakati zake za kulewa anapoanza
uhusiano na Saparata.
Ukengeushi
Wamotoni wengi wanapohamia Peponi huacha
tamaduni zao na kuiga Wapeponi. Bi Marneti shangaziye Afida alipokuwa Motoni
alithamini utu, umoja na hakuwa na tamaa. Alipenda mapenzi safi yasiyo ya pesa,
kuuthamini ukoo wake na hakuropokwa ovyo. Alipohamia Peponi, alichukua tamaduni
za huko na kutupilia mbali tamaduni za Ki-Motoni hasa alipokata uhusiano na
ukoo wake kiasi cha kumdhulumu Afida aliyekuwa kama mtoto wake.Shuhuda rafikiye
Afida aliyetoka Afrika aliiga Uzungu kwa mavazi, ulevi, hulka na hata
lugha.Alivalia vijiguo vilivyomuacha tuputupu kama anavyodai Afida. Alivuta
sigara ambayo inadaiwa kuwa haikumtoka mdomoni . Alienda kwenye mabaa na
kushiriki ukware uliomfanya aambukizwe ukimwi. Mambo haya yote Shuhuda aliyaiga
kutoka kwa Wapeponi ambapo hata Afida hakuamini kuwa ni Shuhuda aliyemfahamu
kule Motoni. Shuhuda anasisitiza kuwa iwapo mwanamke yeyote anagependa mambo
yake yamwendee vyema kule Peponi,hakuwa na budi ila kuonyesha mwili wake .
Ubaguzi
Abiria waliokuwa kwenye basi na Afida
walimtazama kwa chuki naye aliwapa tabasamu la kudanganya.Moyoni alielewa chuki
ya hao abiria hasa bibi mmoja aliyezoea kupanda naye basi lilo hilo kila siku,
kwamba ilikuwa ya kubaguliwa yeye kwani hakuwa Mpeponi. Chuki ilisheheni hata
shuleni alikoenda Afida kwani alidhaniwa kuwa na fahamu ya chini kuliko
wanafunzi wote waliokuwamo darasani. Anasisitiza kuwa wanafunzi walimtenga na
kumuona dude tu. pia dadake Neshboch, Shesheiza anamwuliza Afida maswali ya kumbagua.
Anamwuliza kwamba kama huko kwao pia wanakula vyakula vitamu jinsi vilivyo
peponi.
SIFA
ZA AFIDA
Msomi
Afida anapoelekea peponi anajiunga na chuo cha
peponi huku akigharamiwa na bwana Bawa na bibiye Murneti. Anasoma kwa bidii
mpaka anapita somo fulani na kusemekana kuwa Afida ndiye Mmotoni wa kwanza
kupita kiasi hicho baada ya miaka kumi na mitano, japo Afida hamalizi shule
wala kufuzu anaonyesha nia ya kutaka kuendeleza masomo yake japo anakumbwa
vizingiti kama kuolewa na bwana Neshboch.
Msaliti
Afida anayasaliti mapenzi yake na Shabaan ingawa
alimwahidi kwamba angeasi mapenzi hayo, pia anasaliti walezi wake kama Sinangoa
na Mamake kwa kutoshulika na wao anapofika peponi, anaandikiwa barua nyingi na
wamotoni ambayo anayapuuza Afida.
Mkengeushi
Afida pamoja na Shuhuda wanauacha utamaduni wa
motoni na kuiga utamaduni wa Peponi ,hili linadhihirisha katika nguo
anazong’ara Afida, na ulevi wa kupindukia na hata hulka zake.
Mwenye
bidii
Anapoolewa na Saparata anajitahidi kufanya kazi
kwa bidii ili ahikimu matakwa ya mtoto wao Mkombozi, ili ni baada ya Saparata
kukataa kutoa msaada kwa mtoto wake Mkombozi.
Mpenda
anasa
Afida anapopata talaka kutoka kwa mzee Neshboch
maisha yake yanachukua mkondo upya, anaanza kujiingiza katika vitendo vya
anasa, hili linaanza pindi anaponyang’anywa mtoto wake dinda. Hajiheshimu tena
anauza mwili wake kingono katika harakati za kupata pesa za kustahihisha
mahitaji yake. Anaenda kwenye baa na kutamka wazi kwamba anataka mtoto na
angependa apewe, maisha yake Afida yanachukua mkondo upya asiwe afida
aliyedhaniwa kuwa na msimamo dhabiti.
Mlevi
Afida anaponyanganywa mtoto wake Dinda baada ya
kusingiziwa na majirani yake kuwa mlevi, anajiingiza katika ulevi wenyewe huku
maisha yake yanazoroteka katika ulevi.
Mwenye
msimamo dhabiti
Anapoambiwa na bwana Bawa ba bibiye Murneti
awapee mtoto wamtunzie anakataa wazo hilo na kutafautiana na mumewe na
shangaziye. Pia yakrobich anapomtakia uhusiano wa kimapenzi anakataa na kuona
isiyokuwa na maana.
B. TAMTHILIA
YA KIFO KISIMANI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka
wa Mberia 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd. Ina idadi nyingi ya
wahusika ikiwemo mwelusi, mtemi Bokono Gege ,Tanya Azena Atega Kame na
Askari 1 ,11 na 111,Mweke Talui Andua Kaloo
Mhusika mkuu ni Mwelusi. Mwelusi ni kiongozi
katika shughuli za ukombozi wa butangi.
Anashikwa na kuteswa katika harakati zake za
kuleta ukombozi butangi, mwishowe anauliwa baada ya kusalitiwa na nduguye Gege.
MAUDHUI
YANAYOJITOKEZA KATIKA KIFO KISIMANI
Unafiki
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambia
kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni
unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame walipanga
jinsi watakavyo muua.
Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi
yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa
mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake
tangu ujana wao.huu ni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi pia tanya
anapompelekea mwelusi chakula gerezani askari 1 na 11 wanamwahidi kuwa watampa
Mwelusi chakula Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee
rafiki yake mkate wa wishwa
Dhuluma
na mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza
mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za
miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na
kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni .
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na
hajahukumiwa.Batu anapomtembelea baada ya kumshawishi akiri kutochochea
Wanabutangi na kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na
amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri
kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapokataa Batu anamwambia
kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawapa
ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda
Ubinafsi
Gege anamuua Mwelusi nduguye ili apate kuozwa
Alida bintiye Mtemi.Gege anamuambia Mwelusi hajali maisha yake aachane na
jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine anajijali yeye mwenyewe.Kaloo
anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi aliyoamuru mtoto wake
apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono
ili apate mali zaidi.
Gege pia anapinga hoja ya kuenda kumtazama
nduguye mwelusi gerezani, anamwambia mamake tanya asimzomee anapoulizwa , yeye
anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua . Hili
linadhihirisha kuwa anawathamini wasichana kuliko nduguye mwelusi.
Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa
kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu kukomboa
Butangi kutokana na utawala Mbaya.
Uongozi mbaya
Mtemi Bokono pamoja na vikaragosi wake Batu na
Zige ni viongozi wabaya katika jamii ya Butangi, wanamshika mwelusi na kumtesa
bila ya makosa anachapwa gerezani kinyama huku analia ingawa yeye anatetea haki
za wanabutangi ,kisha utawala wa viongozi hawa unamshauri nduguye mwelusi Gege
aue nduguye Mwelusi kwa ahadi ya uongo wa kumpoza bintiye mtemi kwa jina
Alida.
Uongozi
mzuri
Kame, Askari 1 wanaonyesha uongozi mzuri
wanapomtetetea haki za mwelusi wanaonyesha utu kwa maisha ya binadamu. Batu na
Zige wanapotaka kumuua mwelusi Kame anasema aachwe kwa kuwa hana makosa.
SIFA
ZA MWELUSI
mjasiri – anaamua kukabiliana
na utawala wa Mtemi Bokono. Haogopi kuteswa na askari 11,111, batu na zige.
mwerevu- anauelimisha umma wa
Butangi kuhusu uovu wa utawala wa Butangi na namna wanavyoweza kujikwamua
kutokana na uongozi huo-mbaya
mzalendo- anapenda nchi yake
ndiposa anajitolea mhanga kupigania mabadiliko, pia anaongoza harakati za
kukomboa Butangi kutokana na uongozi mbaya wa mtemi Bokono.
Mwenye busara- anajaribu kuwazindua
wanabutangi kimawazo dhidi ya uongozi mbaya
Mwenye maarifa –
anatumia maarifa kutoroka kizuizini kwa kukereza minyororo kwa tupa
mbishi- anabishana na Zigu pale kisimani kuhusu
matumizi ya kisima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni