Jumatatu, 12 Februari 2018

MSTAHIKI MEYA

MSTAHIKI MEYA
MAUDHUI
Migogoro
  • Mgogoro wa Meya na wafanyakazi ili kuboresha mazingira ya kazi.
  • Baina ya Meya na Siki kwa kutotaka ushauri wake.
  • Baina ya Meya na Diwani III kwa kutotaka ushauri wake.
  • Baina ya Meya, diwani I na II na diwani III kwa kuwa mwadilifu na wanamtenga na Bili kuingizwa.
  • Viongozi na raia kwa kukiuka majukumu kunakosababisha migomo.
  • Viongozi na wanataaluma kama vile Siki na Waridi kutokana na mazingira mabaya ya kazi.
  • Baina ya Meya na jamii yote kwa umaskini na huduma duni za kijamii.
  • Baina ya Meya na askari kwa kuchoka kutumiwa kisha kumkamata na wenzake.
Nafasi ya mwanamke katika jamii
  • walezi/mzazi-mama
  • wahudumu-Dida
  • Anayekata tama/kupoteza matumaini-Waridi
  • Jasiri-mama Dadavuo Kaole
  • Wavumilivu-Dida
  • Watiifu-Waridi
  • Hapewi nafasi ya uongozi
Udanganyifu/uongo  
  • Meya kudanganya baraza halina raslimali za kulipa wafanyakazi ilhali madiwani wanaongezewa
  • mishahara mara kwa mara.
  • Kudanganya shehena nyingi zipo katika bahari kuu
  • Dawa zingewasili baada ya siku tatu na baada ya siku tatu kupokewa hospitalini.
  • Meya kudanganya dawa ziko njiani (shehena nyingi) kuonyesha baraza linajitahidi kuwajibika.
  • Baada ya kuiba fimbo wangedanganya raia kuwa ilipotea wakati wa rabsha.
  • Kumdanganya mhubiri kwamba ana wito wa kuacha uMeya na kumfuata.
  • Meya kumwambia Gedi awaambie wanahabari kuwa yuko mkutanoni.
  • Meya-baraza ni miongoni mwa yanayolipa waajiriwa vizuri
  • ukweli
  • Diwani kutoboa siri kwamba ahadi za Meya ni za uwongo.
  • Anatengwa na Meya kwa sababu anafahamika ni mkweli.
  • Meya anakiri kuwa aliyoambiwa na diwani III ni ukweli.
Unafiki
  • Meya anajifanya anafanya kazi kwa manufaa ya umma ilhali anajinufaisha na washirika wake.
  • Meya na baraza lake wanataka kuonekana wawajibikaji kwa mameya wa nje ilhali sivyo.
  • Meya anajifanya mcha Mungu, mpole na mnyenyekevu na kwamba ana wito wa kumtumikia Mungu
  • ilhali sivyo.
  • Meya kujifanya mpole kabisa anapomkaribisha mhubiri
  • Meya anajifanya ameguswa na mhubiri na kuwa husukumwa aache uMeya awe mhubiri.
  • Bili anajifanya anamshauri Meya kumbe anakusudia kujinufaisha.
  • Diwani I na II wanajifanya wanamshauri Meya kumbe wanajali maslahi yao.
  • Mhubiri anamuunga mkono Meya ilhali akijua hali ya raia ni mbaya ili anufaike.
  • Gedi anamtii Meya kwa maslahi yake kwa vile anavujisha siri kwa Siki.
  • Baraza linataka kuonyesha picha nzuri kwa wageni ili lipewe mikopo.
Ukatili
  • Askari wanaua watu katika kutuliza migomo.
  • Dida anafurahi wafanyakazi wanapofurumishwa kwa risasi.
  • Meya kutoona tatizo kwa mtoto mmoja kufa.
  • Meya hajali hali ngumu za wafanyakazi.
  • Diwani I anapendekeza nguvu zitumike kuzima mgomo.
  • Diwani I anaringia nguvu inayotumika kuwavurumisha wafanyakazi.
  • Diwani II anataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wachochezi-wapigwe ili watulie nyumbani
  • Meya anacheka wafanyakazi wanapotawanywa na polisi.
Utu
  • Siki ana utu kwa kumhudumia mama mwenye mtoto aliyezidiwa licha ya kutokuwa na hela.
  • Kwa kuendelea kuhudumia raia licha ya mazingira mabaya ya kazi.
  • Meya hana utu kwa kuwapa wafanyakazi chakula kilichopimiwa mbwa.
  • Siki ana utu kwa kumhudumia mama.
  • Askari hawana utu kwa kuwashambulia watu kwa risasi, magari ya maji na vitoa machozi hata kuwaua.
Usaliti
  • Askari kumgeuka Meya na kumkamata na kumuondoa mamlakani licha ya kuwalipa vizuri.
  • Askari badala ya kulinda raia wanalinda uongozi wa Meya.
  • Meya kusaliti waliomchagua kwa kutoleta maendeleo.
  • Meya kusaliti juhudi na ndoto za kupigania uhuru kwa kurudisha unyonyaji.
  • Diwani I na II kuwasaliti wananchi kwa kutumia madaraka kujinufaisha badala ya kuwanufaisha
  • waliowachagua.
  • Bili anamsaliti Meya baada ya mambo kuharibika.
  • Mhazili kuungana na wafanyakazi kugoma licha ya kumuajiri bila sifa za kuajiriwa.
  • Gedi kutoa siri kwa Siki kuwa Meya hataki kumuona.
  • Diwani III aliyeteuliwa na Meya katika kamati yake kupinga mipango ya kumnufaisha Meya na
  • kuungana na wafanyakazi.
  • Siki kuungana na wafanyakazi kuhimiza harakati za ukombozi dhidi ya Meya aliye binamu yake.
  • Wafanyakazi waliopaswa kumtii Meya kumgeuka na kumgomea.
  • Meya anamsaliti diwani III kwa kumtenga katika maamuzi (utengano)
  • Waridi anasaliti taaluma yake kwa kusisitiza wasio na pesa wasipate huduma na kujiuzulu kazi yake na
  • kuwaacha wagonjwa wakiteseka.
Dini
  • Viongozi hutumia dini kuficha na kuendeleza maovu yao.
  • Meya anamtumia mhubiri kuendeleza uongozi wake mbaya.
  • Viongozi wa dini huweza kurubuniwa na waumini wasio waaminifu.
  • Meya anamdanganya mhubiri kwamba ana wito wa kuacha uMeya na kumfuata jambo ambalo si kweli.
  • Kuna wahubiri wanafiki na wenye tamaa ambao huunga maovu mkono ili wanufaike.
  • Meya anaahidi kutoa mafuta ya mhubiri na sadaka kubwa kila mwezi.
  • Bili kusema angemweka mikononi mwa bwana hakuna ambalo lingemshinda.
Uongozi mbaya/utumizi mbaya wa mamlaka
  • Kutowashirikisha watu katika maamuzi-Siki
  • Meya na baraza lake wana uongozi mbaya.
  • Meya anatumia mali ya baraza vibaya.
  • Meya hajali hali ya wafanyakazi kwa kutoshughulikia madai yao.
  • Hajali elimu ya umma kwani anapeleka wanawe wakasomee nje.
  • Anapuuza ushauri wa Siki na diwani II na kuenzi ushauri mpotovu wa diwani I na II na Bili.
  • Meya anatumia vyombo vya usalama (polisi) kuendeleza uongozi wake mbaya.
  • Hafuati kanuni za baraza anapoongezea madiwani na askari mishahara na kandarasi kwa
  • kutojali nakisi katika bajeti.
  • Madiwani I na II hawamshauri Meya vizuri bali wanamuunga mkono ili wanufaike.
  • Meya kutumia wahudumu wake (Gedi na Dida) kama watumwa.
  • Anatumia nguvu na mabavu kuzima migomo badala ya kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi.
Ukombozi/uhuru/utetezi wa haki
  • Wafanyakazi wa mji wanagoma na kupigania haki zao.
  • Diwani III kupinga wazo la Meya kufuta kazi wafanyakazi waliogoma.
  • Siki na Diwani III wanaungana na wafanyakazi kupigania haki zao.
  • Wafanyakazi wa sehemu nyingine kama vile mhazili, wafanyakazi wa uwanja wa ndege na bohari
  • wanaungana na wafanyakazi kupigania haki zao.
  • Askari wanachoshwa na uongozi wa Meya na Diwani I na II na kuwatia mbaroni wawapeleke makao
  • makuu kuelezea hali ya mambo hivyo
  • kuporomosha uongozi wa Meya.
  • Waridi kuacha kazi kwa kuzorota kwa mazingira ya kazi.
  • Wawakilishi wa wafanyakazi kupeleka malalamiko yao kwa Meya
  • Wanaomba wawe na washiriki katika baraza watetee maslahi yao wenyewe.
  • Wafanyakazi kugoma.
  • Kufanya maandamano.
Ufisadi
  • Kutibiwa mafua na kujifungulia ng’ambo kwa kutumia pesa za baraza.
  • Meya anatumia cheo kupata mashamba na kuwagawia marafiki pia.
  • Meya kumgawia Bili rafiki yake vipande vya ardhi.
  • Daktari katika zahanati ya mji wa Cheneo (Siki) ni binamu yake Meya Sosi.
  • Bili kupendekeza kesi ya mwanakandarasi iende dhidi ya baraza ili lilazimike kulipa fidia naye awatolee fungu.
  • Meya anakubali kushirikiana na mwanakandarasi ili apate gawio.
  • Kutumia gharama kubwa katika mapokezi ya MaMeya.
  • Wanakubaliana na Bili na Madiwani I na II kuiba fimbo ya Meya na kuiuza ng’ambo.
  • Kumlipa Bili kwa huduma za ushauri kinyume na taratibu.
  • Meya kumwajiri mhazili wake bila kuwa na sifa stahiki.
Umaskini
  • WanaCheneo hawawezi kumudu mahitaji ya kimsingi kama vile:
  • Gharama za dawa
  • Wagonjwa kukosa hela za kulipia huduma hata karatasi ya kunakilia.
  • Nchi ni maskini ombaomba kama anavyosema Waridi.
  • Gharama za elimu
  • Kutomudu lishe bora kukosa chakula chakula hata wanakula chakula kidogo kilicholala makombo ya
  • mbwa, mizizi na matunda ya mwitu.
  • Kukosa kawi/moto kwa vile makaa na mafuta ya taa yamepanda bei tangu sheria ya misitu ishike kasi
  • (utunzaji wa mazingira).
  • Mama mfanyakazi wa baraza la Cheneo anashindwa kumudu kununua mafuta ya taa wala makaa.
  • Mtoto ana kiriba kwa utapia mlo
  • Wafanyakazi kuishi mabandani na kuenda kazini kwa miguu.
  • Baraza ni maskini.
  • Linategemea misaada/mikopo kutoka ugenini kulipia mishahara ya wafanyakazi.
  • Halina fedha za kuwalipa wafanyakazi.
  • Wanashindwa kulipa wafanyakazi kwa wakati.
  • Limeshindwa kuongeza wafanyakazi mishahara kwa vile bajeti ina nakisi.
  • Huduma za elimu na matibabu zimezorota.
Utabaka
  • Tabaka la juu kama vile Meya na madiwani
  • Tabaka la kati kama vile wafanyakazi wanaolipwa mishahara duni na inayocheleweshwa.
  • Tabaka la chini kama akina Kerekecha.
  • Tabaka la juu wanatibiwa ng’ambo wakati wengine wanashindwa kumudu gharama za matibabu.
  • Wanapata elimu ng’ambo wakati wengine wanashindwa kumudu gharama ya elimu.
  • Wanakula chakula kizuri.
  • Wana nyumba zenye samani nyingi.
  • Wanatibiwa mafua na kujifungulia ng’ambo.
  • Wanapata fursa ya kuburudika k.v. kula katika mikahawa ya kifahari.
  • Diwani II anamshauri Meya kuendeleza utabaka kwa kusema wafanyakazi walifaa kusukumwa mpaka
  • wajue kuna wenye nchi na wananchi.
Mapendeleo
  • Meya anaongeza mishahara ya madiwani na askari ilhali wafanyakazi wengine hawaongezewi.
  • Anamwajiri mhazili asiye na sifa za kazi hiyo ilhali wapo vijana wengi waliomaliza chuo kikuu wasio na kazi.
  • Kujiongezea mishahara minono.
  • Nyongeza kuja baada ya muda mfupi.
  • Kupata mshahara wote ilhali wa wafanyakazi unacheleweshwa.
  • Wana bima ya matibabu ilhali wafanyakazi hawana.
Uoga
  • Meya kuzirai na kuanguka kutoka kitini askari wanapoelekea kumtia pingu kwa kuogopa kwenda jela.
  • Diwani I na II wanababaika askari wanapokwenda kuwakamata baada ya mambo kuharibika.
  • DI na II kushikwa na butwaa askari wanapoenda kuwashika wachukuliwe wakaeleze hali ya mambo.
  • Anapata hofu anapoSikia Siki amemtembelea kwa kuhisi anampelekea habari mbaya.
  • Anashtushwa na sauti za wafanyakazi waliogoma.
  • Anaogopa kuongea na wanahabari.
  • Anawakwepa wafanyakazi, hataki kuongea nao.
  • Ana hofu watu wanataka cheo chake.
  • Diwani III anasema Meya ana uwezo mkubwa na kushidana aye ni kama kushindana na ndovu (ana uwezo
  • mkubwa) na utapasuka-kupata madhara.
  • Meya kushtushwa na sauti za wafanyakazi.
  • Meya kunyong’onyea anapoSikia habari za mgomo.
  • Meya na mhubiri kuinua mikono juu na kushtuka askari wanapoingia wakiomba kwa kudhani ni watu
  • wabaya wamemwingilia Meya.
  • Meya kushtuka na kushika tama tatu anaposema hawawezi kufuata sharti la kumaliza mgomo na kurejea
  • kazini na wanapewa nguvu na uchafu/uvundo.
  • Meya anapoSikia wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamegoma, ananyong’onyea.
Ujasiri/ukakamavu
  • Diwani III kumkaBili Meya na kutoa maoni kuhusu nyongeza ya mishahara ya madiwani ilhali wafanyakazi
  • wamegoma.
  • Pia kuongoza wafanyakazi kupigania haki zao.
  • Siki kumkaBili Meya na kumkosoa bila hofu.
  • Hasiti kuendelea na harakati za mageuzi licha ya vitisho vya Meya, uwezo wake na kuitwa mchochezi.
  • Mama ni jasiri. kwa kumpeleka mwanawe hospitalini bila pesa. Anajitoma ndani kwa daktari wakati watu
  • wengine wanamsubiri.
  • Siki kumkaBili Meya na kumwambia ukweli. Iwapo umefanya, yapo mendi hayakunyoka. Mnajifikiria tu.
  • Si watu waliowachagua.
  • Tatu kumkaBili Meya na kumwambia hawawezi kufuata sharti la kurudi kazini ili malalamoko yao
  • yashughulikiwe.s
Subira/kutokata tamaa
  • Siki haachi kazi japo mazingira ya kazi ni mabaya.
  • Aliendelea na kazi hata mishahara ilipokuwa midogo.
  • Alivumilia mishahara ilipochelewa.
  • Aliendelea na kazi hata wafanyakazi walipokuwa wanadharauliwa.
  • Anasema hali ikibadilika, mshahara nao utakuja…
  • Anashauri wafanyakazi kuvuta subira badala ya kutumia migomo.
  • Diwani III anaelewa ugumu wa kufanya mapinduzi lakini hakati tamaa.
  • Waridi anakata tamaa na kuamua kuacha kazi baada ya kuona mazingira ya kazi yakiwa mabaya na mtoto
  • wao anapokufa kwa
  • kukosa dawa.
  • Diwani III hajafa moyo kuendelea kushauri Meya.
Ushauri/mawaidha
Mzuri/wa busara
  • Siki kumshauri tatu kuwa mgomo si njia bora ya kutatua matatizo.
  • Kumshauri asikate tamaa kutafuta nafasi ya kumwona Meya kumweleza matatizo yao.
  • Siki kumshauri Waridi asiache kazi.
  • Siki kumshauri Meya kushughulikia matatizo ya ukosefu wa dawa, mishahara midogo, na kuongezeka kwa
  • gharama ya maisha.
  • Alimshauri kutofuata maagizo ya nchi za nje kwani huo ni ukoloni mamboleo. Wazungu kuhimiza mfumo
  • wa kugawana gharama, nchi ni changa. Kupunguza idadi ya wafanya kazi, kufyonza uchumi wa nchi kupitia
  • mikopo.
  • Alimshauri asipumbaze watu kwa kutumia nyimbo za uzalendo.
  • Alimshauri kuwaSikiliza watu badala ya kuwakwepa.
  • Alimshauri asipime mafanikio ya mji kwa kujilinganisha na miji mingine ambayo ni duni kwao.
  • Diwani III kumshauri Meya kutoongeza mishahara ya madiwani pekee kwani ingeleta mivutano zaidi.
  • Madiwani walipe kodi ili nakisi ipungue.
  • Asitumie nguvu kuzima migomo bali aSikilize.
  • Kutafuta suluhisho la kudumu
  • Kuongeza mishahara kusitishwe mpaka uchumi utakapoimarika.
  • Meya alipuuza ushauri huu na kuwaona kama wachochezi wanaomtusi na kutaka kumpindua (usugu).
  • Harekebishi makosa akisahihishwa.
  • Siki kumshauri tatu watumie kongamano la maMeya la kila mwaka, wamweleleze Meya shida na
  • asiporidhia shughuli za usafi zizidi kususiwa.
Ushauri mbaya
  • Bili rafiki yake Meya na mfanyakazi wa jiji la Cheneo wanapanga na Meya kuiba fimbo.
  • Kumshauri Meya kupuuza madai ya wafanyakazi na kutumia nguvu.
  • Kushirikiana na mwanakandarasi kulifisidi baraza.
  • Kuuza fimbo ya Meya.
  • D I –Meya abuni kamati za kumuunga mkono-Meya kusema walipwe vizuri
  • Diwani II kumhimiza Meya kuendelea kumtenga diwani III.
  • Diwani I na II kumshauri Meya kutumia nguvu kuzima migomo.
  • Kuongeza mishahara ya madiwani na walinda usalama.
  • Atumie mashindano ya nyimbo za uzalendo kuwapumbaza vijana.
  • D I –wafanyikazi wafutwe na kuajiriwa wengine
  • D II –walinda usalama waongezewe mishahara na marupurupu kwa 20%
  • Wasitozwe kodi
  • Kutenga watetezi
Vikwazo vya uogozi/si lelemama/si rahisi
  • Wafanyakazi wanapigwa na kuvurumishwa na askari kwa vitoa machozi/mabavu
  • Waliogoma wanatishwa kufutwa kazi.
  • Gedi awaambie wafanyakazi watafutwa kazi na Meya.
  • Hongo.
  • Washauri wabaya na wenye tamaa.
  • Kamati za huduma za jamii.
  • Kutengwa/tenga utawale-Tunatengwa na maamuzi kufanywa-Diwani III
  • Sheria za kumlinda Meya
  • Kupumbaza watu-Vijana kushindania zawadi kwa kubuni, kutunga na kucheza nyimbo na kupewa zawadi
  • ndogondogo na kuonyeshwa katika vyombo vya habari.
  • Kuogofwa-anawasomea acts barazani
  • Meya kupewa uwezo mkubwa/nguvu nyingi- katiba/Sheria zinazompa uwezo Mayors act-inayompa uwezo
  • wa kuchukulia mtu hatua kali-Diwani III
  • Riot act-Anaweza kuitumia kukunja aliye chini yake kama ua wakati wa alasiri.
  • Collective responsibility-Kulazimisha kuwajibikia baraza badala ya wananchi
  • Diwani III anawaambia kujitolea kwa baraza kutetea demokrasia na hasa uhuru wa kujieleza.
  • Vitisho- Meya kusema atakayetaka kufanya kichwa basi na afanye.
Kiburi/majigambo/majivuno
  • Wewe tu ndiye hujui mimi ndiye Meya wa baraza la mji wa Cheneo?-Meya kwa Sosi
  • Lakini mimi Meya wako-kwa Sosi
  • Ni baraza gani lenye udhabiti kama letu ambalo linaongozwa na mstahiki Meya Sosi? Lipi katika ujirani
  • wetu?
  • Meya Sosi kujigamba ana pesa nyingi sana na anaweza kuchaguliwa hata mara sita.
  • Bili kujigamba kwa starehe anazopata.
  • Diwani II kujigamba kuwa ana uwezo wa kutumikia kamati ya Meya.
  • Hata mkitaka nne, tano na sita bado watanipa-Meya akijigamba anaweza kuchaguliwa na watu mara zaidi.
  • Akili hii walisema ni mali-majivuno ya Meya.
  • Udhibiti na ushawishi wa mambo ninao-Meya.
  • Diwani II kusema mzee alifahamu kuwa sisi ndio wenye uwezo na unamfaa
  • Nisipokuwa nazo, nani atakuwa nazo?-Meya
Dharau/Ujeuri
  • Meya kufahamisha wawakilishi wa wafanyakazi hana muda wa kupoteza kwa vile
  • baraza lilikuwa latarajia wageni siku iliyofuata.
  • Dida anatufahamisha kuwa wanatusiwa na kudhalilishwa na Meya.
  • Meya kutomSikiliza Siki
  • Meya kudharau elimu katika shule za umma-elimu ya kawaida isiyomvaa mzazi anayeona mbali.
  • Bili-ya kina yakhe-elimu ya maSikini
  • Bili-hakuna wakunga wazuri Cheneo
  • Madaktari wa kubabaisha
Hasira
  • Za watu dhidi ya viongozi
  • Meya ana hasira nyingi
  • Hasira-Unaona sasa? Mlinidanganya.-Meya anapoarifiwa vijana hawawezi kukubali kuchukua nafasi za
  • wafanyakazi wanaogoma kwani wameshapata picha mbaya ya baraza.
  • Anawajibisha wafanyakazi kwa hasira
  • Anamkemea Gedi.
  • Dida anamtumikia kwa kutetemeka.
  • Anapoudhiwa na Siki midomo inamcheza kwa hasira na kuita Gedi amwondoe.
  • Waridi anawakemea wagonjwa-mama Dadavuo Kaole.
  • Hivi uzionavyo-Meya anapoulizwa na Siki habari za leo ndugu Sosi
Anasa
Bili anajiandaa kisha amwombe Meya aende na mkewe na watoto wakajinafasi.
Haki
  • Siki ni mtetezi wa haki.
  • Anahimiza watu watibiwe hata kama hawana fedha.
  • Diwani III pia.
  • Haki za wanaCheneo zimekiukwa
  • Haki ya elimu
  • Haki ya kuishi-mtoto kufa kwa kukosa dawa
  • Haki ya kupata chakula
  • Haki ya kuishi katika mazingira safi
  • Haki ya usemi
  • Haki ya mishahara mizuri
  • Haki ya utulivu-wafanyakazi kuvurumishwa na askari
  • Haki ya huduma za matibabu
Uchochezi
  • Siki anachochea wafanyakazi kudai haki yao.
  • Siki amewahi kuchochea mgomo na Meya anataka kujua kama amechochea mwingine.
  • Anamchochea diwani III kuendelea kumshawishi Meya.
  • Ukosefu wa huduma za kijamii kuchochea wafanyakazi kugoma.
  • Siki kuchochea madiwani kuungana kuendelea kumpinga Meya.
  • Diwani II kumchochea Meya kuchukua hatua kali dhidi ya wachochezi.
  • Wananchi wengine kama vile Siki na viongozi wa wafanyakazi kuchochea kuleta mapinduzi.
Tamaa/uroho/kiu/kutotosheka
  • Bili kujifanya mshauri ili afaidike.
  • Meya anakula vyakula vingi vilivyoandikwa mezani.
  • Kutamani mkewe akajifungue ng’ambo.
  • Kutamani watoto wakasomee nje.
  • Kutamani kuvinjari au kujiburudisha katika mahoteli ya kifahari.
  • Anamwambia Meya ampeleke akastarehe.
  • Diwani I na II wanaomba posho wakati wafanyakazi hawajalipwa mishahara yao midogo.
  • Meya ananyakua vipande vinane vya ardhi na kuuza vitatu na kubakiwa na vitano.
  • Diwani 1-nguo nzuri
  • Diwani 1 kudai marupurupu-overtime
Ubinafsi
  • Meya kuagiza chupa moja ya maji ilhali wenzake hawaagizii.
  • Meya kujilimbikia mali ilhali wanaCheneo wengi ni maskini.
  • Madiwani kutotozwa kodi wakati mama muuza ndizi analipa kodi.
  • Meya, Diwani I na II na Bili wanakubaliana kuuza fimbo ya Meya ili kujinufaisha.
  • Waridi anajali maslahi yake zaidi-kuuliza Siki kazi hii ina faida gani kwangu?-anapotaka kuacha kazi.
  • Maji safi yanapatikana nyumbani kwa Meya tu.
  • Meya kuagiza yeye pekee mishahara ya madiwani iongezewe bila kushauriana na mtu.
  • Kubinafsisha hazina ya baraza ili kuimarisha umashuhuri wake.
  • Madiwani wana bima ya hospitali wakati watu wengine hawana.
  • Watoto wa Meya wanapata elimu bora ng’ambo wakati watu wengine wanapata elimu duni.
  • Meya anakula vizuri ilhali wafanyakazi wake wanakula makombo na viporo k.v.
  • mamake Dadavuo Kaole.
  • Diwani I anaamini jambo lililo muhimu ni yeye kushiba.
  • Anapendekeza waongezewe posho licha ya bajeti ya baraza kuwa na nakisi ya 120,000,000.
  • Diwani I anataka wanunuliwe suti nzuri sawa na madiwani wa nje.
Dhiki/shida/malalamiko
  • Za watu wa Cheneo
  • Kushindwa kumudu gharama za matibabu
  • Kukosekana kwa dawa-ahadi nyingi dawa zingeletwa
  • Gharama za maisha kuzidi kupanda
  • Mahitaji yao kuzidi kuongezeka
  • Kutopata kwa mishahara/duni
  • Kufa kwa njaa
  • Watu kufa kwa sababu ya kukosa dawa
  • Kutakiwa walipie dawa ilhali hata chakula walacho ni cha kuokota
  • Diwani III-watu wengi hawana ajira
  • Walio na ajira mishahara yao haitoshi/duni
  • Mishahara kucheleweshwa-hata kwa miezi mitatu hailipwi kwa wakati na hulipwa -nusu
  • Ukosefu wa ajira-vijana wbgi waliohitimu kutoka chuo kikuu hawana ajira-Meya.
  • Wafanyakazi wa baraza kutolipwa kwa wakati-Diwani 111
  • Hakuna maji ya kutosha hospitalini-Siki
  • Wafanyakazi kuosha vyoo bila glavu-Medi
  • Ahadi za uwongo
  • Ukosefu wa maji hata hospitalini
  • Uchafu hospitalini
  • Kukosekana kwa dawa
  • Kutakiwa kulipia matibabu/dawa ilhali madiwani wana bima
  • Tatizo la usafiri hadi kazini-kwa miguu kutoka mabandani mpaka viatu kuliwa na lami
  • Kuosha vyoo bila glavu
  • Kutoongezewa mishahara baraza likidai hakuna pesa ilhali lawaongezea madiwani.
  • Kukosa watetezi katika vikao vya maamuzi.
Ujinga
  • Diwani I haelewi kazi ya wafanyakazi kwa kufikiri ndege zinaweza kutua bila waelekezi.
  • Dida haoni haja ya kufanya mageuzi japo hali ni mbaya.
  • Anaomba msamaha hata kwa makosa ambayo hajafanya.
  • Meya haoni mbali. Hajui kuongezeka kwa shida za watu kuna kiwango kinachoweza kustahimiliwa.
  • Anatumia mali ya baraza la Cheneo kwa njia za kijinga ambazo hazileti faida.
  • Hajui mambo ananavyokwenda Cheneo. Anakuja kujua hatimaye kwamba
  • maji yanachukuliwa mtoni kwa punda.
  • Anadanganywa kwa urahisi na madiwani na rafiki yake Bili.
  • Wanamsukuma kwa njaa na tamaa yao lakini hatambui.
  • Waridi anaamini haraka anayoambiwa kama vile ahadi za Meya kuhusu dawa.
  • Mama haelewi umuhimu wa lishe bora
  • Mama kutofahamu usafi-kutotokosa chakula kabla ya kumpa mwanawe (Dadavuo Kaole)
  • kunakosababisha augue
  • Ujinga wa watu ndio chanzo cha uongozi mbaya.
  • Meya kutegemea mikopo kulipia mishahara-kuachia wajukuu ambao hawakufaidika na mkopo mzigo
  • Kuendesha baraza kwa mikopo na wageni wanaowapa mikopo ni washirika katika
  • maendeleo-riba ni mzigo kwa
  • kizazi kijacho-si uzalendo.
Busara
  • Diwani III anatambua sheria zinazomlinda Meya na madhara ya kushindana naye.
  • Anatambua kuwa watu wameamka na hawadanganyiki.
  • Siki anatumia busara kuwapa wagonjwa matumaini ya kuendekea kuishi.
  • Anaonelea wafanyakazi wasigome ili kuzuia kuteseka zaidi-mgomo una
  • madhara yake ni kufutwa -Siki kwa Tatu
  • Anaelewa kuwa watu wenyewe ndio huchangia uongozi mbaya.
  • Diwani II anatambua kwa wepesi hali inapoharibika.
  • Anaelewa mfuata nyuki hula asali kwa kukubali kila wazo linalotolewa na Meya.
Ubarakala
  • Diwani I ni mfuasi kipofu kwa kudharau na kukweza wale Meya anaowakweza.
  • Diwani I na II wanatenda mambo kumfurahisha Meya ili wafaidike kutoka kwake.
  • Kufurahisha Meya kwa kupiga vita waliotuchagua-Diwani 111.
  • Kufaa na kujifaa-wapaswa kujifaa kwa kufaa watu wao-Diwani III
  • Kuunga mkono hata yasiyofaa-Diwani 111
Huduma duni za jamii na athari zake
  • Afya-vifo vya wagonjwa
  • Afya-kukimbilia kutibiwa ng’ambo.
  • Elimu-kukimbilia shule na vyuo vya ngambo
  • Uchafu-magonjwa
  • Migomo
  • Wafanyakazi kuuawa
  • Viongozi kupoteza madaraka
  • Baraza kukosa wafadhili
Mapuuza
  • Hali ya kutojali
  • Meya anapuuza wafanyakazi na madai yao.
  • Meya hajali wagonjwa wanakufa.
  • AnapoSikia mtoto alikufa anauliza huyo mmoja tu. Unadhani wangapi wananiunga mkono?
  • Hajali baraza lina nakisi ya bajeti bali anaendelea kupanga matumizi zaidi.
  • Hajali wafanyikazi wake.
  • Hajali ushauri wa Siki na diwani III.
  • Meya hajali wafanyakazi wanapogoma-Wenye kugoma acha wagome. Vijana ambao wangeajiriwa kwa
  • mshahara wa chini.
  • Kupuuza Siki na wawakilishi wa wafanyakazi.
  • Kupuuza ushauri wa diiiiwani 111.
Uwajibikaji
  • Diwani III anaungana na kufanya kazi na Meya na madiwani japo wamemtenga.
  • Anafanya kazi yake kwa mujibu wa kanuni na taratibu za baraza.
  • Gedi anamjulisha Meya wageni wajapo, kupeleka maagizo kwa wengine na kumfahamisha
  • Meya yanayotokea.
  • Dida anamhudumia Meya barabara.
  • Waridi anatekeleza majukumu yake ya kutibu watu.  
  • Siki anapatikana kazini mara nyingi.
  • Anaulizia hali ya wagonjwa kila wakati.
  • Anawatibu na kuwapa wagonjwa matumaini japo hakuna dawa.
  • Anafanya jitihada ya kukutana na Meya kujua kuhusu kukosekana kwa dawa.
Utiifu
  • Waridi kufuata maagizo ya baraza kutotibu watu wasio na pesa.
  • Gedi anatekeleza maagizo yote ya Meya.
  • Askari wanatii maagizo ya Meya ya kutumia nguvu kuzima migomo.
Ubadhirifu
  • Utumiaji mbaya wa pesa au mali.
  • Meya anatumia vibaya pesa za baraza la Cheneo.
  • Kusomeshea watoto wake ng’ambo.
  • Kumpeleka mke wake kujifungulia ng’ambo.
  • Kumpeleka mke wake kutibiwa mafua ng’ambo.
  • Kutumia pesa nyingi kuwakaribisha maeya wageni katika mahoteli ya kifahari na vyakula
  • kutoka kila utamaduni duniani na mvinyo ulioagizwa kutoka urusi na divai kutoka ufaransa.
  • Kupanga kutumia pesa za baraza kumfurahisha na kumvutia mhubiri.
  • Kunyakua viwanja vya baraza pamoja na wandani wake na kuuza ili apate pesa.
  • Kumpeleka Bili katika hoteli za kifahari.
  • Kumpa Bili marupurupu japo si mfanyakazi wa baraza.
  • Kuongezea madiwani mshahara kiholela ili apate umashuhuri.
  • Watoto wa madiwani kusafirishwa kwa magari ya baraza hadi shuleni.
Udikteta
  • Meya anatumia mabavu kutawala.
  • Hatoi nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao.
  • Anatoa maamuzi kinyume na kanuni za baraza k.v. amri ya nyongeza ya mishahara kwa madiwani,
  • sadaka kwa mhubiri, kumlipa Bili na si diwani.
  • Ni mkali kwa wafanyakazi wake na wanamwogopa.
  • Kutumia nguvu kuzima mgomo wa wafanyakazi.
Vitisho
  • Meya kutishia kuwafuta wafanyakazi wakiendelea na mgomo.
  • Anamtisha Siki akirudi kwake atamwadhibu.
  • Anamtisha Siki asimchezee hata kama ni binamu yake.
  • Anamtisha Siki asipinge mipango ya milenia.
Ulaghai/ujanja
  • Meya kushawishi wafanyikazi warudi kazini ndipo madai yao yashughulikiwe.
  • Meya, madiwani na Bili kupanga kuiba fimbo ya Meya waiuze ng’ambo-Diwani 1
  • atoke nayo na kudanganya iliibwa wakati wa rabsha.
  • Kudanganya umma kwamba anaujali.
  • Kudanganya dawa ziko njiani.
  • Kupora vipande vya ardhi vya Cheneo.
  • Bili kumpa Meya mbinu ya kuibia pesa kwa kushirikiana na mwanakandarasi kuvunja mkataba, ashtaki,
  • atake alipwe fidia, wagawane, wakubaliane ampe fungu lake baada ya kulipwa.
  • Bili ni mjanja au kitatange kwa vile anawaingiza watu katika shida na kutoweka.
Udhabiti wa msimamo
  • Madiwani I na II hawana misimamo dhabiti kwani wanaunga lolote mkono lisemwalo na Meya
  • hata kama ni potovu.
  • Siki hayuko tayari kuacha kazi hata kama mazingira ya kazi ni mabaya na mishahara inachelewa.
  • Hakuyumbishwa na ushawishi wa Meya
  • Hakushawishika na diwani III na Tatu kumwona Meya kwa kuwa ni binamu yake.
  • Wawakilishi wa wafanyakazi Tatu, Medi na Beka wana msimamo imara.
  • Diwani II mwanzoni anamuunga mkono Meya kuwasukuma wafanyakazi lakini hatimaye anaona mbinu hiyo haifai.
  • Mwanzoni aliunga mkono kuwafuta kazi wafanyakazi waliogoma lakini mambo yalipobadilika
  • anapinga hatua hiyo.
Uzalendo
  • Siki hakubaliani na kuiga mambo yanayoamuliwa na nchi nyingine.
  • Anataka uongozi kuendeleza Cheneo badala ya kujiendeleza wenyewe.
  • Hakujali mahusiano ya kidugu na Meya bali maslahi ya Cheneo nzima.
  • Hafurahi kuliona jiji la Cheneo likiwa chafu.
  • Meya si mzalendo kwa kufuja pesa za baraza la Cheneo na kuiba fimbo.
  • Tatu, Medi na beak ni wazalendo.
  • Diwani III kupinga mipango ya kufuja mali ya umma.
  • Siki kutoacha kazi ili awasaidie wagonjwa-Afadhali kuteseka na hawa
  • wagonjwa-kujali maslahi ya wengine-si mbinafsi
Heshima
  • Mama kumwambia Waridi tafadhali mwanangu nihurumie
  • Siki ana heshima kwa Waridi
  • Madiwani kumsimamia Meya
  • Diwani 111 anamheshimu Meya
Walio waaminifu na wasio waaminifu
  • Diwani III kupinga mipango mipotovu na kutengwa.
  • Hana tamaa
  • Ni mkweli
  • Hana ubinafsi
Maudhui mengine
    1. uozo/ukosefu wa maadili/mkengeuko/utovu wa maadili
    2. wizi
    3. mauaji
    4. Uadilifu
    5. Uaminifu
    6. Majuto- Meya anajuta akisema heri angemSikiliza Bwana uchumi na kazi mambo yanapoharibika
Sifa/Hulka za wahusika
Kunao:
Waadilifu na wasiowaadilifu
Bidii
Wanaowajibika na wasiowajibika.
Wenye utu na wasionao
Walio na uzalendo na wasionao
Wenye tamaa na wasio nayo.
Wanaokata tamaa na wasiokata tamaa
Wavumilivu na wasio wavumilivu
Wenye msimamo na wasio nao
Wajasiri na waoga
Wenye mapuuza
Wafisadi
Watetezi wa haki/wakombozi
Wadanganyifu
Wanafiki
Wasaliti
Walaghai/wajanja
Wapenda anasa
Wabunifu
Washauri mbaya/mpotoshaji na washauri wema
Maskini
Wapole/Wanyenyekevu
Wajinga
Wenye kiburi/majivuno/majigambo
Wenye dharau
Wasioshaurika/sugu
Wenye hasira
Wabadhirifu
Walafi
Watiifu
Wenye mapuuza
Mabakala
Waaminifu na wasio waaminifu.
Meya hajali kesho-tuyashughulikie ya leo.
Ana masimango-Meya-kuwapatia kazi na mshahara.
Umuhimu wa Wahusika
  • Bili ni kielelezo cha marafiki wanaoweza kupotosha viongozi.
  • Mfano wa watu wenye tamaa iliyokithiri.
  • Bili, D1 na D11 ni vielelezo vya washauri wanaopotosha viongozi.
  • Vielelezo vya viongozi wasiowajibika.
  • Vielelezo vya viongozi wanaohujumu uchumi wananchi.
  • Vielelezo vya watu walio imara kuleta mageuzi.
  • Dida ni kielelezo cha wafanyakazi wanaohatarisha juhudi za ukombozi.
  • Askari ni vielelezo vya jinsi vyombo vya dola hutumiwa kuendeleza uongozi
  • dhalimu-askari kulinda baraza.
  • Mhubiri ni kielelezo cha jinsi dini inavyoweza kutumiwa kuendeleza uongozi dhalimu.
  • Mhubiri ni kielelezo cha viongozi wa dini wanafiki na wanaotumia dini kwa manufaa yao wenyewe.
  • Mama ni kielelezo cha wananchi wanaoathirika na uongozi mbaya.
  • Diwani III ni kielelezo cha uadilifu katika mazingira ya waliopotoka.
  • Madiwani I na II ni vielelezo vya ubarakala.
  • Wanatudhihirishia maudhui gani?
  • Wanatusaidia kutambua sifa za wengine vipi?
MATUMIZI YA LUGHA
Tashbihi
  • Kupinga haya ni sawa na kumkama simba mwenye watoto-Meya akimwonya Siki
  • asithubutu kupinga hoja zake.
  • Watu kujifia kama nzi.-tatu kwa Siki-kutokana na magonjwa kwa kukosa dawa
  • Juzi mtoto wa kerekecha amekufa kama nzi.
  • Inasimama (bahati) kama mtende-Siki anapompata D111 kwake.
  • Kushindana na Meya ni kama kushindana na ndovu-Diii-kuonyesha uwezo mkubwa alio nao Meya.
  • Inasimama kama ya mtende-Siki kwa D111-kufanikiwa kumpata kwake
  • Mimi na Meya ni mfano wa mafuta na maji-Siki na Meya hawapatati-mahasimu.
  • Kukunja walio chini yake kama ua wakati wa alasiri-riot act
Sitiari
  • Kueleza sifa za kitu kwa kusema ni kingine.
  • Himizeni hiyo miamba kuangalia maslahi ya watu-Siki akimwambia kheri.
  • Vitu hivi viwili (njaa na tamaa) kwa pamoja ni ugonjwa mbaya kuliko tauni.-D111-chanzo cha ushauri
  • mpotovu unaoharibu mji
  • Unakanyaga nyoka mkia.
  • Siku zote tumeshuhudia wasiotosheka wakipuliza tarumbeta zao za uzushi na sisi tukazizima kwa kukohoa
  • Ndiyo huko kuwaua ndege watatu kwa jiwe moja.
  • Lazima kwanza mhakikishe kuwa huyo sumu hapati hata fununu ya jambo hili-Meya kurejelea D111
  • Hii ni bomu inayoweza kutulipukia usoni-Meya-mpango wa wizi wa fimbo kuweza kuwatia matatani ukijulikana.
  • Duniani kuna watu na viatu, paka na panya-Dida
  • Bunduki inayotema risasi tatu tatu.
  • Magari yanayotapika maji.
  • Mshumaa kuwaka-kuendelea kuishi, kuwatia matumaini hadi dawa ziwasili.
  • Wana njaa na kiu ambayo haikuzimwa-Siki kwa Meya-malalamiko ambayo hayakushughulikiwa.
  • Kumtetea macho, maSikio na sauti Dwani I-ubarakala
  • Matunda ya jasho letu-Meya
  • Ni kawaida ya debe tupu kupiga kelele-Bili udharau wafanyakazi-wajinga.
  • Nina hakika sasa yuko kanisani mwake akiwahudumia kondoo wake-waumini
  • Njaa ina nguvu, imeangusha miamba-malalamiko ambayo hayakushughulikiwa huangusha viongozi.
  • Siasa ni mchezo mchafu-D111
  • Siasa bwana ina vituko vyake. Utapakwa tope si haba.
  • Umya hauna pato kubwa. Ofisi ndiyo ina mianya mingi ya kujipatia utajiri-kupewa majukumu ya
  • kuamua na hivyo kutumia fursa
  • kujinufaisha na wenzake.
  • Viongozi ni picha ya umma uliowachagua.-D111
  • Bili kumuuliza Meya kama mkewe alishapata mgeni-mtoto
  • Tumekuwa watumwa siku nyingi-Medi.
Jazanda
  • Uozo wa mji unamaanisha uozo wa uongozi wa Cheneo
  • Sumu inatumika kumrejelea Siki
  • Bomu kumrejelea Siki
  • Harufu mbaya-kiwakilishi cha uozo ulio ndani.
  • Punda kumaanisha wafanyakazi
  • Ndovu kurejelea uwezo wa Meya
  • Ndege watatu kumaanisha mambo watatu
  • Vyakula vya aina mbalimbali mezani-ulafi
  • Watu wenye matumbo yasoyotulia huwa akili zao nazo hazitulii.-watu wenye shida ambazo
  • hazijashughulikiwa hupigana hadi malalamiko yao yashughulikiwe.
  • Kukuna matumbo baada ya muda huanza kukuna vichwa
  • Kutembea nyuma ya punda aliyeudhika
  • Cheo kumlevya mtu kama mtoto na chakula. Atakienzi akiwa na njaa, Akishiba atakipiga teke,
  • hana habari
  • wapo wenzake wanakihitaji wala muda ukipita atakihitaji.
  • Beka -ni mgao wa wakubwa kula kwanza na sisi wengine kupigania makombo yanayoanguka chini
Tashhisi
  • Kiriba chaongoza
  • Kauli zinazoanguliwa katika matamshi hazitekelezwi
  • Wakisubiri ugonjwa nao utasubiri ?-Siki
  • Sembe na sukumawiki vinawatoa jasho kuvitia mezani-kushindwa kugharamia-Sosi kwa Meya.
  • Unadhani nyimbo zinawashibisha na kukata kiu ya uhitaji wao?-kushughulikia matakwa yao.
  • Bahati haifungui milango yake zaidi ya mara moja-Bili kwa Meya
  • Usafi umetwaliwa na nzi-Waridi kwa hospitali kukosa maji.
  • Mlango hatimaye huenda ukasalimu amri-Siki akimhimiza Tatu waendelee  kushinikiza kumwona Meya
  • huenda wakafaulu.
  • Cheo kinaweza kumlevya mtu asahau alipokuwa jana-D111
  • Viatu kuliwa na lami-Tatu kueleza jinsi wafanyakazi wanavyosafiri kwa miguu hadi kazini mpaka viatu
  • vinachakaa chini kwa kukwaruzwa na lami.
Mdokezo
  • Kukatiza usemi
  • Tatizo … utapia mlo lipo – Siki
  • Huenda itasaidia kidogo… mtoto aandaliwe mchanganyiko wa sukari na chumvi. (tashtiti)-si matibabu.
  • Meli kupambana na mawimbi-kuwasili
  • Lakini daktari ha…-Waridi kwa Siki-mama hajalipa/hana hela
  • Ni kama… talk of the devil-Bili
  • Lililoandikwa…-D III majaaliwa kukutana kwa D111 na Siki.
  • Nashangaa hiki chaleta taabu…
  • Nimefika kukuona kama ndugu…-Sosi kwa Meya
  • Huenda isichukue muda mrefu… (utabiri wa Sosi unaomtia Meya woga.)
  • Hali ikibadilika, mshahara nao utakuja…
  • Ni…ni…ni…-Gedi akisita wakati anataka kumfahamisha Meya wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamegoma
  • kuwaunga mkono wenzao waliogoma.
Balagha
  • Hilo pia wanatuletea sisi hapa?-Waridi
  • Dawa gani?-Waridi anapoulizwa na Siki kama dawa zimeigia.
  • Lakini si sasa waona matokeo yake-Waridi kwa mama-matokeo ya kumpa mtoto chakula ambacho hakikutokoswa.
  • Mpaka sasa wapo watu wasioelewa umuhimu wa lishe bora?-Waridi
  • Walipie kitanda kisicho dawa?-Siki
  • Tutafanya lipi jingine bora kuliko hili?
  • Kasi yote ya nini Waridi? Au dawa zimeingia?
  • Kweli kilio chetu kiliSikika pale pale. Nani atakuelezea?
  • Siasa gani hiyo?
  • Hilo tumefanya lakini wapi?
  • Chaguo la wananchi kwa nini basi kulalamika?
  • Au unafikiri pakawa na fursa nyingine hii leo ya kuchagua viongozi matokeo yatakuwa tofauti sana?
  • Kama wakubwa wenyewe wameisha sema sisi tutafanya nini?-kugawana gharama
  • Huoni mstari ulivyo mrefu hapo nje?-Waridi kwa mama.
  • Au unadhani hao wengine hawajakuja kutibiwa?-Waridi kwa mama.
  • Wewe tu ndiye hujui mimi ndiye Meya wa baraza la mji wa Cheneo?-Meya kwa Sosi-kuonyesha kiburi.
  • Ni baraza gani lenye udhabiti kama letu ambalo linaongozwa na mstahiki Meya Sosi? Lipi katika ujirani
  • wetu?-Meya-kuonyesha kiburi
  • Utatosheka lini wewe-Meya kwa Sosi
  • Huoni Cheneo ni kisiwa cha kupigiwa mfano?
  • Iwapo mama muuza ndizi analipa kodi ili kulijenga taifa, iweje kwamba madiwani wasilipe kodi?
Tabaini
  • Si vyombo vya habari, si wanasiasa, si wasomi-Waridi anapoulizwa na Siki nani alisema nchi ni maskini.
Kinaya
  • Meya kuwa na wokovu ilhali anatenda matendo yasiyofaa.
  • D1-kuitwa Bwana usalama ilhali anahatarisha usalama wa wafanyakazi kwa kuagiza askaris wawashambulie.
  • D11-Bwana uhusiano mwema
  • Ulimwenggu wataka watu kama wewe-Meya kwa Bili kwa wazo la mwanakandarasi
  • Anwani na jina mstahiki Meya-hastahili kuwa kiongozi
  • Bili, mshauri mkuu wa Meya kutopatikana mambo yanapochacha
  • Meya kumpa mhubiri sadaka ya laki moja kila mwezi ilhali amekosa kuwapa wafanyakazi wa baraza
  • mshahara na mji unakuwa mchafu mpaka unaanza kuvunda.
  • Ndugu Sosi-Siki
  • Sasa naona mnautusi ukarimu wetu-Meya kwa wawakilishi
  • Meya kuwaambia wawakilishi wa wafanyakazi kuwa baraza lina kanuni zake ambazo lazima ziheshimiwe
  • ilhali haziheshimu.
  • Kama hawataki kuonyesha shukrani kwa wanayofanyiwa na baraza letu tukufu, nitawafuta kazi
  • Meya kusema anapenda urasimu ilhali anaidhinisha mambo kama vile nyongeza kinyume na kanuni za baraza.
  • Nzuri tatu-tatu anapomuuliza daktari habari za siku nyingi.
  • Meya kushukuru madiwani kwa kufika kuhudumia baraza lao.
  • Ni baraza gani lenye udhabiti kama letu ambalo linaongozwa na mstahiki Meya Sosi? Lipi katika
  • ujirani wetu?-Meyakuonyesha kiburi
  • Meya kulinganisha baraza la Cheneo na majirani dhaifu ilhali wanaweza kufanya vyema
  • Huoni Cheneo ni kisiwa cha kupigiwa mfano?-Meya kwa Sosi-wakati kuna shida nyingi.
  • Miaka hamsini baada ya uhuru-miaka mingi kupita na watu wana umaskini-uhuru bandia
  • Mstahiki Meya-hastahiki/hastahili kuwa Meya
  • Akili hii walisema ni mali-Meya-hana akili
  • Kutaka idhaa za baraza zicheze nyimbo za uzalendo kabla na baada ya vipindi maarufu.-Meya
  • si mzalendo. Njia za kupumbaza watu.
  • Meya kusema Gedi ni miongoni mwa watu wenye uelewa.
  • Mji una amani na utulivu-Meya kwa Gedi
  • Lengo la mji ni afya bora na ya bure ilhali watakiwa kulipia matibabu
  • Mpango wa maendeleo wa miaka kumi. Meya ana malengo ya kimaendeleo ya milenia.
  • Tumeshaingia katika kiwango cha kimataifa.
  • Utetezi kuitwa uchochezi-Siki
  • Ndugu Meya-mhubiri kwa Meya
  • Wageni wanaokuja ni washirika wetu wa kimaendeleo-Meya kwa D111
  • Di kuwaita wafanyakazi wajinga-mtu mjinga hahitaji kubembelezwa ilhali ndio wajinga wa…
  • Sisi na yeye, nani ana akili zaidi-Bili akirejelea D111
  • Meya kusema wafanyakazi hawawezi kuwakilishwa katika baraza kwani lina kanuni zake ambazo mpaka
  • zifanyiwe mabadiliko ilhali hazifuati.
Kuchanganya ndimi
  • What do you think this is? Food poisoning?-Siki
  • Oh, yes
  • I understand
  • Dawa ni painkillers tu
  • Meya kuitisha glasi ya kunywea maji.
  • Yes sir-Gedi kwa Meya
  • Nina entertainment vote ya Meya yangoja ualishi tu.
  • Kuna mayers act, riot act
  • Kile kinachoitwa collective responsiBility
  • Hii ni grand idea-wazo la kusitiri wizi/kuzuia watu kuwashuku
  • Bloody hens-kudharau kuku waliotaga mayai
  • Nonsense-Meya anapokabwa na yai kwa kulibwakia
  • Fridge-jokofu/friji anakotumwa Gedi amtolee Meya chupa moja ya maji.
  • Faili-file
  • Kula sukumawiki na dona (doughnut)
  • Entertainment vote ya Meya ambayo yangoja ualishi-idhini ya pesa za burudani za Meya-ubadhirifu
  • Wawakilishi wa wafanyakazi wanapotaka kumwona Meya, wanaambiwa diary (shajara) yake imejaa-mapuuza.
  • Collective responsiBility-kunyima uhuru wa kwenda kinyume na jambo linaloungwa mkono na wengi.
  • Ikiwa hii si insubordination ni nini?-Meya kwa diwani III-kukosa utiifu
  • Full- proof-dii baada ya mipango ya kuiba fimbo kumaanisha haiwezi kugundulika.
Utohozi/uswahilishaji
  • Daktari
  • Nesi
  • Meya
  • Hospitali
  • Sista-mtawa wa kikatoliki
  • Wadi ya watoto
  • Ofisini-office
Takriri
  • Wafanya kazi wa jiji jinsi hospitali yenyewe ilivyo ya jiji.
  • Njiani ni njiani na hospitalini ni hospitalini.
  • Huna habari kuwa walinichagua hao hao watu-ujinga wa watu ndio chanzo cha uongozi mbaya.
  • Safi. Safi kabisa-Meya kuonyeshwa kuridhishwa na heshima za Gedi.
  • Sauti ni sauti tu!-Bili-kumhimiza Meya apuuze sauti za wafanyakazi.
  • Udumu milele na milele-mhubiri akiombea uongozi wa Meya.
  • hujui ngoja ngoja huumiza matumbo/Ngoja ngoja hii haisaidii matumbo-Siki kuhusu dawa
  • Mkumbushe tena na tena mpaka apate mwanga wa kile unachokisema-Siki kwa D111
  • Endelea, endelea Tatu-Medi akimhimiza aendelee kusema malamiko yao kwa Meya.
Misemo
  • Akili hii walisema ni mali-Meya-majivuno
  • Fununu sio mbali na ukweli-Meya-kuna wachochezi katika baraza-D111 kuuliza Meya kama ana hakika na
  • anayosema.
  • Na kumbuka mtumwa hauawi-Bili kwa Meya hawezi kufungwa kwa sababu alichukua hatua kwa niaba ya
  • baraza.
  • Bahati haifungui milango yake zaidi ya mara moja-Bili-kuhimiza asipoteze fursa ya kujipatia pesa kupitia
  • mwanakandarasi.
  • Mtu haukati mkono unaomlisha-Meya-hakikisho hawezi kumsahau Bili akipewa pesa na mwanakandarasi.
  • Wasemao mchana usiku watalala-Bili
  • Kelele za chura hazimzuii ng’ombe kunywa maji-Bili-sauti za wafanyakazi
  • Kubahatisha ndiko kupata-Siki anapompata D111 nyumbani kwake.
  • Lililoandikwa halifutiki kwa kweli
  • Eti siasa ni mchezo mchafu
  • Watu hujifunza kutokana na makosa yao
  • Mambo haya tunayafahamu tangu utandu hadi ukoko
  • Mambo yalikuwa yametiwa chumvi
  • Dawa ya adui ni kummegea unachokula-Bili kuhusu mwanakandarasi
  • Jina si kitu, tumbo ndilo muhimu
  • Misimu-kuwa mteja siku mbili-Bili kutopatikana baada ya mambo kuhariiiibika
  • Mtu hali kanuni
Methali
  • Huenda hizi ni dalili za mvua
  • Hujui ngojangoja huumiza matumbo-ugonjwa hauwezi kungojea dawa.
  • Kelele za chura hazimzuii ng’ombe kunywa maji-Bili-Meya hawezi kuathirika na mgomo
  • Haraka haraka haina baraka-Waridi kwa Siki
  • Ganga ganga za mganga humlaza  mgonjwa na matumaini
  • Wasemao mchana usiku watalala
  • Hizi ni Mbio za sakafuni-Bili-mgomo hautafanikiwa
  • Heri nusu shari kuliko shari kamili-Siki kwa Tatu-kucheleweshwa kwa mishahara ni bora kuliko kukosa kabisa.
  • Sikio la kufa haliSikii dawa-D111 kwa Siki anapomwambia anaweza kumshawishi Meya-ukaidi/hashauriki
  • Msiba wa kujitakia hauna kilio
  • Asante ya punda ni teke-kukosa shukrani -Meya anaposema aitiwe mhazili na kuambiwa na Gedi
  • ameshaondoka-alimpa kazi licha ya kutokuwa na hitimu zinazofaa.
  • Wengi wape-Meya kwa DIII
  • Mazoea yana taabu-kuacha tabia ni vigumu
  • Lililoandikwa…(halifutiki)-majaaliwa ya mungu kuonana na D111
  • Mtu huvuna alichopanda-viongozi wabaya huchaguliwa na wananchi.-D111
  • Mhitaji siku zote ni mtumwa-Meya kuonyesha wafanyakazi waliogoma wangelazimishwa kurudi kazini
  • na mahitaji yao ya kila siku.
  • Hakuna bwana, hakuna mtwana-D111 Meya anaposema wafanyakazi ni watumwa kuonyesha kuwa
  • wao na baraza wanahitajiana/huhudumiana.
  • Msiba wa kujitakia kilio kamwe hauna-Meya anapoSikia wafanyakazi wakivurumishwa
  • Mpiga ngumi ukuta…-Meya wakivurumishwa.
  • Yaliyopita yamepita. Tugange yajayo-D1 kwa Meya anapojuta kutomSikiliza D111
  • Ya mungu ni mengi-askari wanapoingia ofisini kumtia mbaroni Meya na washirika wake.
Majazi
  1. Sosi-kutokana na source kumaanisha chanzo cha matatizo au msimu uaomaanisha kula kwa kutumia
  2. cheo kujilimbikia mali.
  3. Kheri-kutokana na uadilifu kwa vile hana tamaa kama wenzake au baraka kwa jamii kwa kupinga maovu.
  4. Siki-kitu kichungu kinachotumiwa kama kiungo. Anasababisha machungu kwa viongozi kwa kupinga uovu
  5. wao. Anaongoza maandamano na kushauri Meya kushughulikia malalamiko ya wafanyakazi.
  6. Waridi-aina ya ua linalovutia lakini hunyauka punde tu linapotolewa mtini. Anawapa matumaini wagonjwa.
  7. Ghafla anajiuzulu na kuacha wagonjwa wateseke.
  8. Cheneo-kitu kilichoenea na kutapakaa kila mahali. Kuenea kwa uozo, mogomo, ukatili, shida n.k.
  9. Shuara –mji ambako ndege zilielekezwa baada ya wafanyakazi wa uwanja wa ndege kugoma-shwari, utulifu.
  10. Kajifahari-mkahawa ambao Meya na Bili waliuzuru-maarufu.
Ulinganuzi
  • Kuweka vitu viwili pamoja ili kusisitiza tofauti
  • Meya na diwani III
  • Diwani 111 na Diwani 1 na 11
  • Siki na Waridi
  • Shuara na Cheneo
  • Tatu, Beka na Medi na Gedi na Dida
Uzungumzi nafsia
  • Mhusika mmoja kuongea peke yake.
  • Hivi huyu ana nia gani-Meya Dida anapopeleka viyai vidogo
  • Meya kuongea peke yake kuhusu dhifa murua ambayo angewapa wageni mameya.
  • Meya anapojisemea mwenyewe kuhusu viyai vidogo alivyotengenezewa
  • Meya anapojisemea mwenyewe kuhusu mapokezi ya mameya ambao wangezuru Cheneo –vile angewapokea
  • kifahari ili watoe ufadhili.
  • Siki anapojisemea kuhusu matatizo ya Cheneo-vile mji umejaa njaa na kuongozwa na wenye njaa ni hatari sana.
  • Meya kujisemea diwani III anapomshauri akutane na viongozi wa wafanyakazi tu lakini si kila mtu.
  • Meya ofisini akipanga mapokezi ya mameya wageni-Cheneo si mji hivi hivi, wauone ukarimu na maana ya undugu wetu.
  • Meya kijisemea D111 anapoondoka-hawa wanaotaka uwaSikilize ni mzizi wa vizazi vya kesho! …Nafikiri ninaweza
  • kuzungumza na viongozi wao si kila mtu-tenga utawale
  • Meya kujizungumzia akiwa ofisini kupanga mapokezi ya wageni-atamfurusha mwanakandarasi, hatamu mpya, mipango mipya.
  • Dida katika wimbo wake jinsi wafanyakazi walivyofurushwa kwa risasi, vitoa machozi na magari ya maji.
Nidaha/siyahi
  • Pole!-Dida akimpa Meya pole
  • Alaa!-dii kushangaa anapoSikia wafanyakazi wa uwanja wa ndege wamegoma.
  • Kisha unamruhusu kunipunja kwa kuleta viyai kiasi hiki? Eeh?-hasira
  • Naam!-Waridi akimwitikia Siki
  • Alaa!-Siki akishangaa kwa wagonjwa kufika kwa wingi licha ya dawa kutokuweko.
  • La hasha!-Siki akisisitiza si habari za kugoma amepelekea Meya.
  • Sadakta! Bora usinisahau-sawa Bili-kuridhika
  • Pole!-Siki kwa Waridi kwa jamaa yake kufa-mtoto wa mamake mdogo-binamu
  • Asante-Tatu anapokaribishwa na Siki
  • Aamen-Meya akiitikia maombi ya mhubiri.
Mbinu rejeshi
  • Siki anarejelea amewahi kuanzisha mgomo mwingine
  • Uongo wa dawa kuwa bahari kuu unarejelewa mara kwa mara
  • Kitoto kufia mokononi mwa Siki kwa njaa na ugonjwa
  • Tunafahamishwa na Meya kuwa Siki alikuwa na utundu utotoni.
  • Bili kutukumbusha yeye na Meya wamewahi kwenda katika mkahawa wa kajifahari wiki mbili zilizopita kujistarehesha.
  • Meya amewahi kumpa Meya ushauri uliomdumisha mamlakani
  • Kuna mwanakandarasi aliyekuwa na mkataba na baraza alilomwambia.
  • D111-zamani Meya alikuwa anamSikiliza na kutilia maanani
  • Bili kutufahamisha jinsi wafanyakazi walivyovurumishwa na askari kila mtu na mguu wake kumponya
  • wanapoongea na Meya na madiwani.
  • Dida katika shairi lake anatufahamisha jinsiwatu walivyovurumishwa wakatimua mbio sana kwa kuogopa kuuawa.
  • Beka kueleza jinsi juzi mtoto wa kerekecha alikufa kama nzi mikononi mwa kerekecha akitazama.
  • Mama akieleza Siki mtoto alianza kuendesha lini siku iliyotangulia baada ya chakula alichotoa kwa bwana
  • kwa kutokitokosa wali na maharagwe yaliyolala.
  • Meya kutufahamisha kuhusu mwanakandarasi aliyepewa kandarasi na Meya wa zamani ya kupelekea
  • baraza bidhaa na ana mkataba ambao haujakwisha
  • na ungeisha miaka mitatu iliyofuata.
  • Siki kueleza jinsi mara ya mwisho alipokuwa kwa Meya jinsi aliamuru asiruhusiwe kuingia kwake
  • nyumbani au ofisini
  • Jinsi alivyofahamishwa hilo na mfanyakazi mmoja wa Meya aliyesoma naye shule moja.
  • Kufahamishwa na DI jinsi Bili alikuwa akipigiwa simu tangu siku kabla iliyopita na hakuwa akipatikana.
Taharuki
  • Mtoto kulazwa, kupewa mchanganyiko wa sukari na chumvi hatima yake gani?
  • Sauti za wafanyakazi
  • Askari wanapoingia Meya akiombewa na mhubiri-Nini kimejiri?
  • Wafanyakazi wa uwanja wa ndege kugoma wageni wakitarajiwa siku hiyo, nini kitajiri?
  • Mama anapoingia ghafla bila kufuata utaratibu Waridi anamkemea watakubali kumhudumia kwa dharura aliyo nayo?
  • Pale Gedi anapoingia ofisini ya Meya wakiwa na D1 na D11 akihema na akiongea kwa kusitasita, kimetokea nini?
  • Wageni kukaribia kuwasili na mji ni mchafu na hakuna uwezekano wa kuajiri vijana nini kitajiri?
  • Wafanyakazi kugoma na wageni wanatarajiwa kuwasili siku hiyo saa tano unusu usiku. Nini kitatokea?
Nahau/semi
  • Meya kumwambia Gedi amwambie Dida aende mbio
  • Yamenifika shingoni
  • Unamkanyaga nyoka mkia-Siki kwa Meya
  • Watu sasa wanafahamu mbivu na mbichi-D111 ukweli.
  • Ndiyo huko ndiko kuwaua ndege watatu kwa jiwe moja
  • Mlango huenda hatimaye ukasalimu amri
  • Wanakipeleka chombo mrama
  • Ni kazi ya kijungu meko/jiko-Beka-ya kumpatia mtu riziki tu.
  • Tangu utandu mpaka ukoko-wawakilishi kusema wanaelewa vyema yanayoendelea katika baraza,
  • kutenga DIII na
  • kufanya maamuzi na wanaomuunga mkono.
  • Kupiga hatua-kupata ufanisi/maendeleo mapya kila uchao-Meya
  • Unadhani nyimbo zinawashibisha na kukata kiu ya uhitaji wao?-kushughulikia matakwa yao.
  • Nyumba yangu aione paa-Meya-Gedi asimruhusu Siki asiwahi kuingia kwake.
  • Mbivu na mbichi-Diwani III
  • Kupunguza joto
  • Bili-ya kina yakhe-elimu ya maSikini
  • Bili kutaka kujua kama mkewe Meya ashajifungua-kupata mtoto.
  • Msikate tamaa-Siki kwa Tatu-msipoteze matumaini.
  • Inavunja moyo-kuona watu wakivurumishwa na askari-kuSikitisha
  • Si wengi wanaoweza kuwakosoa jamaa zao wanapokipeleka chombo mrama
  • Mimi niko radhi kutekeleza uyatakayo ingawa shingo upane-DIII kwa Meya anapomshinikiza-bila hiari.
  • Kazi ya kijungu meko-beka-isiyo na akiba/cha kuweka.
  • Tangu utandu hadi ukoko-Medi-wanajua yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho yanayoendelea katika
  • baraza.
  • Anaungana na mahasidi kunitoa roho-Meya anarejelea mhazili-kuporomosha uogozi wake.
  • Yote haya yametiwa chumvi na wanahabari-Meya akielekea kushikwa-kufanywa yaonekane makubwa.
  • Halafu nitiwe ndani-Meya kwa Bili –afungwe gerezani
  • Uma na kuvuvia-dhuru mtu kwa kutumia ujanja asielewe.
Taswira
  • Mwandishi anapotueleza kuhusu meza ya maakuli ya Meya kwamba imejaa mayai na vyakula
  • kutuchorea picha ya ulafi.
  • Maelezo ya Waridi huleta hali halisi ya zahanati.
  • Uvundo na maji ya taka unachora picha ya mji ilivyo.
  • Wafanyakazi wanavyokabiliwa na polisi kutembeza virungu na risasi.
  • Siki anapomwambia Meya kwamba anaingiza kidole kwenye mzinga wa nyuki-hatari.
  • Picha ya mtoto mgonjwa ya Waridi akimwambia Siki-kitoto chenyewe kiriba
  • chaongoza-kuvimba tumbo kwa utapia mlo.
  • Dida-picha ya hali ya mambo wafanyakazi walivyofurushwa-wazee kutimua mbio, bunduki,
  • magari ya maji.
  • Picha ya usafiri wa wafanyakazi na madiwani wakielekea kazini-kwa kutembea kutoka mabandani
  • jua likiwaka au kukinyesha na
  • viatu kuharibiwa na lami na madiwani wanasafiri katika magari yenye vifaa vya kusafisha hewa.
Tashtiti/kicheko/vichekesho/dhihaka
  • Meya kujifanya mwokovu na kutoa matamko ya kidini-Aamen, Aamen.
  • Meya kutumia pesa vibaya na wagonjwa wanapewa mchaganyiko wa chumvi na sukari.
  • Pale diwani na wandani wake wananaswa na askari baada ya mambo kufikia kiwango kibaya na
  • Bili hajulikani aliko
  • Diwani I na II wanacheka baada ya kuambiana kwamba siku zote wanazizima tarumbeta za
  • wasiotosheka kama kwa kukohoa tu.
  • Meya anacheka baada ya kujisemea kuhusu maandalizi ya wageni wanaokuja.
  • Diwani I na II wanacheka baada ya kuambiana kwamba siku zote wanazizima tarumbeta za
  • wasiotosheka kama kwa kukohoa tu.
  • Meya anacheka baada ya kujisemea kuhusu maandalizi ya wageni wanaokuja.
  • Dida anacheka baada ya kuigiza matendo ya askari walivyovurumisha wagomaji.
  • Meya na mhubiri kupokezana mikono wakicheka.
Utatu
  • Mtoto mgonjwa ana miaka mitatu
  • Alikufa akiwa na miaka mitatu
  • Kuua ndege watatu kwa jiwe moja
  • Madiwani watatu
  • Wawakilishi watatu wa wafanyakazi
  • Dawa zingefika bandarini baada ya siku tatu na baada ya siku tatu zingefika hospitalini
  • Meya na madiwani wawili wanakamatwa-jumla ya waliokamatwa ni watatu
  • Bunduki inayotema risasi tatu tatu-Dida akieleza kuhusu kuvurumishwa kwa wafanyakazi na askari.
Nyimbo
  • Sauti ya Siki anapojisemea
  • Njaa ina nguvu, imeangusha miamba-viongozi
  • Mwenye tumbo tupu anahitaji ashughulikiwe bila kucheleweshwa.
  • Sauti za wafanyakazi zinachukua muundo wa ushairi
  • Kilio-wanataka kuSikilizwa
  • Kudai haki, jasho, damu
  • Maslahi yao kuangaliwa
  • Malipo bora
  • Huduma za afya
  • Kudhalilishwa
  • Kupuuzwa daima
  • Mshahara zaidi
  • Dawa hospitalini
  • Sauti ya Dida
Kweli kinzani
  • Tumetembea lakini hatuendi mbele-Siki
  • Kwenda tunaenda lakini kinyumenyume
Chuku
  • Kufanya Cheneo kote kuwaka moto wa mafanikio-maendeleo makubwa
  • Kupuuzwa daima-sauti ya wafanyakazi-kukataa kabisa kusikilizwa
  • Wanadai takriban kila kitu-Gedi anapoulizwa na Meya wafanyakazi wanataka nini
  • Vijana waliohitimu kushindwa kupata hata utopasi-kusisitiza ukosefu wa ajira.-Meya
  • Udumu milele na milele-mhubiri akiombea uongozi wa Meya.
  • Kumbe wazee huwashinda mbio vijana-Dida-kutimua mbio sana kujinusuru.
Sadfa

  • Siku wageni wanatarajiwa kuwasili kusadifiana na mgomo wa wafanyakazi wa uwanja wa ndege na wale wa
  • bohari kuwaunga wenzao mkono.

  • Siku Siki anaenda kwa Meya na kwa DIII anawakuta wakiwemo.
  • Siku ambapo Meya na DI na II wanapokutana ndipo wanatiwa mbaroni.
  • Gedi kumpelekea Meya maji kunasadifiana na upepo kubadili mkondo wa harufu ya taka
  • na kufanya Meya kulalamika kuhusu maji.
  • Siki ni binamu ya Meya. Binamu yake Waridi kufa kwa kukosa dawa.
  • Bili-kusitiri wizi/kukomesha malalamiko-kutangaza fimbo imeibwa na uchunguzi unafanywa mara moja kisha kuanzisha
  • mazungumzo na wafanyakazi
  • na kufanya waonekane wao ndio wasiotaka suluhu.
  • Wizi kupagwa kusadifiana na mgomo ili kusingizia rabsha.
  • Ziara ya mameya wageni inasadifiana na migogoro baina ya baraza na wafanyakazi.
  • Ule wakati Meya anasema hali yataka kutumia nguvu na angewapa askari amri kunyoosha mambo ndipo askari wanatokea
  • si kufanya analotaka bali kumtia mbaroni.
  • Kutiwa mbaroni kwa Meya na diwani I na II kunasadifiana na wao kuwa katika mkutano wa kujaribu kutatua mambo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni