Jumatatu, 12 Februari 2018

KILIO CHA HAKI

  Tamthilia ya kilio cha haki
Katika tamthilia hii, Mazrui anakubaliana na mawazo ya wanauhalisia wa kijamaa, hayo yanadhihirika katika
utunzi wake wa tamthilia yenyewe. Anapowakuza wahusika wake haswa mhusika wake mkuu ambaye ni Lanina
anadhihirisha kutimia kwa mihimili wa uhalisia wa kijamaa. Anayakubaliana na mawazo ya uhalisia ya kijamaa
kupitia njia zifuatazo:
Katika nadharia ya kiuhalisia wa kijamaa kunakwepo  na wahusika wa kimaendeleo. Hawa ni wahusika wanao
lengo la kupindua na kubadili hali yao ya kimaisha, haya yanadhihirika katika tamthilia hii ya kilio cha haki kupitia
kwa wahusika kama Lanina, Dewe na Musa. wanajitolea kwa hali na mali kupinga uongozi mbaya wa mwajiri
wao Delamon. Japo wanasalitiwa na wafanyakazi wenzao kama vile Tereki, wahusika hawa wa kimaendeleo
wanakataa dhuluma dhidi ya wafanyakazi, jambo hili la utetezi wa haki za wanyonge linapelekea Lanina
kushikwa mara nyngi na kusingiziwa kuwa yeye ni malaya pia Delamon anapanga njama ya kumhonga Lanina ili
asitishe kauli yake kali ya uanamapinduzi.


Katika nadharia ya uhalisia wa kijamaa kunakwepo na hali inayonuia kuleta matumaini hasa katika kizazi cha
binadamu, hii ina maana kwamba mtu au watu fulani watakuwa na ushindi dhidi ya unyonyaji na unyanyasaji.
Katika juhudi zake Lanina, Dewe na Musa, wanao lengo la kuwapa matumaini wafanyakazi na kuwarai ili
wajiunge nao katika harakati zao za kiuanamapinduzi. Haya yanadhihirika wazi pale kwake mzee Ingeli
ambapo Lanina anaenda kufanya kazi kama mhudumu wa mkahawa lake mzee Ingeli kufuatia kufutwa kwake
kazi na bwana Delamon. Lanina anajihusisha katika maongezi na wateja waliokuja mkahawani kwa lengo la
kuhudumiwa. Hapo mkahawani Lanina anawashawishi wafanyakazi hawa wajiunge na Azimio lake la
kiuanamapinduzi, wateja hawa wanafurahishwa sana na mawazo yake Lanina. Mawazo haya yanaungwa
mkono na Mtu I anasema “ hawa washenzi wametuchambua kweli! Tunaumia sasa jamani!”
Uhalisia huu unaonyesha kwamba kunakwepo na harakati za kimapambano baina ya matabaka.katika
tamthilia yenyewe, haya yanadhihirika kunakozuka tabaka la juu linalotawaliwa na mabwenyenye kama
Delamon na tabaka la wachochole linalotawaliwa na kina Lanina. Mabwenyenye hawa wakiongozwa na
Delamon wanawatumia waafrika vibaya kwa kazi ngumu na mwishowe wanawapa malipo duni.  Wafanyakazi
wanapogomea hali duni za kufanyia kazi na pia kupinga mishahara duni wanayolipwa licha ya kuwekwa
kufanya kazi ngumu. Delamon anaita wawakilishi wa wafanyakazi hao ofisini mwake, wawalilishi hawa wa
kiwa Lanina na Tereki. Hapa anataka kuwaletea chai wanywe ili aweze kuwashawishi lakini Lanina anakataa.
Anawaambia kwamba watu hawapaswi kutoshana  kwa malipo, kwa hivyo anawaambia wakubaliane ili hao
wakaweze kuongezwa mishahara kina naye katika harakati zake za kufanya kazi, wafanyakazi hawa wanakata
a kukubaliana na uamuzi wa Delamon wa kutenga wafanyakazi wengine katika ongezeko la mshahara. Jambo
hili linapelekea kushikwa kwa wawakilishi wa wafanyakazi hawa. Japo Tereki anawasaliti imani ya
wafanyakazi wengine, Lanina anashimama na wafanyakazi wake bila kuongwa kwa njia yoyote. Hapa
Delamon anadhihirisha wazi kwamba katika jamii lazima pazuke matabaka tofauti tofauti ambazo zitakuwa
katika harakati ya kuzozana.
Pia Delamon anatumia nguvu na rasilimali aliyo nayo kuwatawanyisha wafanyakazi wanaogoma, hii inatokea
pale ambapo Delamon anampigia mkuu wa polisi bwana Hendeson anayekuja na kikosi cha askari
wanaotawanya wagomaji kisha kuwatia mbaoni wawakilishi wa wafanyakazi hawa.
Ijapokuwa kuna shida nyingi zinazowakumba wahusika hawa wa kiuanamapinduzi, hawakati tamaa,
wanajitolea kwa hali na mali kuhakikisha ya kwamba hali nzui ya maisha ya wafanyakazi umetekelezwa.
Baadhi ya matatizo anayopata Lanina ni  kama ; kukanwa na babake Lanina kwamba amekiuka maadili ya
kijamii haswa ya kiutamaduni kwa kujifanya mwanamume jambo hili linapelekea babake Lanina kumfukuza na
hata kumpiga mamake Lanina kwa tuhuma la kukosa kumfunza bintiye kuhusu maadili ya kitamaduni.
 Mwengo bwanake Lanina pia anapata shida sana na mkewe katika harakati zake za kutafuta mabadiliko.
Anakosa kumwamini mkewe tena kwa kuwa mara nyingi anamwona akishirikiana na wanaume. Jambo hili
linapelekea Lanina kuitwa malaya. Mwengo anapowapata wafanyakazi wenza wake Lanina nyumbani
kwake,anaanza vita na wao. Pia lanina akiwa korokoroni analazimishwa kukubaliana na mawazo yake
Delamon, anapokataa kachero I anampiga Lanina.
Mafanikio yanaonekana kutimia katika shamba la Delamon, hii baada ya bepari huyu kuuliwa pamoja na
vikaragosi wake Shindo na Tereki. Lanina anashikwa tena na kusomewa mashtaka ya mauaji ya Delamoni
kupitia maneno yake pale kwake mzee Ingeli.
                                    


Maoni 9 :