Jumatatu, 12 Februari 2018

KIFO KISIMAANI

                   TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd. Ina idadi nyingi ya wahusika ikiwemo mwelusi, mtemi Bokono Gege ,Tanya Azena Atega Kame  na Askari 1 ,11 na 111,Mweke  Talui Andua Kaloo
Mhusika mkuu ni Mwelusi. Mwelusi ni kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.
Anashikwa na kuteswa katika harakati zake za kuleta ukombozi butangi, mwishowe anauliwa baada ya kusalitiwa na nduguye Gege.
        MAUDHUI YANAYOJITOKEZA KATIKA KIFO KISIMANI
                                   Unafiki
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambia kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame walipanga jinsi watakavyo muua.
Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake tangu ujana wao.huu ni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi pia tanya anapompelekea mwelusi chakula gerezani askari 1 na 11 wanamwahidi kuwa watampa Mwelusi chakula Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa wishwa
                            Dhuluma na mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni .
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batu anapomtembelea baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapokataa Batu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawapa ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda
         
                                     Ubinafsi  
Gege anamuua Mwelusi nduguye ili apate kuozwa Alida bintiye Mtemi.Gege anamuambia Mwelusi hajali maisha yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine anajijali yeye mwenyewe.Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi aliyoamuru mtoto wake apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege pia anapinga hoja ya kuenda kumtazama nduguye mwelusi gerezani, anamwambia mamake tanya asimzomee anapoulizwa , yeye anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua . Hili linadhihirisha kuwa anawathamini wasichana kuliko nduguye mwelusi.
Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
                          Uongozi mbaya
Mtemi Bokono pamoja na vikaragosi wake Batu na Zige ni viongozi wabaya katika jamii ya Butangi, wanamshika mwelusi na kumtesa bila ya makosa anachapwa gerezani kinyama huku analia ingawa yeye anatetea haki za wanabutangi ,kisha utawala wa viongozi hawa unamshauri nduguye mwelusi Gege aue nduguye  Mwelusi kwa ahadi ya uongo wa kumpoza bintiye mtemi kwa jina Alida.
                              Uongozi mzuri
Kame, Askari 1 wanaonyesha uongozi mzuri wanapomtetetea haki za mwelusi wanaonyesha utu kwa maisha ya binadamu. Batu na Zige wanapotaka kumuua mwelusi Kame anasema aachwe kwa kuwa hana makosa.


                              SIFA ZA MWELUSI
mjasiri – anaamua kukabiliana na utawala wa Mtemi Bokono. Haogopi kuteswa na askari 11,111, batu na zige.
mwerevu- anauelimisha umma wa Butangi kuhusu uovu wa utawala wa Butangi na namna wanavyoweza kujikwamua kutokana na uongozi huo-mbaya
mzalendo- anapenda nchi yake ndiposa anajitolea mhanga kupigania mabadiliko, pia  anaongoza harakati za kukomboa Butangi kutokana na uongozi mbaya wa  mtemi Bokono.
   Mwenye busara- anajaribu kuwazindua wanabutangi  kimawazo dhidi ya uongozi mbaya
   Mwenye maarifa – anatumia maarifa kutoroka kizuizini kwa kukereza minyororo kwa tupa
  mbishi- anabishana na Zigu pale kisimani kuhusu matumizi ya kisima








                                          HITIMISHO
Kwa kuhitimisha inabainika kwamba mhusika mwelusi katika tamthilia ya kifo kisimani , kifo chake hatimaye kinaleta ukombozi kwa wanabutangi anapofungwa na uongozi mbaya Butangi unafikia kikomo. Japo ukombozi huu umepiganiwa kwa muda mrefu , mwishowe unashuhudiwa Butangi.
Katika riwaya ya mhanga nafsi yangu mhusika Afida anajipata pabaya zaidi kinyume na jinsi alivyofikiria kwamba kwenda kwake peponi kunngesuluhisha matatizo aliyokumbwa nayo, maisha yake yanasambaratika na hajiheshimu tena alivyojiheshimu Motoni kwa kujiingiza katika anasa.

















                                      MAREJELEO
Kithaka wa Mberia, (2001) Kifo Kisimani, Marimba Publications limited, Nairobi Kenya.
Mohamed, S. A. (2012). Mhanga Nafsi Yangu. Longhorn publishers.
Mugambi, P. J. M; (1982): “Uhakiki wa Maudhui katika Tamthilia za Kiswahili za Kenya Zilizochapishwa”.Tasnifu ya M.A: Chuo Kikuu Cha Nairobi
Wamitila, K.W; (2002): Uhakiki wa Fasihi Misingi na Vipengele Vyake.Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni