Jumatatu, 12 Februari 2018

SIKATE TAMAA

Mashairi ya Sikate tamaa
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa mashairi, yametungwa na mwandishi Said Ammed Mohammed. Mwandishi
huyu amefanikisha kuangazia swala la uhalisia wa kijamaa kupitia katika utunzi wake wa mashairi kadhaa
kama vile shairi la  ewe sarahangi, nimeamka,wananambia mchafu, nimeona, mbele ya  safari, nyoosha
mkono, watu hawajali, ukoloni na ukoloni mamboleo, viumbe vya Mungu  na hata katika shairi la imani
ya mwana.
Anaangazia dhana ya uhalisia ya kijamaa kupitia njia zifuatazo:
Wanauhalisia wa kijamaa huwa na lengo la kiupinduzi na kubadilisha hali yao ya maisha, haya yanadhihirika
katika shairi la ewe sarahangi. Mtunzi anahimiza kauli ya kuzindukana ili chombo isije kwenda mrama.
Anasema bado watu wanazozana ila bado ni mapema. Anahimiza harakati za watu kuelewana ili kusuluhisha
mzozano wao anahimiza kuwepo kwa kiongozi mmoja haya yanadhihirika anaposema kwamba  …nahodha
wengi chombo chaenda mrama.


Katika shairi la nimeamka mtunzi anaonyesha kauli ya kuzinduka na kuonyesha hiari fulani wa kutekeleza
upinduzi. Anakataa dhidi ya kudanganywa na  mahubiri matupu. Hapa anajaribu kupinga ahadi za uwongo.
Anakataa kutozungukwa na hawa watu  ambao ni mabepari wanaoeneza uwongo wao ili kufanikisha uongozi
wao duni. Anasema kwamba tiyari amelipenyeza jicho lake kuangalia dosari na anaibua maficho wenye viburi
. Katika shairi hili mtunzi anakubaliana na mawazo ya uhalisia wa kijamaa anapopinga kuzungushwa na
mabepari ambao wanaeneza uongo kwa wachochole.


Kunakwepo na tumaini katika uhalisia wa kijamaa juu ya  kizazi cha binadamu, hii inaonyesha kuwa hatimaye
mtu atakuwa mshindi dhidi ya unyonyaji ama unyanyasaji, wa aina fulani. Katika shairi la  mbele ya safari,  
mtunzi anasema kwamba safari walipoanzisha, ilijawa na shida na dhiki ya kila aina lakini walishikana pamoja
kupigania haki yao. Mtunzi anajaibu kueleza kwamba safari hiyo ilikumbwa na njaa, kiu lakini hawakukata
tamaa . walijawa na matumaini katika ari yao ya kutaka mabadiiliko. Mtunzi anaonyesha kwamba japo safari
yenyewe ilikumbwa na mashaka ya kila aina, walijawa tumaini kwamba mwishowe wangepata ushindi na haki
zao kutimia.


Katika uhalisia wa kijamaa kuna mgao wa kitabaka  katika jamii yaani tabaka la juu na lile la chini, haya
yanadhihirishwa na munzi wa shairi la  naandika . katika shairi hili mtunzi analalamika  hadi siku gani
watavumilia maovu hayo. Mtunzi analalamika kwamba wamechoka kuvumilia maovu, analeta swala la
utabaka  anaposema ...hawa wanaotulimiya,dhiki wavumiliayo hawa. Hapa linabainika wazi kwamba
wachochole  wananyanyaswa na mabepari fulani kuwafanyisha kazi ngumu. Anaendelea kusema kwamba
mabepari hawa hufaidika kwa kuwaponza hao na kuwadhulumu maskini. Wao kazi yao ni kujipa unene tu.
Kunazuka unyang’anyi na dhuluma dhidi ya wachochole katika uhalisia wa kijamaa, haya yanadhihirika katika
shairi la  sisimizi. Mtunzi analalamika kwamba wanakanyagwa, kupondwa na hata kuhujumiwa na mabepari
bila hao hata kuwaona kama binadamu.
Swala la utabaka pia linaangaziwa katika shairi la viumbe vya Mungu mtunzi anasema kwamba wapo
masikini wasiokuwa nacho vile vile kuna matajiri wenye fujo. Anasema kwamba wote ni viumbe vya Mungu.
Hapa kwenye shairi hili linadhihirika kwamba katika jamii la mtunzi kunazuka na masikini ambao hawana chao
ila kuna matajiri wanaowatelekeza kwa fujo.Anawahimiza kuweka subira kwake Mungu hatimaye wakafanikiwa.
Katika shairi la kisa mtunzi anatumia fumbo la kipanga na kifaranga anasema kwamba kipanga anaposhika
kifaranga kagwia, kipanga kimewakilisha mabepari na vifaranga wakawa wachochole, mtunzi anaeleza jinsi
mabepari hunyanyasa wachochole. Hivi kwamba wachochole wanatelekezwa katika hali duni ya  maisha yaliyojaa
dhuluma.










Maoni 1 :