Jumatatu, 12 Februari 2018

UHAKIKI

 

                                MHANGA NAFSI YANGU
Mhanga nafsi yangu ni riwaya iliyoandikwa na Ammed Said Mohamed katika mwaka wa 2012, kimechapishwa na  Longhorn publishers. Inazunguka katika maisha ya  Mhusika wake mkuu ambaye ni Afida
                                              MAHUDHUI                                                                                 
                                                  Usaliti
Usaliti unajitokeza kwenye wahusika wengi wakiwemo Afida anayesaliti ukoo wake na kukata minyororo yao huku akilalamika kurudishwa nyuma na utegemezi wa motoni.Afida pia anamsaliti mpenziwe Shabaan aliyemwandikia barua kila wakati tangu alipoenda peponi, Afida anakataa kujibu hizo barua, anadai kwamba mapenzi yake kwa Shabaan yaliisha. Usaliti huu unampelekea Shabaan kuugua ugonjwa wa moyo na hatimaye Shabaan anafariki. Vile vile Afida anawasaliti wazazi na walezi wake huku akisingizia kuwa alishafika alikotaka, Afida na Shuhudia wanaisaliti dini yao,kulingana na dini yao hakufaa kuingilia ulevi ambayo ni uasi wa kidini. Neshbosh bwanake Afida vile vile anasaliti ndoa yao na hatimaye kumfukuza Afida nyumbani pake. Majirani wake Afida wanamsaliti kwa kumsingizi Afida kwamba alikuwa akimlelea mtoto akiwa mlevi na kumdhalilisha, jambo hili linampelekea korti kutoa uamuzi wa kunyang’anyanywa mtoto wake Dinda.
                               Umaskini
Mataifa haya ya peponi wameyadhibiti masoko ya Motoni ambapo tunawaona wageni hawa wakija Motoni na kununua matunda kwa bei ya chini. Hii inasababisha umasikini kwa Wamotoni kwani hawafaidiki katika juhudi zao za kuzalisha mali.Kuhamia kwa Afida Peponi kulikuwa na msukumo wa kuasi ulitima na kusaka mali Peponi.Tunaelezwa kuwa Motoni kulikumbwa na umasikini kiasi kwamba hakuna jambo njema lolote lililoweza kumea, kuwa au kukua katika nchi hii . Afida alilalamika Jinsi kule kutegemeana kwa ukoo wa motoni kunavyozidisha umasikini hivi kwamba, mtu akionekana kufaulu, lazima ukoo ugawane mafanikio yenyewe hata kabla hayajazalisha. Eti mtu akifanikiwa kidogo, anakuwa mateka wa ukoo unaomnyofoa nyama harakaharaka na kumegwa kila upande hadi mtu huyo abaki mifupa mitupu. Hii ni ishara tosha kuwa Afida ametoka katika jamii iliyokumbwa na umasikini. Pia Katika maelezo ya Bi Sinangoa, tuanona kuwa Afida alilelewa kwa ukata kwani mara nyingi akienda kwa bibi huyu (Sinangoa) kupata angalau chakula. Wakati mwingine Afida akipata kwa Singangoa hakukuwa na chakula, bibi huyu alikuwa akimtafutia angalau visenti vidogo ilikununua chakula duni huko vijijini.Kazi aliyoifanya Bi. Mwamda baada ya kifo cha mumewe ni ishara tosha ya umasikini.
                                          Ndoa
Kunazuka ndoa kati ya bwana Bawa na bibiye Marneti ambaye ni mmotoni, ndoa hii inadumu ila inasongwa na tatizo la kutopata mtoto, jambo hili linawapelekea wapange njama ya kumsawishi Afida kuwapa mtoto wake Dinda. Afida anakataa jambo hili na kupelekea uhusiano wake na shangaziye Murneti kusambaratika.
Pia kunazuka ndoa kati ya Afida na Neshboch, ndoa hii imejawa na matatizo ya kila aina.Afida anadhalilishwa na kuulizwa maswali ya kumdhalilisha na dadake Neshboch kwa jina la Sheshaiza, anamwuliza siku ya harusi kama huko kwao Motoni amewahi kula vyakula vitamu kama vilivyo huko peponi, hatimaye ndoa hii inavunjika Neshboch anapomfukuza bibiye, Afida anajipata katika ndoa ya pili kwa lengo la kupata mtoto baada ya kunyanganywa pinda mtoto wake, anakuwa katika ndoa na saparata na wanapata mtoto kwa jina mkombozi.
                                 Tamaa
Wamotoni wengi wana tamaa ya kwenda peponi, wengine wameishi kufa kwa tamaa hii. Mwandishi anasema kuwa kuna wengine waliojaribu kukata jangwa la Sahara na kuishiwa kukumbwa na joto, kiu na kitaushi cha maji mwilini na ambacho  mara humpoteza mtu uhai wake, jambo hili linawapelekea wamotoni kuhamia Peponi wanakobaguliwa na kudhalilishwa, Afida pia anahamia peponi kwa tamaa ya kujiboresha kimaisha na kuiacha umaskini uliomkumba.Tamaa ya utashi unampelekea Afida kuolewa na mzee Neshbosh aliyemzidi umri.
                                   Ulevi
Ulevi inajitokeza kupitia kwa wahusika kama Afida, Neshboch, saparata na shuhuda, Afida na saparata wanaathiriwa zaidi na ulevi. Punde tu Neshboch anapomfunza ulevi, ndoa yao inaingia msukomsuko. Baada ya Afida kutalakiana na mumewa Neshboch anasingiziwa ulevi na majirani wake na hatimaye kunyang’anywa mtoto wake Dinda, hapo ndipo Afida anajipagaza hilo jina  na hatimaye kuwa mlevi wa kupindukia. Ulevi huu unampelekea Afida kuishiwa na pesa kwani baada ya talaka hakupata pesa tena kutoka kwa Neshboch. Hatimaye mtoto wake Mkombozi anapata katika harakati zake za kulewa anapoanza uhusiano na Saparata.
             Ukengeushi
Wamotoni  wengi wanapohamia Peponi huacha tamaduni zao na kuiga Wapeponi. Bi Marneti shangaziye Afida alipokuwa Motoni alithamini utu, umoja na hakuwa na tamaa. Alipenda mapenzi safi yasiyo ya pesa, kuuthamini ukoo wake na hakuropokwa ovyo. Alipohamia Peponi, alichukua tamaduni za huko na kutupilia mbali tamaduni za Ki-Motoni hasa alipokata uhusiano na ukoo wake kiasi cha kumdhulumu Afida aliyekuwa kama mtoto wake.Shuhuda rafikiye Afida aliyetoka Afrika aliiga Uzungu kwa mavazi, ulevi, hulka na hata lugha.Alivalia vijiguo vilivyomuacha tuputupu kama anavyodai Afida. Alivuta sigara ambayo inadaiwa kuwa haikumtoka mdomoni . Alienda kwenye mabaa na kushiriki ukware uliomfanya aambukizwe ukimwi. Mambo haya yote Shuhuda aliyaiga kutoka kwa Wapeponi ambapo hata Afida hakuamini kuwa ni Shuhuda aliyemfahamu kule Motoni. Shuhuda anasisitiza kuwa iwapo mwanamke yeyote anagependa mambo yake yamwendee vyema kule Peponi,hakuwa na budi ila kuonyesha mwili wake .
                                 Ubaguzi
Abiria waliokuwa kwenye basi na Afida walimtazama kwa chuki naye aliwapa tabasamu la kudanganya.Moyoni alielewa chuki ya hao abiria hasa bibi mmoja aliyezoea kupanda naye basi lilo hilo kila siku, kwamba ilikuwa ya kubaguliwa yeye kwani hakuwa Mpeponi. Chuki ilisheheni hata shuleni alikoenda Afida kwani alidhaniwa kuwa na fahamu ya chini kuliko wanafunzi wote waliokuwamo darasani. Anasisitiza kuwa wanafunzi walimtenga na kumuona dude tu. pia dadake Neshboch, Shesheiza anamwuliza Afida maswali ya kumbagua. Anamwuliza kwamba kama huko kwao pia wanakula vyakula vitamu jinsi vilivyo peponi.
                           SIFA ZA AFIDA
                                 Msomi
Afida anapoelekea peponi anajiunga na chuo cha peponi huku akigharamiwa na bwana Bawa na bibiye Murneti. Anasoma kwa bidii mpaka anapita somo fulani na kusemekana kuwa Afida ndiye Mmotoni wa kwanza kupita kiasi hicho baada ya miaka kumi na mitano, japo Afida hamalizi shule wala kufuzu anaonyesha nia ya kutaka kuendeleza masomo yake japo anakumbwa vizingiti kama kuolewa na bwana Neshboch.
                             Msaliti
Afida anayasaliti mapenzi yake na Shabaan ingawa alimwahidi kwamba angeasi mapenzi hayo, pia anasaliti walezi wake kama Sinangoa na Mamake kwa kutoshulika na wao anapofika peponi, anaandikiwa barua nyingi na wamotoni ambayo anayapuuza Afida.
                           Mkengeushi
Afida pamoja na Shuhuda wanauacha utamaduni wa motoni na kuiga utamaduni wa Peponi ,hili linadhihirisha katika nguo anazong’ara Afida, na ulevi wa kupindukia na hata hulka zake.

                            Mwenye bidii
Anapoolewa na Saparata anajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili ahikimu matakwa ya mtoto wao Mkombozi, ili ni baada ya Saparata kukataa kutoa msaada kwa mtoto wake Mkombozi.
                           Mpenda anasa
Afida anapopata talaka kutoka kwa mzee Neshboch  maisha yake yanachukua mkondo upya, anaanza kujiingiza katika vitendo vya anasa, hili linaanza pindi anaponyang’anywa mtoto wake dinda. Hajiheshimu tena anauza mwili wake kingono katika harakati za kupata pesa za kustahihisha mahitaji yake. Anaenda kwenye baa na kutamka wazi kwamba anataka mtoto na angependa apewe, maisha yake Afida yanachukua mkondo upya  asiwe afida aliyedhaniwa kuwa na msimamo dhabiti.

                                 Mlevi
Afida anaponyanganywa mtoto wake Dinda baada ya kusingiziwa na majirani yake kuwa mlevi, anajiingiza katika ulevi wenyewe huku maisha yake yanazoroteka katika ulevi.
                     Mwenye msimamo dhabiti
Anapoambiwa na bwana Bawa ba bibiye Murneti awapee mtoto wamtunzie anakataa wazo hilo na kutafautiana na mumewe na shangaziye. Pia yakrobich anapomtakia uhusiano wa kimapenzi anakataa na kuona isiyokuwa na maana.
B.        TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd. Ina idadi nyingi ya wahusika ikiwemo mwelusi, mtemi Bokono Gege ,Tanya Azena Atega Kame  na Askari 1 ,11 na 111,Mweke  Talui Andua Kaloo
Mhusika mkuu ni Mwelusi. Mwelusi ni kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.
Anashikwa na kuteswa katika harakati zake za kuleta ukombozi butangi, mwishowe anauliwa baada ya kusalitiwa na nduguye Gege.
        MAUDHUI YANAYOJITOKEZA KATIKA KIFO KISIMANI
                                   Unafiki
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambia kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame walipanga jinsi watakavyo muua.
Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake tangu ujana wao.huu ni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi pia tanya anapompelekea mwelusi chakula gerezani askari 1 na 11 wanamwahidi kuwa watampa Mwelusi chakula Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa wishwa
                            Dhuluma na mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni .
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batu anapomtembelea baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapokataa Batu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawapa ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda
         
                                     Ubinafsi  
Gege anamuua Mwelusi nduguye ili apate kuozwa Alida bintiye Mtemi.Gege anamuambia Mwelusi hajali maisha yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine anajijali yeye mwenyewe.Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi aliyoamuru mtoto wake apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege pia anapinga hoja ya kuenda kumtazama nduguye mwelusi gerezani, anamwambia mamake tanya asimzomee anapoulizwa , yeye anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua . Hili linadhihirisha kuwa anawathamini wasichana kuliko nduguye mwelusi.
Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
                          Uongozi mbaya
Mtemi Bokono pamoja na vikaragosi wake Batu na Zige ni viongozi wabaya katika jamii ya Butangi, wanamshika mwelusi na kumtesa bila ya makosa anachapwa gerezani kinyama huku analia ingawa yeye anatetea haki za wanabutangi ,kisha utawala wa viongozi hawa unamshauri nduguye mwelusi Gege aue nduguye  Mwelusi kwa ahadi ya uongo wa kumpoza bintiye mtemi kwa jina Alida.
                              Uongozi mzuri
Kame, Askari 1 wanaonyesha uongozi mzuri wanapomtetetea haki za mwelusi wanaonyesha utu kwa maisha ya binadamu. Batu na Zige wanapotaka kumuua mwelusi Kame anasema aachwe kwa kuwa hana makosa.


                              SIFA ZA MWELUSI
mjasiri – anaamua kukabiliana na utawala wa Mtemi Bokono. Haogopi kuteswa na askari 11,111, batu na zige.
mwerevu- anauelimisha umma wa Butangi kuhusu uovu wa utawala wa Butangi na namna wanavyoweza kujikwamua kutokana na uongozi huo-mbaya
mzalendo- anapenda nchi yake ndiposa anajitolea mhanga kupigania mabadiliko, pia  anaongoza harakati za kukomboa Butangi kutokana na uongozi mbaya wa  mtemi Bokono.
   Mwenye busara- anajaribu kuwazindua wanabutangi  kimawazo dhidi ya uongozi mbaya
   Mwenye maarifa – anatumia maarifa kutoroka kizuizini kwa kukereza minyororo kwa tupa
  mbishi- anabishana na Zigu pale kisimani kuhusu matumizi ya kisima

KIFO KISIMAANI

                   TAMTHILIA YA KIFO KISIMANI
Tamthilia ya Kifo Kisimani imeandikwa na kithaka wa Mberia 2009.kimechapishwa na Marimba Publications Ltd. Ina idadi nyingi ya wahusika ikiwemo mwelusi, mtemi Bokono Gege ,Tanya Azena Atega Kame  na Askari 1 ,11 na 111,Mweke  Talui Andua Kaloo
Mhusika mkuu ni Mwelusi. Mwelusi ni kiongozi katika shughuli za ukombozi wa butangi.
Anashikwa na kuteswa katika harakati zake za kuleta ukombozi butangi, mwishowe anauliwa baada ya kusalitiwa na nduguye Gege.
        MAUDHUI YANAYOJITOKEZA KATIKA KIFO KISIMANI
                                   Unafiki
Batu anapomtemebelea Mwelusi gerezani anamwambia kuwa ni rafiki yake na kumuomba ajiunge naye katika kuitumikia Butnangi.Huu ni unafiki kwani kabla ya hapo alipokuwa kwenye mkutano na Zigu na Kame walipanga jinsi watakavyo muua.
Mweke na Talui wanamhadithia Gege jinsi harusi yake na Alida itakavyokuwa. Wanamwambia Gege amuue Nduguye Mwelusi na atapewa mali pamoja na kuoa mtotot wa Mtemi Bokono.
Batu anapomtembelea Tanya anamwita rafiki yake tangu ujana wao.huu ni unafiki kwani Batu yuko pale kumtafuta Mwelusi pia tanya anapompelekea mwelusi chakula gerezani askari 1 na 11 wanamwahidi kuwa watampa Mwelusi chakula Askari wanakula chakula hiki na Kumuomba askari 1 ampelekee rafiki yake mkate wa wishwa
                            Dhuluma na mateso
Askari 11 anaeleza jinsi walijaribu kumgeuza mhutumiwa Fulani aache kuwa jiwe awe binadamu.Walimng’oa kucha za mkono na za miguu, walimgeuza kuwa popo na baadaye walifika katikati ya miguu yake na kupiga kambi hapo.badaye walimuua na kumzika msituni .
Mwelusi anafungwa gerezani kama hakuna kesi na hajahukumiwa.Batu anapomtembelea baada ya kumshawishi akiri kutochochea Wanabutangi na kushindwa anawaagiza Askari wazidi kumchapa na kumtesa
Batu anajaribu kuukinga uongozi wa Bokono na amamuomba mwelusi kuacha uchochezi na kuomba msamaha.Mwelusi anapokataa kukiri kwamba anatumiwa na majirani ili kuchafua Butangi. Anapokataa Batu anamwambia kuwa amepotoshwa . Batu anatoa ishara kwa Askari na kuondoka. Yeye anawapa ruhusa Askari wamtese mwelusi badala ya kumlinda
         
                                     Ubinafsi  
Gege anamuua Mwelusi nduguye ili apate kuozwa Alida bintiye Mtemi.Gege anamuambia Mwelusi hajali maisha yake aachane na jamii. Gege hajali maisha ya wnabutangi wengine anajijali yeye mwenyewe.Kaloo anamtuma zigu kwa Bokono amshukuru kwa ajili ya kazi aliyoamuru mtoto wake apewe.kaloo pia hajali juu ya Butangi yeye anataka awe na uhusiano na Bokono ili apate mali zaidi.
Gege pia anapinga hoja ya kuenda kumtazama nduguye mwelusi gerezani, anamwambia mamake tanya asimzomee anapoulizwa , yeye anaendelea kutengeneza ala na kusema kuwa wasichana watamtambua . Hili linadhihirisha kuwa anawathamini wasichana kuliko nduguye mwelusi.
Bokono,Batu,Zigu , Mweke na Gege wamefungwa kamba baada ya kufumaniwa na Waandamanaji.Hivyo wanaukombozi wanafaulu kukomboa Butangi kutokana na utawala Mbaya.
                          Uongozi mbaya
Mtemi Bokono pamoja na vikaragosi wake Batu na Zige ni viongozi wabaya katika jamii ya Butangi, wanamshika mwelusi na kumtesa bila ya makosa anachapwa gerezani kinyama huku analia ingawa yeye anatetea haki za wanabutangi ,kisha utawala wa viongozi hawa unamshauri nduguye mwelusi Gege aue nduguye  Mwelusi kwa ahadi ya uongo wa kumpoza bintiye mtemi kwa jina Alida.
                              Uongozi mzuri
Kame, Askari 1 wanaonyesha uongozi mzuri wanapomtetetea haki za mwelusi wanaonyesha utu kwa maisha ya binadamu. Batu na Zige wanapotaka kumuua mwelusi Kame anasema aachwe kwa kuwa hana makosa.


                              SIFA ZA MWELUSI
mjasiri – anaamua kukabiliana na utawala wa Mtemi Bokono. Haogopi kuteswa na askari 11,111, batu na zige.
mwerevu- anauelimisha umma wa Butangi kuhusu uovu wa utawala wa Butangi na namna wanavyoweza kujikwamua kutokana na uongozi huo-mbaya
mzalendo- anapenda nchi yake ndiposa anajitolea mhanga kupigania mabadiliko, pia  anaongoza harakati za kukomboa Butangi kutokana na uongozi mbaya wa  mtemi Bokono.
   Mwenye busara- anajaribu kuwazindua wanabutangi  kimawazo dhidi ya uongozi mbaya
   Mwenye maarifa – anatumia maarifa kutoroka kizuizini kwa kukereza minyororo kwa tupa
  mbishi- anabishana na Zigu pale kisimani kuhusu matumizi ya kisima








                                          HITIMISHO
Kwa kuhitimisha inabainika kwamba mhusika mwelusi katika tamthilia ya kifo kisimani , kifo chake hatimaye kinaleta ukombozi kwa wanabutangi anapofungwa na uongozi mbaya Butangi unafikia kikomo. Japo ukombozi huu umepiganiwa kwa muda mrefu , mwishowe unashuhudiwa Butangi.
Katika riwaya ya mhanga nafsi yangu mhusika Afida anajipata pabaya zaidi kinyume na jinsi alivyofikiria kwamba kwenda kwake peponi kunngesuluhisha matatizo aliyokumbwa nayo, maisha yake yanasambaratika na hajiheshimu tena alivyojiheshimu Motoni kwa kujiingiza katika anasa.

















                                      MAREJELEO
Kithaka wa Mberia, (2001) Kifo Kisimani, Marimba Publications limited, Nairobi Kenya.
Mohamed, S. A. (2012). Mhanga Nafsi Yangu. Longhorn publishers.
Mugambi, P. J. M; (1982): “Uhakiki wa Maudhui katika Tamthilia za Kiswahili za Kenya Zilizochapishwa”.Tasnifu ya M.A: Chuo Kikuu Cha Nairobi
Wamitila, K.W; (2002): Uhakiki wa Fasihi Misingi na Vipengele Vyake.Nairobi: Phoenix Publishers Ltd.



MHANGA NAFSI YANGU

MHANGA NAFSI YANGU
Mhanga nafsi yangu ni riwaya iliyoandikwa na Ammed Said Mohamed katika mwaka wa 2012,
kimechapishwa na  Longhorn publishers. Inazunguka katika maisha ya  Mhusika wake mkuu ambaye ni
Afida.
                           MAHUDHUI
                                 Usaliti
Usaliti unajitokeza kwenye wahusika wengi wakiwemo Afida anayesaliti ukoo wake na kukata minyororo
yao huku akilalamika kurudishwa nyuma na utegemezi wa motoni.Afida pia anamsaliti mpenziwe Shabaan
aliyemwandikia barua kila wakati tangu alipoenda peponi, Afida anakataa kujibu hizo barua,anadai kwamba
mapenzi yake kwa Shabaan yaliisha. Usaliti huu unampelekea Shabaan kuugua ugonjwa wa moyo na
hatimaye Shabaan anafariki. Vile vile Afida anawasaliti wazazin na walezi wake huku akisingizia kuwa
alishafika alikotaka, Afida na Shuhudia wanaisaliti dini yao,kulingana na dini yao hakufaa kuingilia ulevi
ambayo ni uasi wa kidini. Neshbosh bwanake Afida vile vile anasaliti ndoa yao na hatimaye kumfukuza
Afida nyumbani pake. Majirani wake Afida wanamsaliti kwa kumsingizi Afida kwamba alikuwa akimlelea
mtoto akiwa  mlevi na kumdhalilisha,  jambo hili linampelekea korti kutoa uamuzi wa kunyang’anyanywa
mtoto wake Dinda.
                               umaskini
Mataifa haya ya peponi wameyadhibiti masoko ya Motoni ambapo tunawaona wageni hawa wakija
Motoni na kununua matunda kwa bei ya chini. Hii inasababisha umasikini kwa Wamotoni kwanihawafaidiki
katika juhudi zao za kuzalisha mali.Kuhamia kwa Afida Peponi kulikuwa na msukumo wa kuasi ulitima na
kusaka mali Peponi.Tunaelezwa kuwa Motoni kulikumbwa na umasikini kiasi kwamba hakuna jambo njema
lolote
lililoweza kumea, kuwa au kukua katika nchi hii . Afida alilalamika Jinsi kule kutegemeana kwa ukoo wa
motoni kunavyozidisha umasikini hivi kwamba, mtu akionekana kufaulu, lazima ukoo ugawane mafanikio
yenyewe hata kabla hayajazaliwa. Eti mtu akifanikiwa kidogo, anakuwa mateka wa ukoo unaomnyofoa
nyama harakaharaka na kumegwa kila upande hadi mtu huyo abaki mifupa mitupu. Hii ni ishara tosha kuwa
Afida ametoka katika jamii iliyokumbwa na umasikini. Pia Katika maelezo ya Bi Sinangoa, tuanona kuwa
Afida
alilelewa kwa ukata kwani mara nyingi akienda kwa bibi huyu (Sinangoa) kupata angalau chakula. Wakati
mwingine Afida akipata kwa Singangoa hakukuwa na chakula, bibi huyu alikuwa akimtafutia angalau visenti
vidogo ilikununua chakula duni huko vijijini.Kazi aliyoifanya Bi. Mwamda baada ya kifo cha mumewe ni ishara
tosha ya umasikini.
                                          Ndoa
Kunazuka ndoa kati ya bwana Bawa na bibiye Marneti ambaye ni mmotoni, ndoa hii inadumu ila inasongwa
na tatizo la kupata mtoto, jambo hili linawapelekea wapange njama ya kumsawishi Afida kuwapa mtoto wake
Dinda. Afida anakataa jambo hili na kupelekea uhusiano wake na shangaziye Murneti kusambaratika.
Pia kunazuka ndoa kati ya Afida na Neshboch, ndoa hili limejawa na matatizo ya kila aina.Afida
anadhalilishwa na kuulizwa maswali ya kumdhalilisha na dadake Neshboch kwa jina la Sheshaiza, anamwuliza
siku ya harusi kama huko kwao Motoni amewahi kula vyakula vitamu kama vilivyo huko peponi, hatimaye
ndoa hii inavunjika Neshboch anapomfukuza bibiye, Afida anajipata katika ndoa ya pili kwa lengo la kupata
mtoto baada ya kunyanganywa pinda mtoto wake, anakuwa katika ndoa na saparata na wanapata mtoto kwa
jina mkombozi.
                                 Tamaa
Wamotoni wengi wana tamaa ya kwenda peponi, wengine wameishi kufa kwa tamaa hii. Mwandishi anasema
kuwa kuna wengine waliojaribu kukata jangwa la Sahara na kuishiwa kukumbwa na joto, kiu na kitaushi cha
maji mwilini na ambacho  mara humpoteza mtu uhai wake, jambo hili linawapelekea wamotoni kuhamia
Peponi wanakobaguliwa na kudhalilishwa, Afida pia anahamia peponi kwa tamaa ya kujiboresha kimaisha na
kuiacha umaskini uliomkumba.Tamaa ya utashi unampelekea Afida kuolewa na mzee Neshbosh aliyemzidi
umri.
                                   Ulevi
Ulevi inajitokeza kupitia kwa wahusika kama Afida, Neshboch, saparata na shuhuda, Afida na saparata
wanaathiriwa zaidi na ulevi. Punde tu Neshboch anapomfunza ulevi, ndoa yao inaingia msukomsuko. Baada
ya Afida kutalakiana na mumewa Neshboch anasingiziwa ulevi na majirani wake na hatimaye kunyang’anywa
mtoto wake Dinda, hapo ndipo Afida anajipagaza hilo jina  na hatimaye kuwa mlevi wa kupindukia. Ulevi huu
unampelekea Afida kuishiwa na pesa kwani baada ya talaka hakupata pesa tena  kutoka kwa Neshboch.
Hatimaye mtoto wake Mkombozi anapata katika harakati zake za kulewa anapoanza uhusiano na Saparata.
             Ukengeushi
Wamotoni  wengi wanapohamia Peponi huacha tamaduni zao na kuiga Wapeponi. Bi Marneti shangaziye
Afida alipokuwa Motoni alithamini utu, umoja na hakuwa na tamaa. Alipenda mapenzi safi yasiyo ya pesa,
kuuthamini ukoo wake na hakuropokwa ovyo. Alipohamia Peponi, alichukua tamaduni za huko na kutupilia
mbali tamaduni za Ki-Motoni hasa alipokata uhusiano na ukoo wake kiasi cha kumdhulumu Afida aliyekuwa
kama mtoto wake.Shuhuda rafikiye Afida aliyetoka Afrika aliiga Uzungu kwa mavazi, ulevi, hulka na hata
lugha.Alivalia vijiguo vilivyomuacha tuputupu kama anavyodai Afida. Alivuta sigara ambayo inadaiwa kuwa
haikumtoka mdomoni . Alienda kwenye mabaa na kushiriki ukware uliomfanya aambukizwe ukimwi. Mambo
haya yote Shuhuda aliyaiga kutoka kwa Wapeponi ambapo hata Afida hakuamini kuwa ni Shuhuda
aliyemfahamu kule Motoni. Shuhuda anasisitiza kuwa iwapo mwanamke yeyote anagependa mambo yake
yamwendee vyema kule Peponi,hakuwa na budi ila kuonyesha mwili wake .
                              Ubaguzi
Abiria waliokuwa kwenye basi na Afida walimtazama kwa chuki naye aliwapa tabasamu la kudanganya
.Moyoni alielewa chuki ya hao abiria hasa bibi mmoja aliyezoea kupanda naye basi lilo hilo kila siku, kwamba
ilikuwa ya kubaguliwa yeye kwani hakuwa Mpeponi. Chuki ilisheheni hata shuleni alikoenda Afida kwani
alidhaniwa kuwa na fahamu ya chini kuliko wanafunzi wote waliokuwamo darasani. Anasisitiza kuwa
wanafunzi walimtenga na kumuona dude tu. pia dadake Neshboch, Shesheiza anamwuliza Afida maswali ya
kumbagua. Anamwuliza kwamba kama huko kwao pia wanakula vyakula vitamu jinsi vilivyo peponi.
                           SIFA ZA AFIDA
                              Msomi
Afida anapoelekea peponi anajiunga na chuo cha peponi huku akigharamiwa na bwana Bawa na bibiye
Murneti. Anasoma kwa bidii mpaka anapita somo fulani na kusemekana kuwa Afida ndiye Mmotoni wa
kwanza kupita kiasi hicho baada ya miaka kumi na mitano, japo Afida hamalizi shule wala kufuzu anaonyesha
nia ya kutaka kuendeleza masomo yake japo anakumbwa vizingiti kama kuolewa na bwana Neshboch.
                             Msaliti
Afida anayasaliti mapenzi yake na Shabaan ingawa alimwahidi kwamba angeasi mapenzi hayo, pia anasaliti
walezi wake kama Sinangoa na Mamake kwa kutoshulika na wao anapofika peponi, anaandikiwa barua
nyingi na wamotoni ambayo anayapuuza Afida.
                           Mkengeushi
Afida pamoja na Shuhuda wanauacha utamaduni wa motoni na kuiga utamaduni wa Peponi ,hili linadhihirisha
katika nguo anazong’ara Afida, na ulevi wa kupindukia na hata hulka zake.


                            Mwenye bidii
Anapoolewa na Saparata anajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili ahikimu matakwa ya mtoto wao Mkombozi, ili
ni baada ya Saparata kukataa kutoa msaada kwa mtoto wake Mkombozi.
                           Mpenda anasa
Afida anapopata talaka kutoka kwa mzee Neshboch  maisha yake yanachukua mkondo upya, anaanza
kujiingiza katika vitendo vya anasa, hili linaanza pindi anaponyang’anywa mtoto wake dinda. Hajiheshimu
tena anauza mwili wake kingono katika harakati za kupata pesa za kustahihisha mahitaji yake. Anaenda
kwenye baa na kutamka wazi kwamba anataka mtoto na angependa apewe, maisha yake Afida yanachukua
mkondo upya  asiwe afida aliyedhaniwa kuwa na msimamo dhabiti.


                              Mlevi
Afida anaponyanganywa mtoto wake Dinda baada ya kusingiziwa na majirani yake kuwa mlevi, anajiingiza
katika ulevi wenyewe huku maisha yake yanazoroteka katika ulevi.
                     Mwenye msimamo dhabiti
Anapoambiwa na bwana Bawa ba bibiye Murneti awapee mtoto wamtunzie anakataa wazo hilo na
kutafautiana na mumewe na shangaziye. Pia yakrobich anapomtakia uhusiano wa kimapenzi anakataa na
kuona isiyokuwa na maana.