1.2 Mofolojia Dhana ya mofolojia
imeshughulikiwa na wanaisimu wengi kama vile Matthews (1974), Hartman (1972),
Richard et.al. (1985) miongoni mwa wengine. Neno hili limetoholewa kutoka kwa
neno la Kiingereza morphology. Neno hili limetumika katika taaluma zingine
kama vile:
Utabibu (human
morphology and anatomy) Sayansi ya mimea (plant morphology)
Jiografia (geomorphology)
Katika taaluma ya isimu
neno hili limekuwa likitumika kwa zaidi ya karne moja na linatumiwa kwa maana
ya somo au tawi la isimu ambalo huchunguza maumbo ya maneno na aina zake. Tawi
hili la isimu hushughulikia hasa kipashio cha neno. Wanaisimu mbali mbali
wameeleza maana ya dhana ya mofolojia.
Mathews (1974) anaeleza
mofolojia kama tawi la taaluma ya isimu ambalo linachunguza maumbo ya neno
hususan maumbo ya mofimu.
Hartman (1972) anaeleza
mofolojia kama tawi la sarufi ambalo hushughulikia kuchunguza na kuchambua
maumbo, fani, na aina za maneno yalivyo sasa pamoja na historia yake.
Kamusi Sanifu ya Isimu
na Lugha (1990) inaeleza mofolojia kama tawi la isimu ambalo huchunguza maneno
na aina za maneno.
Kwa ujumla, wanaisimu
wanakubaliana kwamba mofolojia inaweza kugawanywa katika makundi mawili makuu:
Mofolojia ambishaji
Mofolojia nominishaji
(i) Mofolojia Ambishaji
Hii ni mofolojia ya mnyambuliko wa maneno. Hapa vipashio hupachikwa na
kuongezewa kwenye mizizi ya maneno na kuzalisha maneno ya ziada yenye maana
tofauti. Mzizi wa neno haubadiliki kamwe. Matokeo ya minyambuliko si kupata
neno jipya bali ni kuongezea maana fulani ya kisarufi katika neno hilo. Kila
lugha ina taratibu zake zinazoongoza minyambuliko.
mzizi maneno
yaliyonyambuliwa mtu jitu, watu cheza chezwa, chezea, chezacheza, chezeana nk.
ruka rukia, rukiana, rukiwa, rukaruka, rukwa nk.
(ii) Mofolojia
Nominishaji Aina hii ya mofolojia pia hujulikana kama mofolojia ya uundaji.
Katika aina hii ya mofolojia, viambishi mbali mbali huongezwa kwenye mzizi wa
neno tukapata neno jipya kabisa. Neno linalozalishwa huenda likawa si la aina
moja na neno asilia. Kwa mfano, katika Kiswahili nomino huundwa kutokana na
vitenzi.
vitenzi nomino imba
wimbo, mwimbaji, kuimba, mwimbishaji
kivumishi kitenzi refu
refusha
1.3 Uainishaji wa Lugha
Kimofolojia Somo la mofolojia linatokana na hamu ya wanaisimu kutaka kujua
maumbo ya lugha tofauti tofauti. Katika kutekeleza jambo hili mofolojia
imewawezesha wanalugha kuziainisha hizo lugha katika makundi mbali mbali kwa
kuzingatia yale maumbo yake ya ndani. Uainishaji lugha kimuundo ndio umetumika
zaidi kuliko aina zingine za uainishaji kwa kuzingatia miundo ya lugha
mbalimbali. Jamii zifuatazo za lugha zimebainishwa.
(i) Lugha Tenganishi
Katika lugha hizi maneno huundwa kwa mofimu moja moja ambayo huwa ni neno zima.
Maneno katika lugha hizi hayaambishwi wala kutenganishwa katika vijisehemu
vidogo vidogo. Mfano mzuri wa lugha kama hii ni Kichina ambapo tutapata
sentensi kama hii:
Kichina Maana Wô mâi
jûzî chî I buy orange eat Kiingereza kina sifa hii pia lakini si sana. Tazama:
She will go He will come
(ii) Lugha Ambishi
Bainishi Katika lugha kama hii maneno yana viambishi mbali mbali. Viambishi
vinajidhihirisha moja kwa moja na mizizi ya maneno inajitokeza kwa uwazi.
Mizizi haichanganyishwi na
viambishi. Lugha kama
hii ina viambishi vya awali, kati na mwisho. Kila kiambishi hudhihirisha maana
fulani. Mfano wa lugha kama hizi ni pamoja na Kiswahili, Kijapani, Kifini na
Kituruki. Tazama mifano ifuatayo kutoka kwa lugha ya Kiswahili.
{m} {kulim} {a} {a} {ta}
{kuj} {a} {vy}{eti} {n}{zuri} {m}[toto]
(iii) Lugha Ambishi
Mchanganyo Lugha ambayo huchanganya viambisho na mizizi ya maneno kiasi kwamba
mtu hawezi kutenganisha viambishi na mzizi kwa urahisi. Mifano ya lugha kama
hizi ni pamoja na Kigiriki, Kilatini na Kiarabu. Katika lugha hizi maneno mengi
huwa changamano na husitiri zaidi ya mofimu moja. Kiingereza kina sifa hii kwa
kiasi. Tazama;
mouse mice come came go
went
Mifano hii ya Kiingereza
inadhihirisha mchanganyiko wa viambishi vya wingi kwa mfano (mice) na wakati
uliopita (came, went) na mizizi ya maneno.
Zoezi la 1.1 ?Je, somo la Mofolojia
lina umuhimu gani?
Kufikia hapa,
tumeangazia somo la mofolojia na matawi yake. Hebu sasa tuchunguze na kueleza
dhana zinazotumika sana katika somo hili ili kuliangazia zaidi.
1.4 Dhana Mbalimbali
Katika Somo la Mofolojia (a) Dhana ya Mofu Dhana hii ni gumu kufafanua
hata hivyo mofu ni udhihirishaji wa mofimu kama ilivyo foni kwa fonimu. Mofu ni
yale maumbo halisi yanayozua mofimu. Kwa mfano katika Kiingereza tuna neno cat
kwa umoja na cats kwa wingi. Neno cat ni mofu moja inayozua
mofimu ya kileksika. Neno cats ni mofu mbili inayozua mofimu ya
kileksika (cat) na mofimu ya kiambishi cha wingi (s).
(b) Dhana ya Mofimu Mofimu ni kipashio
kidogo cha kisarufi kilicho na maana (Hockett, 1988). Ni tamko ndogo lenye
maana. Mofimu ina sifa zifuatazo. (a) Mofimu ina umbo halisi (b) Ina umbo la
kifonetiki (c) Huwa na maana (d) Ina nafasi ya kisintaksia katika kuunda
vipashio vikubwa vya kisarufi.
kmf. neno mtoto lina
mofimu {m} + {toto} {m }- mofimu ya ngeli ya /1/ {toto} - mzizi
Ilhali neno anasoma lina
mofimu zifuatazo: {a } - {na } - {som } - {a}
nafsi - wakati - mzizi -
kiishio
Kuna aina kadha za
mofimu.
(i) Mofimu Huru Ni mofimu
zinazojisimamia kimaana na ambazo haziambatanishwi na viambishi vingine.
Zinakaa peke yake na zina maana kamili. Zinajitosheleza kimaana bila
kuunganishwa na viziada vyovyote kmf. kalamu, paka, taa. Aina hii ya mofimu
hujitokeza kama mofimu za kileksia na mofimu za kiwamilifu (Yule, 1985).
Mofimu za Kileksia Kundi
hili huwa na maneno ya kawaida pamoja na vivumishi. Mofimu hizi ndizo hubeba
ujumbe au maana ya ujumbe katika sentensi kmf. Sungura, Nairobi, Kenya, kaka,
kalamu, simba nk.
Mofimu za Kiwamilifu
Haya ni maneno yanayotenda kazi fulani katika lugha nayo huwa ni viunganishi,
vihusishi au vielezi. Tazama:
Viunganishi: lakini,
aidha, bila, ilhali, lakini nk. Vihusishi: nje, ndani, juu, pekee, kwa nk.
Vielezi : sana, leo, saa tatu nk.
Mofimu huru ni maneno
halisi.
(ii) Mofimu Funge Mofimu funge
haijitoshelezi kimaana bila viziada. Huambatanishwa na viambishi vingine kuleta
maana kamili. Hazikai peke yake na lazima ziunganishwe na mofimu zingine ili
zikamilike. kmf. kiambishi cha ngeli ya kwanza /m/ katika neno m-kora ni
mofimu funge. Hali ya mofimu hizi kukosa kujisimamia imepelekea wanaisimu
kuziita mofimu tegemezi. Zimegawanyika katika makundi mawili.
Mofimu Ambishi Mofimu
hizi ni viambishi ambavyo haviwezi kujisimamia na mara nyingi havibadilishi
mzizi wa neno. Kuna viambishi vifuatavyo:
mwanzo m-kulima kati
a-li-tumbukiz-a mwisho som-ek-a (ek ni mofimu mwisho kabla ya kiishio cha
kibantu -a)
Mofimu Nominishaji Hizi
ni mofimu ambazo hutumiwa kuunda maneno mapya. Maneno yaliyoundwa mara nyingi
huwa katika kikundi tofauti na maneno asilia.kmf.
kitenzi nomino pika
mpishi, mapishi, upishi ongoza kiongozi, mwongozo, uongozaji
(iii) Mofimu Tata Mofimu tata huwa na
maana zaidi ya moja. kmf. panda, paa, tunda, mbuzi nk.
(iv) Mofimu Changamano Huelezwa katika mkabala
wa muundo. Mofimu changamano ni mofimu ambazo huundwa kwa kuweka pamoja angalau
mashina au mizizi miwili ya maneno ambayo kwa kawaida huwa huru kmf.
mwanahabari, mwanasiasa, kiinuamgongo.
(v) Mofimu Kapa Hizi ni aina za mofimu
ambazo hazidhihiriki kwani ni za kidhahania. Mofimu kapa hazionekani katika
neno. Mofimu hizi hatuzioni, hatuziandiki wala kuzitamka ijapokuwa athari zake
zinahisika na kueleweka kmf. Nomino za ngeli ya 9/10 katika lugha ya Kiswahili
huwa na mofimu kapa. Tazama: nguo – nguo (neno hili lina mofimu
kapa kwani halibadiliki katika wingi. Pia maneno kama vile samaki au maji
ambayo yanapatikana katika ngeli ya 9/10. Maneno mengine katika ngeli ya
tano na sita (Ji/Ma) pia huwa na mofimu kapa katika umoja na wingi; kmf. debe,
kasha nk.
(vi) Mofimu Mzizi Mofimu mzizi ni ile
sehemu ya mofimu ambayo haibadiliki na ambayo hubeba maana ya kimsingi ya neno.
Hii ni mofimu ambayo inatufafanulia maana ya neno na mara nyingi mofimu za
ziada huambatanishwa nayo katika unyambuaji. Tazama mfano ufuatao; kutokana na
mofimu mzizi pik (pik-a) tunapata pikapika , pikwa, kupika, pikiwa,
pikiana nk.
Zoezi la 1.2 ? 1. Bainisha dhana
zifuatazo: mofu, mofimu na alomofu. 2. Huku ukitoa mifano kutoka kwa lugha ya
Kiswahili, bainisha aina mbali mbali za
mofimu
Hapa juu tumeeleza aina
mbali mbali za mofimu. Hebu sasa tuangalia jinsi ya kutambulisha mofimu na
kuzitenga.
1.5 Uainishaji wa Mofimu
Nida (1948) anaeleza
mofimu kama kipashio cha kiisimu ambacho hakifanani kifonetiki na kisemantiki
na kipashio kinginecho. Mofimu basi itatambulika kwa urahisi. Tazama mifano
ifuatayo katika lugha ya Kiswahili na lugha ya Kiingereza;
{m}{chez}{o}
{ha}{ta}{end}{a} {paka} {taa} {boy} {boy}{ish} {mad} {mad}{den}{ing}
Ili kutambua mofimu kwa
njia hii utalinganisha maneno yenye muundo karibu sawa kisha uyalinganishe na
utenganishe mofimu za maneno. Tazama;
{pik}{a}
{pik}{i}{a} {pik}{ik}{a}
{pik}{ian}{a}
1.5.1 Kanuni za Kutambua
Mofimu Nida(1949)
amependekeza kanuni sita za kutambua mofimu. Hizi kanuni zinategemeana na
hakuna ile inayojitosheleza.
● Kanuni ya kwanza inasema
kwamba maumbo ambayo yanafanana kifonetiki na kisemantiki yanabainishwa kama
mofimu moja. Maumbo haya yanapojitokeza huwa yanasimamia mofimu moja. Kmf.
katika Kiingereza kipashio {-er} kinapounganishwa na baadhi ya vitenzi kinaleta
maana ya mtu anayetekeleza kitendo fulani, na ni mofimu moja.
run runn-er dance
danc-er sing sing-er
Hata hivyo wakati
mwingine, kipashio hiki kinapojitokeza katika maneno mengine, kinaleta maana
tofauti. Tazama; broad-er, furth-er, clean-er na smart-er
● Kanuni ya pili ya
kutambua mofimu ni kuangalia maumbo yenye maana moja lakini yanayotofautiana
katika umbo la kifonetiki ambalo linaweza kuelezeka kifonolojia ( tunaweza
pengine kueleza athari zinazotokana na sauti zinazofuata). Maumbo haya huwa ni
mofimu moja ijapokuwa yanatofautiana kifonetiki lakini kisemantiki yana maana
moja. Katika Kiingereza kipashio cha kinyume hujitokeza kifonetiki kwa namna
tofauti tofauti ijapokuwa maana ni moja. Tazama;
{il} {il}legal
{il}literate
{im} {im}possible
{im}practical}
{in} {in}complete
{in}capable
{un} {un}necessary
{un}healthy
{ir} {ir}reversible
{ir}rational
Wakati mwingine maana
hubadilika kama inavyodhihirika katika mifano hii: invaluable, incredible,
infamous, ingenious, indispensable nk.
● Maumbo ambayo yana maana
sawa lakini yanatofautiana katika umbo la kifonetiki huwa ni mofimu moja. Mara
nyingi tofauti hizi za kifonetiki haziwezi kuelezeka kwa urahisi kifonolojia na
tena hazidhihirishi utaratibu maalum. Tazama mofimu ya wingi katika lugha ya
Kiingereza.
boy boys {-iz} pie pies
{-s) issue issues {-z}
ox oxen {-en} sheep
sheep {φ}
Hatuwezi kueleza
mabadiliko ya mofimu hii kwa urahisi.
Katika ngeli ya Ji/ma
katika lugha ya Kiswahili tunaona sifa hii kwa kiasi ambapo sura ya umoja na wingi
katika baadhi ya maneno inabadilika. Si rahisi kutambua mara moja majina katika
ngeli hii. Viambishi vya wingi ( na wakati mwingine vya umoja) kwa mfano katika
ngeli ya 6 vina maana moja lakini vina maumbo tofauti ya kifonetiki (wingi: ma,
me na φ; umoja ji, φ ) na haviwezi kuelezeka
kifonolojia.
mofimu za umoja/wingi
umoja wingi (ji) (me) jino meno jiko meko ( φ ) (ma) karatasi makaratasi
umbo maumbo ( φ ) ( φ ) jambazi jambazi
debe debe
● Kanuni ya nne ni
kutazama maumbile ya neno. Kama maneno yanatofautiana kimaumbile tu huweza kuwa
mofimu moja. Ikiwa katika maumbo tofauti inayojitokeza ni ya kimaumbile tu basi
maneno haya huwa ni mofimu moja. Tazama:
foot feet
● Homofoni hutambulikana
kuwa mofimu moja au mofimu tofauti kwa misingi ifuatayo. Homofoni ni maneno
yanayotamkika kwa njia sawa lakini yana maana tofauti. Tazama jozi za maneno
yafuatayo ya Kiingereza:
meat meet flour flower
pail pale threw through
bare bear tare tear sew
so Kumbuka
-homofoni zenye maana
tofauti huwa ni mofimu tofauti kabisa -homofoni zenye maana moja huwa ni mofimu
moja
● Kanuni ya sita ni
kuangalia mofimu katika mikabala tofauti. Mofimu inaweza kutambulikana kama:
(i) Inaweza kujitenga (kmf. mofimu huru {paka}) (ii) Inaambatishwa kwenye
kipashio kinachoweza kujitenga (kmf. mofimu tegemezi
{dance} +{er}
,{pig}+{an}+{a} (iii) Hujitokeza kama kiambishi pekee kama kitengo kinachoweza
kujitegemea kmf.
mwanajeshi mwana + jeshi
mwana hewa mwana + hewa askarijeshi askari + jeshi mitishamba miti + shamba
Katika mifano ya (iii)
hapo juu, sehemu mbili za neno zinajitegemea nazo ni mofimu tofauti.
Zoezi la 1.3 ? 1. Tumia kanuni
zilizopendekezwa na Nida (1949) kuainisha mofimu katika maneno
yafuatayo; Kuangaliana,
ng’oa, tembeleanatembeleana, ua, kula, choo, mwanafunzi, mwanaharamu.
1.6 Alomofu Alomofu ni maumbo
tofauti ya mofimu. Alomofu ina sifa mbalimbali. (a) Umbo halisi ambalo ni
sehemu ya neno. (b) Ni mofu mojawapo ya mofu za mofimu moja.
Alomofu basi ni sura
tofauti za mofimu moja.
Kwa mfano alomofu za
wakati ni pamoja na /li/, /na/, /ta/, /po/, /ka/ nk. Alomofu za umoja katika
ngeli ya kwanza ni /m/ , /mu/ na /mw/. Tazama:
mtu watu mwalimu walimu
muumba waumba
Kauli ya kutendeka ina
alomofu zifuatazo:
/ek/ shoneka pondeka
/ik/ pikika limika /lek/ toleka leleka /lik/ valika vulika /ikan/ takikana
patikana /ekan/ onekana ezekana /likan/ julikana
tambulikana /lekan/ ?
Jinsi ya kufanyiza ina
alomofu kadha wa kadha:
/iz/ fanyiza /ez/
pendeza /ish/ pigisha /esh/ endesha /liz/ tuliza /lez/ koleza /lish/ zalisha
/lesh/ tolesha
Alomofu huonyeshwa kwa
alama za msharazi / /.
Kufikia hapo tumeeleza
somo la mofolojia, dhana zinazotumika katika somo hili pamoja na mbinu/kanuni
za kutambua mofimu. Unaweza kutazama marejeleo yafuatayo kwa maelezo zaidi.
1.7 Maswali 1. Bainisha aina tofauti
tofauti za mofimu kwa kutoa mifano kutoka kwa lugha mbali
mbali za Kiafrika. 2.
Tumia kanuni zilizopendekezwa na Nida (1949) kuainisha mofimu katika lugha yako
ya kwanza.
Marejeleo ya Lazima Hartman, R. 1972:
Dictionary of Language and Linguistics. London: Applied Science Publisher.
Hockett, C. F. 1958: A
Course in Modern Linguistics. Newyork: Macmillan.
Matthews, P. 1974:
Morphology: An Introduction to the Theory of Word Structure.
Cambridge: Cambridge
University Press.
Nida, E. A. 1949:
Morphology: The Descriptive Analysis of Words. Michigan: Michigan University
Press.
Yule, G. 1985: The Study
of Language. Cambridge: Cambridge University Press.
SOMO LA 2 Uundaji wa Maneno
1.0 Utangulizi Mbali na kutuwezesha
kuziainisha aina za lugha, somo la mofolojia linahusisha uundaji wa maneno,
istilahi na utoaji wa maana ya maneno haya katika lugha husika (Nida, 1956).
(Tutapitia haya katika somo la 2)
Katika somo hili la pili
tutachunguza mbinu mbalimbali za uundaji wa maneno ambazo hutumika katika lugha
kwa ujumla. Pili tutaangazia kwa jinsi ambavyo mbinu hizi hutumika kuunda
maneno na istilahi katika lugha ya Kiswahili na pia tutazitathmini kwa
kuangalia matatizo yanayotinga uundaji wa msamiati na istilahi katika lugha ya
Kiswahili.
2.1 Shabaha •Baada ya kulipitia somo
hili, ninatarajia kwamba utaweza: 1. Kubainisha mbinu mbali mbali za kuunda maneno
katika lugha. 2. Kutathmini mbinu hizi kwa kuonyesha ni ipi zalishi zaidi. 3.
Kutoa mifano kutoka kwa lugha ya Kiswahili katika mkabala wa mbinu hizi.
2.2 Uundaji wa maneno Katika jamii, dhana,
matukio na vifaa mpya huzuka ambazo huhitaji kuzungumziwa. Basi panakuwa na
haja ya kuzua msamiati mpya kuzungumzia juu ya matukio haya mapya katika jamii.
Baadhi ya sababu zinazofanya watu wazue msamiati na istilahi mpya ni pamoja na:
1. Kuelezea dhana mpya zinazobuniwa. 2. Kwa sababu ya maendeleo ya haraka
katika nyanja mbalimbali za maarifa ya
binadamu kmf. sayansi,
uchumi, teknolojia, sheria, siasa, uchumi nk. 3. Uchakavu wa maneno ya awali
kmf. neno la zamani la damu katika Kiswahili ni ngeu
ambalo halitumiki tena.
4. Sababu za mila, aibu au wasifu ambazo watu hukwepa kutumia. 5. Maingiliano
ya kijamii yanasababisha haja ya kuunda maneno mapya kuwakilisha
maingiliano ya jamii
hizi. 6. Kufanikisha mawasiliano baina ya taasisi, matabaka na mashirika mbali mbali
Mbinu tofauti hutumika
ili kuunda msamiati mpya.
Zoezi 2.1 ? 1. Kwa nini maneno
katika lugha yaundwe?
2. Toa sababu ambazo
zimepeleka lugha ya Kiswahili kuunda istilahi
mbalimbali.
2.3 Mbinu za Kuunda
Msamiati na Istilahi (a) Mwambatano Mbinu hii inahusu kule kuunganishwa kwa maneno
mawili kuzua neno moja lenye maana mpya tofauti na maneno yaliyoiunda.
N + N mwana + jeshi → mwanajeshi
duara + dufu → duaradufu mbata +mzinga → mbatamziga mlango +mfuto
→ mlangomfuto
N + Kt nukta + tulia → nuktatuli
mwamba + dukiza → mwambadukiza
N + KV ng’ombe + jike → ng’ombejike
kiini + tete → kiinitete mja + mzito → mjamzito fundi + sanifu → fundisanifu pembe + nne → pembenne chungu + -zima → chungunzima
Kt + N pima + mvua → kipimamvua changa + moto
→ changamoto saga + gego → sagagego chemsha + bongo
→ chemshabongo fungua +
kinywa → kifunguakinywa
Kt + Kt yeyusha + ungana
→ myeyungano
Kt + KL ona + mbali → kionambali
●Upungufu wa mbinu hii ni
kwamba: Maneno mawili yenye maana tofauti uambatanishwa pamoja kuzua neno moja,
jambo ambalo lina uzito wa kisemantiki. Lakini yafaa maneno yatumike mpaka
yazoeleke.
(b)Unyambuaji Katika mbinu hii
viambishi vinaongezwa katika mizizi mwafaka kuizua neno mpya. Aina tofauti za
unyambuaji hutokea.
(1) Unyambuaji kwa kutumia
viambishi. Hapa maana mpya la neno hupanuka kupitia viambishi. kmf. Kutokana na
mzizi piga - tutapata
kupiga pigo pigana
mapigano
Kutokana na mizizi
mingine tutapata; mzizi neno lililoundwa zuri uzuri jamaa ujamaa ulevi mlevi,
vileo
Kupitia unyambuaji wa
viambishi nomino huundwa kutokana na vitenzi. Kitenzi nomino tafiti utafiti
chuma uchumi tawala utawala weza uwezo, mweza
(c) Kukopa Kukopa ni mbinu
inayotumiwa na lugha zote za ulimwengu kurutubisha msamiati wake. Kukopa
kunatokana na mambo fulani;
● Huenda neno linalokopwa
linasimamia kitu ambacho hakipo katika utamaduni kopaji.
● Kasumba ya uzungumzaji
hivi kwamba wazungumzaji hupendelea kutumia maneno fulani kuliko mengine kmf.
neno asili- neno la
kukopa kuanguka-kufeli kupita-kupasi pinde- kona mungu-mola
● maingiliano marefu ya
kitamaduni na kijamii
● Utabaka: Lugha
inayohisiwa kuwa ni ya tabaka la chini hukopa kutoka kwa lugha ya tabaka la
chini
Kiswahili huunda
msamiati, maneno na istilahi mpya kupitia mbinu ya kuazima maneno kutoka kwa lugha
zingine. Kiswahili kimeazima maneno kutoka kwa lugha za Kiarabu, Kiingereza,
Kifaransa, Kihindi, Kireno, Kituruki, Kishirazi, na Kijerumani nk. Maneno
yakiazimwa hubadilishwa kuchukua muundo wa KV ambao ndio asili kwa lugha ya
Kiswahili. Kiswahili kimeazima maneno kutoka kwa lugha za Kiafrika pia. (Mifano
tuliyotoa hapa chini imechanganyisha mbinu zote za ukopaji hata hivyo baadaye
tutazungumzia juu ya mbinu tofauti za ukopaji). Lugha Kopeshaji mfano wa maneno
Kishirazi mnara, nanga, kiwida Kihindi pesa, bima, laki, godoro Kituruki
baruti, bahasha, korokoroni
Kireno karata, pera,
bendera, mvinyo Kijerumani hela, barawani, shule Kiingereza Mei, daktari,
kampuni, eropleni Kiarabu Rehema, faraja, alhamisi
Kutoka lugha zingine za
Kiafrika tunapata ukopaji wa maneno kama yafuatayo;
Kinyamwezi ikulu,
kabwela, bunge Kikuyu matatu Kipare kitivo Kihaya lweya Kimasai mbuti, ngalemu
Ukopaji unakuwa ni wa
njia nyingi:
(i) Kukopa kwa
Tafsiri Katika mbinu hii vifungu katika lugha asilia hutafsiriwa katika
lugha kopaji. Kiswahili kimetumia mbinu hii kujenga msamiati na istilahi zake.
Tazama mifano ifuatayo:
Commissioner General
Kamishena mkuu District Officer Mkuu wa Wilaya Opposition Party Chama cha
Upinzani Rainbow Alliance Muungano wa Upinde wa mvua Basic principle Kanuni
Msingi Publicity Section Sehemu ya Uenezaji Electoral Commission Tume ya
Uchaguzi
●Upungufu wa mbinu hii ni
kwamba unaweza kupata tafsri ambazo hazileti maana inayokusudiwa kmf.
mobile phone - simu za kurandaranda
(simu za mikono) sick leave - likizo ya ugonjwa dictatorship -
uongozi wa imla (uongozi wa kimabavu yafaa zaidi)
(ii) Utohoaji Kupitia
kwa mbinu hii wanalugha wanachukua maneno kutoka kwa lugha asilia na kunukuu
kwa kuangalia fonolojia ya lugha pokezi . Neno linatamkika kwa utaratibu wa
lugha pokezi. Maneno yaliyotoholewa hupata maana kutokana na lugha asilia kmf.
atom - atomi virus -
virusi office -ofisi
doctor -daktari
● mbinu hii ina upungufu
mkubwa hasa pale ambapo utaratibu maalum haufuatwi tunaweza kuzalisha zaidi ya
neno moja. Tazama
dance- dansi, densi bank-
banki, benki officer- afisa, ofisa
●Utohozi wafaa kutilia
maanani utamkaji katika lugha pokezi ili tuzue maneno yasiyo tatanishi.
(iv) Kukopa sisisi Huu ni ukopaji wa moja
kwa moja. Hapa maneno yanachukuliwa yalivyo katika lugha changizi na kutumiwa
katika lugha kopaji.
Neno Lugha Changizi
Kitivo Kipare Ikulu Kinyamwezi Kasri Kihindi mbunge Kisukuma matatu Kikuyu
(d) Ufupishaji
Kuna mbinu kadhaa
zinazotumika katika kufupisha maneno ukapata mengine mapya.
(i) Ufupishaji mkato
Katika mbinu hii, neno hufupishwa kabisa na vifungu vichache hutumika. Tazama
mifano ifuatayo kutoka katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Kiswahili Kifupisho
bibi bi baba ba
Kiingereza Kifupisho jumbojet jumbo television teli examination exam
memorandum memo
refrigerator fridge photograph photo fanatic fan papa pa
(ii) Akronimu
Kutumia silabi za mwanzo
za maneno fulani katika kirai kuunda neno kmf.
Ukosefu wa Kinga Mwilini
UKIMWI
Taasisi ya Uchunguzi wa
Kiswahili TUKI Chama Cha Kiswahili cha Taifa CHAKITA
(iii) Uhulutishaji Ni
mbinu ambayo hutumika kwa kufupisha virai kupata maneno. Mara nyingi sehemu ya
mwanzo ya kirai cha kwanza huunganishwa na sehemu ya kwanza ya neno la pili
kuunda neno jipya. kmf.
msikwao mtu + asiye +
kwao
chajio chakula + jioni
mwambayavu mwamba + kama yavuyavu mala maziwa +lala
●Udhaifu wa mbinu hii ni
kwamba visehemu ambavyo si vya mwanzo hutumika pia. Tazama:
huhaba huduma hadi
bandarini
runinga rununu + maninga
● Wakati mwingine shina
nzima hutumika katika kuunda neno jipya. Tazama:
Kiua + dudu kiuadudu ute
+ mayai uteyai (egg yolk)
●Ukosefu wa mantiki wa
kutekeleza mbinu hii kwa ujumla. Hasa kwa kuamua ni kirai kipi kitakachotumika
kmf. fupaja kutoka kwa mfupa wa paja, je kwa nini si mfupaja kama
ilivyo mkono, mguu nk.
(e) Kubuni Hii ni mbinu ya kuunda
maneno isiyo ilihamu ya kifonolojia, kimofolojia au kiothografia. Kuna njia
mbali mbali za kubuni msamiati kwa kubuni. (i) kubuni kwa kinasibu (ii) kubuni
kwa kuongozwa na vigezo maalumu.
Kubuni kwa kinasibu
Huku ni kuzipanga fonimu
za lugha kulingana na utaratibu wa ujenzi wa lugha inayohusika iili kuunda neno
ambalo halipo katika lugha . Kwa njia hii maneno mapya ya lugha huundwa kwa
kuzingatia kanuni za isimu za lugha husika kisha yakapatikana dhana mbali
mbali. Njia hii hutatua tatizo la kuchukua maneno ambayo tayari yapo katika
lugha ya kushindiria mzigo mwingine.
ndege - kisopo golo - bureau
de change
●Mara nyingi neno
linaloundwa halina uhusiano na dhana linalosimamiwa au kitu kinachotajwa.
Tunakosa uhusiano wa kitajo na kitajwa. Pana tatizo kama watumiaji neno hilo
hawakuhusishwa na uundaji wake.
Kubuni kwa kuongozwa na
vigezo maalumu Vigezo kama maumbile, tabia au matumizi ya kitu vinaweza
kutumiwa kuongoza kubuniwa kwa neno. Hapa tunapata ubunifu ukifuata misingi ya
kionomatopea kupata majina kama vile;
pikipiki tingatinga
kengele firimbi gari la
moshi kifauwongo ndege msumeno nyeleo barua pepe mtandao
● Upungufu wa mbinu hii ni
kwamba inamfunga mwundaji istilahi kuambatanisha neno na kitajwa, jambo ambalo
haliwezekani kila mara.
(f) Uwawilishaji/
Uhamishaji Mbinu hii inahusu kuhamisha vipashio vya neno kuchukua nafasi
tofauti katika neno jipya linaloundwa. Pia uhamishaji maana wa neno la awali
likapata maana mpya. Tazama; -Vyaa (kwa maana ya zaa ) tunaunda avya (
kuhamisha sauti).
-Kupe (mnyama
anayenyonya ng’ombe damu) linatumika kwa mtu anayetegemea mwingine -Kifaru
(mnyama) linapata maana ya gari la vita
(g) Kuradidi Hii
ni mbinu ya kurudia neno au sehemu ya neno ili kuleta maana mpya. Kwa mfano;
kizunguzungu pilkapilka
wayowayo pikipiki polepole
(h) Ugeuzaji Hapa neno linageuzwa
kutoka kikundi kimoja kisarufi na kuingizwa katika kikundi kingine. Kmf.
mchezo mchezaji okoa
mwokozi, wokovu
2.4 Kumbuka!
Matatizo katika Uundaji
wa Maneno (a)
Maneno kubeba uzito kimaana. Tatizo hili linaweza kutatuliwa iwapo
maneno yatatumika mara
nyingi yazoeleke (hasa maneno ya kisayansi na teknolojia). (b) Kuwepo kwa
istilahi/maneno mbalimbali kwa neno moja kmf.
nomino, jina, nauni
runinga, televisheni mavi, kinyesi, mlima, kimba (c) Kutokuwa na utaratibu
maalum. Ukosefu wa ruwaza moja. Tazama mifano ifuatayo
kutoka somo la Biolojia;
Plasmagene - utoroji Plasmalema - ugoziuwili Plasmadesta -
kiuzichembe
Tazama pia mifano
ifuatayo kutoka somo la Isimu;
base - msingi, kiini cha
neno baseform - umbo msingi basecompound - neno ambatano (neno msingi lapotea
katika maana ya tatu) (d) Maneno mengine yanakosa “ukubalifu wa kimataifa”.
Katika biolojia kwa mfano, maneno fulani yametungwa lakini inaonekana kwamba
yanakosa ukubalifu wa kimataifa na ingekuwa mwafaka zaidi kama yangekopwa na
kuswahilishwa moja kwa moja.
Neno Neno
lililopendekezwa Neno ambalo lina umataifa mirage mazigazi miraji hydrophte
yungiyungi hidrofite hydrotropism ubadilihali hidrotropisimu
(e) Kuwepo kwa istilahi
chungu nzima kwa dhana moja. Ukosefu wa kutosanifisha istilahi ni pigo kubwa.
Katika somo la isimu kwa mfano, sauti za /m, n, ng' na ny/ huitwa sauti za
nasali /nazali / ving’ong’o au vipua. (f) Dhana zilizotoholewa hasa katika
lugha za Kiafrika ni gumu kufasiri kama mtu
hajui lugha asilia: kmf.
neno lugha asilia maana Kiangata Kisiu hob Chonyo Kipemba oedima Mlulu
Kipare Peata (g) Kutafsiri istilahi katika lugha za kigeni mara nyingine
kunapotosha dhana ya msingi liyokuwa katika istilahi za lugha chasili kmf.
lugha msingi tafsiri
Ofisi ya vipimo vya Taifa National Bureau of Standards Mapokeoni Reception
Zoezi la 2.2
?1. Jadili kwa kutoa mifano
njia mbali mbali ambazo Kiswahili kimetumia kujenga msamiati na istilahi zake.
2. Onyesha kasoro za
mbinu hizi. 3. Toa maoni yako kuhusu njia za kuboresha uundaji wa msamiati
katika lugha ya Kiswahili.
Kufikia hapa tumeona
mbinu mbali mbali za kuunda maneno na matatizo yanayotinga uundaji wa istilahi
katika lugha ya Kiswahili. Hata hivyo lugha ya Kiswahili imeendelea kujitahidi
katika uundaji wa istilahi na msamiati ili kufikia uasiriaji.
Marejeleo ya lazima Temu, W.C. 1984:
''Kiswahili Terminology: Principles Adopted for the Enrichment of the
Kiswahili Language'' katika Kiswahili Volume 51/1 na 51/2
uk. 112 –126. Dar es
Salaam: TUKI.
Mdee, J.S. 1986:
''Matatizo ya Kuunda Istilahi kama Yanavyojitokeza katika Kiswahili'' Katika
Mulika uk. 47 – 69. Dar es Salaam: TUKI.
Tumbo-Masabo, Z.M. 1982:
''Towards a Systematic Terminology Development in
Kiswahili'' katika
Kiswahili Juzuu 48/1 Dar es Salaam: TUKI.
SOMO LA 3 Nadharia ya Sarufi
3.0 Utangulizi Katika mada hii,
nitajadili nadharia ya sarufi mapokeo kama mkondo wa sarufi. Nitaeleza pia aina
mbalimbali za dhana ambazo hutumika katika mkondo huu wa sarufi. Aidha,
nitaeleza aina za maneno mbalimbali yanayofungamana na nadharia hii. Mwishowe
nitaitathmini nadharia hii kama mkabala mojawapo wa sarufi.
3.1Shabaha •Baada ya kulipitia somo
hili ninatarajia ya kwamba wanafunzi wataweza: 1. Kubainisha mikondo mbali mbali ya
sarufi. 2.Kufafanua dhana mbalimbali za sarufi mapokeo. 3.Kufafanua aina
mbalimbali za maneno. 4.Kutathmini nadharia ya sarufi mapokeo kama mkondo wa
sarufi.
3.2 Utangulizi Uchambuzi wa lugha ambao
umekuwa ukiwashughulisha wanaisimu kwa muda mrefu sasa umepita katika mikondo
mitatu mikuu. Misimano hii imesababisha kuzuka kwa nadharia tofauti za sarufi
ya lugha kwa kila mkondo. Nadharia hizi ni:
Sarufi Mapokeo ( pia
huitwa jadi) Sarufi Miundo ( pia hujulikana kama muundo/maumbo) Sarufi Zalishi
3.3 Sarufi Mapokeo
Historia Yake Mtazamo wa awali zaidi
ambao ulishughulikia lugha ulikuwa wa kifalsafa. Sarufi mapokeo iliasisiwa na
wanafalsafa wa ulaya hasa Ugiriki. Hawa walishughulikia lugha tangu karne ya
kumi na tatu. Wakati huu, lugha iliangaliwa kama kipengele kimoja cha uchunguzi
wa taaluma nyingine (za falsafa) kama historia, fasihi, dini, mantiki na
baalagha. Kule Ugiriki, kipengele cha lugha kilishughulikiwa katika taaluma ya
falsafa. Wachunguzi hodari wa falsafa ya kigiriki walikuwa Aristole na Plato.
Sarufi ya awali zaidi
ilitungwa na Myunani aliyeitwa Dionysus Thrax na iliitwa Techne Grammatike (The
Art of Grammar). Baadaye warumi walitumia mfumo wa kisarufi wa Wayunani katika
lugha ya Kilatini bila mabadiliko mengi.
Kati ya karne ya 12 hadi
ya 14 kikundi cha wasomi kilichoitwa Modistae kilitoa kazi mbalimbali
zilizojikita katika sarufi ya makisio. Mtazamo wao wa kisarufi ulikuwa
ukiitwa grammatica
speculativa. Waliamini kwamba kuna sarufi bia moja inayohimiliwa na
uhalisia na urazini wa binadamu. Kufikia karne 17, maoni tofauti ya kisarufi
yaliendelezwa. Kufikia mwaka wa 1700, sarufi za lugha 61 zilikuwa zimeandikwa
zikiwemo zile za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu na Kiitaliano.
Sarufi nyingi za mwanzo
ziliandikiwa kwa makusudi ya kufundishia. Pia walitaka kuzisanifisha kupitia
maandishi.
Katika kipindi hiki cha
maendeleo ya sarufi, wataalamu waligawanyika kimaoni wengine wakipendekeza
sarufi fafanuzi au elezi na wengine sarufi elekezi.
3.4 Misingi Ya Nadharia
ya Sarufi Mapokeo Mkabala wa Sarufi Mapokeo una misingi yake katika sifa maalum
ambazo zinaibainisha sarufi hii. Nadharia ya sarufi mapokeo basi inajikita
katika misingi ifuatayo:
● Lugha iliyochukuliwa
kuwa msingi wa sarufi ilikuwa Kilatini. Hii ni kwa sababu mambo mengi ya
kitaalamu wakati huo yalichunguzwa na kuandikwa kwa Kilatini. Lugha ya Kilatini
ilikuwa mojawapo ya lugha awali sana kuwa na maandishi. Lugha zote
zilichunguzwa kwa misingi ya Kilatini. Lugha zote ulimwenguni zilichukuliwa
kuwa na sarufi moja. Kwa muda mrefu lugha ya Kilatini ilichukuliwa kama
kielelezo cha matumizi ya kiwango cha juu kabisa cha lugha. Kwa hivyo
wanamapokeo, walichunguza na kuishilia na kanuni na sheria zilizoeleza matumizi
yake. Kanuni hizi zilichukuliwa kama kigezo cha kuchambulia lugha nyingine za
ulimwengu – hata Kiingereza. Kmf. Kilatini kina sifa ya kunyambulika kwa
maneno. Kwa kutumia kigezo hiki wanamapokeo walikiona Kiingereza kuwa na chembe
za sarufi kwani hakina sifa hii sana kikilinganishwa na Kilatini ilhali Kichina
ambacho hakina tabia hii kilisemekana kuwa hakina sarufi.
Kutumia Kilatini kama
kigezo cha kupimia lugha zingine ni makosa kwani kila lugha ina sauti, mitindo,
mbinu na sarufi ya kipekee. Isitoshe maoni kwamba lugha zote zinafanana
kimuundo na kiumbo ni dhaifu. Lugha zinatofautiana kwa njia mbalimbali. kmf..
Kwa upande wa msamiati tutapata maneno kama haya; Kiingereza Kiswahili
Kitharaka Gikuyu Kikamba water maji ruji mai kiw'u
Mawazo kama haya
yalizusha maoni kwamba hadhi ya Kilatini ilikuwa ya juu zaidi. Hata hivyo lugha
zote ni sawa kihadhi. Kila lugha inatimiza mahitaji ya wazungumzaji wake
kijamii. Tazama jamii nyingi za Kiafrika ambazo hazina maneno asili ya dhana
kama condom, computer, missile na rocket. Lakini zina maneno
yanayoshughulikia maisha ya kawaida ya jamii.
● Sarufi mapokeo
ilipendekeza kanuni za lugha Sarufi mapokeo ilieleza kwa jinsi ambavyo mtu
anatakiwa kuongea na kuandika. Kulikuwa na kanuni ambazo zilipasa kufuatwa
katika kutumia lugha kwa njia sahihi. Wanamapokeo walitoa sheria zilizoelekeza
namna ya kutumia lugha. Udhaifu wa kufanya hivi ni kwamba sarufi haipaswi kuwa
ya kulazimishwa inapaswa kuwa ya
kueleza. Walisahau
kwamba sarufi yapaswa kuangalia lugha kama ilivyo na kuieleza sio kulazimisha
sheria. Wazungumzaji hawatungiwi kanuni za jinsi ya kuongea lugha yao. Kila
mzungumzaji wa lugha fulani anazifahamu sheria za lugha yake bila sheria hizo
kutolewa wala kuandikwa. Sheria za lugha ni za kiasilia. Kwa kutumia umilisi
wake, mzungumzaji asilia anafahamu sheria zinazoongoza kwa mfano; wingi/uchache,
ukubwa nk.
● Kazi za kisanaa
zilihusishwa na falsafa. Kazi mbalimbali za wasomi mashuhuri wakati huo
zilichukuliwa kuwa ndizo zilizotumia lugha kwa njia sahihi zaidi. Matumizi ya
lugha nje ya ilivyotumika katika kazi hizi yalichukuliwa kuwa ni makosa. Hivyo
mtazamo wa lugha ukawa kuwa mabadiliko ya lugha yalikuwa ya kuharibu na kuwa
hatua ya awali ya lugha fulani ilikuwa bora na sahihi zaidi kuliko hatua ya
baadaye. Udhaifu wa mawazo haya ni kwamba walichukulia kwamba lugha haikui.
Kutokana na maoni haya vitabu vya sarufi vilivyoonyesha kanuni za utumiaji
sahili wa lugha vilitungwa.
●Walionelea lugha kuwa ni
ya kionomatopea Wanamapokeo walionelea kwamba kulikuwa na uhusiano wa moja kwa
moja kati ya neno na kile kinachorejelewa na neno hilo. Maneno kama kengele,
tingatinga na pikipiki – yanatokana na sauti inayotolewa na vyombo hivi. Katika
lugha nyingi za ulimwengu sio maneno yote ambayo yanaweza kuhusishwa moja kwa
moja na vyombo/vifaa vinavyozungumziwa. Maneno mengi hayachukui utaratibu huu.
Katika Kiswahili kwa mfano, maneno kama meza, kiti, ua na mengine mengi hayana
uhusiano na vifaa hivi.
● Walijishughulisha na
kueleza kategoria za sarufi kmf. nomino na vitenzi. Wanamapokeo walihakiki
sentensi kwa kutambua vipashio vyake mbalimbali. Waliangalia jinsi vipengele
hivi vilivyotumiwa – vizuri au kimakosa katika sentensi, pia walijaribu
kuvieleza vijisehemu hivi na kuvitolea maana. Walipanga vipashio vya lugha
katika makundi pia.
● Walionelea kwamba lugha
ya maandishi ilikuwa bora kuliko lugha ya mazungumzo. Kwa wanamapokeo, lugha
ilikuwa ile iliyoandikwa. Maoni haya yalishikiliwa sana na Wagiriki. Maoni yao
yanafungamana na neno la Kigiriki grammar yaani sarufi linalotokana na
neno la Kigiriki grammatike linalotumiwa kwa maana ya 'kuandikwa'. Kutokana
na neno hili basi wanamapokeo wakachukulia kwamba lugha yoyote ambayo haikuwa
imeandikwa au kuandikiwa sarufi haikuwa lugha kamwe. Lugha ya Kilatini ndiyo
iliyokuwa imeandikwa wakati huo. Sarufi za lugha zote za ulimwengu ziliegemezwa
kwa lugha ya Kilatini ambayo ilikuwa lugha ya wasomi wakati huu na tena
iliyoandikwa. Udhaifu wa mawazo haya ni kwamba lugha ya kuongea ndiyo kongwe
zaidi kuliko lugha ya kuandikwa, kabla maandishi yavumbuliwe, watu walikuwa
wakitumia lugha kwa kuwasiliana. Maandishi ni mbinu ya kuhifadhi lugha. Lugha
si maandishi wala maandishi si lugha. Kuna lugha nyingi za ulimwengu ambazo
hazijaandikwa kmf. Kidorobo na Kiogiek. Je hizi si lugha? Lugha ya kuongea
ndiyo yenye msamiati kamili. Maandishi yanawakilisha lugha ya kuongea. Isitoshe
sio rahisi kuandika maneno yote ya lugha au sentensi zake kwani mzungumzaji
asilia wa lugha fulani ana uwezo wa kuzua maneno na sentensi kochokocho.
Lugha ya mazungumzo
ndiyo yenye nguvu zaidi kwani inabadilika kutegemea historia. Lugha
iliyoandikwa haibadiliki. Mazungumzo yanazidi kubadilika kila mara kutegemea
wakati. Tazama Kiingereza cha wakati wa Shakespeare na cha sasa. Lugha ya
mazungumzo ni hai/tamu. Kupitia kwa mazungumzo mtu anatoa hisi zake
(kukasirika, furaha nk.). Isitoshe ishara hutumiwa katika mazungumzo. Kiimbo
katika lugha nyingi kinajidhihirisha zaidi katika lugha ya mazungumzo. Mara
nyingi maneno yanayotofautishwa na kiimbo hayaonyeshwi katika maandishi.
ZOEZI LA 3.1 ? 1.Toa historia fupi ya
lugha yako ya kwanza. 2. Unaweza kueleza baadhi ya sheria za sarufi za lugha
yako? 3. Eleza sifa bainifu za sarufi mapokeo 4. Je, nadharia hii inadhihirisha
kasoro gani? Zijadili
3.5 Dhana za Sarufi
Mapokeo Katika
sehemu hii nitaeleza dhana mbalimbali zinazotumika katika nadharia ya sarufi
mapokeo kama vile sentensi, kishazi, kirai na neno.
Neno Bloomfield (1933) katika
Language anaeleza neno kama kipengele cha lugha ambacho ni kidogo na ni huru.
Kipengele hiki huweza kutamkika peke yake. Katika sarufi mapokeo, neno
hutazamwa kama kipengele cha kimsingi. Neno lilitumiwa na wanasarufi mapokeo
lakini hawakutoa maelezo au ufafanuzi unaotosheleza. Tatizo hili lilitokana na
matumizi yao ya lugha andishi peke yake. Waliegemeza maana ya ''neno'' na
sarufi andishi.
Katika maandishi, neno
linatambulikana kwa urahisi. Tunaweza kutambua maneno katika sentensi kwa
kuangalia nafasi inayoyagawa na kuyatenganisha. Ikiwa kuna nafasi kati ya
vipashio viwili, basi kila kipashio kinachukuliwa kuwa neno. Katika lugha ya
mazungumzo, nafasi hizi zinafikiriwa kuwa zinasimamiwa na kituo au mtuo. Lakini
ukweli ni kwamba hatutui baada ya kutamka kila neno. Labda baada ya kila
sentensi, au kishazi au kifungu cha maneno. Tunaposikia lugha tusiyoielewa,
hatuwezi kusema ni wapi maneno yanapoishia. Hili linatufafanulia wazi kuwa
mazungumzo/au lugha ya kuongewa hujitokeza katika mkondo au mfululizo bila
kutua kwokwote. Ijapokuwa wanasarufi mapokeo walitumia neno bila kutia maelezo
yanayotosheleza, bado tunahisi kwamba dhana hii ipo. Tunaweza kuifafanua
kupitia kwa mitazamo mitatu.
●Mtazamo wa kwanza ni
kufafanua neno kama kipashio cha kisemantiki au maana. Hiki ni kipashio cha
kiisimu chenye maana moja. Hivyo basi, kila neno linasimamia maana moja. Tatizo
kuu hapa linatokea kwa sababu ni vigumu kueleza maana moja ni gani. Hili
hudhihirika zaidi tunapoangalia lugha ambazo si tenganishi yaani lugha za
uambishaji na lugha za unyambuaji (uainishaji huu ni wa Wihelm von Humboldt,
1836 aliyetajwa katika John Lyons, 1968). Lugha za uambishaji kama vile lugha
ya Kiswahili hutumia vipashio aghlabu vidogo vidogo na kuviongeza kwenye
vipashio vingine ili kupanua/kuongeza maana. Lugha za unyambuaji kama vile
Kilatini huongeza viungo
kwenye vipashio ili
kuonyesha uhusiano wa kisarufi huku viungo hivyo vikiongeza maana ya kisarufi.
Ikiwa kipashio kina
mofimu zaidi ya moja, inakuwa vigumu kushikilia kwamba kina maana moja kmf. mtoto.
Asilimia kubwa ya maneno ya Kiswahili yanayoonyesha idadi pamoja na ngeli kmf. mtu
au katika Kiingereza singer – sing + er. Kuna pia vipashio vyenye
maana moja lakini vikiungana, maana nyingine tofauti inajitokeza kmf. kula
rushwa; put up with. Ikiwa tunaeleza neno katika mkabala wa lugha
tenganishi, basi mtazamo huu unafaa. Lakini ikiwa tutakumbana na vipashio
vyenye maumbo tata, basi dhana ya maana moja inatatanisha.
●Namna ya pili ya
kufafanua neno ni kuliangalia kama kipashio cha kifonolojia au kifonetiki. Katika
mtazamo huu, neno hutambuliwa kwa kutazama sifa za kisauti. Katika baadhi ya
lugha, neno linaweza kuwa na ulinganifu wa vokali – yaani vokali zote
zinahusiana/zinashirikiana kisifa. Sifa hizi ni kama vile kuviringa, ambapo
vokali zote zina mviringo, kuwa juu, au chini na mbele au nyuma. Maneno ya
lugha ya Kiswahili huwa na tabia hii kmf. piga – pigia; choma – chomoa; tia –
tilia
Hata hivyo si lugha zote
ambazo zinazodhihirisha ulinganifu huu wa kifonetiki katika maneno yake. Mkazo
pia huweza kutumika ikiwa unapatikana katika mazingira maalum ya neno. Katika
Kiswahili, mkazo hupatikana katika silabi ya pili kutoka mwisho. Hivyo tunaweza
kutambua kipashio fulani kama neno tunapotia mkazo katika silabi hii. Katika
neno mwana + hewa = mwanahewa (tutaweka mkazo katika silabi-ha).
(mkazo: utamkaji wa
nguvu zaidi katika sehemu fulani ya neno)
●Neno linaweza
kufafanuliwa kwa kufuata mbinu mbalimbali za kiisimu. Mtazamo huu hulenga
kwenye wazo kwamba neno linaweza kutengwa ili lijisimamie. Vile vile haliwezi
kuchanganuliwa na ndani yake mkapatikana maneno mengine. Namna moja ya
kufafanua neno katika mtazamo huu ni kulichukua kama kipashio chenye uwezo wa
kufuatwa na mtuo. Kwa hivyo, hata kama katika matamshi mtuo haupatikani, bado
(tunatarajiwa/tunajua kwamba uwezo huo upo. Kutogawanyika kwake kunamaanisha
kwamba hatuwezi kuingiza viungo vyo vyote ndani yake. Namna hii inaweza
kutumika tu pale ambapo umbo la neno halina utata. Maelezo haya yanaonyesha
kwamba ni vigumu kufafanua dhana ya neno. Hata hivyo, tunaweza kulitambua
katika uchambuzi.
Sentensi Wanasarufi mapokeo
walifafanua sentensi kama tamko lenye fikra iliyokamilika. Dhana hii ya fikra
iliyokamilika inatatiza kwa vile ni vigumu kuieleza. Je, neno halisimamii
fikra? Je, fikra ni nini? Je, fikra iliyokamilika ni gani, na ni gani ambayo
haijakamilika? Hata kama tutachukua sentensi kama fikra, bado itakuwa vigumu
kueleza dhana ya sentensi changamano au sentensi ambatano. Namna mwafaka zaidi
ya kufafanua sentensi ni kuangalia muundo wake. Kila sentensi imeundwa kwa
vipashio maalum vilivyopangwa kwa mpangilio maalum. Ikiwa tunaweza kueleza muundo
huu, basi tutakuwa tumeonyesha kipashio kinachoweza kuitika sentensi kmf. S → N+Kt Juma amefika
S → N+KV+Kt
Jua kali limemchoma S → N+Kt+N
mbwa amemuuma mtoto
Kila kipashio katika
sentensi kina nafasi yake ambayo kinachukua. Hakiwezi kuchukua nafasi ya
kingine bila kutatiza maana. Tunapochukua muundo kama kigezo cha kufafanulia
sentensi, basi sentensi inakuwa kipashio kikubwa zaidi ambacho kinaweza kuwa na
muundo wa kisarufi. Uainishaji wa sentensi katika makundi matatu – yaani
sentensi sahili, changamano na ambatano unajikita kwenye vipashio vilivyoiunda
Kirai Katika sentensi,
mnapatikana maneno ambayo yana kazi moja. Maneno haya yanaweza kuchukuliwa kama
kipashio kmf. mti mrefu/umeanguka. Vipashio vya aina hii huitwa virai (
Pia huitwa vifungu au vikundi) navyo hupatikana kama sehemu moja ya sentensi.
Virai haviwezi kujisimamia. Kila sentensi ina virai viwili vikuu vinavyoiunda
–Kirai Nomino (KN) na Kirai Tenzi (KT). Virai hivi huchukua nafasi maalum
katika sentensi. Lazima kila kirai kiwe na neno kuu linaloongoza mengine kmf.
KN lazima kiwe na nomino au kikundi cha maneno chenye nomino inayoyaongoza au
kiwakilishi kinachosimamia nomino. KN huchukua miundo tofauti. Muundo wa KN
Kiswahili KN → N – mtoto ( amelala) KN → N + KV – mtoto mchanga
(amelala) KN → N + KV1 + KV2 – mtoto mchanga mnyamavu
(amelala) KN → Kiw – Yeye (amelala) KN→ KV +N Yule mtoto
(amelala) KN→ N1 +N2+ Kt
(kishirikishi) + KV Juma na Ali ni wakora KN→Ø Lete mpira
Inadhihirika hapa kwamba
KN kinaweza kuwakilishwa na neno moja ambalo lazima liwe ama nomino au
kiwakilishi. Kila lugha ina muundo wa kirai ambao unaweza kuwa tofauti na
miundo ya lugha nyingine kmf. KN cha Kiswahili huanzia kwa nomino, kisha
kivumishi, kikafuata ihali KN cha Kiingereza huanzia kwa kibainishi (KB, yaani;
the, a, an) kisha kivumishi halafu nomino
kmf. Kiswahili KN N + KV KT
mtu mrefu aliingia
Kiingereza KN KB + KV + N + KT
A tall man arrived
Muundo wa KT cha
Kiswahili ni tata. Kila KT huwa na mofimu tegemezi zinazopachikwa kwenye mzizi
pamoja na maneno mengine kama vile vielezi.
kmf. Mzee alikula jana S
→ KN + KT + KL
Mtoto alikula jana
(Tutaangalia kwa undani
mambo haya tutakavyoendelea). Lakini kwa sasa tutazame kirai tenzi kwa kifupi.
KT cha Kiswahili huchukua miundo tofauti pia.
KT→ Kt+ KL Alianguka vibaya
KT→ Kt(kisaidizi)+ Kt
(kikuu) Mtoto angali analala KT→ Kt+ N+ KL1+ KL2 Alipiga mkewe vibaya sana KT→ Kt + KKH (Juma) Alilala
juu ya kitanda KT→ Kt + KN (Juma) Alikimbilia Mkate
KT→ Kt(kishirikishi) + KL
(Juma) ni hodari
Kishazi Virai huungana na kuunda
vipashio vikubwa zaidi vinavyoitwa vishazi. Hivi huwa na uzito wa sentensi.
Sentensi sahihi ni kishazi kimoja (kina kiima na kiarifu kimoja).
kmf. Kamau alilala jana
Kuna aina mbili za vishazi. Kishazi huru kinaweza kujisimamia kama sentensi
ilhali kile tegemezi hakiwezi. Sentensi huainishwa kutegemea vishazi
vilivyotumiwa kuiunda.
Kmf. Kamau alifariki
jana ( hiki ni kishazi huru)
Kamau (ambaye ni mwalimu
mkuu wa shule yetu) alifariki jana (kishazi tegemezi kimepigiliwa mstari)
ZOEZI LA 3.1
? Tofautisha vipashio
mbali mbali vya Kisarufi kwa kuvitumia katika sentensi.
3.6 Aina za Maneno Wanasarufi mapokeo
waliainisha maneno katika makundi manane. Haya ni: Nomino/jina/nauni
Kitenzi/kitendo/kiarifu(a) Kiwakilishi/pronouni/kijina Kivumishi/sifa
Kihusishi/preposisheni Kiunganishi Kielezi/kisifa Kihisishi/kiigizi/maneno ya
mshangao
Je, maneno haya yapo
katika lugha yako ya kwanza? Yatambue!
1. Nomino/Majina Nomino pia huitwa majina
na ni neno linalotumiwa kusimamia kitu. Kitu hiki kinaweza kuwa mtu, mahali nk.
Jina ni neno linalotaja kitu, hali au jambo lolote hata kama ni la kufikiriwa
tu (Nkwera, 1978:8). Kutokana na sifa zao mbalimbali nomino zimegawanyika
katika aina zifuatazo.
a. Majina ya pekee
Haya ni majina
yanayotaja vitu maalum kama vile watu, miji nchi nk. kmf.. Maria, Nairobi,
Tanzania, Jamatatu, Februari nk. Yote huanza kwa herufi kubwa.
b. Majina ya kawaida
Haya ni majina
yanayotaja vitu au mambo yote ambayo si maalum au ya pekee kwa mfano: kiti,
gazeti, samaki, jembe nk. Katika majina ya kawaida kuna ya wingi, jamii na
dhahania
(i)Majina ya dhahania
Haya ni majina
yanayotaja vitu vinavyoweza kufikirika au kudhaniwa tu, vitu visivyoweza
kuonekana au kushikika kwa mfano: usingizi, upole, uzalendo.
(ii)Majina ya wingi
Haya hutaja vitu
vinavyopatikana katika hali ya wingi tu. kmf.. maji, mafuta na mchanga.
(iii) Majina ya jamii
Haya hutaja vitu ambavyo
asili yake ni mkusanyiko au jamii ya vitu vingine, kmf. timu, batalioni,
baraza, kikosi na familia.
2. Vivumishi
Ni maneno yanayotoa sifa
zaidi za jina – yanavumisha majina. Hutoa habari zaidi za mtu/kitu/mahali –
alivyo au jinsi kilivyo, jinsi kinavyoonekana au jinsi kinavyofikiriwa kwamba
kina tabia fulani au kipo katika idadi fulani/hali fulani.
Aina ya Vivumishi
(i)Vivumishi vya sifa Maneno yanayotaja tabia, yaani namna watu walivyo au
jinsi kitu kilivyo: mfano – dogo, -ema, -chafu, -geni, safi, stadi nk.
(ii)Vivumishi vya idadi
Ni maneno yanayoonyesha idadi ya watu, vitu, au mambo kmf. moja, mbili,
chache,-ingi nk.
(iii)Vivumishi
vimilikishi Hujulisha mali ni ya nani kmf. –angu, -ake, -ao, -enu na -etu .
(iv)Vivumishi vionyeshi
Maneno yanayoonyesha ujirani wa kitu au umbali wa kitu kwa uhusiano wa kingine
kmf. huu, hiki, hizi, hili, mle, kule, zile pale nk.
(v)Vivumishi viulizi
Kama vile: -Ipi, -ngapi na gani.
(vi)Vivumishi vya pekee
Navyo ni: –enye, -enyewe, -ingine, -ote na o–ote
(vii)Vivumishi vya a
–unganifu kmf. katika sentensi zifuatazo
jeshi la mgambo
Jeshi la mzee mtu wa watu lugha ya wazee Viatu vya shule
3. Viwakilishi/
pronomino au pronauni Haya ni maneno yanayosimama badala ya majina. Viwakilishi ni vya
namna tano:
(i)Viwakilishi Vionyeshi
Huyu analala Ile naipenda Huku hakukaliki Humo hamkaliki/mnapendeza
(ii)Viwakilishi Viulizi
Matumizi yake yanaonyeshwa katika sentensi zifuatazo. Yupi unayemtaka ? (kuku)
Ngapi zimeshonwa ? (nguo) Wangapi wamebaki ? (kondoo)
(iii)Viwakilishi
vimilikishi Hivi ni kama -angu,- etu, -ake na -ao . Kwake kuna mbwa (nyumbani
kwake ...) Pako pachafu (mahali)
Yake imepotea (nguo)
(iv)Viwakilishi
vibainishi Hivi vinatumika kwa njia hii katika sentensi ili kutoa maelezo
zaidi. Kmf. Kazi ambayo haukuifanya jana utaifanya leo
(vi)Viwakilishi nafsi
Vinatumika hivi katika sentensi. Nilisema (mimi) ulisema (wewe) Alisema (yeye)
Viwakilishi nafsi huru
ni pamoja na mimi, wewe, yeye, sisi, wao, ninyi Viwakilishi nafsi
viambata vimepigiliwa mstari; nilisema, ulisema, alisema
4. Vitenzi Ni neno linaloeleza
kufanyika kwa jambo. Ni maneno yanayoonyesha kitendo kinachotendeka. Kuna aina
mbalimbali.
(i)Vitenzi Vikuu Ambavyo
hutaja matukio mbalimbali kmf. taarifa, hali ya kitendo na kauli/jinsi ya
kitendo kmf. Maria anaandika barua, Musa anaruka, Joel anateta,
Moi anatawala
(ii)Vitenzi Vishirikishi
Hufanya kazi ya kushirikisha au kuleta uhusiano baina ya jina, kiwakilishi,
kivumishi au kielezi na jina, kiwakilishi, kivumishi au kielezi kingine
kmf. Baba ni mwenyekiti
wa kijiji, Mama ni hodari, Ali atakuwa baharia, Yeye ni mrembo,
Yeye ni hatari, Tausi alikuwa mwalimu.
(iii)Vitenzi Visaidizi
Hutumika sambamba na vitenzi vikuu katika sentensi ili kukamilisha maana. kmf.
Juma angali analima Wanajeshi walikuwa wanapanda mlima
5.Vielezi Kielezi ni neno au
maneno yanayoelezea kuhusu tendo linavyofanyika
(i)Vielezi vya mahali
Hueleza zaidi matendo kuhusu mahali yanapofanyika Anapanda juu Ametokea kusini
Ameingia ndani Ameenda Nairobi
(ii)Vielezi vya wakati
Hufafanua wakati matendo yanapotokea Alifika jana Gari litawasili asubuhi
Mtihani utaanza saa tatu
(iii)Vielezi vya idadi
Hutujulisha tendo limetokea mara ngapi Nimekuja mara tatu Mponda hufika shuleni
mara chache Hii ndiyo mara yake ya kwanza kupaona
(iv)Vielezi vya
namna/jinsi Hueleza jinsi tendo linavyofanyika Anatembea polepole Walianguka
chubwi Alilala fofofo Alivaa kizungu
6.Viunganishi Huunganisha neno kwa
neno, neno kwa kikundi au sentensi kwa sentensi. Watoto wanacheza na wazee
wanapumzika Mtoto hakulia wala hakufanya matata Viunganishi vingine ni lakini,
au, ila, kwa sababu, hata, kama, ilhali, halafu, na kwa kuwa nk.
7.Vihisishi Ni maneno yanayodokezea
hisia, mguso au vionja vya ndani vya mzungumzaji. Maneno haya hudhihirisha
iwapo mzungumzaji ana kebehi, uchungu, furaha, shangwe, mshangao au utambuzi
kmf. Ala, ebo, aka, masalaale, kumbe na lo.
8.Kihusishi Hili ni neno
linaloonyesha uhusiano uliopo baina ya maneno, fungu la maneno au sentensi kmf.
wa, ya, cha, kwa na za
Mifano ya sentensi: Nguo
za Juma zimepotea Alisafiri kwa gari Aliwekelea kitabu juu ya meza
3.7 Udhaifu wa kutenga
maneno katika aina nane Kama tutakavyoonyesha, ufafanuzi wa aina za maneno una upungufu
mkubwa ambao unadhihirisha tatizo kubwa la nadharia ya sarufi mapokeo.
●Kuna maneno ambayo
yanapatikana katika makundi tofauti. Baadhi ya vivumishi hutumika kama vielezi
au nomino. kmf. Vitabu vizuri (kivumishi)
Ametembea vizuri
(kielezi) Uzuri ni utu.(nomino) Tazama pia;
Uzuri wake unababaisha
(nomino) Mtu mzuri anababaisha (kivumishi) Mtu yule anacheze vizuri (kielezi)
Ni vigumu kuainisha
mzizi kama –zuri katika mkabala huu kwa kuwa unapatikana kama nomino, kivumishi
na kielezi. Ingekuwa rahisi kama maneno yangeainishwa kutegemea utendakazi wake
katika sentensi.
● Maelezo na maana ya aina
hizi za maneno si dhahiri. Hayatokani na utafiti wowote, hayaeleweki,
hayatenganishwi vilivyo na iwapo mtu hayajui hapo awali/kutoka mwanzoni hawezi
kusema ni aina gani la neno linalozungumziwa. Wanamapokeo ueleza nomino/jina
kama neno litumiwalo kutaja mtu, mahali au kitu nk. Kutokana na maelezo haya
basi jina halipewi ufafanuzi wa kutosha.
● Isitoshe maelezo yenyewe
yalijitokeza kama kilinge. Wangeanza kutoka mahali fulani na kuishilia
palepale! Kmf. nomino ni jina la kitu. Kitu ni nomino.
● Kiwakilishi (pronauni)
kilielezwa kama neno litumiwalo badala ya nomino. Maelezo haya hayaridhishi
kwani neno lolote lile linaweza kutumika badala ya nomino.
● Mbona pia tuwe na aina
nane tu. Huenda lugha zingine zikawa na zaidi ya aina nane za maneno. Isitoshe
kikundi cha vielezi kinaonekana kuwa kina maneno ambayo hayana uhusiano wowote
kmf. haraka, sana nk. maneno haya hayana uhusiano. Tazama pia tofauti za
vielezi 1. alikimbia sana (kielezi 1) 2. Alikimbia haraka sana (kielezi 2) 3. Mtoto
mzuri sana (kivumishi)
Maneno kama sana, mno na
kabisa yanaonekana kuwa na utendakazi maradufu licha ya kuwa vielezi
Kumbuka
Licha ya udhaifu huu wa
kutenga maneno katika aina nane bado tunahitaji kategoria hizi ili kuweza
kuandika sarufi na kuitumia. Hii ni kwa sababu sarufi huelezwa kwa njia ya
kategoria na aina za maneno. Jambo muhimu basi ni kuweza kueleza kila kategoria
ya neno kulingana na matumizi yake au utendakazi wake katika sentensi.
3.8 Umuhimu wa Nadharia
ya Sarufi Mapokeo. Ijapokuwa kazi yao inadhihirisha kasoro nyingi wanamapokeo
walichangia katika kuendeleza sarufi.
● Isimu iliibuka kwa
sababu ya/au kutokana na mwamko wa wayunani wa kuihakiki lugha. Mwamko huu
ulifanya watafiti wengine kutoka sehemu zingine za ulimwengu kuishughulikia
lugha. Utangulizi uliofanywa na wanamapokeo basi ulikuwa kitangulizi na
kichocheo cha kuanzishwa kwa nadharia zingine za kutazama sarufi.
●Walitoa dhana za
kisarufi zinazotumika mpaka wa leo. Istilahi na dhana nyingi zinazotumika
katika isimu leo kama vile nomino, vitenzi, sentensi na vishazi zilitokana na
kazi ya wanasarufi mapokeo.
● Istilahi zilizozuliwa na
wanamapokeo zinaendelea kutumiwa na kupanuliwa huku zikipewa mtazamo mpya ili
ziweze kutumika katika lugha nyingi iwezekanavyo.
●Wayunani ndio waliokuwa
watu wa kwanza kutumia kategoria za kisarufi zinazotumiwa leo kama jinsia, unyambulishaji,
idadi, wakati na hali.
3.9 Dhana zaidi za
Sarufi Usarufi
Sentensi inaelezwa kuwa
na usarufi endapo haijavunja sheria yoyote ya uundaji wake, yaani imefuata
mpangilio wa maneno unaokubalika kuwa ni sahihi. Sentensi itakosa usarufi ikiwa
maneno, vifungu/vikundi au hata vishazi ambavyo havikubaliwi kufuatana
vimefanya hivyo. Hapa sentensi itakosa kukubalika katika kiwango cha sintaksia
kmf. *Mzuri mtoto sana alimpiga Juma **Sana alimpiga mzuri mtoto Juma
Usarufi hasa unahusu
kule kuundwa kwa njia nzuri kwa sentensi kisarufi na kisintaksia. Sentensi ya
pili hapo juu imekosa usarufi kwa sababu kisintaksia muundo wake haulingani na
sheria za lugha ya Kiswahili. Sentensi ya kwanza imeundwa kufuatia sheria za
kisarufi za Kiswahili. Imefuata mpangilio wa maneno ambao ni sahihi katika
sarufi ya Kiswahili.
Ukubalifu Sentensi zenye ukubalifu
ni zile ambazo zina uwezekano wa kuzalishwa, zinaeleweka, hazina utata mwingi
na zina uasilia. Ukubalifu ni dhana pana zaidi kuliko usarufi. Ikiwa sentensi
inafasirika, basi inaweza kukubalika katika kiwango cha maana kmf. Msichana hii
imekuja jana. Sentensi imekosa ukubaliano wa kisarufi lakini tunaweza kuifasiri
sentensi hii kwanza kwa kuisahihisha. Mara nyingi tunaweza kuwasiliana kwa
kiwango fulani bila kutumia sentensi zenye usarufi. Sentensi inaweza kuwa
imeundika barabara kufuatia sheria za lugha lakini isikubalike katika kiwango
cha maana:
kmf. Mtoto mzee
alinyonya kwa funjo/Fisi analia/chai ni kavu Sentensi hizi zina usarufi lakini
hazikubaliki kwa sababu zina utata mwingi, hazina uasilia na hazionyeshi
uwezekano wa kuzalishwa na mzawa wa lugha. Ukubalifu unaenda sambamba na uwezo.
Mzungumzaji asilia ana uwezo wa lugha yake ya kiasilia.
Wakati mwingine
wazungumzaji hutoa sentensi za kisarufi ambazo kwa kiwango cha maana
hazikubaliki
kmf. Mtoto mzee
alinyonya kwa fujo. Mtoto hawezi kuwa mzee. Nyonya ni kitendo cha mtoto. Fujo
inahusu kulewa hasa sio kunyonya Mfano maarufu wa Chomsky ni: Colourless green
ideas sleep furiously ( ** Colourless cannot be green. Ideas cannot sleep).
Sleeping is a passive experience and so it cannot be furious.
Ukubalifu unapatikana
katika viwango vyote vya udhibiti wa lugha. kmf. katika kiwango cha fonolojia
tutapata sentensi kama hizi.
Unasema gama nani?
(Unasema kama nani?) Gutoga haba trive-in nitaenda mara mocha (Kutoka hapa
Drive-In nitaenda mara moja)
Kumbuka
Washairi wanaweza
kufasiri semi kama hizi na basi kuzikubali.
Kiswahili kina sheria za
ukubalifu
1. N (-kawaida)→ (-Ashiria) Nomino ambayo
si ya kawaida haifuatwi na viashiria au haiambatanishwi na viashiria Kmf.
Hatusemi Nairobi hii ni chafu au Wamalwa huyu ni kiongozi mzuri
2. Kt (kishirikishi) → (+KN/KV) Kitenzi
kishirikishi hufuatwa na nomino au kivumishi Ali ni mwalimu Mtoto ni mfupi
3. Kt(Shamirishi) → (+KN) Kitenzi shamirishi
hufuatwa /huambatanishwa na nomino Alijenga nyumba Alinunua gari
4. Kt(sishamirishi)→ (-KN/KV) Kitenzi
kisichoshamirishi hakifuatwi na nomino wala kivumishi. Maria anacheka vibaya
Maria anasoma sana
Shamirishi=elekezi
Sishamirishi=kisoelekezi
Kufikia hapo nimeeleza
nadharia ya sarufi mapokeo, dhana zake, udhaifu na nguvu zake. Nimeeleza kwamba
licha ya matatizo yanayojitokeza katika mkabala huu wa sarufi, bado ni muhimu
katika kufasiri sarufi za lugha za ulimwengu.
Marejeleo ya Lazima Bornstein, P. D. 1984:
An Introduction to Transfomational Grammar. Lanham: University Press of
America.
Liles, B. I. 1971: An
Introductory Transformational Grammar. Eaglewood Cliffs: Prentice Hall Inc.
Yule, G. 1985: The Study
of Language. Cambridge: Cambridge University Press.
SOMO LA 4 Sarufi Miundo
4.0 Utangulizi Katika somo hili
nitajadili mkondo wa pili wa nadharia ya sarufi ambao ni sarufi miundo. Sarufi
miundo pia inaitwa sarufi fafanuzi au sarufi elezi. Mkondo huu aidha
unajulikana kama sarufi muundo au sarufi maumbo. Katika somo hili nitaeleza
misingi ya sarufi miundo, dhana na mambo muhimu yanayojitokeza katika nadharia
hii pamoja na baadhi ya vitengo vya nadharia hii. 4.1Shabaha •Baada ya somo hili
ninatarajia kwamba wanafunzi wataweza: 1. Kueleza misingi ya nadharia ya sarufi miundo.
2. Kufafanua dhana mbali mbali za sarufi miundo 3. Kubainisha vitengo mahususi
vya sarufi miundo 4. Kutathmini nadharia ya sarufi miundo kama mkondo wa
sarufi.
4.2 Maana ya Muundo Sarufi mapokeo hutumia
mtazamo wa uelekezaji kwa kuelezea matumizi ya lugha katika mkabala wa matumizi
bora. Uchanganuzi wake wa lugha unajikita kwenye kanuni zinazopaswa kufuatwa
ili usemi usiwe na makosa. Baada ya muda mrefu baadhi ya wanasarufi walianza
kuhisi kwamba mtazamo huu una upungufu mkubwa. Walihisi kuwa kanuni
zilizoainishwa na wanamapokeo hazikuwa na uwezo wowote wa kupimia matumizi ya
lugha, yaani hazingeweza kutumika kama kigezo cha kuainishia matumizi bora na
yasiyo bora. Henry Sweet, katika A new English Grammar (1891, Vol.I:5) anapinga
kanuni za sarufi mapokeo kwa kusema; “Kanuni za kisarufi hazina thamani yoyote
kwani zinaarifu kuhusu hali maalum. Matumizi yoyote ya lugha yana usarufi
endapo yanatumika kwa ujumla na watu”
Sweet alidhamiria
kuchambua lugha kwa mtazamo wa kisayansi. Sarufi ilichukuliwa kama
sayansi kwa kufuata mbinu au njia za kisayansi za kuchunguza mambo. Sarufi
miundo inachukuliwa kama chanzo cha uchambuzi wa kisayansi wa lugha. Lugha hapa
inachukuliwa kama mfumo uliojengeka kwa mpangilio maalum. Mfumo huu una miundo
inayodhihirisha ruwaza maalum zinazorudiwarudiwa. Uchambuzi wa lugha basi
unajikita katika uelezaji wa ruwaza hizi.
Ili kuweza kuielewa
nadharia ya sarufi miundo yafaa kwanza tufasiri dhana ya muundo kwa ujumla
wake.
Kwa mujibu wa Kamusi
Sanifu ya Isimu na Lugha (1990) muundo ni mpangilio wa vipashio mbalimbali
katika lugha.
Kamusi ya Kiswahili
Sanifu (1982) inaeleza muundo kama umbo la kitu kutokana na jinsi kilivyoundwa
au kutengenezwa. Aidha ni namna ya utengenezaji wa kitu.
4.3 Misingi ya Nadharia
ya Sarufi Miundo
Sarufi hii imejikita
katika misingi ifuatayo.
● Hujaribu kueleza lugha
na kuifafanua
●Wanamiundo wanaeleza
matumizi yote ya lugha yaani kueleza jinsi lugha ilivyo bila kujikita kwenye
matumizi bora, safi au ufuataji wa sheria/kanuni zilizowekwa.
● Wao walitegemea miundo
au maumbo ya lugha yanayoonekana yaani maumbo ya nje yaliyo dhahiri. Haya ni
maumbo tunayoyaona katika maandishi au tunayoyasikia katika mazungumzo.
●Wanamiundo walishikilia
kwamba maumbo ya lugha yanaweza kuelezeka kwa urahisi kwa vile yanaweza
kufikika au kuonekana wakati wa uchanganuzi.
●Kiini cha uchanganuzi
wao ni muundo au umbo la lugha sio maana. Walipanga vipengele vya isimu
kulingana na data sio maana.
● Walieleza muundo kama
mpangilio wa ruwaza zinazojirudiarudia ambazo zina nafasi zilizojazwa na
vipengele vya kisarufi. Kmf.
N Kt KL Mtoto analia
sana Kiatu kilipotea jana Vyumba vimesafishwa leo
● Kwao, miundo ya vipashio
ni kitu cha kidhahania ambacho huonyesha kazi ya kipashio iliyobuniwa ili
kusaidia kutoa maelezo ya kile kiwezacho kusemwa au kuandikwa katika hadhi ya kipashio.
● Kwao, lugha imejengwa
kwa mofimu, mofimu ikiwa ndicho kipashio kidogo chenye maana katika neno.
● Wanamiundo walichunguza
jinsi vipashio vinavyojenga tungo kwa kutumia mtindo wa kugawa sentensi ili
kuweza kuzichanganua.
● Wanasarufi mapokeo walifafanua
dhana zao katika mkabala wa maana – wanamiundo nao waliazima istilahi/dhana
hizi za wanamapokeo na kuzieleza upya. Walizichukulia kama vipashio vya lugha
vinavyotenda kazi kwa namna maalum. Kwa mujibu wa wanamiundo, basi utendakazi
au uamilifu ukawa ndicho kigezo cha kwanza cha kueleza dhana na istilahi
mbalimbali.
● Wanamiundo walieleza
maumbo ya vipashio hivi pamoja na uhusiano wake na vipashio vingine katika
sentensi. Walishirikisha kigezo cha maana kwa kuangalia uhusiano wa vipashio na
vingine kmf. Wanamapokeo walieleza nomino kama jina la mtu, mahali au kitu. Wanamuundo
wanaangalia nomino kama neno linalofanya kazi fulani/au kwa namna fulani (yaani
wanaangalia utendakazi wa vipengele) Wanaangalia nomino kwa uhusiano wa
vipashio vingine – kama neno linalolazimisha au kutumiwa kuleta ukubaliano wa
kisarufi katika maneno mengine ya sentensi.
● Wanamiundo walithamini
zaidi uhusiano wa vipashio au maneno katika sentensi zaidi ya maana ya vipashio
vyenyewe.
●Uhusiano wa vipashio
ndio unaounda msingi wa uchanganuzi wa wanamiundo. Kwao maana ya sentensi
inatokana na muundo wake.
Kwa ujumla mtindo wa
wanamiundo wa kugawa sentensi kwa kuangalia vipashio vyake uliitwa mtindo au
mbinu ya uchanganuzi wa viambajengo (immediate constituent analysis) or IC
Analysis.
Zoezi 4 .1 ? 1.Linganisha misingi ya
nadharia ya sarufi mapokeo na ya sarufi miundo.
2.Wanamiundo walikuwa na
msukumo upi?.
4.4 Uchanganuzi
Kiuambajengo Uchanganuzi kiuambajengo ni mojawapo ya vitengo vya nadharia ya
sarufi miundo. Uchanganuzi kiuambajengo ulitumiwa mwanzo katika mofolojia.
Katika mofolojia, mofimu hufuatana kwa namna au ruwaza maalum katika uundaji wa
maneno. Ruwaza hii huitwa muundoambajengo. Neno lenye umbo tata linaweza
kugawanywa katika viambajengo vifuasi yaani linaweza kugawanywa katika
viambajengo viwili ambavyo vinaweza pia kugawanywa kila kimoja katika
viambajengo viwili hadi kufikia mofimu au viambajengo ambavyo haviwezi
kugawanywa tena. Hivi huitwa viambajengo tamati. kmf. neno kupigana lina
viambajengo vifuasi ku+pigana, vya pigana ni pig+ ana, viambajengo tamati ni ku
+ pig + an + a Uchanganuzi kiuambajengo ulitumiwa katika sintaksia kama mbinu
ya kugawanya maneno au makundi ya maneno.
Wazo kuu hapa ni kuwa
katika sentensi yoyote, baadhi ya maneno yana uhusiano zaidi ya mengine.
Sentensi huchukuliwa kama muundo ulioundika kwa viambajengo ambavyo vinaweza
kugawanywa katika sehemu mbili hadi kufikia sehemu ambazo haziwezi kugawanyika
tena. Kila sehemu inadhihirisha maneno au makundi ya maneno yaliyokaribiana au
kuhusiana zaidi. Sehemu ambayo haiwezi kugawanywa tena huitwa kiambajengo
tamati.
Msingi wa uchanganuzi kiuambajengo
unajikita kwenye swala la ubadilishaji yaani kila kiambajengo
kilichochanganuliwa kinaweza kubadilishwa na kingine katika nafasi au mazingira
yale yale. Hivi tunaweza kuelewa ni vipi aina za maneno zimetawanyika katika
sentensi. Swala la ubadilishaji ni la kimsingi katika sarufi miundo.
Uchanganuzi kiuambajengo
ni mbinu ya uchanganuzi iliyodhihirisha uhusiano hasa wa kikundi nomino na
kikundi tenzi pamoja na viambajengo vyao. Hivyo aina za maneno kutambulika
kutegemea jinsi zilivyotawanyika na kuhusiana katika sentensi.
Uhusiano wa karibu Sentensi sio mfululizo
wa maneno. Kwa mujibu wa wanamiundo sentensi inaelezwa kama viwango vya
viambajengo. Hivyo basi ule uwezekano wa kuigawa hadi vipashio vya chini zaidi.
Kwa mujibu wa wanamiundo, kwa wazungumzaji asilia wa lugha fulani, ni dhahiri
kwamba maneno fulani ya lugha yana uhusiano wa karibu kuliko yalivyo na mengine
katika sentensi – kwa mujibu wa wanamiundo basi, sentensi ingegawanywa
kutegemea uhusiano huu wa karibu kmf.. paka waliwakamata panya.
Paka / waliwakamata
panya (mgao wa kwanza) paka / waliwakamata // panya (mgao wa pili)
paka / wa /// li /// wa
/// kamat /// a //panya (mgao wa tatu)
paka + wa li + kamata +
panya N1
+
wingi wakati + kitenzi + N2 Kwa mujibu wa wanamiundo dhana ya wingi (wa)
katika mfano huu ina uhusiano wa karibu na nomino paka kuliko ilivyo nao na
viambajengo vingine. Dhana ya wakati uhusiana mno zaidi na kitenzi. Katika
sentensi za Kiswahili ni dhahiri kwamba wingi/uchache unahusiana na nomino
ilhali nyakati/hali uhusiana na kitenzi.
Maneno mengine
yanayohusiana na nomino ni kama vionyeshi [yule, huyu, wale]; au vivumishi kama
vile [mzuri, kirefu, mnene ]. Vielezi [ kmf. polepole, haraka, hodari]
navyo vina uhusiano wa
karibu na kitenzi. kmf. mtoto huyu anacheza vizuri sana. Sentensi hii
itachanganuliwa hivi; mtoto huyu/ anacheza vizuri sana mtoto huyu/ anacheza//
vizuri sana mtoto huyu/ anacheza// vizuri ///sana
m////toto huyu/
a////na////chez////a vi////zuri ///sana
Zoezi 4.2 ?1.Changanua sentensi
hizi ukifuata mtindo wa wanakiuambajengo (a) kiatu chake kimepotea (b) mtoto
alilia usiku kucha (c) simba mkali aliwavamia mbuzi wake (d) vioo vyote
vimevunjika
Kwa ujumla upanuzi wa
sentensi katika nadharia ya sarufi miundo ulifanywa bila kuzipa
sehemu/vipengele tofauti majina na kuendelea kuzipanua na kuzipanga mradi
zinaonyesha uwiano katika ruwaza yake. kmf.. Juma anaenda Juma anaenda sokoni
Juma anaenda sokoni kununua matunda Juma anaenda sokoni kununua matunda
aliyotumwa na shangazi yake ..... anayeitwa Asha ..... ambaye ni mgonjwa sana
Je, walijuaje watakatia
wapi sentensi kwa kuangalia ruwaza kama hizi?.
Ruwaza za aina hii pia
ziliwezekana. Juma anaenda/Mary anakula/Rose anasoma Jethro ni mpole/Auma ni
mrefu/Mti ni mfupi
Ijapokuwa vipashio hivi
havikupewa majina, hadhi ya vipashio ilionekana kuchukua orodha hii. Sentensi
ambacho ndicho kipashio kikuu, kishazi, kirai, neno, mofimu na fonimu (sauti)
Njia nzuri ya kuonyesha
mtindo huu ni kwa kutumia kielelezo cha aina ya mti. Matawi mbalimbali ya mti
hudhihirisha migao mbalimbali.
Paka // mweusi a /// li
/// m /// fuata // panya Kwa kutumia mtindo huu sentensi za aina nyingi [kmf.
sentensi sahili, ambatano, changamano] zinaweza kugawanywa na kuchanganuliwa.
Kmf. Panya mweusi ambaye alikuwa akiwasumbua kina Juma alifuatwa na paka mweupe
Paka mkubwa mweusi
alimfuata panya mweupe
paka mkubwa mweusi a li
m fuat a panya mweupe
Mchoro huu wa mti
unaonyesha wazi hadhi ya vipashio. Vipashio vidogo zaidi huunda kwa
kuunganishwa pamoja kuleta vipashio vikubwa zaidi kutoka chini hadi juu. Dhana
ya upanuaji ndiyo hutumika zaidi. Vipashio husemekana kuwa vimepanuliwa kutoka
vingine iwapo vipashio hivyo vinaweza kuchukua nafasi yake kmf. a, b ni
upanuaji wa A iwapo a,b vinaweza kuchukua nafasi ya A. kmf.
a b paka mweusi alimfuata
panya mweupe
A Mtindo wa upanuaji ni
dhana kuu katika uchanganuzi wa wanamiundo. Pia, wazo la vipashio kuchukua
nafasi ya vingine ni mahususi.
Kmf. paka mweusi
alimfuata panya mweupe
Mbwa
mkali................................. Kuku mwekundu...........................
Mnyama mwingine.......................
Zoezi 4.3 ? Je, huchukuaji nafasi ni
upi? Ueleze kwa kutoa mifano ya sentensi
Hapo juu tumegusia dhana
ya upanuaji. Hebu tuieleze zaidi. Katika sentensi hii: Mti mrefu
ulikiangukia kiti cheusi (A). Sentensi hii inaweza kupanuliwa ikawa Mti
mrefu aina ya mchungwa ulikiangukia kiti cheusi cha mzee Juma (B) inaweza
pia kufupishwa ikawa mti ulikiangukia kiti.
B ni upanuaji wa A
Upanuaji hapa ni mbinu inayotumiwa kuonyesha huchukuaji nafasi wa viambajengo
fulani na vingine. Pia upanuaji huleta maana ya kule kuongezea vipengele fulani
kwa sentensi hivi kwamba tunaanza na neno moja hatimaye kuwa na maneno mengi.
Tazama; Chungwa limeiva Chungwa lililoiva lilitundwa na Eva Jana chungwa
lililoiva lilitundwa na Eva na Adam Inasemekana kwamba chungwa lililoiva
lilitundwa na Eva na Adam shambani mwa Eden.
Njia nyingine ya
kuwasilisha mgao wa viambajengo inaonyeshwa hapa chini:
Mtoto huyu anasoma
polepole
(mkato 1) Mtoto huyu
anasoma polepole
(2) mtoto huyu anasoma
polepole
(3) m toto huyu a na som
a polepole
Zoezi 4.4 ? Changanua sentensi
zifuatazo kwa kutumia uchanganuzi kiuambajengo. (a) Mtoto wake amepona (b) Wezi
walikamatwa jana (c) Rehema aliamka mapema sana
4.5 Faida za Uchanganuzi
Kiuambajengo
●Viambajengo huonyesha
mpangilio wa kimstari au mfuatano wa maneno na vijengo vingine katika sentensi.
●Mtindo huu huonyesha
hadhi ya viambajengo hadi kufikia kile chenye hadhi ya chini kabisa.
● Uambajengo kwa kiasi
fulani huweza kupambana na shida ya utata wa kimuundo katika umbo la sentensi.
kmf. Baba Juma amefika
Baba Juma / amefika Baba
/ Juma amefika
● Ni njia ya kimsingi au
njia ya kuendelea kuchanganua sentensi katika kujenga viwango vya vipashio.
Mbinu hii ilipisha njia zingine zilizofana zaidi yake.
4.6 Udhaifu wa
Uchanganuzi Kiuambajengo
● Mtindo wa viambajengo
mwanzo ulichukulia kwamba sentensi imeundwa na mfululizo wa maneno yaliyopangwa
kwa mstari. Kwa hivyo mtindo huu hauwezi kugawa vizuri sentensi ambazo zina
maneno ambayo hayajitokeza katika mfululizo (ruwaza ya mfuatano). kmf. (a)
Unataka kuondoka je! →hawangeeleza
kipashio je.
(b) She made the whole
story up
‘up’ inahusiana zaidi na
‘made’ (made + up)
● Mtindo huu haungeeleza
baadhi ya utata katika sentensi, jambo ambalo linawezekana iwapo viambajengo
tofauti vitapewa majina. kmf. baba Juma amefika
S S
KN KT KN KT
N1 N2 nafsi wkt mzizi N1 N2 Kt
nafsi wkt mzizi kiishio
Baba Juma a me fika Baba
juma a me fik a
Baba Juma amefika Baba
Juma amefika
KN KT KN KT
● Mtindo huu haukuonyesha
jinsi ya kuunda na kuzalisha sentensi mpya na zaidi isipokuwa zile
zinazopatikana katika data.
● Kigezo cha kugawa
hakikuonyeshwa vilivyo.
● Hawakuonyesha majina ya
viambajengo.
● Uchanganuzi kiuambajengo
ulishindwa kutumika kwa baadhi ya sentensi ambapo viambajengo vikuu
havikudhihirika kwa urahisi. Kmf.
Je, mzazi wangu aliitwa na
mwalimu mkuu? Mtoto hakulia wala hakuleta matata Mwalimu alipigwa na mzazi
● Uchanganuzi kiuambajengo
ulishindwa kudhihirisha mahusiano maalum kati ya sentensi kama vile sentensi
msingi na sentensi zalishwa kmf. uhusiano wa kauli tendi na kauli tendwa katika
sentensi kama vile
(a) Juma alipiga mtoto.
(b) mtoto alipigwa na
Juma.
●Uchanganuzi huu
ulijikita kwenye semi maalum yaani semi zilizorekodiwa ambazo huitwa kongoo.
Uchanganuzi kama huu unaofuata mtazamo elezi huishilia kuorodhesha data. Sarufi
iliyokamilika sharti iweze kueleza sentensi au semi zilizotolewa na mzungumzaji
pamoja na zile ambazo bado hazijatolewa yaani lazima ueleze umilisi/uwezo wa
mzungumzaji asilia unaomwezesha kuzalisha sentensi zisizokuwa na kikomo au
sentensi kochokocho. Lazima sarufi iweze kutilia maanani sentensi
zilizorekodiwa na zile ambazo hazijarekodiwa. Sarufi miundo ambayo ni mfano
mzuri wa sarufi elezi inashindwa kutekeleza jambo hili.
Zoezi 4.5 ? Tathmini mbinu ya
uchanganuzi kiuambajengo kama njia ya kuchanganua lugha?
Marejeleo ya Lazima Bornstein, P. D. 1984:
An Introduction to Transfomational Grammar. Lanham: University Press of
America.
Liles, B. I. 1971: An
Introductory Transformational Grammar. Eaglewood Cliffs: Prentice Hall Inc.
Yule, G. 1985: The Study
of Language. Cambridge: Cambridge University Press.
SOMO LA 5
Sarufi Miundo Virai 5.0 Utangulizi Kufikia hapo tumepitia
mikondo ya awali ya sarufi. Katika somo hili, tutabainisha kitengo kingine cha
nadharia ya sarufi miundo kinachojulikana kama Sarufi Miundo Virai. 5.1 Shabaha •Baada ya somo hili
wanafunzi wataweza: 1. Kueleza misingi ya nadharia ya sarufi miundo virai. 2.
Kufafanua dhana mbali mbali za sarufi miundo virai. 3. Kufafanua sentensi kwa
kutumia vielelezo tungo. 5. Kuchanganua sentensi kwa kutumia kanuni miundo
virai. 6. Kutathmini nadharia ya sarufi miundo virai kama mkondo wa sarufi.
5.2 Alama za Sarufi
Miundo Virai Zifuatazo ni alama tutakazotumia katika kufafanua nadharia ya
sarufi miundo virai. S Sentensi N Nomino Kt Kitenzi KL Kielezi KV Kivumishi KW
Kiwakilishi KU Kiunganishi KH Kihusishi KI Kihisishi
KN Kirai Nomino KT Kirai
Kitenzi KKH Kirai Kihusishi KKL Kirai Kielezi KKV Kirai Kivumishi
5.3 Misingi ya
Kinadharia Uchanganuzi kiuambajengo hushughulikia sentensi ambazo tayari
zimetamkwa au zimetolewa. Ala yenye nguvu zaidi ingekuwa ile inayotambua
viambajengo kisarufi (umuhimu wa sarufi) pamoja na kudhihirisha sentensi
zinazoweza kuundika katika lugha. Ala kama hii sharti iwe zalishi ili iweze
kuzalisha sentensi zote za lugha zenye usarufi. Sarufi miundo virai ina sifa
hii kwa kiasi. Sarufi miundo virai ni kitengo cha Sarufi Geuza umbo na
hujihusisha tu na uambajengo.
Sarufi miundo virai
hushabihiana na uchanganuzi kiuambajengo katika matumizi yake ya ubanaji na
matumizi ya mikato/migao. Viambajengo katika sentensi hutambuliwa kwa kubanwa.
Alama hutumiwa kusimamia viambajengo mbalimbali kmf.: KN; KT; KKH.
Kila mabano
yaliyokamilika (bano la kufungua na kufunga) hudhihirisha kiambajengo kifuasi
kmf. viambajengo vifuasi vya sentensi ifuatayo vinaweza kubanwa hivi
[[[mtoto] [mtukutu]]
[[aliitwa] [[na] [[mwalimu] [mkuu]]]]]
Ubanaji/mkato katika
sarufi miundo virai huwakilisha/husimamia muundo kirai wa sentensi ambao pia
huweza kuwakilishwa katika mchoro matawi/kielelezo matawi.
S
KN KT
N KV Kt KKH
KH KN
N KV
Mtoto mtukutu aliitwa na
mwalimu mkuu (mkufu tamati)
Mchoro matawi au ubanaji
kama kielelezo cha muundo kirai wa sentensi huitwa kielelezo tungo.
Hatima yake ni kudhihirisha viambajengo vifuasi vilivyoiunda sentensi.
Mahali matawi mawili
yanapokutana huitwa kifundo. Isipokuwa vistari vya mwisho, kila kifundo
kinawakilisha kiambajengo ambacho husimamiwa na alama kmf. KN, KT, N, K nk. na
ambacho ni kipashio cha kisarufi. Ikiwa kifundo kinapatikana juu ya kingine,
basi kinasemekana kuwa kinakiongoza au kinakimiliki. Uongozi huu unadhihirisha
vile kiambajengo kikubwa kinaweza kuundwa kwa viambajengo vidogo vidogo. Mchoro
matawi vilevile huonyesha ni kiambajengo kipi hutangulia kipi na ni kipi
hufuata.
Kmf. KN cha kwanza
hufuatwa na KT. Kt hufuatwa na KN cha pili nk.
Michoro matawi ya miundo
virai hutupa maelezo kuhusu muundo wa sentensi lakini haituelezi ni vipi
sentensi mpya zinaweza kuzalishwa. Hili hufanyika kupitia kwa kanuni miundo
virai .
Zoezi la 5.1
?Fafanua dhana zifuatazo:
(i) kifundo (ii) kielelezo tungo (iii) ubanaji
5.4 Kanuni Miundo Virai Kanuni miundo virai
hutumiwa katika kuonyesha na kueleza viambajengo vya sentensi. Kanuni hizi zinaonyesha
maana ya sentensi. Kanuni hizi ndizo huunda sarufi miundo virai. Kwa kutumia
kanuni hizi, sarufi hii inaweza kuzalisha sentensi nyingi. Kupitia kwa kanuni
hizi vijisehemu tofauti vya tungo vinaweza kupewa majina na pia kuelezwa
kisarufi. Jambo hili halingewezekana kupitia uchanganuzi wa viambajengo. Kanuni
miundo virai ni sheria za kuandika upya. Sheria hizi huandika upya sehemu zote
za tungo hadi kufikia kiwango cha mofimu.
Jinsi ya kueleza kanuni
hizi kmf.
Mti mrefu uliangukia nyumba nzuri Sentensi hii inaweza kuzalishwa kwa kupitia
kanuni sita. 1. S → KN + KT 2. KN → N + KV 3. KT → Kt + KN 4. N → m-ti, nyumba 5. KV → m-refu, n-zuri 6. Kt → u-li-anguk-i-a
Tunaweza kutumia kanuni
hizi na kuunda sentensi nyingine kwa kutumia maneno yale yale lakini katika
nafasi tofauti (ni muhimu tutilie maanani upatanisho wa kisarufi. Kmf: Nyumba
nzuri iliangukia mti mrefu. Nyumba ndefu iliangukia mti mzuri. Mti mzuri
uliangukia nyumba ndefu.
Sentensi zaidi zinaweza
kuundwa kwa kubadilisha maneno yaliyotumiwa katika sentensi hii na mengine ya
aina moja. kmf. kuku → mtoto → mbwa
mweusi → mrefu → mchoyo fukuza → piga → meza Kanuni hizi
zinaweza kufasiriwa kwa namna mbalimbali. Kanuni ya KT → Kt + KN haimaanishi
kwamba ni lazima kila KT kiweze kupanuliwa hivi. KT kinaweza kupanuliwa na kuwa
kitenzi pekee kmf. Mtoto amekuja. Kanuni mwafaka zaidi ingekuwa
KT → Kt (-KN). Ikiwa hivi
basi, kiambajengo cha KN katika KT si cha lazima. KT kinaweza kupanuliwa kwa
namna nyingine pia kmf. KT → Kt + KL Asha alikimbia haraka KT → Kt + KV Kamau ni mzuri KT → Kt + KKH Mtoto alipanda
juu ya meza KT → Kt + KN + KN Mwalimu alimpatia mtoto kitabu KT → Kt (kisaidizi) + Kt
(kikuu)
Mtoto angali analala Mtu
alikuwa amepotea Walimu wamewahi kumtembelea Ng'ombe wamekwisha kukamuliwa KT → Kt + N + KKL
Alipiga mkewe vibaya
sana KT → Kt + N + KU + KL
Alishona nguo kwa kasi
KT → Kiw + Kt
Amelala KT → Kiw1 + Kiw2 + Kt + N + KL
Yeye (a)lifika Nairobi
jana
Kanuni hizi hupanua
kategoria za kisarufi katika kategoria nyingine za kisarufi kama vile S → KN + KT; KT → Kt + KN; KN → N + KV kmf. kanuni 1-3.
Hizi huitwa kanuni kategoria
Kanuni zingine 4 – 6
hupanua kategoria za kisarufi na kuzifanya maneno maalum kmf. Kt → uliangukia; N → mti, nyumba KV → mrefu, nzuri nk. Ili
kanuni hizi (4-6) ziweze kuzalisha sentensi zinazokubalika katika lugha ni lazima
zionyeshe kwa mfano vitenzi vinavyoweza kupanuliwa na kuwa na Kt na KN na vile
ambavyo haviwezi. Hii ndiyo sababu vitenzi hugawanywa katika makundi mawili
kitenzielekezi/kitenzi shamirishi na kitenzi kisoelekezi/kitenzi sishamirishi.
Tunahitaji kanuni za uchopekaji wa maneno/leksika ambazo zitatuonyesha kwamba
kitenzi piga lazima kifuatwe na KN ilhali kitenzi lala si lazima
kifuatwe. Uchopekaji wa maneno humaanisha hali ya kuweka maneno katika nafasi
zilizochukuliwa na alama, yaani kupanua kategoria za kisarufi katika maneno.
Kanuni zinazotuonyesha
neno ambalo likitumika lazima lifuatwe na kategoria ya kisarufi huitwa kanuni
za kategoria tegemezi. Jambo muhimu la kutilia maanani kuhusu kanuni
hizi ni kuwa zinaongoza maneno kwa kuonyesha ni yapi yanayoweza kufuatwa na
kategoria zingine za kisarufi.
Kuna kanuni zingine
zinazoongoza matumizi ya maneno ili yasitumike/yasiwekwe katika sentensi moja
na mengine hivi tunajiuliza ni kitenzi kipi kinaweza kutumika na nomino ipi; ni
nomino ipi inaweza kutumika na kivumishi kipi nk. kmf. kitenzi kunywa kinaweza
kutumiwa pamoja na nomino ambayo haina sifa ya kimaana ya kunywa kmf. ugali?
Bila kanuni hizi, mzungumzaji ataishilia kuunda sentensi zisizokubalika kimaana
kwa
kutumia kanuni za
kategoria za kisarufi pamoja na zile za kanuni za kategoria za sarufi tegemezi.
Kanuni hizi ndizo hutuwezesha kuzalisha sentensi ambazo zinaweza kufasirika
kimaana kmf. tazama: - Ouma anakula ugali - Ouma anakula maji - Ouma analala
motoni
Colourless green ideas
sleep furiously Kanuni zinazoongoza matumizi ya maneno ili kitenzi kmf.– kula
kisifuatwe na maji kwa mfano huitwa kanuni teuzi. Kanuni hizi ni za
kimaana na wala si za kisarufi. Zisipofuatwa, sentensi zenye usarufi zinaweza
kuzalishwa lakini zikakosa maana. Kanuni hizi hujikita kwenye lugha maalum kmf.
Kiingereza drink – (+N liquids) Kiswahili kunywa – (+N majimaji) Kikamba kunywa
– (+N majimaji + sigara + bangi + moshi+ tobako Kanuni teuzi huwa maalum katika
kila lugha.
5.5 Kanuni Miundo Virai
na Unyambuaji Kwa kutumia kanuni miundo virai, tunaweza kunyambua sentensi.
Unyambuaji ni tendo la kupachika vipashio kwenye kiini ili kujenga maneno. Hapa
unyambuaji utachukuliwa kama mkufu wa alama zilizopangwa. Mkufu huu wa alama
unajenga sentensi. kmf. 1. S → KN + KT Juma amefika 2. KN → N Juma 3. KT → Kt amefika 4. Kt → Kiw + wkt uliopo + mzizi (kit)
Kwa kutumia unyambuaji:
1. # S # 2. # KN + KT # 3. # N + Kt # 4. # N + Kiw. + wkt + mzizi
wa kitenzi # 5. # N + Kiw. nafsi ya kwanza
+ wakati uliopo + mzizi wa kitenzi #
N → Juma Kt → amefika (# ni mipaka ya sentensi )
Unyambuaji hufuata
utaratibu maalum. Alama hunyambuliwa moja baada ya nyingine mpaka (hadi)
tunafikia wakati alama haziwezi kunyambuliwa tena. Unyambuaji unaweza kugeuzwa
hadi kielelezo tungo
-1- S
-2- KN KT
-3- N Kt
-4- Kiw wkt mzizi
kiishio
Uliopo
-5&6- Juma a me fik
a
mf. 2 Mwalimu mkuu
alifukuza watoto wote (unyambuaji) 1. S → KN + KT 2. KT → Kt + KN 3. KN → N + KV 4. Kt → Kiw + wkt + mzizi
Uliopita 5. N → mwalimu, watoto 6. KV → mkuu, wote 7. Kt → alifukuza
mwalimu mkuu alifukuza
watoto wote
S
KN KT
N KV Kt KN
N KV
M-walimu m-kuu
a-li-fuk-uz-a wa-toto w-ote
Viatu vyangu vyote
viliibiwa jana usiku
S
KN KT
N KKV Kt KKL
KV1 KV2 KL1 KL2 (wakati) (wakati)
Viatu vyangu vyote
vilibiwa Jana usiku
Rhoda na Monica wangali
wanaugua
S
KN KT
N KU N Kt (kikuu)
Kt Kisaidizi
Rhoda na Monica wangali
wa na ugu a
Juma ni mzuri ( mkali,
mnene, hodari)
S
KN KT
N Kt(kishirikishi) KV
Juma ni mkali (mwalimu,
mnene, hodari)
S
KN KT
N KV Kt KN
Kiw wkt kiini kiishio
N KV
idadi
Mwalimu mkuu a li fukuz
a watoto wote
Yeye angali mgonjwa
S
KN KT
N Kt KV
Kiw. Kionyeshi kisaidizi
Yeye angali mgonjwa
Juma ni mkali
S
KN KT
N Kt KV
(kishirikishi)
Juma ni mkali
Zoezi la 5.2 ?Fafanua sentensi
zifuatazo huku ukitumia ama unyambuaji au vielezo tungo
1. Chakula kile ni
kitamu 2. Cha mlevi huliwa na mgema 3. Tutakapofika kwake tutafurahia 4. Leo
mvua nyingi imenyesha 5. Twawaombea Mola awape nguvu
5.6 Umuhimu wa Kanuni
Miundo Virai
● Kanuni miundo virai
huongoza viambajengo katika sentensi na kutaja muundo wa viambajengo
vinavyopatikana katika sentensi fulani. Pia hutaja vipashio vinavyounda
sentensi kmf..
S → KN + KT Hutaja kwamba
vipashio vingine vya sentensi vimeundwa kwa maneno kadha wa kadha kmf.
KKH → K + KL + Kl
Kwa haraka sana
Ilhali vipashio vingine
vimeundwa kwa neno moja N → mti
● Kanuni miundo hujenga
msingi wa sarufi miundo virai wa lugha na sarufi inayotumia kanuni hizi huitwa
sarufi miundo virai.
● Sheria/kanuni miundo
virai zinaweza kuzalisha sentensi zote ambazo ni za kisarufi katika lugha
husika.
● Zinaonyesha mpangilio wa
viambajengo katika sentensi. Huonyesha jinsi viambajengo vinavyoambatana kwa
utaratibu. Kmf.. S → KN + KT sio
S → KT + KN hata katika
sentensi Kama
(1) Alienda itakuwa
S → KN + KT na pia (2) Lete
itakuwa S → KN + KT
Sio S → KT (pekee).
Sheria hizi zinaonyesha
baadhi ya vipashio hadi kufikia kiambajengo cha chini kabisa.
S → KN + KT KN → N Juma KT → Kt analima Kt → Kw + wkt + mzizi + kiishio
(A-na-lim-a)
●Huonyesha majina ya
vipashio na uhusiano wake.
5.7 Vielelezo Tungo
Jukumu la sarufi ni
kutoa maelezo ya sentensi. Sarufi hueleza ishara S → KN + KT na
kuziambatanisha na sentensi halisi. Haya huwezekana kwa mujibu wa sheria za
sarufi hiyo (ya lugha husika) S → KN + KT inatuagiza tuandike sentensi kama kirai nomino (KN) na
kirai kitenzi (KT). Haya kwa kutumia kielelezo tungo huonyeshwa kama:
S
KN KT
Asha amelala
Sheria za kielelezo
tungo hufuatwa kutoka kushoto hadi kulia. KT huweza kupanuliwa pia kama
KT
K KN
N
Alimwaga Chai
Ni vizuri itambulikane
ya kwamba mara nyingi pana uwezekano wa kuwa na KN mbili kmf.
S
KN1 KT
N Kt KN2
N
Mtoto a li tema mate
KN ambayo inamilikiwa na
S moja kwa moja ndiyo kiima cha sentensi hiyo. KN2 inayomilikiwa na KT
ndiyo yambwa ya sentensi hiyo.
5.7. Dhana Za Ziada
5.7.1 Dhana za Kielelezo
Tungo (a)
Kifundo
Katika kielelezo cha
matawi, kifundo huwakilisha mahali ambapo viambajengo sisisi hutengana kmf.
- V - Vifundo
Jina la kategoria la
kisarufi linalojitokeza katika kifundo huitwa jina la kifundo. Kuna vifundo
ambavyo huwa na matawi na vile ambavyo havina matawi. Tukichukua mfano wa
sheria hii X → YZ tunaweza kuwa na mti
huu:
X
Y Z
Katika mfano huu X
humiliki Y na Z. Y na Z ni ‘watoto’ ‘mazao’ ya X ilhali Y na Z ni vifundo dada.
Y na Z ni vifundo watoto wa X. Majina haya hutumiwa katika sarufi miundo virai
ili kufafanua utaratibu wa kupanga vipashio katika muundo wa ndani wa sentensi.
Dhana ya njia hutumiwa
kueleza mstari wa moja kwa moja kutoka kifundo kimoja hadi kingine kmf.
X YZ ni vifundo watoto
wa X
YZ ni vifundo dada Y Z
ZB ni njia
A B
Kutokana na mchoro huu,
tunaweza kueleza kwamba X inamiliki Y na Z ilhali Z inamiliki A na B.
Kifundo kilicho juu
zaidi ndicho kinachomiliki vifundo vya chini au vilivyo chini yake.
Kifundo ambacho
hakimiliki vingine huitwa kifundo tamati kmf. B. Kile ambacho humiliki
vingine sio kifundo tamati kwani kinaweza kupanuliwa kmf. Z. Kifungu cha
sentensi ambacho hujitokeza chini ya vifundo mwisho, yaani mwisho wa kielelezo
tungo huitwa mkufu tamati.
X
Y Z
A B
Alienda sokoni mkufu
mwisho/tamati
5.7.2 Dhana za Sarufi
Miundo (a)
Kifundo tamati na kifundo ambacho si tamati Aina ya vifundo hivi
hupatikana katika kielelezo tungo. Vifundo tamati ni aina ya vifundo ambavyo
havimiliki vingine au haviongozi vingine. Vifundo ambavyo si tamati vinaweza
kunyambuliwa kwa kutumia sheria za kuandika upya. Vifundo ambavyo si tamati
humiliki vingine. Vifundo tamati hujenga mkufu tamati. Mfano wa vifungo tamati
ni (Juma amefika) mkufu tamati N + Kt. Vifundo ambavyo si tamati mf. KN + KT
Tutaonyesha haya kwa
njia ya unyambuaji: S → KN + KT (Vifundo ambavyo si tamati) KN → N Juma (kifundo tamati)
KT → Kt amefika (kifundo
tamati)
(Kt → Kw + wkt + mzizi +
kiishio)
A- me- fik -a Juma
amefika (mkufu tamati) Maelezo haya yanaweza kuonyeshwa katika kielelezo tungo.
-1- S
-2- KN KT
-3- N K
-4- Kiw wkt mzizi
-5- Juma a me fik a
1,2,3 → vifundo ambavyo si
tamati 4 → kifundo tamati 5 → mkufu tamati
(b) Jina amilifu Jina
amilifu huonyesha kazi/jukumu la kiambajengo fulani katika kielelezo tungo kmf.
kiambajengo kinachotekeleza kazi ya;
KN kama vile (mwalimu
mkuu) KT kwa mfano (alifukuza wanafunzi wote)
(c) Jina kategoria